MICHAEL RICHARD WAMBURA
P.O. BOX 22557,
TEL. 0713/0754/O787 326 485
DAR ES SALAAM.
September 15, 2012
Mr A. Ndolanga
MWENYEKITI,
KAMATI YA Uchaguzi ya DRFA
CHAMA CHA MPIRA WA MIGUU- DSM(DRFA)
YAH: PINGAMIZI JUU YA KAMATI YA UCHAGUZI , WAPIGA KURA, NA WAGOMBEA KATIKA UCHAGUZI WA CHAMA CHA MPIRA WA MIGUU CHA DAR-ES-SALAAM(DRFA) ULIOPANGWA KUFANYIKA OCT ,2012
Nimelazimika kuleta maombi ya pingamizi langu mbele yako na kamati yako kuhusiana na uchaguzi tajwa hapo juu wa
DRFA kutokana na uvunjifu wa kanuni, maagizo na Katiba ya TFF sambamba
na katiba ya DRFA na sheria za nchi katika mchakato mzima wa kuelekea
katika uchaguzi huo , malalamiko yangu ambayo sehemu kubwa ni ya
kisheria na kikatiba malalamiko yangu ni kama ifuatavyo.
- Uundwaji
wa kamati ya chaguzi ya DRFA umevunja kanuni ya uchaguzi wa wanachama
wa TFF (TFF MEMEBERS STANDARD ELECTROL CODE) Ibara ya 3(2) inakataza mtu
mmoja kuwa mjumbe wa kamati mbili za uchaguzi za wanachama wa TFF au wanachama washiriki wa TFF “The members of the Committee shall
under no circumstances be member of the executive body of TFF or
Executive body of the Association or Executive of other TFF member
Association or the Elections Committee of the other member association of TFF or Executive body /Elections Committee of a subordinate” kwa
kuwa Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya DRFA Muidin Ndolanga Pia
Mwenyekiti wa kamati ya Uchaguzi ya FRAT(taifa ambao wote ni wanachama
wa TFF basi uhalali wake wa kuwa m/kiti wa kamati ya Uchaguzi wa DRFA
unakuwa haupo kwa kuwa unavunja kanuni za uchaguzi , kwa maana hiyo naomba tamko la kuwa mchakato mzima wa uchaguzi ufutwe na kuanza upya kwa kuwa haukufuata taratibu na kanuni husika .
- Katiba ya DRFA toleo la 2008 ibara ya 1(6) inatamka kuwa “DRFA itaheshimu Katiba, Kanuni Maagizo na Maamuzi ya TFF na kuhakikisha kuwa zinaheshimiwa na wanachama wake” TFF
kupitia barua yake kumbukumbu TFF/ADM/EC/36 ya tarehe 22/7/2011 yenye
kichwa cha habari “ Katiba za Wanachama na Wanachama wao” kwenda kwa makatibu ambapo iliagiza kufanyika mabadiliko katiba zao ili ziendane kikamilifu na katiba ya mfano ya TFF aidha TFF kupitia barua yake ya tarehe 12/12/2012 yenye kumbukumbu TFF/TECH?GC11/115 kwenda kwa makatibu wa wilaya ikikumbushia kurekebisha katiba zao ili ziendane na Katiba ya mfano ya TFF, Kwa kuwa Katiba za wanachama wa DRFA na DRFA hazijafanyiwa marekebisho na wahusika ni wazi hawajatekeleza maagizo ya TFF hivyo kwenda
kinyume na Katiba ya TFF 12(d)(e) & (n) na Ibara ya 9 ya kanuni za
uchaguzi za TFF na Wanachama wake. Na hata kama marekebisho yamefanyika
ni wazi hayatakuwa yamezingatia matakwa ya kisheria na maamuzi ya TFF
kwani katiba hiyo haijapitishwa na kamati ya sheria, Katiba na hadhi za
wachezaji kama maagizo ya awali ya TFF yalivyo agiza.
- KUKIUKWA KWA KATIBA YA DRFA
Marekebisho ya Katiba yanayodaiwa kufanywa hayakuzingatia katiba ya DRFA “kazi
mojawapo ya Mkutano mkuu wa DRFA ni kufanya na kupitisha marekebisho ya
katiba” kwa kuwa marekebisho hayajapitishwa na mkutano mkuu wa DRFA”
kama katiba inavyo elekeza basi marekebisho hayo ni batili kwa mujibu wa
katiba ya DRFA
- Kwa kuwa wilaya wanachama wa DRFA hawakufuata kanani za Uchaguzi za TFF na Wanachama wake, kumepelekea baadhi ya viongozi waliochaguliwa kutokuwa na sifa ikiwemo ya Elimu isiyopungua kidato cha Nne ikiambatana na Cheti cha Matokeo kama ilivyoagizwa na TFF katika barua yake kwa wanachama wake na
wilaya, kwa kuwa viongozi hao wa wilaya wanakosa sifa ya kuwa viongozi
ni wazi pia wanakosa sifa ya kupiga kura katika Uchaguzi wa DRFA,
itakumbukwa katika Uchaguzi wa Chama cha mpira Mkoa Mara(FAM) ambapo
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF (Nd Lyato) alikuwepo ambapo Nd
MAGOTI ambaye alikuwa Katibu wa Chama cha mpira Wilaya ya Bunda aliondolewa katika kugombea na
hakurusiwa kupiga kura baada ya kuonekana hakuwa na sifa ya kuwa Katibu
wa wilaya kutokana na tatizo la Elimu halikadhalika Katibu wa Wilaya ya
Serengeti Ombeni Magati nae aliondolewa katika kugombea ujumbe wa
kamati ya Utendaji na pia hakuruhusiwa kupiga kura na nafasi
walizokuwa wanazishikilia kutangazwa kuwa ziko wazi, hivyo ni matumaini
yangu hata katika DRFA na wanachama wake mkondo utafuata huo huo.
- kiongozi
anaemaliza muda wake atakuwa na haki ya kutetea nafasi yake ili mradi
awe na sifa kwa mujibu wa Katiba na kanuni za DRFA na TFF , itakumbukwa
kwenye uchaguzi wa Klabu ya Simba Mwenyekiti aliyekuwa anamaliza muda
wake Mzee Hasan Dalali aliondolewa kugombea kwa sababu ya kukosa sifa ya
Elimu ya kidato cha nne huku
Mwenykiti wa sasa wa DRFA ndugu Amin (AKA Bakhresa) na Nd Damas Ndumbaru
wakiwa wajumbe wa Kamati ya Uchaguzi ya Simba iliyotekeleza na
kuzingatia Kanuni za uchaguzi za TFF, aidha Nd A. Bulembo nae
aliondolewa kwa vigezo hivyo hivyo katika uchaguzi wa timu Villa Squad
ya DSM, kanuni haikuishia hapo iliendelea mpaka kwa timu ya Coastal
Union ya Tanga, kwa misingi hiyo ni wazi kamati hii haitafumbia macho kwenye hili la DRFA.
Aidha ninapenda
kuikumbusha kamati yako kuwa Kamati ta uchaguzi ya TFF hivi karibuni
ilisitisha chaguzi za mikoa ya Kilimanjaro na Manyara kutokana na dosari
za Vyeti vya elimu kwa wagombea kwa kuzingatia kanuni za uchaguzi za
wanachama wa TFF
6.0 PINGAMIZI KWA MGOMBEA AMIN MOHAMED SALIM (AKA BAKHRESA
6.1 Mgombea mtajwa hapo juu ni mmoja wa wagombea ambae jina lake limetajwa kupitishwa kugombea nafasi ya mwenyekiti katika uchaguzi wa DRFA, Katiba ya DRFA ibara ya 29(3) inamtaka mgombea kuwa
na sifa zilizo ainishwa kwenye ibara ya 30(2) ya Elimu ya kidato cha
Nne, aidha ibara ya 9 ya kanuni za Uchaguzi wa wanachama wa TFF inatamka
ibara ya 9(2) amboyo ina tamka wazi kuwa mgombea yoyote lazima awe na Elimu ya kidato cha nne inayo ambatana na cheti cha matokeo any person contesting any position “ Must have minimum academic qualification of form Four and holder of a certificate of ordinary Secondary Education” .
Kwa kuzingatia maelezo na sifa za kanuni za uchaguzi wa wanachama wa
TFF, Katiba na maagizo mbalimbali ya TFF na katiba ya DRFA Mgombea mtajwa Nd AMIN MOHAMED SALIM (BAKHRESA) anakosa
sifa ya kuwa mgombea Mwenyekiti wa DRFA kwa kuwa hana Elimu ya Kidato
cha Nne kinachoambatana na cheti cha matokeo hivyo jina lake liondolewe
katika orodha ya wagombea waliopitishwa kugombea uongozi wa DRFA.
6.2 Nd AMIN MOHAMED SALIM (BAKHRESA) hana sifa ya
kugombea kwa mujibu wa ibara ya 9 ya kanuni za uchaguzi wa wanachama wa TFF “The person contesting any position in the association must have integrity and the capacity of performing fulfilling and implementing Association obligations and objectives” kwa sababu zifuatazo:
1. 20/01/1993
aligombea uongozi kwa nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji ya FAT.
Alijaza form ya maombi ya Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na kutoa
maelezo ya uongo ya kuwa ana elimu ya kidato cha nne na kutoa kiapo huku
akijua maelezo yake ni ya uongo ANNEXED “A” Aidha pamoja na form hiyo
Nd AMIN MOHAMED SALIM (BAKHRESA aliasilisha cheti cha kugushi kuwa
amemaliza kidato cha Nne katika shule ya sekondari Tambaza (school
living Certificate)mwaka 1974 huku akijua kuwa Hasemi ukweli ANNEXED “B”
6.3 Nd AMIN MOHAMED SALIM (BAKHRESA) huku akijua hasemi ukweli mwaka 1994/Dec/17 Katika form yake ya kuomba uongozi FAT alieleza ya kuwa Amehitimu Darasa la Nane(STDVIII) mwaka 1965 na mwaka huo huo akawa mchezaji wa Cosmopolitan akipingana na barua aliyoiwasilisha mwaka 2000 kutoka Wizara ya elimu ya Serekali ya mapinduzi Zanzibar ANNEXED “C” inayosema kuwa Amemaliza miaka 8 ya mafunzo katika shule ya Msingi Darajani 1965 uhalali wa barua hiyo unatia shaka hivyo inahitaji kuhakikiwa uhalisia wake.
6.4 Mwaka 2005 Ndugu AMIN MOHAMED SALIM (BAKHRESA) alifunguliwa jarada la mashtaka ya kugushi maandishi na Nd OPIYO jalada CD/RB/6236/05 na CD/IR/2707/05 la kosa la kugushi vyeti jambo ambalo mlalamikaji yuko tayari kuwaslisha ushahidi mbele ya kamati yako
7.0 PINGAMIZI DHIDI YA WAPIGA KURA WAFUATAO
1. ABEID MZIBA –KINONDONI
2. SALEH NDONGA-TEMEKE
3. PETER MUHINZI- TEMEKE
4. DAUDI KANUTI- ILALA
5. GUNGULUGWA TAMBAZA-ILALA
6. Na wengine
Majina niliyo
yataja hapo juu ni wajumbe na wanawakilishi wilaya zao katika mkutano
mkuu wa DRFA, kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi za wanachama wa TFF ,
maagizo mbalimbali ya TFF, katiba za mfano zilizotolewa na TFF pamoja
Katiba ya DRFA nilio wataja hapo juu wanakosa sifa za kuwakilisha wilaya katika mkutano mkuu wa DRFA kwa kukosa Elimu ya Kidato cha Nne kinachoambatana na cheti cha matokeo.
Naomba kamati
yako itamke kuwa viongozi hao walichaguliwa kimakosa bila kuzingatia
kanuni za uchaguzi za TFF hivyo nafasi zao zitangazwe ziko wazi ili
wapatikane watu wenye sifa za kikanuni kugombea, pia wasiruhusiwe
kushiriki kupiga kura katika Uchaguzi wa DRFA, aidha ninapenda ufahamu
jambo kama hili lilifanyika katika Uchaguzi wa Mkoa wa Mara(FAM) ambapo
Kamati ya Uchaguzi ya TFF taifa ilishiriki na ilitoa mwongozo na
kusimamia utekelezaji wake.
Kwa kuzingatia Maelezo hayo hapo, Ninawasilisha pingamizi langu lenye sehemu tatu(3) pamoja na nakala za maagizo mbali mbali ya TFF kwa wanachama wake:
8.0 Kwa kuzingatia Maelozo hayo hapo, Ninawasilisha katika maombi ya dharura kama ifuatavyo:
(a) Tamko kuwa Kamati ya Uchaguzi ya DRFA imeundwa bila kufuata kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF, hivyo ivunjwe na kuundwa upya.
(b) Tamko kuwa Mchakato mzima wa uchaguzi uanze upya mara baada ya Kamati mpya kuundwa.
(c) Tamko katiba ya DRFA ina kinzana na katiba Kanuni na Maelekezo ya TFF hivyo ifanyiwe marekebisho. yanayostahili kabla ya kuitisha uchaguzi mwingine.
(d) Tamko
la kufanyika kwa Uhakiki wa sifa za viongozi wa wanachama na wanachama
washiriki wa DRFA ili kuridhia matakwa ya kanuni za uchaguzi na katiba
za Mfano za wiliya zilizotolewa na TFF.
(e) Tamko kuwa kuiruka kamati ya sheria na Katiba ya TFF katika kuipitisha katiba ya DRFA ni ukiukwaji wa maagizo ya TFF
(f) Jina la Mgombea Nd AMIN MOHAMED SALIM (BAKHRESA) liondolewa kwenye orodha ya wagombea
(g) Wapiga kura wote wasio na sifa ambao wamegombea waondolewe kwenye orodha ya wagombea.
(h) Jambo au uwamuzi mwegine wowote ambao kamati itaona unafaa kwa maendeleo DRFA na taifa kwa Ujumla
………………………………….
MICHAEL RICHARD WAMBURA
MLALAMIKAJI/MPINGAJI
15th Sept, 2012
CC:Nd L.C Tenga Rais shirikisho la Mpira wa Miguu(TFF)
CC: Nd D. Lyatto M/kiti Kamati ya Uchaguzi ya –TFF
CC: A Mgongolwa - Mwenyekiti-kamati ya Sheria, Katiba na Hadhi
za wachezaji