KAMPUNI ya
Bia Tanzania (TBL), kupitia bia yake ya Kilimanjaro, mchana huu imekabidhi basi
jipya kwa Timu ya Taifa, Taifa Stars.
Basi hilo lenye thamani ya zaidi ya Sh milioni
200, lilikabidhiwa leo katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya TBL jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa TBL, Robin Goetzsche. Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na
maofisa kutoka TFF, wafanyakazi za TBL, wadau wa soka na vyombo mbalimbali vya
habari.
TBL imenunua
basi hilo ikiwa ni sehemu ya ufadhili kama ilivyoanishwa katika mkataba baina ya
pande hizo mbili. Mkataba huo ulitiwa saini Mei mwaka jana na lengo kuu ni
kuinua kiwango cha Taifa Stars.
Akizungumza
katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa TBL alisema: Imeshatimia miezi 10 tangu
tuanze kuifadhili Taifa Stars na malengo yetu kama wadhamini ni kuiona timu
ikipata ushindi uwanjani ma hivyo kuongeza sifa ya timu na tumeridhika na
matokeo.”
Mkurugenzi
huyo alisema, kukabidhi kwa basi hilo ni ishara kwamba TBL itaendelea kuisadia
timu ya taifa na hivyo kupandisha kiwango cha soka nchini na aliwataka wahusika
kulitunza basi hilo kwa manufaa ya timu na taifa kwa ujumla. “Tutaendelea kutoa
msaada na tunatarajia kuwa nanyi kwa nafasi yenu mtafanya bidii na hivyo kutupa
moyo wa kuendelea na uwekezaji. Tunaamini mtafanya vizuri katika mechi nyingi za
kimataifa na hivyo kupanda kwenye viwango vya FIFA.”
Kwa upande
wake, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe alisema basi hilo lenye uwezo
wa kubeba abiria 51, limenunuliwa kutoka Yutong na thamani yake ni zaidi ya Sh
milioni 200.
Akitoa
ufafanuzi, Kavishe alisema basi hilo kutoka Kampuni ya Yutong lina Chassis ya
4X2, uwezo wa injini ni 300 HP Cummins, huku likiwa na uwezo wa kumeza lita 800
za mafuta. Mbali na hayo kila siti ina mkanda wa abiria kwa ajili ya usalama
wakati wa safari, luninga mbili, redio yenye spika nane, mafriji mawili,
viyoyozi na milango ya kisasa inayojifungua na pia nafasi kutoka kiti kimoja
hadi kingine ni kubwa.
“Wachezaji
wetu lazima wawe na nafasi nzuri ya kupumzika wakati wa safari, na hiyo ndiyo
sababu iliyotufanya tumumue basi hili la kisasa zaidi likiwa na vifaa muhimu
ambavyo pia ni vya kisasa…tunawaomba kulitunza basi hili,” alisema Kavishe na
kuongeza kuwa ni jukumu lao kufanya hayo kwa mujibu wa mkataba ili kuinua
kiwango cha timu.
Baada ya
makabidhiano hayo, basi lilifanya ziara katika maeneo mbalimbali ya Dar es
Salaam ili mashabiki walione na kupiga picha huku kukiwa na matukio kadhaa ya
kusisimua kama vile kucheza na kuimba.
Naye Rais wa
TFF, Leodgar Tenga aliipongeza TBL kwa udhamini wake wa uhakika na kusisitiz
akuwa tangu wameanza wameshatekeleza ahadi walizoahidi na moja wapo ikiwa ni
kuhakikisha basi jipya linanunuliwa.
“Hawajawahi
kuchelewesha malipo hata mara moja na kwa hilo tunawashukuru sana,” alisema Rais
Tenga.
Bia ya
Kilimanjaro ilianza kuifadhili Taifa Stars Mei mwaka jana kwa mkataba
uliogharimu zaidi ya Sh bilioni 2 kwa mwaka katika kipindi cha miaka mitano na
TFF.
STRIKA
USILIKOSE
Thursday, February 21, 2013
Floyd Mayweather kurejea ulingoni Mei $, alamba mkataba mpya
Floyd Mayweather |
BINGWA wa Dunia wa WBC asioyepigika, bondia Floyd Mayweather ameoata mkataba mnono utakaomwezesha kupigana hadi mara sita ndani ya kipindi cha miezi 30.
Mkataba huo mnono utamfanya Mayweather kuwa mwanamichezo wa kwanza duniani
kuingia mkataba mkubwa kuliko mwana michezo yoyote.
Mkali huyo ambaye anarekodi ya kupigana mapambano 43 akishinda yote, ikiwamo 26 ya kuwapiga wapinzani wake kwa KO, ataanza kuutumikia mkataba huo Mei 4 mwaka huu kwa kuvaana na Robert
Guerrero.
Pambano hilo litakuwa la kwanza kwa mkali huyo aliyepanda mara ya mwisho ulingoni Mei 5 mwaka jana na kumtwanga Miguel Cotto kabla ya baadae kupelekwa jela kuitumikia kifungo kwa kosa la kumtwanga mpenziwe.
Mayweather atavaana na Guerrero mwenye rekodi ya kuicheza ,apambano 35, akishinda 31, 18 yakiwa kwa KO, kupigwa moja na kutoka sare moja katika pambano linalosubiriwa kwa hamu kuona kama mkali huyo bado yupo moto au jela imempunguza makali yake.
Katika mkataba wake mpya unahusisha matangazo na kumfanya avune mahela, mbali na mikataba yake mingine iliyomwezesha kuwa mmoja wa wanamichezo wenye noti duniani.
Subscribe to:
Posts (Atom)