MWANADADA anayetamba kwenye filamu nchini, Aisha Bui amekanusha taarifa kwamba amekamatwa na dawa za kulevya na kufungwa kifungo cha miaka mitano nchini Brazil.
Akizungumza na MICHARAZO kutoka Afrika Kusini, Aisha Bui alisema ameshtushwa na taarifa hizo za kunaswa na 'bwimbwi' Brazili, ilihali yeye yupo Afrika Kusini salama wa salimini.
Aisha alisema angependa kuwafahamisha watanzania kwamba yu salama na wazichukulie taarifa hizo kama uzushi kwa sababu hajawahi na wala hajishughulishi na biashara hiyo ya 'unga'.
Pia mwanadada huyo alitupia ujumbe katika 'wall' yake Facebook akisisitiza suala hilo kwa kuandika;
Dear Friends, Fans n Family Naskia kuna habari flani mbaya zimetolewa na baadhi ya vyombo vya habari, napenda kuwajulisha wote kua hiyo si kweli Mimi ndio kweli niko safari lkn niko salama salmin Hakuna kitu Kama Hicho n namuomba mungu aniepushe na mambo hayo. Niko poa Kabisa n nawapenda wote.