|
Henry Joseph |
|
Redondo |
BENCHI la Ufundi la Klabu ya Simba limewarejesha kikosini viungo wake nyota, Ramadhani Chombo 'Redondo' na Henry Joseph kwa ajili ya mechi yao ya kumalizia duru la kwanza dhidi ya Ashanti United.
Wachezaji hao waliokuwa wameshushwa katika kikosi cha pili cha timu hiyo, wamejumuishwa na wenzao na kuingia kambini Bamba Beach, Kigamboni nje kidogo ya jijini la Dar kwa ajili ya pambano hilo la Jumatano.
Kwa mujibu wa Afisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga, wachezaji hao wamewaridhisha benchi lao la ufundi ndiyo maana wamewarejesha kikosi cha kwanza na huenda wakashuka dimbani keshokutwa dhidi ya Ashanti.
Kamwaga alisema kikosi chao kinajiandaa vyema kwa lengo la kupata ushindi kwa Ashanti ili kumaliza duru la kwanza wakiwa katika nafasi nzuri baada ya kutetereka hivi karibuni na kushika nafasi ya nne.
Pia aliongeza kuwa wachezaji Zahoro Pazi na Nassor Masoud 'Chollo' wameshindwa kuingia kambini kwa ajili ya pambano hilo la Ashanti kutokana na matatizo mbalimbali.
Alisema Pazi ameshindwa kuungana na wenzake kwa kusumbuliwa na homa ya Malaria wakati Chollo ni majeruhi.
Katika hatua nyingine uongozi wa Simba umekanusha taarifa ya mpango wa kufanya mabadiliko ya benchi lao la ufundi kwa kutaka kuwaondoa makocha wao wa sasa, Abdallah Kibadeni na Jamhuri Kihwelu 'Julio'.
Kamwaga alisema taarifa zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari leo ni uzushi na zenye lengo la kutaka kuwachanganya wanasimba kwa sababu Kamati yao ya uetndajni haijakutana siku za karibuni kujadili lolote.
Kibadeni na Julio wamekuwa wakielezwa wapo kwenye kitimoto ndani ya Simba kutokana na matokeo mabaya yaliyoipata timu yao na kuporomoka toka nafasi yua kwanza hadi ya nne, japo nna tayari wachezaji hao naki ukweli Simba haipo pabaya kiasi cha kuanza kupandwa na presha.