STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, July 11, 2013

Airtel yagawa futari kwa yatima wa mikoa mi4


Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando akiongea na waandishi wa  habari (hawapo pichani) kwenye hafla fupi ya makabidhiano  ya vyakula  vya kufuturisha watoto yatima atika vitu vilivyopo mikoa ya Dar es  salaam, Mbeya, Arusha, Mwanza katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani  iliyofanyika  katika ofisi za Airtel jijini Dar Es Salam ,akifuatiwa  na meneja wa huduma za Jamii wa Airtel bi Hawa Bayumi.
Meneja  Uhusiano wa Jamii wa Airtel bi Hawa Bayumi  akimkabidhi  mwakilishi wa Bakwata Ustadh Hassan Malangali vyakula vya kufuturisha  katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani  vilivyotolewa kwa vituo vitatu  vya watoto yatima Dar es Salaam (hawapo pichani)  vituo  vitakavyofaidika zaidi ni vya Dar es salaam, Mbeya, Mwanza, Arusha  hafla ya makabidhiano iliyofanyika  katika ofisi za Airtel  Morocco  jijini Dar Es Salam .
 
 Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Airtel, Hawa Bayumi  akimkabidhi tende Saida Makope ambaye ni mwakilishi wa vituo vitatu vya watoto yatima Dar es Salaam  katika  hafla ya makabidhiano  ya vyakula vya kufuturisha katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani  vilivyotolewa katika ofisi za Airtel, Dar es Salaam  jana. Anayeshuhudia ni mwakilishi wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), Ustaadh Hassan Malangali.
Na Mwandishi wetu.
KAMPUNI za simu za mkononi za Airtel Tanzania kupitia Kitengo chake cha huduma kwa Jamii wametoa msaada kwa vituo vitatu jijini Dar Es Salaam vya watoto yatima katika mwezi mtukufu wa Ramadhani vikifuatiwa na vituo vingine katika mikoa ya Arusha, Mwanza na Mbeya ili kusaidia watoto wanaolelewa kwenye vituo hivyo.
Msaada huo umetolewa kwa lengo la kuwalenga watoto kutoka mikoa minne ambayo ni Dar Es Salaam, Arusha, Mwanza na Mbeya kwa watoto hawa wanaohitaji upendo  hususani katika kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhani. Baadhi ya vitu vilivyotolewa ni Mchele,Sukari, maharagwe,unga, mafuta ya kupikia,maziwa, juice, majani ya chai na sabuni vyenye dhamani ya shilingi milioni tano na nusu.

Akizungumza katika hafla hiyo ya makabidhiano iliyoandaliwa katika makao makuu ya  Airtel jijini Dar Es Salaam, Meneja uhusiano wa huduma kwa Jamii bi Hawa Bayumi alisema "kwa kutambua umuhimu wa Jamii tunayofanya nayo biashara kampuni ya Airtel tumeamua turudishe kiasi cha faida tunayopata kwa wananchi ili iwasaidie.

Akifafanua alisema kwa muda wa miaka 11 iliyopita tumeweza kusaidia Jamii mbalimbali ya watanzania ndani ya mfungo wa Ramadhani na bila kuacha nyanja za elimu, michezo kwa watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu na kukosa huduma mbalimbali za kijamii.

Kwa mwaka huu kupitia Kitengo chake cha huduma kwa Jamii tutarudisha tulichokipata na tutaweza kufikia watoto zaidi ya 300 wa mikoa ya Dar Es Salaam, Arusha , Mwanza na Mbeya na mpaka sasa  kwa mwaka huu Airtel imegharamia zaidi ya shilingi millini 150 katika kukuza kiwango cha elimu kwa watoto wetu hapa Tanzania," alisema Bayumi.

Bayumi aliongeza kwa kusema kwamba Airtel inapenda kuwatakia kheri na Baraka katika mwezi huu mtukufu na tangu kuanza kwa Mwezi mtukufu wa Ramadhan, wateja wa Airtel wanaweza kufurahia huduma maalumu ya Ramadhani kwa kutuma neno RAMADHANI kwenda namba 15322 kwa shilingi 153 tu kwa siku. Katika huduma hii mteja atapokea dua, nukuu za
qurani, mawaidha na taraweh salat moja kwa moja kwenye simu yake, kila siku.

Naye katibu mkuu wa Bakwata Sheikh Suleiman Lolila  ambaye alikuwa mgeni rasmi alisema mbali ya hafla hiyo makabidhiano ya chakula imetoa fursa kwa waislam kutoka maeneo mbalimbali kukutana pamoja na kukumbushana juu ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Aidha Lolila licha ya kuishukuru Airtel Tanzania kwa misaada inayotoa kwa Jamii alisema jambo hilo linahitaji pongezi na kutaka liungwe mkono na kuigwa na kampuni zingine hapa nchini.

Aliyetumbukiza kichanga chooni afungwa miaka mi5 jela


Samahani kwa baadhi ya picha juu ya tukio la kichanga hicho.

 Rukia Haruna (31) pichani aliye kutwa na hatia ya kutupa mtoto chooni.
 Rukia Haruna (31)  akitolewa nje  na Askari wa Jeshi la Polisi akitolewa nje ya  Mahakama kwenda Gerezani kutumikia kifungo cha miaka 5 Jela


****************************
HIVI NDIVYO ILIVYO KUWA JUNI 14 .2013 ENEO LA MANGA A JIJINI MBEYA


*********************
Mwanamke mmoja mkazi wa Manga A Jijini Mbeya amehukumiwa kifungo cha miaka 5 jela kwa kosa la kutupa mtoto wake chooni.
 
Tukio hilo lilitokea Juni 14, Mwaka huu katika eneo hilo baada ya watoto waliokuwa wakicheza kugundua kuwepo kwa Mtoto katika choo cha shimo.
 
Mtuhumiwa baada ya kukamatwa amekiri kutenda kosa hilo na kwamba alifanya hivyo baada ya mzazi mwenzie kumkataa.
 
Ameongeza kuwa amelazimika kutupa katika choo cha jirani kwa sababu ni cha shimo tofauti na chao ambacho asingeweza kutupa mtoto huyo.
 
Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Archiles Mulisa mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Mbeya, Zabibu Mpangula, amemtaja Mtuhumiwa kuwa ni Rukia Haruna (31) mkazi wa Manga A Jijini Mbeya na kwamba kosa lake ni kinyume cha kifungu  218 kifungu kidogo cha 35 sura ya 16 ya mwaka 2002.
 
Na  Mbeya yetu

Moto wateketeza nyumba yote Mbeya...Inasikitisha

 Gari la zima moto likielekea eneo la tukio kwa kasi
 

 
Kikosi cha zima moto na uokoaji wakiwa katika juhudi za kuzima moto huo
Juhudi zikiendelea lakini  hakuna kilicho okolewa wala majeraha
 Nyumba ikizidi kuteketea
 Upande wa nyuma nao ukizidi kuteketea
 Jengo likiwa limeteketea kabisa
Baadhi ya majirani wakimpokea mama mwenye nyumba  baada ya kuitwa kutoka msibani
 Mashuhuda wakiangalia kwa uchungu mabaki ya jengo

 Moto ukiendelea baada ya gari la zima moto kuishiwa maji
 Moja kati ya Askari wa zima moto wakikata moja ya madirisha ili kuendelea na uzimaji wa moto huo
 Hakuna kilicho okolewa kama unavyo ona mabaki haya
 Mke mmiliki wa nyumba aliye tambuliwa kwa jina la Mama Mkisi akiwa anafarijiwa na majirani katika nyumba hiyo baada ya kupewa hifadhi

PICHA ZOTE NA MBEYA YETU


Man United, Bayern zitauana kwa Thiago

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjyIG-FdMrwZIyQB3Fut8UQBMbFu5KYdfl2xFg59M8G-jWGIEitujeF3vD47t9lZVxoqC1uoJY4iiMcXBLMECvKIOI06aULU3hiXJfYb5mciLHll2GItkfAJBhyfqkoihC-MO8hhPWcT7on/s400/img-pas-de-jo-pour-thiago-alcantara-1341498767_620_400_crop_articles-159070.jpg
Thiago Alcantarra anayezitoa udenda Bavarian na Mashetani wekundu
 WAKATI kukiwa na tetesi kwamba dili la usajili wa nyota wa timu ya taifa ya Hispania U21 kwenda Manchester United limekamilika Bayern Munich wameibuka na kutangaza dhamira ya kumnyakua mchezaji na kuibua upinzani mkali juu ya Thiago Alcxantarra watu atatua katika ya klabu hizo mbili.
Kocha wa Bayern Munich Pep Guardiola akizungumza na waandishi wa habari hii leo amesema kuwa anamfahamu vizuri Thiago na angependa kumsajili kwa kuwa ana uwezo wa kucheza nafasi zaidi ya nne au tano .
Guardiola amesema kuwa kwa sasa mchezaji ambaye angependa kumsajili ni Thiaggo na kama hataweza kushawishi kujiunga na Bayern basi hatasajili mchezaji mwingine . Kauli hii ya Guardiola inamaanisha kuwa timu hizo mbili za United na Bayern kwa sasa zitakuwa zikihaha kila moja ikijaribu kumshawishi nyota huyo kusaini kwenye  timu mojawapo.
United imekuwa ikitajwa kujiandaa kumtangaza mchezaji huyo kama mchezaji wa kwanza mwenye jina kubwa kusajiliwa na David  Moyes baada ya usajili wa beki wa Uruguay Guillermo Varella na kiungo huyo (Thiago) amekuwa akijaribu kuondoka Barcelona alikoshindwa kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza .
Thiago Alcantarra ana malengo ya kuingia kwenye kikosi cha kwanza cha timu ya taifa ya Hispania kwenye michuano ya kombe la dunia huko nchini Brazil mwakani na amekuwa akipambana kuondoka Barcelona ili aende mahali ambako atamshawishi kocha Vicente Del Bosque kumpa nafasi . Mkataba wa Alcantara unaonyesha kuwa asipocheza kwenye asilimia 60% ya mechi za timu hiyo anaweza kuuzwa kwa bei ya Euro Milioni 18 na kwa msimu uliopita hakucheza kwa kiwango hicho hali inayofanya kuondoka kwake kuwa rahisi .

Dereva wa daladala asusiwa maiti ya denti, kisa...!


 Mwenyekiti wa Mtaa wa Ihanga Kata ya Ilomba Emanuel Mwasibata akiwa amesimamia kikao cha usuruhishi
 Dereva wa daladala Aswile Mwalukoba aliyeshika fimbo baada ya kurejea nyumbani na kuhudhuria kikao cha usuruishi  ambapo alikili kuzaa  na mwanafunzi huyo na kukubali kuzika .
 Daladala iliyobeba mwili wa Marehemu kutoka Uyole.
 Wakazi wa Uyole wakiwa wameshikwa na butwaa baada yakumkosa mwenyeji wao
 Mwili wa mtoto ukiwa umefunkwa na kitenge na kutelekezwa kwenye kiti
 Kulia ni Carolina Kyando akiwa na dada yake baada ya kuleta mwili wa mtoto nyumbani kwa Mwalukoba eneo la Mama John jijini Mbeya
Majirani pande zote mbili wakingojea kujua hatma ya mazungumzo yanayo endelea baada ya Mwalukoba kurejea


******************
Ezekiel Kamanga
Vitendo vya ukatili dhidi ya  watoto na wanawake  jijini mbeya vimeendelea chukua sura mpya  baada ya dereva wa daladala jijini humo kumzalisha mwanafunzi Masomo ya jioni kituo cha Juhudi kilichopo  Ilomba.

.

 Tukio hilo limetokea hivi karibuni  eneo la mama John Mtaa wa Ihanga Kata ya Ilomba ambapo dereva wa daladala aliyefahamika kwa jina la Aswile Mwalukoba (45 ) kutelekezewa wa miezi saba ambaye alikwisha fariki baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Akizungumzia tukio hilo Mwenyekiti Mtaa huo Ndugu Emanuel Mwasibata amesema kuwa mgogoro huo umetokana  na dereva huyo kugoma kuuzika mwili huo kwakile alicho dai kuwa hivi sasa haishi na binti huyo kwa muda mrefu sasa.

Kwa upande wake binti huyo aliyefahamika kwa jina la Calorina Kyando amedai kuwa kitendo cha yeye kuuchukua mwili wa mtoto huyo hadi kwa baba yake unatokana   kutelekezwa na bwana huyo kisha kupigwa marakwa mara na kusababishiwa ulemavu wa sikio la kushoto baada ya kung’atwa na mwanaume huyo.

Mwanamke huyo amefafanua kuwa mara baada ya mtoto huyo kufariki wakati akipatiwa matibabu katika Hospital ya Igawilo jijini humo aliamua kumpigia simu mzazi mwenzie kwa lengo la kumpa taarifa za msiba huo.

Amesema mara baada ya kutoa taarifa hiyo mwanaume huyo alikubali na kumueleza mwanamke huyo kuwa yuko tayari kwa ajili ya mazikoya mtoto huyo ambapo anafanya taratibu za kuwasiliana na ndugu zake walioko Tukuyu Wilayani Rungwe.

Amesema katika siku iliyofuata mwanaume huyo hakupatikana kwa simu ya kiganjani na wala hakuwepo nyumbani kwake anapo ishi eneo la Mama John hali iliyo plelekea baadhi ya majirani na mwanamke huyo kutoka Uyole kusaidiana na kuutoa mwili huo Hospitalini hapo kwa lengo la kufanya taratibu nyingine .

Aidha majirani hao waliamua kuchukua mwili huo hadi nyumbani kwa Mwalukoba ambapo waliuweka kwenye kiti ndani ya nyumba yake huku wakiendelea kumsubiri mwalukoba arudi aliko  ambapo baadaye alirudi nyumbani hapo akisindikiazwa na Mdogo wake aliyefahamika kwa jina Gabriel Mwalukoba hadi nyumbani hapo.


Kitendo hicho cha kurejea kwa mwanaume huyo kilifanya mwenyekiti wa mtaa huo Ndugu Emanuel Mwasibata kuhoji juu ya  kutoweka kwa nyumbani kwakwe kwa muda wa siku mbili huku kukiwa hakuna mawasiliano yoyote.

 Baada ya kikao cha muda mrefu kati ya pande zote mbili mwanaume huyo alikubali kuupokea mwili huo na hivyo kuanza kufanya taratibu za mazishi ambapo mazishi hayo yalifanyika katika makaburi ya Iyela mida saa 12 jioni na kuhudhuriwa na familia zote mbili pamoja na majirani wengine kutoka Uyole na Mama John.
NA MBEYA YETU 

UGANDA CRANES YAWASILI KUIKABILI STARS

http://www.newvision.co.ug/newvision_cms/gall_content/2012/3/2012_3$largeimg229_Mar_2012_005111927.jpg
KIKOSI cha timu ya Taifa ya Uganda (The Cranes) imewasili Dar es Salaam leo tayari kwa mechi ya kwanza ya mchujo kusaka tiketi ya Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ligi ya Ndani (CHAN) kati yake na Tanzania (Taifa Stars) itakayochezwa Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

The Cranes inayofundishwa na Mserbia Sredojvic Micho imetua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 5.30 asubuhi kwa ndege ya Air Uganda, na imefikia hoteli ya Sapphire.

Timu hiyo leo (Julai 11 mwaka huu) itafanya mazoezi saa 9 alasiri kwenye Uwanja wa Karume, wakati kesho saa 9 alasiri itafanya mazoezi Uwanja wa Taifa, kabla ya kuipisha Taifa Stars itakayoanza mazoezi saa 10 kamili jioni.

Taifa Stars inayofundishwa na Mdenmark Kim Poulsen, na kudhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager, leo kwa mujibu wa program yake haitakuwa na mazoezi.

Wachezaji wanaounda The Cranes ni makipa Ismail Watenga, Kimera Ali na Muwonge Hamza. Mabeki ni Guma Dennis, Kasaaga Richard, Kawooya Fahad, Kisalita Ayub, Magombe Hakim, Malinga Richard, Mukisa Yusuf, Savio Kabugo na Wadada Nicholas.

Viungo ni Ali Feni, Birungi Michael, Frank Kalanda, Hassan Wasswa, Kyeyune Said, Majwega Brian, Mpande Joseph, Muganga Ronald, Ntege Ivan, Owen Kasule, wakati washambuliaji ni Edema Patrick, Herman Wasswa na Tonny Odur.


TENGA KUZUNGUMZA NA WAANDISHI KESHO

RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga atakuwa na mkutano na waandishi wa habari. Mkutano huo utafanyika kesho (Julai 12 mwaka huu) saa 4 asubuhi kwenye hoteli ya Tansoma.

Kutokana na mkutano huo, sasa mkutano kati ya makocha wa Taifa Stars na The Cranes uliokuwa ufanyike saa 5 asubuhi ofisi za TFF nao umehamishiwa hoteli ya Tansoma. Mkutano huo pia utahusisha manahodha wa timu zote mbili.

Mada Maugo, Benson Mwakyembe kuzipiga Russia

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj254DzVPfok2LZcApNivkvgoTadiEW4ZOogbXkRWC205DrJrbhCJxCGsMxzUdmq63Qe4jvtOGh4415LQlIltnnvbVLAZsCYoXNk78NUZKKnGT67XvAtaShsvYP8YPdyyNB7nZHr_NT6Ak/s400/Mwakyembe2.jpg
Benson Mwakyembe
 
Mada Maugo (kulia) akiwa na Rais wa TPBO-Limited Yasin Abdallah 'Ustaadh'
MABONDIA machachari wa Ngumi za Kulipwa nchini, Mada Maugo na Benson Mwakyembe wanatarajia kuondoka nchini wiki ijayo kwa ajili ya kwenda Russia kupambana na wenyeji wao katika michezo ya kimataifa itakayochezwa mwishoni mwa mwezi huu.
Kwa mujibu wa Rais wa TPBO-Limited, Yasin Abdallah 'Ustaadh' mabondia hao wataondoka Julai 23 ambapo Maugo ataenda kupigana na Movsur Yusupov wakati Mwakyembe yeye ataonyeshana kazi na Apti Ustarkhanov kwenye michezo itakayochezwa kwenye ukumbi wa Trade & Intertainment uliopo mji wa Kasiysk, nchini Russia.
Ustaadh alisema watanzania hao watapigana na Warusi hao katika michezo ya kilo 75 (Super Middle Weight) itakayokuwa na raundi nane kila mmoja.
Rais huyo wa TPBO alisema mpinzani wa Maugo rekodi yake inaonyesha kuwa amecheza mapambano matatu na yote ameshindwa moja likiwa kwa KO wakati mpinzani wa Mwakyemba amecheza mechi mbili na kushinda moja na mwingine kupigwa.
"Pamoja na rekodi ndogo za wapinzani wao, lakini ikumbukwe kuwa mabondia wa Russia na kwingineko Ulaya huwa hawachezi ngumi za kulipwa bila kucheza ngumi za ridhaa na kufikia hatua ya kushiriki michuano ya Olimpiki kwa maana hiyo Maugo na Mwakyembe wakitarajiwe wepesi Russia," alisema Ustaadh.
Ustaadh aliongeza kuwa tayari mabondia hao wa Tanzania wameshaombewa visa za kwenda nchini humo gharama zote zikilipwa na TPBO-Limited na wataondoka nchini wakiongoza na wakala wao kutoka Kenya, Thomas Mutua atakayeondokea Kenya na kukutana na mabondia hao Dubai.

Wajumbe mkutano Mkuu wa TFF kuanza kuwasili kesho Dar

Rais Leodger Tenga na Makamu wake, Athuman Nyamlani wakiteta na Musonye wa CECAFA
Na Boniface Wambura
WAJUMBE wa Mkutano Mkuu Maalumu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) utakaofanyika Jumamosi (Julai 13 mwaka huu) wanawasili jijini Dar es Salaam kesho (Julai 12 mwaka huu).

Mkutano huo wa marekebisho ya Katiba utakuwa chini ya uenyekiti wa Rais wa TFF, Leodegar Tenga na utafanyika ukumbi wa NSSF Waterfront kuanzia saa 3 kamili asubuhi. Wajumbe wote wa mkutano huo watafikia hoteli ya Travertine.

Pia mkutano huo utahudhuriwa na wageni mbalimbali waalikwa wakiwemo kutoka Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) na Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA).

Mechi ya Stand, Kimondo nayo kupiwa J'2


Na Boniface Wambura
MCHEZO wa  marudiano wa Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) kati ya Stand United FC ya Shinyanga na Kimondo SC ya Mbeya uliyokuwa uchezwe Jumamosi (Julai 13 mwaka huu) umesogezwa mbele kwa siku moja.

Timu hizo sasa zitacheza Jumapili (Julai 14 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga. Kimondo ilishinda bao 1-0 mechi ya kwanza iliyochezwa Julai 6 mwaka huu Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.

Mechi nyingine ya ligi hiyo itakuwa kati ya Friends Rangers ya Dar es Salaam na Polisi Jamii ya Mara, na itafanyika kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Mwamuzi wa mechi hiyo ni Hans Mabena kutoka Tanga.

JB amvulia kofia, King Majuto, Bi Hindu

Jacob Stephen 'JB'
http://www.timesfm.co.tz/content/accounts/38/uploads/cache/bi%20hindu_full.jpg
Bi Hindu

King  Majuto
MUIGIZAJI na mtayarishaji wa filamu nchini, Jacob Stephen 'JB' amemwagia sifa msanii mkongwe wa fani ya vichekesho, Amri Athuman 'King Majuto' na kudai ndiyo sababu inayomfanya arekodi naye filamu moja kila mwaka.
Alisema ucheshi wa King Majuto na umakini wake kazini, umekuwa ukimfanya mkongwe huyo kukosa mpinzani nchini na kuendelea kutamba licha ya umri kumtupa mkono.
"Sidhani kama kuna msanii wa kumzuia King Majuto, anajua kazi yake ndiyo maana nimejiwekea malengo kila mwaka niigize naye angalau filamu moja," alisema.
JB alisema King Majuto Majuto na Chuma Suleiman 'Bi Hindu' aliyewahi kung'ara na kundi la Kaole Sanaa ni miongoni mwa wasanii wanaomkosha ndiyo maana kila mara anaigiza nao na sasa amefanya nao kazi nayotarajiwa kutoka mwishoni mwa mwezi huu.
"Wote wawili pamoja na Suleiman Barafu, Shamsa Ford watakuwepo kwenye filamu hiyo ya 'Shikamoo Mzee' na nitaendelea kuwashirikisha hata kwa kazi zangu nyingine wanapendeza na kunogesha filamu," alisema JB anayefahamika pia kama 'Bonge la Bwana'.
Kabla ya filamu ya Shikamoo Mzee, JB alicheza na King Majuto katika kazi iitwayo 'Nakwenda kwa Mwanangu' na aliingiza na Bi Hindu kwenye 'Zawadi Yangu' ambayo kwa sasa inaendelea kukimbiza sokoni.

Arsenal yaongeza dau la Suarez, mwenyewe apagawa

http://www.thenational.ae/deployedfiles/Assets/Richmedia/File/on30-Real-Suarez.jpg
Luis Suarez
LONDON, England
ARSENAL wanaandaa ofa ya paundi za England milioni 35 (Sh. bilioni 82.5) ili kumsajili mshambuliaji nyota wa Liverpool, Luis Suarez, imeelezwa.
Arsenal watatuma ombi la kumtwaa Suarez kwa mara ya pili kwenda kwa Liverpool baada ya ombi lao la awali kukataliwa wiki iliyopita.
Kulikuwa na taarifa Jumatatu isemayo kuwa Arsenal ilituma ofa ya paundi za England milioni 30 (Sh. bilioni 70) kwa Liverpool ili kumtwaa Suarez, na vyanzo vimekaririwa na Goal.com vikieleza kwamba sasa, klabu hiyo ya jiji la London iko tayari kulipa hadi paundi milioni 35 ili kunasa saini ya mshambuliaji huyo wa kutegemewa pia katika timu ya taifa ya Uruguay.
Inafahamika kuwa kocha Arsene Wenger ameamua kuelekeza nguvu zake katika kujaribu kumnasa Suarez baada ya Arsenal kushindwa kulipa dau la kumtwaa mshambuliaji Gonzalo Higuain wa klabu ya Real Madrid ya Hispania.
Suarez anachukuliwa na Wenger kuwa ni mbadala sahihi wa Higuain, ambaye alikaribia kujiunga na Arsenal mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya klabu hiyo kuboresha ofa yake hadi kufikia paundi milioni 23.1 (Sh. bilioni 54).
Hata hivyo, Real Madrid wanasisitiza kuwa hawawezi kumuachia Muargentina Higuain kwa dau la chini ya paundi za England milioni 25.5 (Sh. bilioni 60), na, ingawa Arsenal bado wanamfukuzia Higuain huku kukiwa na uwezekano mkubwa wa kufaulu vita hiyo, Wenger ameamua kuangalia uwezekano wa kupata mshambuliaji mwingine.
Huku wakiwa na kiasi kikubwa cha fedha kilichotengwa kwa ajili ya usajili ghali zaidi katika historia ya klabu ya Arsenal, Mfaransa Wenger amewashtua wengi kwa uamuzi wake wa kumfukuzia Suarez wiki iliyopita.
Ombi la Arsenal lilikutana na tahadhari kutoka kwa Liverpool, ambao wanapambana kumbakiza Suarez aliyekaririwa mara kadhaa akisisitiza kutaka kuondoka katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi, zaidi akikusudia kuhamia Real Madrid.
Arsenal sasa wataongeza nguvu ya kutaka kumtwaa Suarez baada ya wawakilishi wa mchezaji huyo kueleza kwamba yuko tayari kuhamia kwao ili kutimiza dhamira yake ya kucheza katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya msimu ujao.
Katika mahojiano yake na kituo cha redio cha Sport 890 juzi, Suarez alidai kwamba "klabu mbili au tatu hivi" zinataka kumsajili na kwamba amevutiwa sana na taarifa za kutakiwa na Arsenal.
Alicheka kuambiwa kuwa Chelsea wanamtaka, lakini akakiri kwamba amejiandaa kukatisha likizo yake nchini Uruguay ikiwa uhamisho wake utakuwa tayari.
"Je, kuna ombi lolote lililokamilika? Hapana, hadi sasa hakuna lolote. Kuna klabu mbili au tatu ambazo nadhani zinanitaka na klabu yangu inalijua hilo.
"Napaswa kuwapo Liverpool Julai 21 kwa ajili ya ziara yao ya Australia lakini hakuna anayejua kile kitakachotokea. Nimeshasema kile ninachopaswa kusema, na kwanza nitapaswa kuwa pale (Liverpool)  Julai 21 lakini labda mwito wa simu siku moja unaweza kubadili mipango yote hii."
Inafahamika vilevile kwamba kuna kipengele katika mkataba wa Suarez kinachomruhusu kuomba kuzungumza na klabu nyingine ikiwa kutatokea ofa ya kumnunua kwa paundi za England milioni 40 (Sh. bilioni 94) . Hata hivyo, inaaminika kwamba Liverpool wanataka kulipwa paundi milioni 50 (Sh. bilioni 118)ndipo wamruhusu kuondoka.