Uongozi Yanga kitanzini, TFF yaipa wiki 2
SHIRIKISHO
la Soka Tanzania (TFF) limeitaka klabu ya Yanga kuwasilisha rasimu ya
Katiba waliyoipitisha, kwa kuzingatia kuwa Muhtasari wa kikao cha
Mkutano Mkuu wao wa Juni 1 mwaka huu umeainisha baadhi ya marekebisho
waliyofanya kwa tulivyowaelekeza.
Yanga
wanatakiwa kuwasilisha rasimu hiyo kabla ya Oktoba 5 mwaka huu. Ikiwa
itakubaliwa na TFF, itapelekwa kwa Msajili wa Klabu na Vyama vya Michezo
ili waweze kufanya uchaguzi wa viongozi wao.
No comments:
Post a Comment