Rashid Pembe akionyesha makeke yake kwa mashabiki ughaibuni |
Rashid Pembe (kulia) |
Mkurugenzi wa bendi hiyo, Rashid Pembe 'Professa', aliiambia MICHARAZO kuwa, nyimbo mbili za mwisho za albamu hiyo mpya zinatarajiwa kutenmgenezwa nchini Chile na kurekodiwa Ufaransa kabla ya kufanyiwa uzinduzi jijini Dar.
Pembe, nyopta wa zamani wa bendi ya Vijana Jazz, alizitaja nyimbo hizo nne zilizokamilika kuwa ni Tanzania Yetu na Kibule zilizotungwa na yeye (Pembe), Amani wa Balusi Kitembo na Nasoma Namba wa Noel Msuya.
"Nyimbo mbili za mwisho tutaenda kuzimalizia tukiwa kwenye ziara yetu nchini Chile na kuzirekodia Ufaransa, lakini pia tumepanga kurudia upya nyimbo za albamu yetu ya kwanza ambayo imechangia kutupatia mialiko Ulaya na Amerika," alisema.
Alisema wamelazimika kuzirudia upya nyimbo hizo kwa ushauri wa wadhamini wao barani Ulaya ili kuzifanya ziwe na kiwango za kimataifa na kuzidi kujizolea soko nje ya nchi.
Pembe, mkali wa kupuliza 'domo la bata' alizitaja nyimbo zitakazorudiwa Ulaya ambazo ziliitambulisha bendi hiyo iliyoanzishwa mwaka 2006 ni 'Matukio', 'Baba Kaleta Panya', 'Slow Puncture', 'The Girl from Tanzania', 'Amani Tanzania' na 'Angela'.