STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, October 27, 2014

TFF yamlilia Nahodha wa Bafana Bafana

http://www.citypress.co.za/wp-content/themes/canvas/functions/thumb.php?src=wp-content/uploads/2013/08/Meyiwa.jpg&w=630&h=0&zc=1&q=90SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeelezea masikitiko makubwa kufuatia kifo cha golikipa na nahodha wa timu ya Taifa ya Afrika Kusini (Bafana Bafana).
Senzo Meyiwa (27) ambaye alikuwa golikipa na nahodha wa timu ya Orlando Pirates alipigwa risasi na majambazi siku moja baada ya kuiongoza timu yake kwenye ushindi wa 4-1 dhidi ya Ajax Cape Town kwenye robo fainali ya kombe la Ligi.
Katika salamu zake kwa Chama cha Mpira cha Afrika Kusini (SAFA, TFF imesema kifo cha ghafla cha nahodha huyo wa Bafana Bafana ni pigo kubwa kwa familia yake, klabu yake ya Orlando Pirates, familia ya mpira na taifa zima la Afrika Kusini.
” Shirikisho la Mpira Tanzania na familia ya mpira kwa ujumla iko nanyi katika hiki cha maombolezo”. Ilisema sehemu ya salamu hizo iliyotiwa saini na Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Joas Selestine.
” Mwenyezi Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pa amani ya milele”. Amen.
Nakala ya salamu hizo imetumwa kwa Mwenyekiti wa Ligi Kuu ya Afrika Kusini (PSL) na Mwenyekiti wa klabu ya Orlando Pirates.

Simanzi! Nahodha, Kipa Bafana Bafana auwawa na majambazi

http://citizen.co.za/wp-content/uploads/sites/18/2013/10/TL_1081310-602x400.jpgNAHODHA na kipa tegemeo wa timu ya soka ya taifa ya Afrika Kusini, Bafana Bafana, Senzo Meyiwa ameuwawa na Majambazi.
Taarifa kutoka nchini Afrika Kusini zilizotolewa na klabu yake ya Orlando Pirates zinasema kuwa kipa huyo alipigwa risasi akiwa nyumbani kwake Vosloorus Maili 20 Kusini mwa jiji la Johannesburs usiku wa jana.
Ripoti ambazo hazijathibitishwa zinasema kuwa kipa huyo alikuwa na rafiki yake wa kike Kelly Khumalo msanii wa Pop aliyezaa naye mtoto mmoja hivi karibuni, licha ya kwamba kipa huyo alikuwa na ndoa yake. Inaelezwa kuwa watu watatu walivunja nyumba yake na wawili kuingia ndani na mmoja kusalia nje ambapoo waliwaamuru kuwapa simu za mkononi na kisha kupiga risasi ambazo zilimpaka kipa huyo kifuani
Inaelezwa kuwa kipa huyo aliyezaliwa SDeptemba 24, 1987 alifariki wakati akiwahishwa hospitalini.
Kupitia akaunti yao, klabu ya Orlando iliandika katika Twitter; ikielezwa kuhuzunishwa na kipa cha kipa na nahodha wao huyo huku Mwenyekiri wao, Irvin Khoza kuongeza kuwa ' Hii ni huzuni kubwa kumpoteza Senzo huzuni hii ni kwa familia yake hususani watoto wake kwa Orlarando Pirates na taifa klwa ujumla,"

Katumia Pauni 2000 awe kama Wacko Jacko

 michael jackson

SHABIKI maarufu wa Michael Jackson ambaye alikuwa ni Mfalme wa Musiki wa Pop ambaye kwa sasa ni marehemu, ametumia zaidi ya pauni za Uingereza 2000 (sawana shilingi za Tanzania 5,590,621) kuchubua ngozi yake ili kufanana na mwanamuziki huyo.
Shabiki huyo Mbrazil, Antonia Gleidson Rodrigues, 32 ambaye amejitangaza kuwa mtu pekee anayefanana na Michael Jackson kuliko wote nchini Brazil, amefanyiwa upasuaji ili kufanana na Michael huku akitumia zaidi ya saa 4 kila siku kujifunza kucheza filamu na muziki kama Michael Jackson.
“Gleidson Jackson”, kama ambavyo hupenda kuitwa, alifanyiwa upasuaji mara ya kwanza miaka mitano iliyopita, ambapo alirekebishwa pua ili aweze kuimba sauti ya juu.
Baada ya upasuaji wa kwanza, mkazi huyo wa Fortalenza, Brazil aliendelea na mkakati wake wa kufanana na mwanamuziki huyo wa pop kwa kudungwa tindikali ili kuufanya uso wake kuwa mweupe, pamoja na sindano zilizofanya maeneo yanayo zunguka macho kubadilika.
Gliedson ambaye alikuwa mwalimu wa maigizo, alifanyiwa upasuajia ili kuziba nafasi zilizopo meno yake, kurekebisha kope kwa kuzichora kama tattoo. Sasa hivi shabiki huyo anakusanya pesa kwa kumuigiza Michael Jackson ili aweze kulipia upasuaji mwingine zaidi.
Anasema: “Kama nitamudu gharama, nafikiria kufanyia kazi magego iliniondokane na mikunjo ya mdomoni – nataka pia kuchonga nyusi. Ningependa pia paji langu la uso lichorwe (tattoo) na kuchonga pua yangu iwe nyembamba zaidi.”
Gleidson alivutiwa kuwa kama Michael Jackson alipokuwa na miaka 19 baada ya mwanafunzi mwenzake kumwambia anafanana na mkongwe WackoJacko. 
“Ilikuwa ngumu, nilitaniwa kwa siku 15. Mwishowe nikanasa – nikaambukizwa.”
Gleidson anasema kwa sasa alivyo na anavyojitahidi kuwa ni zawadi tosha anayoweza kumpa supastar Michael ambaye kwa sasa ni marehemu. 
“Katika matamasha yangu huwa nasema hakuna kopi inayoweza kuwa nzuri kama origino, licha na hayo nitajitahidi kuwa na kufikia vilele vya ubora – kama Michael”

Kumekucha! Kisiga, Kiemba wasimamishwa, Matola mmh!

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhEwscqrUUC6o1pwPPIlUXJVdoA-xHBn6Qa2u4S3wVMNnyCLYUV5ASTDZtvSlPyyeGUDSAXTRUTE6vW-z_nbzWAqMQGqJjP26vfVhcqw-6gTUr5pTX_xWsNi9VixUX9epRCXlhoh9tIP3iD/s1600/KISIGA+NA+KIEMBA.jpg
Kisiga na Kiemba waliosimamishwa Simba
WACHEZAJI watatu wakiwamo wakongwe Shaaban Kisiga na Amri Kiemba wamesimamishwa na uongozi wa klabu ya Simba kwa kilichoelezwa kuwa ni utovu wa nidhamu na wamesharejeshwa jijini Dar wakati timu ikielekea Morogoro kwa pambano lao dhidi ya Mtibwa Sugar siku ya Jumamosi.
Simba ambayo imekuwa na matokeo yasiyoridhisha tangu msimu uliopita imeelezwa iliwatimua kambini jijini Mbeya wachezaji hao wawili pamoja na Haruna Chanongo bila kuelezwa utovu wa nidhamu waliofanya.
Hata hivyo habari za ndani ya klabu zinasema kuwa watatu hao wametimuliwa kwa tuhuma za kuhusika na kuihujumu timu ili ipate matokeo mabovu katika mechi zake za ligi kuu.
Simba imecheza mechi 11 za ligi tangu msimu uliopita na huu wa sasa bila kupata ushindi ikiwa imeambulia sare tano mfululizo na kuzua maswali mengi kwa mashabiki na wanachama wa klabu hiyo.
Kisiga aliyerejeshwa Simba msimu huu akitokea Mtibwa Sugar ndiye anayeongoza kwa kufunga mabao mengi kwa Simba akiwa na mabao mawili sawa na Emmanuel Okwi.
Aidha taarifa zaidi zinasema kuwa kocha msaidizi, Suleiman Matola na daktari wa timu wapo chini ya uchunguzi na benchi la ufundi kwa ujumla limepewa mechi tatu kuhakikisha wanashinda vinginevyo watatimuliwa.
Imekuwa ni desturi kwa viongozi wa soka nchini kila timu zao zikifanya vibaya badala ya kuangalia mambo ya msingi ikiwamo suala la ufundi hukimbilia kuwatuhumu wachezaji kuzifanyia hujuma bila ya kuwa na uthibitisho kitu kinachodaiwa ni kama kuwatoa KAFARA wachezaji KUFICHA UDHAIFU wao.

Lundenga, Mama Sitti wakanusha Miss Tanzaniua kutema taji

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEioBNuTs0jQ82txNCPeIkBGRMBQ-xV1dvkiqSv1AiKPf4eGOOEkrt3vXXTBS-YFv3jIR75OlXteBST5dAuYb2E_R1sHtxS_3xc39tJACB9MCqx-jN1q-vPv-rRvYhyGHBPpJHrw9ILQNTmv/s1600/misstz1.jpgMKURUGENZI wa Kampuni ya Lino International Agency, Hashim Lundenga, amekanusha uvumi uliosambaa kwenye mitandao ya kijamii mapema jana usiku, kuwa Sitti Abbas Mtemvu (pichani katikati) amelazimika kuvua taji la Urembo la Tanzania (Redd’s Miss Tanzania 2014).
Uvumi wa Sitti kuvua taji hilo umetokana na taarifa zilizotolewa kupitia akaunti ya Facebook mrembo huyo anayelalamikiwa kughushi vyeti vya kuzaliwa, akisema kutokana na vidole vya lawama anavyonyooshewa kiasi cha kukosa amani, amelazimika kuvua taji ili awe huru.
“Habari za jioni Watanzania wenzangu, kutokana na kuwa nimekuwa nikisemwa sana, maneno mengi yasio na tija juu ya hili taji la U-Miss anzania 2014,,mpaka kupelekea nisiwe na amani na uhuru ndani ya nchi yangu Tanzania, kwa roho safi nimeamua mwenyewe kujivua taji hilo na kuacha wanayeona anastahili taji hili apewe ili niendelee na maisha yangu kwa amani ,isiwe shida sana kwani sitegemei taji hili ili kuishi!!” imeandikwa katika ukurasa huo.
Akizungumzia uvumi huo, Lundenga alisema hakuna ukweli juu ya taarifa hiyo, na kwamba kama lingekuwa na ukweli ni wazi kwamba Sitti angeiarifu kampuni yake, inayoratibu kinyang’anyiro hicho kilichotimiza miaka 20 mwaka huu.
“Hakuna taarifa iliyotufikia hadi sasa kuhusiana na taarifa hizo. Sitti anajua anapaswa kufanya nini kama anaamua kulitema taji, ambapo anapaswa kutuarifu sisi kabla ya kuripoti hilo mahali popote. Kwa kuwa hajafanya hivyo, tunaamini hilo halipo na ndio tunamtambua kuwa mrembo wetu,” alisema Lundenga.
Kwa upande wa mama wa mrembo huyo, alisema ameshtushwa na taarifa za mwanaye kujiuzulu na kusema si za kweli, kwani kama angepanga kufanya hivyo asingefanya kwa kificho, badala yake angeitisha mkutao na wanahabari: “Hawezi kujiuzulu kienyeji hivyo na hata mimi mama yake sina taarifa hizo, hayo ni matumizi mabaya ya mitandao.”
credit: Mo dewji blog

Mfanyabiashara ajilipua risasi Arusha, kisa....!


MFANYABIASHARA wa Arusha anayemiliki kampuni ya Tanzania Bush Camp yenye kambi za watalii katika hifadhi za Serengeti mkoani Mara na Manyara iliyopo katika mikoa ya Arusha na Manyara, Timoth Mroki (36) amejiua kwa kujipiga risasi tatu kifuani akiwa katika baa maarufu ya Arusha Raha iliyopo la Shams, jijini hapa.
Kisa cha kujiua kwake kimetajwa ni kusababisha ajali, baada ya kuligonga gari jingine katika eneo la Mbauda wakati akitokea katika makazi yake yaliyopo eneo la Kwa Mrombo, jijini hapa.
Alifikwa na mauti katika tukio lililotokea kati ya saa 1:30 na saa 2:00 usiku, ndani ya baa maarufu ya Arusha Raha.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, Mroki alifika katika baa hiyo baada ya kufanikiwa kuwatishia kwa risasi waendesha bodaboda waliokuwa wamemzingira katika eneo la ajali na kisha kuondoka kwa kasi kwa gari lake aina ya Nissan Navara. 
“Alipiga risasi mbili hewani waliokuwa wamemzunguza wakanywea, akatumia mwanya huo kukimbia na moja kwa moja akafika Arusha Raha pengine kwa lengo la kujificha, na hapo akaanza kunywa…
“Ingawa inaonekana alikotoka alikunywa kidogo, alipofika Arusha Raha alikunywa haraka pombe mbili kali aina ya Valuer na wakati anamalizia ya tatu, akajikuta anazingirwa tena na wale waendesha bodaboda,” anasema mtoa habari huyo na kuongeza kuwa, baada ya kufyatua tena risasi mbili nyingine hewani, lakini bila ya dalili ya watu hao kutishika, ndipo akaamua kujimiminia risasi.
Habari zaidi zinasema wakati anazingirwa, naye akijihami kwa risasi wasamaria wema wakiwa harakati za kupiga simu polisi walishitukia polisi wakiingia katika eneo la tukio lakini tayari Mroki alikuwa ameshajitoa uhai baada ya kujimiminia risasi kifuani.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatusa Sabas hakupatikana kuzungumzia tukio hilo, ingawa ofisi ya Mkuu wa Upelelezi ya wilaya ya Arusha imekiri kuwepo kwa tukio, lakini chanzo chetu kikikataa kutajwa jina gazetini kwa kuwa si wasemaji wa matukio ya jeshi hilo mkoani Arusha.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru.
FK