Adebayor |
Paulinho |
Inaelezwa kuwa Spurs imemnasa Paulinho kwa kitita cha pauni Milioni 17 na kwa sasa inaelekeza nguvu zake zaidi kwa Roberto Soldado wa klabu ya Valencia ya Hispania, ili kumnasa huku ikiwa mbioni kumuuza strika toka Togo, Adebayor kwa timu ya Uturuki Besiktas.
Kocha wa Spurs Andre Villas Boas anamhitaji Soldado ili kusaidia na wakali wengine wa timu yake kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu ya England mwezi ujao.
Inadaiwa kuwa Besiktas ipo tayari kutoa pauni Milioni 5 kumnyakua Adebayor mwenye miaka 29 ambaye alitua katika timu hiyo miaka miwili iliyopita na kulipwa mshahara wa pauni 80,000 kwa wiki kitu ambacho uongozi wa klabu hiyo unaona ni bora atimue zake kutokana na sheria mpya ya kodi nchini England.
Juu ya Soldado, Spurs imenukuliwa kuwa tayari kutoa kitita cha pauni milioni 15 wakati klabu hiyo ya Hispania imesisitiza kuwa bila pauni milioni 25 ambazo ni thamani ya mkali huyo inaweza kumkosa.
Rais wa Valencia, Amadeo Salvo Lillo alinukuloiwa akisema klabu yao inahitaji fedha kutatua matatizo kibao waliyonayo, lakini hawapo tayari kuwatoa wachezaji wao kwa bei chee.
Soldado, 28, amefunga jumla ya mabao 30 katika mechi 46 alizocheza kwa msimu uliopita na Spurs imejipanga kuhakikisha inamnyakua ili kuimarisha kikosi chao.