STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, September 2, 2013

Simba wee acha tu, yaitafuna mafunzo Mrundi atupia mbili

Mshambuliaji wa Simba, Tambwe Amissi (kulia) akitafuta mbinu za kumtoka beki wa Mafunzo, Jumbe Omari Jumbe katika mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, ambapo Simba ilishinda mabao 4-3 na yeye Tambwe kutupia mabao mawili.
Hekaheka katika lango la Mafunzo. 
 Beki wa Mafunzo Ali Vuai Juma (kushoto) akichuana na mshambuliaji mpya wa Simba kutoka Burundi, Tambwe Amissi. katika mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Beki wa Mafunzo, Jumbe Omar Jumbe akimdhibiti mshambuliaji wa Simba, Tambwe Amissi
 Golikipa wa timu ya Mafunzo ya Unguja, Ussi Makame Ussi akiwa hana la kufanya baada ya kushindwa kuzuia kiki iliyopigwa na mshambuliaji wa Simba, Tambwe Amissi (kushoto)  na kuipatia timu yake bao la kwanza katika mchezo wa kirafiki uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. (Picha na Francis Dande)
 Golikipa wa Mafunzo, Ussi Makame Ussi akiruka bila mafanikio kujaribu kuokoa mpira uliopigwa na mshambuliaji wa Simba, Tambwe Amissi na kuhesabu bao la kwanza kwa timu yake.
Mrundi Tambwe Amissi akishangilia bao aliloifungia timu yake

Promota wa Cheka na Mmarekani aachiwa kwa dhamana


Promota Jay Msangi (katikati) akiwa na Bondia Mmarekani (kushoto) aliyekuwa aje kupigana na Bondia Mtanzania, Alphonce Mchumiatumbo katika pambano hilo la juzi.
****************************************

PROMOTA aliyeandaa pambano la Kimataifa la ubingwa wa dunia la uzito wa super middle kati ya bondia Francis Cheka na bondia kutoka Marekani, Phil Williams, Jay Msangi wa kampuni ya Hall of Fame Boxing and Promotion, aliyekuwa akishikiliwa na Polisi tuhuma za kumdhulumu bondia kutoka Marekani, ameachiwa nje kwa dhamana.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Mkoa wa Dar es Salaam, Suleiman Kova, amenukuliwa jioni hii kuwa, promota huyo aliyekuwa amekamatwa juzi Jumamosi mchana maeneo ya Oysterbay kwa mahojiano na kulala ndani kwa saa 24 ameachiwa huku upelelezi juu ya tuhuma zake zikichunguzwa.

Kamanda Kova, alisema promota huyo alikuwa akishikiliwa kwa tuhuma za kushindwa kumlipa Williams kiasi cha Dola za Kimarekani 8,200 walizokubaliana.
Kova ambaye ni Mlezi wa Ngumi nchini, alisema jambo lililofganywa na promota huyo linaweza kuitia doa Tanzania kimataifa na kusababisha watanzania kukosa kuangalia mipambano mikubwa kama iliyochezwa mwishoni mwa wiki kwa wachache wasiokuwa waaminifu.
Hata hivyo alisema jeshi la Polisi litaendelea kuchunguza kwa vile kinachoonekana ni kwamba bodnia huyo wa Marekani na promota huyo walikubaliana wenyewe hivyo watakacopfanya kuhakikisha kila kitu kinakuwa sawa ili kumfanya Mmarekani huyop kurejea kwao akiwa na amani.

Katika pambano hilo  Cheka alimchapa Williams kwa pointi na kutwaa ubingwa wa WBF, ambapo kabla ya mipambano hiyo mabondia kadhaa waliopangwa kupigana siuku hiyo waliogoma kwa muda kupanda ulingoni wakishinikiza walipwe fedha zao.

Mamia wamzika Mwanajeshi aliyeuwawa Congowauwa Congo az

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiongoza mamia ya wanajeshi, wananchi na Ndugu  na jamaa katika Mazishi ya Meja wa Kikosi cha JWTZ  Khatib Shaaban Mshindo, aliyeuawa Nchini DRC akiwa katika shughuli za ulinzi wa vikosivya Umoja wa Mataifa.
  Wapiganaji wa Jeshi la Wananachi wa Tanzania { JWTZ } wakitoa salamu zao za mwisho wakati wa mazishi ya kamanda wao Meja Khatibu Shaaban Mshindo yaliyofanyika kijijini kwake Mangapwani. Meja Khatib Shaaban ambae alikuwa Mkuu wa Kambi ya Kibaha alifariki dunia Mjini Goma Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo akiwa katika ulizi wa amani katika kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa.

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mohammed Aboud Mohammed akitia udongo kwenye kaburi wakati wa mazinshi ya Meja Khatibu Shaaban Mshindo yaliyofanyika kijijini kwake Mangapwani.
 Mwakilishi wa Vikosi vya Umoja wa Mataifa vilivyopo Mjini Goma Nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo Meja E.B. Samuel akitia udongo kuashiria ushiriki wa Umoja wa Mataifa katika mazishi ya  Marehemu Meja Khatibu Shaaban Mshindo yaliyofanyika kijijini kwake Mangapwani.
 Mamia ya wananachi, ndugu na Jamaa walioshiriki kuusitiri mwili ma marehemu Meja Khatibu Shaaban katika mahali pake Huko Mwangapwani Wilaya ya Kaskazini B, Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimfariji Kiongozi wa Familia ya Marehemu Meja Khatibu Shaaban Mshindo bwana Alhaji Machano Mtumweni mara baada ya kukamilika kwa mazishi ya Kamanda huyo yaliyofanyika kijiji kwake Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
******
ASKARI wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania { JWTZ } Meja Khatibu Shaaban Mshindo aliyefariki Dunia akiwa katika shughuli za ulinzi wa amani katika kikosi  cha umoja wa Mataifa kwenye jimbo la Goma Nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo amezikwa kwa heshima zote za Kijeshi.
Meja Shaaban ambaye alijeruhiwa vibaya kwa bomu katika eneo lake la kazi na kusababisha kuvuja damu nyingi na hatimae kusababisha kifo chake akiwa njiani kupelekwa Hospitali alizikwa kijiji kwao Mangapwani Wilaya ya Kaskazini B, Mkoa Kaskazini Unguja.
Makamanda na wapiganaji wa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania , askari wengine wa vikosi vya ulinzi, wananchi , ndugu wa marehemu walishiriki kwenye mazishi hayo wakiongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mohammed Aboud Mohammed.
Marehemu Meja Khatib Shaaban Mshindo alizaliwa Tarehe 29 Septemba 1972 katika Mtaa wa Rahaleo Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi na baadaye kupata elimu yake ya msingi na kuhitimu mwaka 1986.
Alijiunga na Skuli ya Sekondari uchama na kuhitimu kidato cha Nne mwaka 1990 ambapo baadaye akajiunga na kidato cha tano na sita katika skuli ya sekondari ya Alharamain na kumaliza mwaka 1993.
Meja Khatib Shaaban Mshindo alijiunga na Jeshi la wananchi wa Tanzania             { JWTZ } Tarehe 1 machi 1995 na kutunukiwa heshima ya kamisheni tarehe 17 mei 1997.
Katika utumishi wake Meja Khatib Shaaban Mshindo alibahatika kuhudhuria mafunzo ya afisa mwanafunzi chuoni Monduli, kozi ya uongozi wa platuni, uongozi wa kombania pamoja na mafunzo ya operesheni Nchini Canada mwaka 2008.
Kamanda Khatib kutokana na ukakamavu wake alipandishwa vyeo kuanzia nafasi ya Luteni mwaka 1998, kepteni mwaka 2004 na kufikia cheo cha meja mwaka 2010 wadhifa aliokuwa nao hadi kufariki kwake.
Marehemu Meja Khatibu Shaaban Mshindo aliwahi kushika madaraka ya Kamanda wa Kikosi mwaka 1997, Mkufunzi kuanzia mwaka 2000  hadi mwaka 2006 pamoja na kuwa kamanda wa kombania Mkoani Kibaha.
Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kutambua na kuthamini mchango wa Meja Khatibu Shaaban Mshindo alimtunuku nishani ya Miaka 40 ya JWTZ.
Umoja wa Mataifa katika mazishi hayo uliwakilishwa na Kamanda wa Vikosi vya Umoja huo Mjini Goma Nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo Meja D.B Samujeli .
Kamanda Khatibu Shaaban Mshindo aliyelitumikia jeshi la Wananchi wa Tanzania katika kipindi cha miaka 18 miezi saba na siku 28 ameacha kizuka mmoja na watoto watatu.
Mwenyezi Muungu alilaze roho ya marehemu Meja Khatibu Shaaban Mshindo Mahali Pema Peponi. Amin.

ILALA, KASKAZINI UNGUJA ZAANZA COPA KWA SARE



Na Boniface Wambura
Timu za Ilala na Kaskazini Unguja zimetoka sare ya mabao 3-3 katika moja ya mechi za ufunguzi za michuano ya Copa Coca-Cola kwa vijana wenye umri chini ya miaka 15 iliyoanza leo (Septemba 2 mwaka huu) katika vituo mbalimbali nchini.

Wafungaji wa Ilala katika mechi hiyo iliyochezwa asubuhi Uwanja wa Tamco ulioko Kibaha, Pwani yalifungwa na Ally Shaban (mawili) wakati lingine lilifungwa na Haruni Said. Mabao ya Kaskazini Unguja yalifungwa na Jecha Ally (mawili) na Shehe Ally.

Katika kituo cha Mbeya, Njombe imeanza vizuri baada ya kuifunga Katavi mabao 2-1. Mabao ya washindi yalifungwa na Rackson Mligo dakika ya 13 wakati lingine lilifungwa na Kelvin Gama dakika kumi kabla ya filimbi ya mwisho.

Bao la Katavi katika mechi hiyo iliyochezwa uwanja wa Sekondari ya Iyunga lilifungwa dakika ya 15 kupitia Joseph Edward.

Wenyeji Mbeya wameitandika Ruvuma mabao 3-0 katika mechi iliyochezwa Uwanja wa Iyunga. Mabao ya washindi yalifungwa na Joel Mwasambungu dakika 9 wakati mengine yalifungwa na Jackson Mwaibambe dakika ya 18 na 55.  

Kesho (Septemba 3 mwaka huu) katika kituo hicho kutakuwa na mechi kati ya Rukwa na Katavi itakayochezwa saa 4 asubuhi wakati Iringa na Ruvuma zitaumana kuanzia saa 2 asubuhi.

Liunda kutathimini waamuzi CAF

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhUOM9IRMZijo63-gOG0Myp2_FetrrPAa1FMIGgam1cJJeCV3Zw9RJxhccBlTqfqv1BugkRqtKZpQeEqBNDPehsoBY_0JHLwIcpdrPLMoLPcJYFT2o3h3y1-9g6SWu_adMOBBokNV6MFCU/s1600/liunda.JPG
Na Boniface Wambura
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limemteua Leslie Liunda wa Tanzania kuwa mtathmini wa waamuzi kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Coton Sport ya Cameroon na Esperance ya Tunisia.

Mechi hiyo ya kundi B itachezwa Septemba 21 mwaka huu kwenye Uwanja wa Omnisport Roumdeadjia mjini Garoua, Cameroon. Kamishna atakuwa Bema Doumbia wa Ivory Coast.

Waamuzi wanatoka Madagascar wakiongozwa na Hamada Nampiandraza. Wasaidizi wake ni Jean Eric Pierre Andrivoavonjy, Ferdinand Velomanana Linoro na Bruno Marie Andrimiharisia.
 

Kim Poulsen aweweseka amuita Henry Joseph Stars

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjRxitDiN5RLOXCBKIEoybp3pTPr5-aNuxzD0hVSuDnoAKgoQ4f3ZtjaBRCb9TkwcKTZ5q5uGvF_TEoZnFjFk267hPssx6Q6yGFkDj2S3Z4dJfXr2LSHvtVDvfxghJGYOnSCFyliv2DoII/s320/HenryJoseph.jpg
Henry Joseph
Na Boniface Wambura
KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen amemjumuisha mchezaji Henry Joseph wa Simba kwenye kikosi chake kinachojiandaa kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Gambia itakayochezwa Septemba 7 mwaka huu jijini Banjul.

Tayari Joseph amesharipoti kwenye kambi ya timu hiyo iliyoko hoteli ya Accomondia jijini Dar es Salaam. Taifa Stars ambayo iko chini ya udhamini wa Kilimanjaro Premium Lager imeingia kambini tangu Agosti 29 mwaka huu, na leo jioni itafanya mazoezi yake kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume.

Programu ya timu hiyo inaonesha kuwa kesho (Septemba 3 mwaka huu) itafanya mazoezi yake asubuhi na jioni kwenye uwanja huo huo wa Kumbukumbu ya Karume.

Wakati huo huo, kesho (Septemba 3 mwaka huu) saa 6 kamili mchana Kocha Kim Poulsen atakuwa na Mkutano na Waandishi wa Habari.