STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, August 13, 2013

Rais Kikwete akutana na vijana wachoraji walioacha kutumia dawa kulevya


 Kijana Jimmy Changchuu alieachana na matumizi ya dawa za kulevya akimkabidhi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete picha aliyochora yeye na kijana mwenzake wakati vijana hao walimpomtembelea Rais Ikulu jijini Dar es Salaam leo.Vijana hao wanalelewa katika kituo cha Pilli Missanah Foundation kilichopo Kigamboni Jijini Dar es Salaam.
 Vijana walioachana na Matumizi ya dawa za kulevya kutoka katika kituo cha Pilli Missanah Foundation kilichopo Kigamboni jijini Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo.Kulia pembeni ya Rais ni Mwanzilish Kituo hicho Bi.Pilli Missanah na watatu kushoto ni mfadhili mkuu wa kituo hicho Bwana Zacharia Hans Poppe. Picha na Freddy Maro
Picha ya pamoja.

Kumekucha Redd's Miss Ilala 2013, kivumbi kufanyika Ijumaa hii

 Warembo wanaotarajia kushiriki Redd's Miss Ilala, wakiwa wamepozi wakati wa mazoezi kwenye Mgahawa wa Billicanas, Dar es Salaam, tayari kwa mashindano yatakayofanyika Ijumaa kwenye Ukumbi wa Golden Jubilee jijini.
 Warembo wanaotarajia kushiriki Redd's Miss Ilala, wakiwa wamepozi wakati wa mazoezi kwenye Mgahawa wa Billicanas, Dar es Salaam, tayari kwa mashindano yatakayofanyika Ijumaa kwenye Ukumbi wa Golden Jubilee jijini
 Warembo wakiwa katika moja ya miondoko wakati wamazoezi
 Mwalimu wa warembo hao, Akhsas Peter akiwapanga vizuri kabla ya kupigwa picha na wandishi wa habari.
 Warembo wakipita Mtaa wa Makunganya katikati ya Jiji la Dar es Salaam, wakitokea mazoezini katika Mgahawa wa Billicanas.
 Mwandishi Mwandamizi wa Habari za Michezo wa gazeti la Jambo Leo, Asha Kigundula (kulia), akitoa maelezo kuhusu kazi za kila siku za waandishi wa habari kwa warembo wa wanaotarajia kushiriki mashindano ya Redd,s Miss Ilala walipotembelea chumba cha habari cha Jambo Leo
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Jambo Concepts Tanzania Limited (JCTL), Juma Pinto (aliyekaa kulia), akizungumza na warembo hao waliomtembelea ofisini kwake, Dar es Salaam. Aliyekaa katikati ni Mratibu wa mashindano hayo, Juma Mabakila. JCPL ni wachapishaji wa magazeti ya Jambo Leo, Staa Spoti, Dar Metro na jarida la Jambo Brand Tanzania.

Mchakato wa Uchaguzi Mkuu TFF kuweka hadharani kesho


MCHAKATO wa uchaguzi wa kamati mpya ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) unatarajiwa kutangazwa kesho (Agosti 13 mwaka huu).
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Hamidu Mbwezeleni atakutana na Waaandishi wa Habari kwenye ofisi za TFF saa 6 kamili mchana ambapo mbali ya mchakato utakavyokuwa anatarajia kutangaza tarehe mpya ya uchaguzi huo ambao awali ulitarajiwa kufanyika Septemba 29 mwaka huu.
Kamati ya Uchaguzi ya TFF ilikutana Jumapili (Agosti 11 mwaka huu) na inatarajia kuwa na kikao kingine leo (Agosti 12 mwaka huu) ambapo pamoja na mambo mengine itazungumzia maandalizi ya uchaguzi huo.
Mbali ya Mbwezeleni, wajumbe wengine wa Kamati hiyo ni Moses Karuwa (Makamu Mwenyekiti), Mohamed Sinani, Chabanga Dyamwale na Kitwana Manara.
MAGORI, LINA WAINGIA KAMATI ZA CAF
Watanzania Crescentius Magori na Lina Kessy wameteuliwa kuwa wajumbe kwenye kamati ndogondogo (standing committees) mpya za Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) zilizotangazwa juzi na Katibu Mkuu wa shirikisho hilo Hicham El Amrani.
Magori na Lina ambao ni wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF watakuwa kwenye kamati hizo kwa kipindi cha miaka miwili (2013-2015). Magori ameteuliwa kuwa mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Mashindano ya Mpira wa Miguu wa Ufukweni (Beach Soccer) wakati Lina ameingia kwenye Kamati ya Maandalizi ya Mpira wa Miguu kwa Wanawake.
Makamu wa Rais wa TFF, Athuman Nyamlani ameteuliwa tena kuwemo kwenye Bodi ya Rufani ya CAF yenye wajumbe 12 kwa kipindi kingine cha miaka miwili. Nyamlani alikuwepo kwenye bodi iliyopita, na itaendelea kuwa chini ya uenyekiti wa Prosper Abega kutoka Cameroon.
Rais wa TFF, Leodegar Tenga ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya CAF yuko kwenye kamati tano za Shirikisho hilo. Kamati hizo ni Kamati ya Fedha ambayo ni Makamu Mwenyekiti na Kamati ya Maandalizi ya Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN).
Kamati nyingine ni Kamati ya Masoko na Televisheni ambayo ni Mwenyekiti, Kamati ya Ufundi na Maendeleo, na Kamati ya Ushauri na Vyama Wanachama wa CAF.
KAMATI YA SHERIA KUPITIA USAJILI
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji chini ya Mwenyekiti wake Alex Mgongolwa inakutana leo jioni (Agosti 13 mwaka huu) na kesho (Agosti 14 mwaka huu) kupitia na kufanyia uamuzi usajili wa wachezaji wenye matatizo.
Hatua ya kwanza ya usajili imeshamalizika wakati hatua ya pili ya usajili inaanza kesho (Agosti 14 mwaka huu) ikihusisha wachezaji ambao watakuwa hawajasajiliwa katika Ligi Kuu ya Vodacom msimu huu na wale kutoka nje ya Tanzania.
Hivyo, dirisha la uhamisho kwa wachezaji wa kimataifa litafungwa baada ya hatua ya pili ya usajili kumalizika Agosti 29 mwaka huu.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

CHADEMA yalaani tukio la kupigwa risasi kwa Sheikh Ponda


 
CHAMA cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA) kimeungana na vyama na asasi nyingine kulaani vikali tukio la kupigwa kwa risasi na Polisi kwa Katibu wa Jumuiya ya Kiislam Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda.
CHADEMA imelaani tukio hilo katika tamko lake iliyolitoa leo kupitia Mjumbe wake wa Kamati Kuu, Prof  Abdallah Safari.

Kagera Sugar yamaliza ziara Uganda kwa kipigo


BAADA ya jana kuinyuka Bunawaya ya Uganda katika mechi zake za kirafiki za kimataifa za kujiandaa na Ligi Kuu Tanzania Bar, timu ya Kagera Sugar jioni ya leo imemaliza mechi zake nchini humo kwa kucharazwa bao 1-0 na Watoza Ushuru wa URA.
Kagera itakayofungua dimba la ligi kuu Agosti 24 dhidi ya Mbeya City, jana iliitafuna Bunawaya kwa bao 1-0 ikiwa ni mechi yao ya pili baada ya ile ya awali kulazimishwa 0-0, leo ilishindwa kuendeleza ubabe kwa URA ambao waliifunga Simba na kutoka sare ya 2-2 na Yanga kabla ya kulala kwa Coastal Union ilipokuwa nchini Tanzania mwezi uliopita.
Hata hivyo kocha msaidizi wa Kagera, Mrage Kabange amesema wanashukuru mechi hizo zimewasaidia kujiweka vyema na kuwaandaa vizuri wachezaji wao kabla ya kuanza kipute cha ligi msimu mpya.
Msimu uliopita Kagara Sugar ikiwa chini ya kocha King Abdallah Kibadeni, ilimaliza ligi ikiwa nafasi ya nne, ikitanguliwa na vigogo, Yanga, Azam na Simba zilizokuwa kwenye Tatu Bora.

Ashanti wawafuata mabingwa wa Kagame Bunjumbura


KIKOSI cha timu ya Ashanti inaatarajiwa kuondoka mjini Kigoma kesho kuelekea Burundi kwa ajili ya mechi mbili za kirafiki za kimataifa dhidi ya wenyeji wao, ili kujiandaa na pambano lao la fungua dimba kati yao na Yanga.
Ashanti iliyorejea Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu baada ya awali kushuka mwaka 2007 itapepetana na Yanga Agosti 24 katika moja ya mechi za fungua dimba, mchezo utakaochezwa katika uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Timu huyo ilikimbilia Kigoma kuweka kambi na kesho itaavuka mpaka kuelekea katika mji wa Makamba kuumana na timu ya Daraja la Kwanza nchini Burundi iitwayo Makamba.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Kigoma ni kwamba mechi hiyo itachezwa keshokutwa mjini humo kabla ya Ashanti United kusogea mbele hadi Bunjmbura mwishoni mwa wiki na kuvaana na Mabingwa wa Kombe la Kagame 2013, Vital'O.
Kocha wa timu hiyo Mbaraka Hassain anaamini mechi hizo zitawasaidia kuwaweka vyema kabla ya kuwavaa Yanga ambao Jumamosi itajitupa uwanja wa Taifa kupapatana na Azam katika pambano la Ngao ya Hisani litakalochezwa uwanja wa Taifa.
Azama waliokuwa Afrika Kusini kwa ajili ya kambi yao ya mazoezi na kucheza mechi nne za kirafiki na kushinda moja na kupoteza tatu, imetua leo mchana na tayari imejichimbia katika kambi yao iliyopo Chamazi, nje ya jijini tayari kuwasubiri Yanga Jumamosi.

Haya ndiyo majina ya wanaodaiwa wauza Unga na Bangi nchini



Majina ya watanzania 255 wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya   yamejulikana  na  JAMHURI  imeamua kuyachapisha...
 
Uchunguzi uliofanywa umebaini kuwa kwenye orodha hiyo wapo watu maarufu na baadhi wamekuwa wakitoa misaada ,huku wengine wakijifanya ni wazee  wa kanisa na kushiriki  shughuli mbalimbali za kijamii....
 
Uchunguzi wetu usio na chembe ya shaka  unaonesha kuwa orodha hii ya watu watakaoandikwa hapo chini kwa sasa wapo chini ya uangalizi wa mahakama na polisi..
 
"Ni kweli kuna watu tumewapeleka mahakamani, huko wamewekwa chini ya uangalizi na wanatakiwa kuripoti  kwa  muda wanaopangiwa.Tunafanya hivyo baada ya uchunguzi wetu kubaini kwa ni kweli  wanahusika na biashara hii haramu."Alisema  Nzowa
Nzowa aligoma kuyataja majina hayo, lakini uchunguzi uliofanywa na JAMHURI  kutoka ndani ya jeshi la polisi na  mahakama  umefanikiwa  kuyapata  majina  hayo...
Katika orodha hii, yumo mchungaji aliwekwa chini ya uangalizi , na baada ya kumaliza muda huo, siku tatu baadaye alikamatwa na  dawa nchini Brazil.Pia yumo Sheikh anayetoa misaada mbalimbali,lakini baada ya kukamatwa na dawa kilo 211, eneo la Kunduchi Dar es salaam, kwa sasa  amekimbilia  Afrika kusini....
DAWA ZINAVYOINGIZWA NCHINI:
Hadi sasa kiwango kikubwa cha dawa za kulevya kinaingizwa nchini kwa njia ya meli katika bahari ya Hindi.
Baada ya meli kuwasili Tanzania, wasafirishaji hutumia boti ndogo ziendazo kasi kuchukua dawa hizo.Maeneo yanayotumiwa zaidi kuingiza dawa ni Bagamoyo, Zanzibar, Tanga na Mtwara....
Jijini Dar, boti hizo hutia nanga  katika eneo la  Bagamoyo ambako pia ndiko kwenye njia kuu ya uingizaji  wa bidhaa za magendo  zisizolipiwa kodi...
Biashara  hiyo  haramu  huwahusisha  baadhi  ya  polisi  ambao  mara  kadhaa  wamekuwa  wakiwapa  ulinzi   wahalifu  hao.
Viwanja  vya  ndege   vinavyotumiwa  kuingiza  madawa  ya  kulevya  ni  Julius  Nyerere ( DAR )  na  Abeid  Amani  Karume ( ZANZIBAR)
Taarifa  toka  kitengo  cha  kuzuia  dawa  za  kulevya   zinasema  kuwa  wasafirisha  wanaotumia  ndege  wamekuwa  wakibuni  mbinu  mbali  mbali  zikiwemo  za  kutumia  manukato  kwa  ajili  ya  kuwapumbaza mbwa  wenye  mafunzo  ya  kubaini  madawa  ya  kulevya....
Habari zaidi  zinasema  kuwa  kitengo  kimepata  vifaa  maalumu    vya  kubaini  kama  ndani  ya  mizigo  kuna  madawa  ya  kulevya. Vifaa  hivyo  ni  mfano  wa  sindano  ambayo  huchomwa  kwenye  mizigo  na  kuipitisha  kwenye  ngozi  ya  mwili.
Kama  kuna  dawa, ikigusishwa  kwenye  ngozi  unga  hupukutika  na  kama  mzigo  hauna  dawa  za  kulevya  basi  hakuna  kitakachotokea....
Tayari  vifaa  hivyo  vimeanza  kutumika  katika  uwanja  wa  kimataifa wa  Julius  Nyerere.
Lisake gazeti la Jamhuri utaiona orodha nzima ya majina hayo 250.
 
Source: Gazeti la Jamhuri.