Suarez ataendelea kuwatungua makipa leo Brazili? |
Tembo wa Afrika watashangilia tena kama hivi kwa Ugiriki leo nchini Brazili? |
Ivory Coast itavaana na Ugiriki ikihitaji ushindi ili kuungana na Colombia kucheza hatua ya 16 Bora, huku Italia itavaana na Uruguay inayochuana kuwania nafasi ya kuungana na Costa Rica kucheza hatua ya pili.
Italia ilitulizwa na Costa Rica katika mechi yao iliyopita na kuwafanya kuomba dua ishinde leo ili kufuzu hatua ya pili vinginevyo itaunga na England kutoka kwenye michuano hiyo.
England iliyopoteza mechi zake mbili zaawali itakamilisha ratiba kwa kuvaana na Costa Rica katika mechi nyingine ya kundi D ambapo matokoe yoyote hayawezi kubadilisha chochote kwa timu hizo mbili.
Katika mechi nyingine zinazochezwa usiku wa leo, Ivopry Coast wenye pointi tatu nyuma ya Colombia itakuwa na kibarua kigumu kuvaana na Ugiriki, wakati vinara wa kundi C, Colombia watavimbiana vifua na Japan.
Mpaka sasa katika kundi hilo ni Colombi tu iliyojihakikishia nafasi huku Japan, Ugiriki na Ivory Coast zote zikiwa na nafasi sawa kama watafanya vema katika mechi hizo za kufungia ratiba.
Japan ikipata ushindi kwa Colombia na Ugiriki ikailaza Ivory Coast moja ya timu hizo itafuzu kwa uwiano wa mabao au walivyoumana wenyewe kwa kwenyewe kuungana na Colombia.
Hata hivyo Ivory Coast wanaoshika nafasi ya pili wanapewa nafasi kubwa kufuzu hatua ya pili iwapo italazimisha sare dhidi ya Ugiriki, vinginevyo isubiri miujiza kama inayosubiri Italia kwa Uruguay.
Ratiba ya mechi za LEO:
Costa Rica vs England (Saa 1 Usiku)
Italia vs Uruguay (Saa 1 Usiku)
Japan vs Colombia (Saa 5 Usiku)
Ugiriki vs Ivory Coast (Saa 5 Usiku)