MICHARAZO MITUPU

KWA HABARI ZA BURUDANI, MICHEZO NA MATUKIO MBALIMBALI

Saturday, September 22, 2012

Minziro amrithi Saintfeit, Mwalusako arejeshwa Jangwani

Lawrance Mwalusako
KLABU ya soka ya Yanga imemrejesha madarakani Katibu Mkuu wao wa zamani, Lawrance Mwalusako na kumpa nafasi kocha msaidizi wa timu hiyo, Fred Felix Minziro kukaimu ukocha mkuu baada ya kumtimua aliyekuwa kocha wake, Tom Saintfiet.
Taarifa zilizopatikana mapema leo leo asubuhi inasema kuwa, Mwalusako atakaimu nafasi ya ukatibu Mkuu iliyokuwa ikishikiliwa na Celestine Mwesigwe,huku Sekilojo Chambua akiteuliwa kuwa meneja wa timu na mtangazaji wa Cloud's, Abdul Mohammed akimrithi Louis Sendeu aliyekuwa amemaliza mkataba wa kuwa Afisa Habari wa Yanga.
Kutokana na mabadiliko hayo leo Yanga itashuka dimba la Taifa kuvaana na JKT Ruvu ikiwa chini ya safu mpya ya benchi lake la ufundi, Minziro akiongoza kama kaimu kocha Mkuu.
Fred Felix Minziro
Yanga haijashinda mechi zake mbili za awali ikianza na suluhu dhidi ya Prisons ya Mbeya kabla ya kubamizwa mabao 3-0 na Mtibwa Sugar.
Unknown at 12:49 PM No comments:
Share

  MECHI ZA ‘LIVE’ SUPER SPORTS LIGI KUU TANZANIA BARA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Septemba 21, 2012

MUDA WA MECHI ZA ‘LIVE’ SUPER WEEKEND
Mechi tano za Ligi Kuu ya Vodacom za Super Weekend katika mzunguko wa kwanza zitakazooneshwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha Super Sport zitaanza kati ya saa 1-.30 jioni na saa 1 kamili usiku.

Septemba 28 mwaka huu kutakuwa na mechi kati ya Azam na JKT Ruvu itakayofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 1 kamili usiku. Mechi ya Simba na Tanzania Prisons itakayochezwa Septemba 29 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam itaanza saa 11 kamili jioni.

Yanga na African Lyon zenyewe zitapambana Septemba 30 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 11 kamili jioni wakati Ruvu Shooting na Mtibwa Sugar zitaoneshana kazi Oktoba 1 mwaka huu Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam kuanzia saa 10.30 jioni.

Mechi ya mwisho katika Super Weekend itakuwa Oktoba 3 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ikiwakutanisha watani wa jadi Yanga na Simba, na itaanza kutimua vumbi saa 1 kamili usiku.

TWFA YATANGAZA KAMATI YA UCHAGUZI
Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake Tanzania (TWFA) kimetangaza Kamati ya Uchaguzi yenye wajumbe watano kwa ajili ya uchaguzi wake unaotarajiwa kufanyika Novemba mwaka huu.

Kaimu Mwenyekiti wa TWFA, Margreth Mtaki amewaambia Waandishi wa Habari, Dar es Salaam leo kuwa kamati hiyo itaongozwa na Ombeni Zavala, na itarajia kutangaza mchakato wa uchaguzi huo Jumatatu (Septemba 24 mwaka huu).

Aliwataja wajumbe wengine wa kamati hiyo yenye jukumu la kuendesha uchaguzi wa chama hicho kuwa ni Rachel Masamu, Lloyd Nchunga, Nancy Mabula na Maneno Tamba.

Pia aliwataka wadau wa mpira wa miguu wa wanawake kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika TWFA mara Kamati ya Uchaguzi itakapoanza mchakato.

Wakati huo huo, uchaguzi wa vyama vya mpira wa miguu vya mikoa ya Kilimanjaro (KRFA) na Manyara (MARFA) unafanyika kesho (Septemba 22 mwaka huu).


Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Unknown at 11:00 AM No comments:
Share

Mpasuko wa kisiasa waibuka tena Zanzibar


Na Mwinyi Sadallah, Zanzibar

 CHAMA cha Wananchi CUF kimesema kimegundua kuna viongozi wa SMZ  hawataki maridhiano yaliyozaa serikali ya Umoja wa Kitaifa, Novemba mwaka 2010.

Tamko hilo limetolewa na Mkurugenzi wa habari, Uenezi na mawasiliano ya umma wa CUF jana Salim Bimani Abdalla, kufuatia vurugu zilizotokea katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Bububu Septemba 16 mwaka huu.

Alisema kwamba chama hicho tayari kimewafahamu baadhi ya Viongozi kutoka CCM wanaopinga serikali ya Umoja wa kitaifa na tayari wanajitayarisha kuwashitakia kwa wananchi kupitia vyombo vya kutunga sheria Baraza la Wawakilishi Zanzibar (BLW) na Bungeni.

Alisema kwamba hatua hiyo itasadia wananchi kuwatambua viongozi wenye kinyongo na mabadiliko ya 10 ya Katiba ya Zanzibar ambayo yaliruhusu mfumo wa mpya wa serikali  ya pamoja.

“Kuna Viongozi  wa Serikali hawataki maridhiano yalioleta serikali ya Umoja wa kitaifa Zanzibar tumewafahamu kupitia uchaguzi wa Bububu,”alisema Bimani.

Alieleza  kwamba vurugu za askari wa Vikosi kutumia nguvu kubwa ikiwemo kutisha watu kwa risasi za moto ni ushaidi wa kuwepo kuwepo viongozi ambao hawataki kubadilika na kumaliza siasa za uhasama visiwani humo.

Alisema kwamba hakutegemea vikosi vya SMZ  kutumia nguvu kubwa ikiwemo kutumia risasi za moto kupiga hewani wakati Vikosi hivyo vipo chini ya Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais (IKULU).

Aidha alisema kwamba katika kampeni za uchaguzi huo kuna viongozi wa CCM walitumia majukwaa vibaya ikiwemo kutoa lugha za matusi dhidi ya viongozi wa CUF wanaoshiriki kuunda serikali ya Umoja wa kitaifa.

Akizungumzia tuhuma hizo Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai alisema tuhuma za CUF hazina msingi wowote na zimelenga kuficha ukweli na kuwadaganya wananchi.

Alisema kwamba chimbuko la vurugu katika uchaguzi huo limetokana na Viongozi wa CUF kupeleka  Vijana  3000 usiku wa kuamkia uchaguzi na kuwapa kazi ya kutisha watu ikiwemo kuhakiki wapiga kura waliokuwa wanajitokeza wakiwa katika magari kinyume na sheria ya uchaguzi.

Vuai alisema kwamba vijana  wa CUF walikuwa wakizuia watu kwenda kupiga kura hasa wafuasi wa CCM na kutoa vitisho kabla ya askari kuamua kuwatawanya katika maeneo ya vituo vya wapiga kura.

Vuai alisema kwamba wangalizi wa uchaguzi kutoka  CUF wakiwemo mawaziri baadhi yao walifanya kazi  kukagua kadi za  wapiga kura wakati sio majukumu yao.



Alisema kwamba sheria za uchaguzi zilianza kuvunjwa mapema na baadhi ya Mawaziri wa CUF kutokana na kutumia magari ya umma wakati wa kampeni na uchaguzi kinyume na sheria na misingi ya Utawala bora.

Alisema kwamba CCM ilitarajia kuwa CUF watafanya kampeni za kistarabu baada ya kumaliza tofauti za kisiasa tangu kuuda serikali ya pamoja, lakini wameshindwa kubadilika na kuendeleza siasa za chuki na uhasama kinyume na mataraji ya wananchi.

Vuai alisema kwamba katika uchaguzi huo watu wenye asili ya Pemba awakuhojiwa uhalali  wa kupiga kura tofauti na watu wenye asili ya  Bambi, Makunduchi au  Donge katika uchaguzi huo.

Vuai alisema akiwa kama  muasisi wa muafaka kutoka CCM anajuta kwa kupoteza muda kutafuta amani ya Zanzibar baada ya kuibuka wanasiasa wanaorudisha siasa za chuki na ubaguzi na kuvuruga amani na Umoja wa kitaifa.

Alisema kwamba CUF imeshindwa kufanya siasa za kistarabu ikiwemo kukemea vitendo vya kuhatarisha amani na umoja wa kitaifa vinavyoofanywa na Jumuiya ya Uamsho na mihadhara Zanzibar. (JUMIKI).

Alisema Uamsho wamekuwa wakitoa lugha chafu dhidi ya Viongozi wa Kitaifa  na waasisi wa muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

“Najuta kupoteza muda wangu kutafuta muafaka wa amani ya Zanzibar wakati wezetu awataki kuacha siasa za chuki na uhasama,’alisema Vuai ambaye alikuwa Mjumbe wa kamati ya Muafaka.

Alisema kwamba akukuwa na sababu za msingi kwa viongozi wa CUF kuhakiki kadi za wapiga kura katika vituo wakati ndani ya chumba cha wapiga kura kuna mawakala wa vyama na orodha ya majina ya wapiga kura yakiwa na majina na picha za wahusika.

Katika uchaguzi huo mgombea wa CCM Hussen Ibrahim Makungu aliebuka mshindi kwa kumtagulia mgombea wa CUF Issa Khamis issa ambaye amegoma kusaini matokeo na kutangaza kupiga matokeo mahakama Kuu ya Zanzibar.

Mwisho


Unknown at 10:59 AM No comments:
Share

WAISLAM WAWAZIDI KETE POLISI WAANDAAMANA NA KUFANYA KONGAMANO DAR LICHA YA KUPIGWA MKWARA

JUMUIA NA TAASISI ZA KIISLAM TANZANIA WAKIWA KATIKA MAANDAMANO YA KUTOA TAMKO LA WAISLAM NCHINI DHIDI YA MAREKANI KURUHUSU KUTOLEWA FILAMU INAYOUKASHIFU MTUME MUHAMAD

JUMUIA NA TAASISI ZA KIISLAM TANZANIA WAKIWA KATIKA MAANDAMANO YA KUTOA TAMKO LA WAISLAM NCHINI DHIDI YA MAREKANI KURUHUSU KUTOLEWA FILAM INAYOUKASHIFU MTUME MUHAMMADI SAW

JUMUIA NA TAASISI ZA KIISLAM TANZANIA WAKIWA KATIKA MAANDAMANO YA KUTOA TAMKO LA WAISLAM NCHINI DHIDI YA MAREKANI KURUHUSU KUTOLEWA FILAM INAYOUKASHIFU MTUME MUHAMAD

waumini wa kiislam wakiwa katika kongamnao lao la kulaani Marekani kwa kuruhusu kutengenzwa kwa Filamu inayomkashfu Mtume Muhammad 'SAW' jana kwenye viwanja vya Kidongo Chekundu, jijini Dar es Salaam

Umma wa Kiislam ukiwa kwenye kongamano lao lililofanyika jana jijini Dar

Umma wa Mtume Muhammad SAW, ukiwa kwenye kongamano lao la kulaani utengenezwaji wa filamu ya kumkshfu Mtume Muhammad SAW.
CHANZO:MZUKA WA FUNGO
Unknown at 10:59 AM No comments:
Share

IBF YAWATEUA MAKAMU WANNE WA RAIS KATIKA BARA LA AFRIKA, GHUBA ZA UARABU NA UAJEMI

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAREHE 20/09/2012


Shirikisho la Ngumi la Kimataifa IBF limepanua wigo wake wa kusimamia na kuratibu ngumi katiuka bara lka Afrika, Mashariki ya kati, Ghuba ya Urarabu na Ghuba ya Uajemi. Katika miaka ya karibuni kumekuwa na ongezeko kubwa sana la vijana wengi kujiunga na ngumi na hivyo wengi kuhitaji huduma za shirikisho la IBF.
 
Ili kujiweka vizuri katika nafasi ya kutoa huduma nzuri inayotakikana, IBF imewateua Makamu wanne wa rais watakaomsaidia Raia wa Shirikisho hili Bwana Onesmo Ngowi.

Uteuzi huu umefuata mambo yafuatayo: Upendo wa wahusika wenyewe kwa mchezo wa ngumi, nafasi aliyonayo kwenye jamii, ukaribu wake na vijana, uwezo wake kielimu na michango yake kwa michezo.

Wafuatao wameteuliwa kuwa makamu wa Rais kuanzia mwisho wa mwezi huu:

Ayman Saad Bait-Saleem (Oman);

Makamu wa Rais,  Fedha
Ayman ni mhandisi mwenye shahada ya uzamili kutoka katika chuo kikuu cha Karolina ya Kusini (University of South Carolina, Colombia South Carolina, USA.) mwa nchi ya Marekani. Amefanya kazi kama Meneja Mkuu wa bandari ya Sultan Qaboos kwa miaka mingi, Meneja wa kampuni ya APL Moller Group ya Denmark nchini Oman, Kampuni ya Marekani ya ushauri wa Kihandisi na nyingine nyingi. Kwa sasa Ayman ni mfanyabishara mwenye kampuni nyingi nchini Oman mojawapo ikiwa ni AL SWAYNI SPORT SERVICES katika jiji la Muscat, Oman

William Steven Kallaghe

Makamu wa Rais, Utawala na Masoko
William ni msomi aliyebobea katika masuala ya Uchumi na Utawala na alisoma katika chuo kikuu cha Budapest, Hungary. Ana uzoefu mkubwa kwenye masuala ya uchumi na masoko na amefanya kazi na makampuni kadhaa kama Mkurugenzi Mkuu wa benki ya kiislamu ya NBC, Meneja Miradi wa benki ya CRDB, Meneja wa Masoko wa Kanda wa kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kabla ya kuhamishia ujuzi wake kama Mkurugenzi wa Masoko wa Benki ya NBC.

Henry Mann-Spain (Ghana)

Makamu wa Rais, Operations
Henry ni mfanyabishara aliyeboboea kwenye biashara mbalimbali na analimiki makampuni makubwa ya kutengeneza bidhaa za kilimo kama nguo na vyakula vya kugandishwa (Frozen Food).
Ana Shahada ya Uzamili wa Biashara (MBA) kutoka katika Chuo Kikuu cha Harvard kilichopo katika jimbo la Massachusetts nchini Marekani. Henry amefanya kazi kwa miaka mingi na mashirika ya kimataifa yakiwamo UNHCR, ILO na UNDP.
Kwa sasa ni Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya Golden Crescent Ltd yanayojishughulisha na kutengeneza bidhaa kutoka kwenye mazao ya mifugo na kilimo nchini Ghana na kuyauza nchi za Ulaya, Marekani na Asia.


Louaa Debes (Misri)

Makamu wa Rais, Ubingwa na Viwango
Louaa ni mfanya biashara anayeishi katika jiji la cairo nchini Misri na ana uzoefu nkubwa kweney masuala ya biashara za kutengeneza nguo.
Louaa Debes amesoma biashara kwenye Chuo Kikuu cha Cairo na amefanya kazi na taasisi za serikali kabla ya kuanzisha shughuli za biashara. Debes anamiliki makampouni ya ulinzi, maduka makubwa (Super markets) pamoja na kamouni ya ukodishaji wa magari.

Imetolewa na:
Onesmo A.M. Ngowi

Rais
IBF katuka bara la Afrika, Mashariki ya Kati, Ghuba ya Uarabu na Uajemi.
(IBF President for Africa, Middle East, Arabian and Persian Gulfs)
Unknown at 10:41 AM No comments:
Share

KOCHA TOM SAINTFIET ATIMULIWA YANGA BAADA YA SIKU 80 NCHINI

Kocha wa Yanga, Tom Saintfiet siku alipowasili jijini Dar es Salaam Jumatano Julai 4, 2012 na kupokewa kwa mbwembwe.

YANGA imemtimua kocha wake Mbelgiji Tom Saintfiet baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa siku 80 kamili.

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya klabu ya Yanga, Abdallah Ahmad Bin Kleb, amethibitisha kufukuzwa kwa Mbelgiji huyo ambaye ameiongoza Yanga katika mechi 14, kushinda 11, vipigo viwili na sare 1.

Saintfiet aliyetua nchini Jumatano, Julai 4, 2012, amefukuzwa siku moja tu baada ya kuwatuhumu wachezaji kuwa "masharobaro" kama moja ya sababu za mwanzo mbaya wa msimu kwa timu hiyo ambayo inashika nafasi ya 13 katika msimamo wa timu 14 za Ligi Kuu ya Tanzania Bara ikiwa na pointi 1 kutokana na mechi mbili - sare ya 0-0 dhidi ya Prisons Jumamosi na kipigo cha aibu ambacho hakikutarajiwa cha 3-0 ugenini dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro.

Kabla ya kuwatuhumu wachezaji kwa kujiona mastaa wakubwa na kubadili mitindo ya nywele kila baada ya siku tatu ili kupamba kurasa za magazeti, Mbelgiji huyo alianika jinsi walivyolazwa wawili wawili mjini Mbeya wakati walipoenda kucheza dhidi ya Prisons katika mechi ya ufunguzi wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Alilalamikia wachezaji kucheleweshewa chakula na wenye hoteli na kwamba alilazimika kuoga kwa kutumia kopo kutokana na mabomba ya 'mvua' ya kutotoa maji.



Hivi karibuni, Saintfiet alilalamikia kutolipwa mshahara wake wa miezi miwili, kutofurahishwa kwake na maisha ya kukaa hotelini badala ya kutafutiwa nyumba na pia kutopewa gari binafsi ya kutembelea na badala ya kuendeshwa kwenye "kipanya" cha klabu hiyo ambapo yeye amekuwa akikaa siti ya mbele.

Kipigo cha Mtibwa kimethibitisha kuichanganya timu hiyo ambayo mapema leo uongozi wake ulitangaza kuisimamisha kazi Sekretarieti nzima ya klabu, akiwamo Katibu Celestine Mwesigwa na Ofisa Habari, Louis Sendeu, "kutokana na utendaji usioridhisha".

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya klabu Jangwani jijini Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga alisema kwamba maamuzi hayo yamefuatia kikao cha Kamati ya Utendaji kilichofanyika tangu saa 5:30 leo hadi saa 9:30.

Wengine waliosimamishwa ni Philip Chifuka aliyekuwa mhasibu, Masoud Saad, aliyekuwa Ofisa Utawala na Hafidh Saleh aliyekuwa Meneja ambaye atapewa majukumu mengine. Taarifa nyingine zimedai kuwa nyota wa zamani wa klabu hiyo Sekilojo Chambua anatarajiwa kutangazwa meneja mpya.

Sanga alisema watamtangaza meneja mwingine katika kikao kitakachofanyika klabuni hapo kesho saa 3:00 asubuhi. 

Saintfiet ambaye pia alipewa onyo na uongozi kwa "kuongea ovyo na vyombo vya habari", aliiwezesha Yanga kutwaa ubingwa wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati maarufu Kombe la Kagame kwa mara yao ya pili mfululizo baada ya kuifundisha timu hiyo kwa kipindi cha chini ya wiki tatu.  


REKODI YA SAINTFIET YANGA
1. Yanga v JKT Ruvu             (kirafiki)                2-0
2. Yanga v Atletico (Burundi, Kagame)               0-2
3. Yanga v Waw Salam (Sudan, Kagame)          7-1
4. Yanga v APR (Rwanda, Kagame)                   2-0
5. Yanga v Mafunzo (Z’bar, Kagame)                 1-1 (5-3 penalti)
6. Yanga v APR (Rwanda, Kagame)                   1-0
7. Yanga v Azam (Kagame)                                2-0
8. Yanga v African Lyon (kirafiki)                        4-0
9. Rayon v Yanga (kirafiki, Rwanda)                   0-2
10. Polisi v Yanga (kirafiki, Rwanda)                  1-2
11. Yanga v Coastal Union    (kirafiki)                 2-1
12. Yanga v Moro United      (kirafiki)                  4-0
13. Prisons v Yanga  (Ligi Kuu)                          0-0
14. Mtibwa v Yanga (Ligi Kuu)                           0-3


Chanzo:Straikamkali
Unknown at 10:37 AM No comments:
Share
‹
›
Home
View web version

About Me

Unknown
View my complete profile
Powered by Blogger.