Mwenyekiti
wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambae pia ni Mbunge wa
Hai na Kiongozi Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Mh Freeman
Mbowe akitoa tamko la chama chake jioni ya leo katika hoteli ya Kibo
Palace ya Jijini Arusha kufuatia tukio la kushambuliwa kwa mkutano wa
Chadema jana kufunga kampeni za udiwani kwa Kata nne za Arusha Mjini kwa
bomu la kutupa kwa mkono, risasi za moto na mabomu ya machozi, tukio
lililopelekea vifo vya watu watatu na wengine zaidi ya 70 kujeruhiwa.
Timu ya waandishi wa habari waliohudhuria kikao hicho cha kutoa tamko la chama.
Tamko
la Chadema Mauaji ya Bomu Mkutano wa Arusha: Mbowe asema tukio ni la
kisiasa na lilipangwa makusudi; adai hata wakimuua yeye au Lema Chadema
bado itaendelea kuwepo
No comments:
Post a Comment