STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, May 22, 2016

HIVI NDIVYO LIGI KUU BARA 2015-2016 ILIVYOISHA RASMI

Mabingwa Yanga

Simba washindi wa tatu
Majimaji iliyoigomea Yanga mjini Songea
PAZIA la Ligi Kuu Bara limefungwa rasmi jioni hii ikishuhudia timu tatu za jijini la Tanga, Coastal Union, African Sports na Mgambo JKT zikishuka rasmi kwa kushika nafasi tatu za chini, huku Simba ikishindwa kuvunja mwiko wa kukamata nafasi ya pili tangu ilipotwaa ubingwa wake wa mwisho wa Ligi Kuu msimu wa 2011-2012 ikizidiwa ujanja na Azam.
Sports maarufu kama Wana Kimanumanu walilala mabao 2-0 mbele ya Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Manungu Complex, Turiani Morogoro, wakati Wagosi wa Kaya Coastal ikilala tena mabao 2-0 Mkwakwani Tanga mbele ya Prisons-Mbeya licha ya kwamba ilishashuka mapema katika ligi hiyo.
Mgambo JKT ilishindwa kukomaa kujiokoa kama misimu mitatu iliyopita ilivyopambana baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na Azam na kujikuta pointi zake kutotosha kuiokoa isirudi Ligi Daraja la Kwanza baada ya kucheza mfululizo tangu ilipopanda mwanzoni mwa miaka ya 2010.
Simba ikiwa Uwanja wa Taifa ilishindwa kuhimili vishindo vya JKT Ruvu na kulala mabao 2-1 ikiiacha Azam ikitwaa zawadi ya mshindi wa pili nyuma ya Yanga ikiwa msimu wa tano mfululizo kwa Wanalambalamba kutotoka kwenye Mbili Bora ya ligi hiyo tangu mwaka 2011-2012.
Mjini Songea Majimaji ikiwa Uwanja wake wa Majimaji, ililazimishwa sare ya mabao 2-2 na Mabingwa Yanga, huku ikishuhudiwa Ally Mustafa Barthez akifunga bao lake la kwanza katika Ligi Kuu, huku Paul Nonga akiifungia Yanga bao lake la kwanza katika Ligi Kuu tangu aliposajiliwa katika dirisha dogo mwishoni mwa mwaka jana.
Toto Africans imenusurika kushuka daraja licha ya kufungwa bao 1-0 na Stand United Uwanja wa CCM Kirumba, kama ambavyo Kagera Sugar ilivyoponea kwa Wana Shinyanga wengine Mwadui FC waliowazabua mabao 2-0.
Mbeya City ikiwa nyumbani ilishindwa kulipa kisasi cha kufungwa mabao 4-1 na Ndanda katika mchezo wao wa kwanza mjini Mtwara kwa kutoka suluhu kwenye Uwanja wa wa Sokoine, Mbeya.
Kwa namna msimamo ulivyo, Yanga iliyotwaa ubingwa mbali na kunyakua Kombe na Medali, pia imevuta mkwanja upatao Sh. 81,345,723/= kama washindi wa kwanza, wakati Azam  ikizoa Sh. 40,672,861/= za ushindi wa pili.
Simba yenyewe imevuta donge la Sh. 29,052,044/= kwa kushika nafasi ya tatu wakati Prisons iliyokuwa ya nne ikiipiku Mtibwa Sugar imeweka kibindoni Sh. 23,241,635/=
Kadhalika kumalizika kwa ligi hiyo kumempa nafasi Amissi Tambwe wa Yanga kuibuka kinara wa mabao msimu huu akifunga jumla ya 21 na kujihakikishia zawadi ya Sh. 5,742,940/= mbele ya Hamis Kiiza wa Simba aliyekuwa akiongoza kwa muda mrefu kabla ya kupoteza makali yake.

Matokeo kamili na msimamo wa mwisho wa Ligi hiyo ni kama ifuatavyo;



Msimamo wa Ligi Kuu Bara:

                            P  W   D   L   F    A  Pts

1. Yanga               30 22  7   1  70  20  73

2. Azam                30 18 10  2  47  24 64

3. Simba               30 19  5   6  45  17 62

4. Prisons              30 13 12  5  29  22 51

5. Mtibwa              30 14  8   8  33  21 50

6. Mwadui FC         30 11  8  11 29  29 41

7. Stand Utd          30 12  4  14 28  29 40

8. Mbeya City        30  9   8  13 32  34 35

9. Ndanda             30  7  14  9  28  31 35

10.Majimaji           30  9   8  13 22  40 35

11.JKT Ruvu          30  8   8  14 31  43 32

12.Toto Africans     30  7   9  14 26  40 30

13.Kagera Sugar    30  8   7  15 23  34 31

14.Mgambo           30  6  10 14 24  36 28

15.African Sports   30  7   5  18 13  34 26

16.Coastal Union    30  5  7   18 15  41 22
 
Wafungaji: 
 
21-Amissi Tambwe               (Yanga)
19-Hamis Kiiza                      (Simba)
17-Donald Ngoma                (Yanga)
16-Jeremiah Juma               (Prisons)
15-Elias Maguli                      (Stand)
12- Kipre Tchetche                 (Azam)
10-John Bocco                       (Azam)
     Atupele Green              (Ndanda)
9-  Ibrahim Ajib                     (Simba)
     Shiva Kichuya               (Mtibwa) 
     Simon Msuva                  (Yanga)
 8- Shomary Kapombe          (Azam)
     Fully Maganga            (Mgambo)
 
7- Mbaraka Yusuf              (Kagera) 
    Mussa Kiumbu           (JKT Ruvu)
    Waziri Junior                     (Toto)
       Saady Kipanga          (JKT Ruvu) 
6- Danny Mrwanda         (Majimaji) 
  
  AbdulRahman Mussa (JKT Ruvu)
5-Said Bahanuzi               (Mtibwa)
    Samuel Kamuntu       (JKT Ruvu)
    Miraji Athuman                  (Toto)
    Jerry Tegete                 (Mwadui)
    Thabani Kamusoko         (Yanga)
    Mohammed Mkopi      (Prisons)
    Raphael Alpha                (Mbeya)
    Didier Kavumbagu           (Azam)
   Paul Nonga                       (Yanga)

4- Aziz Gillah                   (Mgambo)
    Juma Abdul                      (Yanga)  
    Edward Christopher         (Toto)
3- Michael Aidan            (JKT Ruvu)
    Haruna Moshi                (Mbeya)
    Pastory Athanas              (Stand)
    Adam Miraj                    (Coastal)
    Kiggy Makassy             (Ndanda)
    Omar Mponda             (Ndanda)
    Peter Mapunda           (Majimaji)
   Danny Lyanga                 ( Simba)
   Babu Ally                        (Kagera)
   Mzamiru Yasin               (Mtibwa)
   Bryson Raphael            (Ndanda)
   Joseph Mahundi            (Mbeya)
   Deus Kaseke                  (Yanga)
   Mudathir Yahya              (Azam)
   Kelvin Sabato              (Mwadui)
   Alex Kondo                   (Ndanda) 
2-Malimi Busungu              (Yanga)
   Ally Myovela                 (Prisons)
   Mohamed Ibrahim       (Mtibwa)
   Ally Shomary                (Mtibwa)
   Fabian Gwanse             (Mwadui)
   Jabir Aziz                      (Mwadui)
   Nassor Kapama             (Coastal)
   Thabit Khamis            (JKT Ruvu)
   Frank Domayo                  (Azam)
   Abslim  Chidiebele       (Coastal)   
   Hamad Mbumba            (Sports)
   Ditram Nchimbi     (Mbeya City)
   Kassim Selembe               (Stand)
   Nizar Khalfan                (Mwadui)
   Juma Mahadhi              (Coastal)
   Paul Ngway                    (Kagera)
   Farid Mussa                      (Azam) 
   Japhet Mkala                     (Toto)
   Chande Magoya         (Mgambo)
   Ally Ramadhani               (Sports)
   Salum Kabunda             (Mwadui)
   Kelvin Yondani                 (Yanga)  
   Salim Mbonde              (Mtibwa)
   Abdallah Juma              (Mbeya)
   Stamili Mbonde          (Majimaji)
   Omar Issa                        (Sports)
   Jumanne Alfadhil          (Prisons)
   Hassan Materema         (Sports)
   Frank William                (Prisons)
   Bolly Ajali Shaibu        (Mgambo) 
   Jaffar Ramadhani             (Toto)

Tanga ndio basi tena Ligi Kuu msimu ujao

Mgambo JKT

Africans Sports

Coastal Union
KLABU za Mgambo JKT na Africans Sports zimeungana na Coastal Union kushuka daraja msimu huu ikiwa ni rekodi kwa mkoa mmoja kupoteza timu tatu kwa mpigo katika msimu mmoja.
Sports imelala mabao 2-0 mbele ya Mtibwa Sugar, wakati Mgambo imeambulia sare ya bao 1-1 ambayo imeshindwa kuwabeba mbele ya Azam, na Coastal iliyoshuka mapema ikikubali tena kipigo cha bao 1-0 mbele ya Prisons uwanja wa Mkwakwani Tanga.
Matokeo ya mwisho ya mechi za kufungia msimu tutawaletea hivi punde, lakini ni kwamba Simba imelala mabao 2-1 mbele ya JKT Ruvu na kushindwa kunyakua nafasi ya pili iliyoenda kwa Azam kwa msimu wa tano mfululizo sasa.

Mgambo yachomoa, Mtibwa yazidi kuzamisha jahazi la Sports

Mgambo JKT inapambana kuepukam kushuka daraja
MGAMBO imesawazisha bao dhidi ya Azam kwa mkwaju wa penalti, wakati Mtibwa ikiongeza bao la pili kuashiria inaizamisha rasmi Sports kuwafuata ndugu zao wa Coastal Union ambao mpaka sasa wapo nyuma kwa bao 1-0 dhidi wa Wajelajela wa Prisons Mbeya kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Mgosi afunga bao la kwanza la VPL, Stand ng'aring'ari

JIJINI Mwanza, Toto imetanguliwa bao 1-0 na Stand, huku Taifa Hassan Mussa Mgosi anafunga bao lake la kwanza katika Ligi Kuu msimu huu kwa kuipatia Simba bao la kufutia machozi Game ipo dakika ya 74.

Simba bado, Azam yapata bao, Kagera safii

Azam inayoongoza dhidi ya Mgambo
Uwanja wa Taifa hali bado ngumu kwa Simba ikiwa bado ipo nyuma kwa mabao 2-0, lakini Azam imeweza kupata bao la kuongoza katika kipindi hiki cha pili kupitia Ramadhani Singano wakianza kuielekeza Mgambo JKT mahali pa kutokea kuungana na Wagosi wenzao wa Kaya kushuka daraja, kwani Kagera Sugar wametakata kwa sasa wakiongoza mabao 2-0 dhidi ya Mwadui FC mjini Shinyanga, kwingine kumekabaki kama kulivyo. Usiwe mbali na MICHARAZO upate matokeo.

Van Gaal aaga Man Utd kumpisha Mourinho

http://i2.manchestereveningnews.co.uk/incoming/article10144211.ece/ALTERNATES/s615/JS73121391.jpg
Picha haihusiani na taarifa hii. KOcha Louis Van Gaal
KOCHA Mkuu wa Man United, Louis Van Gaal aliyeisaidia klabu hiy9o kunyakua ubingwa wa Kombe la FA usiku wa jana kwa kuilaza Crystal Palace katika pambano la fainali lililochezwa dakika 120, ameaga rasmi Old Trafford kuashiria anampisha Jose Mourinho kuja kuinoa timu hiyo.
LVG ametoa kauli hiyo mchana huu akizungumza katika mkutano wake na wanahabari hotelini kwa kusema kuwa imetosha, ikiwa ni kama kuweka wazi kuwa anaondoka OT.
Kocha huyo amekuwa na wakati mgumu katika klabu hiyo, mashabiki wakitaka asepe zake kwa kushindwa kuirejesha klabu yao katika heshima kama ilivyokuwa chini ya Sir Alex Ferguson aliyestaafu miaka michache iliyopita.
Jose Mourinho amekuwa akitajwa kumrithi Mholanzi huyo, huku taarifa za jana zilikuwa zikidai kuwa, huenda LVG akawa Mkurugenzi wa Ufundi wa Man United, lakini kwa kaul;i aliyotoa mchana huu ni wazi, ndio basi tena.

Simba tayari ishagongwa 2-0 na maafande

MPAKA muda huu wakati mechi za mwisho za Ligi Kuu Bara zikiendelea kuchezwa, Simba tayari imeshafungwa mabao 2-0 na JKT Ruvu katika pambano lao linalochezwa Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam. Mabao ya maafande wanapigana kuepuka kushuka daraja yamefungwa na Abdulrahaman Mussa na Saady Kipanga likiwa bao lake la saba msimu huu.
Yanga iliyopo Songea, kuumana na Majimaji wapo nguvu sawa na wenyeji wao wa kufungana bao 1-1, wakati Mtibwa ikiwa Manungu, Turiani inaongoza bao 1-0.
Viwanja vingine bado ni vigumu wakati mechi zikiwa mapumzikoni kwa sasa. MICHARAZO itakufahamisha kila linaloendelea katika mechi hizo za mwisho wa msimu wa 2015-2016.

Wazee Yanga wamng'ang'ania Manji Jangwani

Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji
HAKUNA namna. Baraza la Wazee wa Yanga wameibuka na kuweka wazi kuwa, wanamuunga mkono Mwenyekiti wao aliyemaliza muda wake, Yusuf Manji, kuelekea kenye Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Juni 25 mwaka huu.
Manjia amekaa madarakani kwa miaka miwili nje ya utaratibu wa Katiba ya klabu hiyo ya Jangwani.
Akizungumza na Wanahabari leo Jumapili jijini Dar es Salaam, akiweka bayana msimamo wa Wazee wa Yanga akiwa kwa pamoja na Mwenyeviti wa matawi wa mkoa wa Dar es salaam,  Katibu wa Baraza hilo Ibrahim Akilimali, alisema kuwa, wanamuunga mkono Manji kwa asilimia zote kwani ameweza kuisaidia timu hiyo toka akiwa mdhamini mpaka kufikia kuwa Mwenyekiti wa klabu hiyo.
"Kwa upande wa Baraza la Wazee tunamuunga mkono Manji kwani toka Yanga imekuwa chini yake kumekuwa na mafanikio makubwa sana ikiwemo kuweza kuingia hatua ya makundi Kombe la Shirikisho na kama kuna masuala mengine ikiwemo ya uwanja uongozi mpya utakapoingia tutakaa nao kuweza kujua tunafikia wapi malengo yetu ya kujenga kwani tumeshafikia kwenye hatua bado kibali tu," alisema Akilimali.
Akilimali alisema, watu wasitake kuangalia suala la Uwanja kwa Manji tu, bali wakumbuke kuwa kuna viongozi wengine wamepita na hawajajenga cha msingi ni kuangalia wapi tunaelekea na nini kinachotakiwa kufanyika kwa maendeleo ya klabu yao.

Wazee hao walisema kwa pamoja kuwa mbali na hilo pia wanawapongeza wachezaji na benchi la ufundi kwa hatua nzuri waliyofikia ya kuchukua ubingwa kwa mara ya 26 pamoja na kuingia kwenye hatua ya makundi ya Kombe la Shirishiko ikiwa ni moja mafanikio wanayojivunia chini ya Manji.

Juma Abdul noma, ambwaga Ngoma tuzo ya VPL

http://bingwa.co.tz/wp-content/uploads/2016/04/JUMA-ABDUL1.jpg
Juma Abdul
http://izubarirashe.rw/wp-content/uploads/2016/03/1457819591Juma-Abdul-Iranzi.jpg
Juma Abdul (12) akiwajibika kimataifa
HATA Donald Ngoma amemshinda. Kweli Juma Abdul mkali. Kwa soka ambalo beki wa kulia wa Yanga, Juma Abdul alilopiga katika mechi za hivi karibuni, ilikuwa lazima anyakue tuzo. 
Beki huyo anayeichezea pia Taifa Stars ameteuliwa kuwa Mchezaji Bora wa Ligi Kuu Bara kwa mwezi Aprili akimbwaga straika wake,Ngoma na kiungo wa JKT Ruvu, Hassan Dilunga.

Katika rekodi za Bodi ya Ligi Tanzania Bara (TPLB) iliyoketi Jumamosi iliyopita, imeonesha kwamba Abdul alicheza mechi zote tano za Ligi Kuu kwa mwezi Aprili ambapo pia aliifungia timu yake bao katika harakati za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu msimu wa 2015/16.


Rekodi hizo pia zinaonyesha kwamba beki huyo hakuonyeshwa kadi hata moja katika michezo hiyo mitano sambamba na kutoa mchango mkubwa katika michezo aliyoshiriki kwa mwezi Aprili, 2016. 
Beki huyo atazawadiwa fedha Sh. Milioni 1= na wadhamini wa Ligi hiyo, Kampuni ya mtandao wa simu za mkononi ya Vodacom.

Uwezo aliouonyesha Abdul ulisababisha Kocha wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa ‘Master’ kumjumuisha katika kikosi chake kwa ajili ya mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Harambee Stars ya Kenya kadhalika Mafarao wa Misri katika mechi ya kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika utakaofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Juni 4, mwaka huu.

Wachezaji bora wa miezi minne iliyopita ni kiungo Thabani Kamusoko wa Young Africans (Desemba 2015), beki Shomari Kapombe wa Azam (Januari 2016), Mshambuliaji Mohammed Mkopi wa Prisons (Februari 2016) na Shiza Kichuya wa Mtibwa Sugar (Machi 2016).

YANGA KWELI YA KIMATAIFA, RAIS FIFA AIPA TANO

http://www.dw.com/image/0,,19078335_303,00.jpg
Mmetwaa mara mbili? Hongereni sana. Rais wa FIFA, Gianni Infantino ameipongeza Yanga kwa kuwa mabingwa wa Tanzania.
SIKIA hii. Msemaji wa Yanga, Jerry Muro amekuwa akiwatania Simba kuwa wa Mchangani, huku akiipaisha timu yake kuwa ya Kimataifa, lakini leo Jumapili imethibitika ni kweli Yanga ni ya Kimataifa baada ya Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Gianni Infantino kuipongeza.
Infantino ameipongeza Yanga kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara 2015/16.
Yanga imetwaa ubingwa huo kwa msimu wa pili mfululizo, lakini ikiwa ni mara ya 26 tangu kuanza kwa Ligi Kuu Bara mwaka 1965.

Katika salamu zake, kupitia barua yake ya Mei 18, 2016 kwa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Emil Malinzi, Infantino ameelezea ubingwa wa Yanga kwamba umetokana na kazi kubwa iliyofanywa na uongozi wa timu hiyo, makocha, wachezaji pamoja na mashabiki.

“Yanga ndiyo mabingwa wa Tanzania. Napenda kuchukua nafasi hii kuipongeza Young Africans na timu nzima isiyoshindika kwa mafanikio haya makubwa. Taji la Yanga ni matokeo ya mshikamano ulioko ndani ya Young Africans,” amesema Infantino katika barua hiyo yenye kichwa cha habari kinachosema: Salamu za Pongezi kwa Yanga.

Amesema pongezi zake ziende kwa uongozi wa klabu, makocha na benchi nzima la ufundi, wachezaji, madaktari pamoja na mashabiki wote wa Yanga.
“Kwa niaba ya familia ya soka, napenda kuchukua nafasi hii kuishukuru Yanga na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa jinsi mnavyopeleka ujumbe chanya wa soka kwa jamii ya michezo,” alisema Infantino katika barua hiyo iliyotua TFF Mei 21, mwaka huu.

Tayari Rais wa TFF, Jamal Malinzi alikwisha kuipongeza Yanga ambayo imepewa Kombe na medali kwa wachezaji 24, viongozi saba wa benchi la ufundi na viongozi wanne wa Kamati ya Utendaji na kwa sasa wanasubiri zawadi ya fedha Sh 81,345,723.
Klabu hiyo iliyotinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho leo ilikuwa Uwanja wa Majimaji Songea kukamilisha msimu wa 2015-2016 dhidi ya Majimaji.