STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, May 10, 2015

Rasmi Kagame Cup kupigwa Dar kuanzia Julai 11-Agosti 02

http://www.bongo5.com/wp-content/uploads/2012/07/kagame-cup-2012.jpeg 
HATIMAYE imefahamika kuwa, michuano ya Kombe la Kagame kusaka Bingwa wa Afrika Mashariki na Kati kwa ngazi za klabu itapigwa Tanzania.
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limekubali kuwa wenyeji wa michuano ya Kombe la Kagame baada ya kutafakari kwa kina.
Baraza la Vyama vya Soka kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) waliiteua Tanzania kuandaa michuano hiyo, lakini uongozi wa TFF, ulisema ungekutana kujadili kabla ya kutoa tamko.
Hata hivyo kwa mujibu wa taarifa ya shirikisho hilo ilitolewa jana kwa vyombo vya habari TFF imethibitisha kuwa wamekubali kuandaa michuano hiyo na kutangaza kwamba itaanza kutimua vumbi lake kuanzia Julai 11 na kufikia tamati Agosti 2, mwaka huu.
TFF imeweka bayana kwamba Cecafa ndiyo itakayotangaza timu shiriki pamoja na ratiba nzima ya michuano hiyo ambayo mara ya mwisho kufanyika Tanzania ilikuwa mwaka 2012 ambapo Yanga ilitwaa taji kwa mara ya pili mfululizo kwa kuilaza Azam katika fainali iliyopigwa Uwanja wa Taifa. Mwaka mmoja nyuma yaani 2011 Yanga ilitwaa tena taji michuano ilipochezwa jijini Dar es Salaam kwa kuilaza Simba bao 1-0.
Bingwa mtetezi wa michuano hiyo kwa sasa ni wababe wa Azam, El Merreikh ya Sudan ambao walitwaa taji katika fainali zilizochezwa mwaka jana mjiji Kigali, Rwanda baada ya kuilaza APR bao 1-0.

Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika haya hapa

http://45minites.com/wp-content/uploads/2015/02/ES-Setif.png
Watetezi wamewekwa kundi B

http://www.nationalswitchng.com/wp-content/uploads/2015/01/caf-CHAMPIONS-LEAGUE_1.jpg
Kundi A: Smouha (Misri), Moghreb Tetouan (Morocco), TP Mazembe Englebert (DR Kongo) na Al Hilal (Sudan).

Kundi B: Entente Setif (Algeria, mabingwa watetezi), USM Alger (Algeria), Al Merreikh (Sudan), MC Eulma (Algeria)

Mwanariadha Afa kwa Sumu India, wengine taaban

http://i.ndtvimg.com/i/2015-05/kerala-suicide_650x400_61431019961.jpgNEW DELHI, India
POLISI wa nchini India wanachunguza kifo cha mwanariadha wa kike mwenye umri wa miaka 15 na wengine watatu wakinusurika kifo baada ya kula kile kinachodaiwa matunda yaliyowekwa sumu, alisema waziri.

Ilielezwa kuwa wanariadha 10 walikula `othalanga’ matunda pori, ambayo yaliwekwa katika vifungashio vyenye sumu katika kituo hicho cha michezo huko Alappuzha kusini ya jimbo la Kerala kinachoendeshwa na Mamlaka ya Michezo India (SAI).

Wanariadha hao walikutwa wakiwa wamepoteza fahamu katika hosteli yaol Jumatano jioni na walikimbishwa hospitalini ambako mmoja wao alifariki dunia huku wengine watatu wakiwa katika hali mbaya.

Wote wanne inaaminika kuwa walisaini taarifa ya kifo, walisema viongozi hao, lakini hakuna taarifa zaidi zilizotolewa kuhusu barua hiyo.

Walisema ni mapema mno kuhisi kuhusu kifo cha wanariadha hao chipukizi waliokuwa wakifanya mazoezi lakini ndugu wa waathirika hao walisema kuwa wasichana hao walikuwa wameathirika kiakili kutokana na kusumbuliwa na wanariadha wakubwa na makocha katika kituo hicho.

Waziri wa Vijana na Michezo Sarbananda Sonowal alisema polisi wanachunguza na Mkurugenzi Mkuu wa SAI alikuwa akiongoza taasisi hiyo pia.

"Sheria itachukua mkondo wake, lakini nakuhakikishia kuwa kama kuna mtu yoyote kutoka katika mamlaka ya michezo nchini India atapatikana na hatia kuhusiana na suala hili, atachukuliwa hatua za kisheria mara moja," alisema Sonowal katika taarifa yake.

Mkurugenzi Mkuu wa SAI Injeti Srinivas aliwaambia waandishi wa habari kuwa "ni tukio la kushtua sana ".

"Wasichana wanne walijaribu kujiua. Sasa tunataka kuwapatia vifaa vya bora vya afya, " alisema.

Rais TFF awapo pole wahanga wa mafuriko

http://shaffihdauda.co.tz/wp-content/uploads/2015/04/malinzi11.jpg
Rais wa TFF, Jamal Malinzi
Na Rahma White
RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ametuma salamu za pole kwa wakazi wa Dar es salaam na hasa wale walioathirika na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es salaam kwa siku ya tatu mfululizo sasa.
Katika salamu zake kupitia kwa Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Mecky Sadik, Malinzi amesema familia zimepoteza makazi, miundombinu ya usafiri na michezo imeharibika na hata kuwa katika hali ya kutotumika, wanawake watoto, familia, shughuli za kiuchumi na kimichezo zimeathirika na mvua hizi.
TFF inaunga mkono juhudi za Mkuu wa Mkoa Dar es salaam, Serikali na wadau wote wanaoshugulika  kupunguza makali ya janga hili.

Polisi Moro, Masau Bwire warudi Ligi Daraja la Kwanza

Mbeya City wamemaliza kwa ushindi nyumbani dhidi ya Polisi

Polisi wameenda na maji

Yanga walioendelea kutoa takrima kwa timu pinzani
 
Azam walimaliza kwa kishindo nyumbani

JKT Ruvu licha ya kichaapo cha Simba wamenusuurika kushuka draja

Ndanda wamepona baada ya kuilaza Yanga
Simba waliomaliza ligi kwa kishindo kwa kuiparua JKT Ruvu

Prisons wameponea chupuchupu
Mtibwa wamemaliza kwa kichapo nyumbani mbele ya Coastal Union
PAZIA la Ligi Kuu ya Tanzania Bara limehitimishwa kwa michezo saba na kushuhudiwa timu za Polisi Moro na Ruvu Shooting ya Msemaji mwenye tambo nyingi, Masau Bwire wakishuka daraja kwenda FDL.

Ruvu inayonolewa na kocha Mkenya Tom Olaba ilikuwa ugenini Uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga na kujikuta ikipokea kipigo cha bao 1-0 na wenyeji wao Stand United ambayo ushindi huo umeifanya kufikisha pointi 31 katika nafasi ya 10.

Polisi Moro iliyopanda kucheza Ligi Kuu msimu huu, ilikubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Mbeya City na kujikuta ikirudi ilipotoka na hiyo inatokana na mwenendo wa kusuasua tangu kuanza kwa msimu huu ikiwemo uongozi kubadilisha makocha mara kwa mara.

Polisi Moro ndiyo timu pekee msimu huu ambayo imefundishwa na makocha watatu, ilianza na Adolf Rishard 'Adolf' kisha ikamfukuza na kumchukua Amri Said, ambaye naye aliamua kujiondoa na nafasi yake kuchukuliwa na John Tamba, lakini hadi siku jana walijikuta wakiburuza mkia wakiwa na pointi zao 25 katika mechi 26 walizocheza.
Katika uwanja wa Nang'wanda Sijaona mkoani Mtwara, Mabingwa wapya wa msimu huu Yanga waliendelea kuonja shubiri baada ya kupoteza mchezo huo kwa kufungwa bao 1-0 na wenyeji Ndanda FC, Wakati kwenye Uwanja wa Azam Complex wenyeji Azam walitoka sare ya bila kufungana na Mgambo JKT ya Tanga.
Kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kocha, Mbwana Makatta, alifanikiwa kuiokoa timu ya Tanzania Prisons isishuke daraja msimu huu baada ya kuilazimisha sare ya bila kufungana na Kagera Sugar aliyomaliza nafasi ya sita ikiwa na pointi 32, huku sare hiyo ikiwasaidia maafande hao kufikisha pointi 29 na kuepuka janga la kurudi kushuka daraja la kwanza msimu ujao.
Katika uwanja wa Manungu Turiani, Mtibwa Sugar ililala nyumbani kwa kufungwa mabao 2-1 na Coastal Union ya Tanga na matokeo hayo kuifanya timu hiyo iliyokuwa na kipindi kigumu licha ya kunza msimu huu vizuri kumaliza nafasi ya saba msimu huu ikiwa na pointi 31 huku Wagosi wa Kaya wakimaliza nafasi ya tano wakiwa na pointi 34.
Msimamo wa mwisho wa Ligi Kuu ya Bara:
                      P    W    D    L    F     A    Pts

1. Yanga         26  17    4    5    52   18   55
2. Azam         26   13   10   3    36   18   49

3. Simba        26   13    8    5    38   19   47
4.  Mbeya City26    8    10   8    22    22  34
5.  Coastal     26    8    10   8    21    25   34
6.Kagera        26    8     8   10   22    26   32
7. Mtibwa       26    7    10   9    25    25   31
8. JKT Ruvu    26    8    7    11   20    25   31
9. Ndanda      26    8    7    11    21   29   31
10.Stand        26    8    7    11    23   34   31
11. Prisons     26    5   14    7    18    22   29
12. Mgambo   26    8    5    13   18    28   29
13. Ruvu        26    7    8    11   16    29   29
14. Polisi Moro26    5   10   11   16    27   25

Matokeo:
JKT Ruvu       v  Simba            (1-2)
Mtibwa Sugar v  Coastal Union (1-2)
Stand Utd      v  Ruvu Shooting(1-0)
Mbeya City     v  Polisi Moro     (1-0)
Kagera Sugar v  Prisons          (0-0)
Ndanda          v  Yanga           (1-0)
Azam             v  Mgambo JKT  (0-0)

WAFUNGAJI:
17- Simon Msuva                                (Yanga)
14- Amissi Tambwe                             (Yanga)
11- Abaslim Chiidiebele               (Stand Utd)
10-Didier Kavumbagu                         (Azam)
     Rashid Mandawa              (Kagera Sugar)
     Emmanuel Okwi                             (Simba)
9- Malimi Busungu                         (Mgambo)
8- Samuel Kamuntu                      (JKT Ruvu)
    Ibrahim Ajibu                                  (Simba)
    Ame Ali                                         (Mtibwa)  
 7-Rama Salim                                   (Coastal)
6- Kipre Tchetche                                (Azam)
    Danny Mrwanda                             (Yanga)
    Heri Mohammed                             (Stand)
5- Jacob Massawe                           (Ndanda)
    Yahya Tumbo                                    (Ruvu)
    Atupele Green                               (Kagera)
    Mussa Mgosi                                (Mtibwa)
    Nassor Kapama                            (Ndanda)
4- Ally Shomari                                 (Mtibwa)
    Themi Felix                             (Mbeya City)
    Said Bahanuzi                        (Polisi Moro)
    Frank Domayo                                 (Azam)
    Mrisho Ngassa                                (Yanga)
    Kpah Sherman                                (Yanga)
    Gaudence Mwaikimba                   (Azam)
    Andrey Coutinho                           (Yanga)
    Ramadhani Singano                      (Simba)
3- Dan Sserunkuma                            (Simba)
    Elias Maguli                                     (Simba)
    Ally Nassor                                 (Mgambo)
    Raphael Alpha                       (Mbeya City)
    Aggrey Morris                                  (Azam)
    Paul Nonga                             (Mbeya City) 

NB:WAKILISHI WA NCHI, ZILIZOSHUKA DARAJA

Chelsea kupeleka taji laao la ubingwa Thailand

http://soccerblitz.net/wp-content/uploads/2015/03/chelseaWinCapitalOneCup15_large.jpg
Chelsea walipotwaa taji lao la Kombe la Ligi (Capital One)

WAKATI leo wakiwa nyumbani kukabiliana na Liverpool, Mabingwa wapya wa England, Chelsea inatarajiwa kwenda kulitambulisha taji lao nchini Thailand.
Chelsea wamejumuisha katika ratiba yao kuwa Mei 30 wataenda jijini Bangkok, Thailand na kucheza na nyota wa soka wa Thailand. 
Chelsea ambao wamewahi kwenda kucheza mechi za kirafiki nchini Thailand mwaka 2011 na 2013, wanatarajiwa kucheza mchezo huo katika Uwanja wa Rajamangala kabla ya kupaa kuelekea Australia kuchukuana na Sydney FC Juni 2 mwaka huu. Chelsea pia watacheza michuano ya Kombe la Kimataifa nchini Marekani dhidi ya timu za New York Red Bulls, Paris Saint-Germain na Barcelona Julai. Waratibu wa mchezo huo huko Bangkok wamedai kuwa utakuwa mahsusi kuadhimisha miaka 88 ya kuzaliwa mfalme wa Thailand. Chelsea leo watakuwa kwenye uwanja wao wa Stamford Bridge kuwakaribisha vijogoo vya Anfield katika mfululizo wa Ligi Kuu ya England. Mechi hiyo ni muhimu zaidi kwa Liverpool wanaowania nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya mwakani, fursa hiyo imekuja baada ya Soothampton na Tottenham Hotspur kuchemsha katika mechi zao za wikiendi hii kwa kupokea vipigo.

Kibaka amliza Benni McCarthy, ampora kila kitu akiwa saluni

http://3.bp.blogspot.com/-YGgvai_tplY/Tv8nwIMi6YI/AAAAAAAAMrk/8yk4O-snDNU/s1600/32832.jpg

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Afrika Kusini, Benni McCarthy ameporwa na mtu mwenye silaha wakati akiwa saluni ya kunyoa nywele jijini Johannesburg, Afrika Kusini. 
Wakala wa McCarthy, Percy Adams amesema mteja wake huyo alikumbwa na kadhia hiyo akiwa saluni hapo na kuporwa vitu vyake kadhaa vya thamani ikiwemo saa, hereni na pete yake ya ndoa. 
Adams aliendelea kudai kuwa katika tukio hilo hakuna aliyejeruhiwa na wateja wengine waliokuwemo hawakuguswa zaidi ya McCarthy peke yake. 
McCarthy mwenye umri wa miaka 37, amewahi kushinda taji la michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na klabu ya FC Porto ya Ureno huku akishikilia rekodi ya kufunga mabao mengi katika timu yake ya taifa ya Bafana Bafana akiwa na mabao 32. 
Matukio ya uporaji wa kutumia sialaha yanaonekana kuwa ya kawaida nchini humo baada ya golikipa na nahodha wa Bafana Bafana kuuawa mwaka jana katika tukio kama hilo la uporaji akiwa nyumbani.

Yathibitika Yaya Toure kutimka Manchester City

http://www.standard.co.uk/incoming/article9842399.ece/binary/original/Yaya%20Toure.jpg
Yaya Toure anayesemekana anatarajiwa kuikacha Man City kwenda Inter Milan
WAKALA wa kiungo Yaya Toure amedai kuwa ana uhakika wa asilimia 90i kuwa mteja wake huyo ataondoka katika majira ya kiangazi. 
Aprili, Toure ambaye amebakisha mkataba wa miaka miwili ambao unamuingizia kitita cha Euro 265,000 kwa wiki, alikuwa akitaka kufanya mazungumzo na maofisa wa City kuhusiana uhamisho katika majira ya kiangazi. 
Meneja wa Inter Milan, Roberto Mancini ameonyesha nia ya wazi ya kutaka kumsajili kiungo huyo ambaye anatimiza miaka 32 Mei 13, na wakala wake Dimitri Seluk amekiri kuna uwezekano mkubwa wa kuondoka City. 
Seluk amesema ingawa hakuna kilichoamuliwa mpaka sasa lakini ana uhakika wa asilimia 90 kuwa mteja wake anaweza kuondoka katika timu hiyo majira ya kiangazi. 
Toure alijiunga na City akitokea Barcelona mwaka 2010 na amefanikiwa kushinda mataji mawili ya Ligi Kuu na moja la Kombe la FA, pia taji la Mataifa ya Afrika akiwa na timu yake ya taifa ya Iviry Coast mapema mwaka huu.

Ngumi kupigwa mjini Bagamoyo, Super D kugawa vifaa kwa wakali

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiQeWrEKx0_mnCSl1J8PJPUA6_zw9p_yAOeZomH3PlujJqmd-14VYhlB3pKSf7PHU9eX1DZtKUMI9cS9-QGU2VjQhu79Pbzw72lNYISSHPE4Pp4xjpa8cUno_Tb72KVlAzOr64GIftMRVk/s1600/10702151_751229401589872_1190688698899816254_n.jpg
Super D akionyesha baadhi ya DVD anazosambaza kwa ajili ya kutoa mafunzo ya ngumi,
Na Rahim Kimwaga
NDONGA zinatarajiwa kupigwa mjini Bagamoyo wakati mabondia Idd Pialali wa Kiwangwa atakapopanda ulingoni kuzipiga na Adam Ngange wa Chanika katika pambano liotakalochezwa Mei 16.
Mpambano huo utapigwa kwenye ukumbi wa Che kwa Che, uliopo mjini humo na tyari kila bondia ameanza tambo akijigamba kuibuka na ushindi siku hiyo.
Mbali na pambano hilo lililoandaliwa na kampuni ya Sharrif Promotion, pia siku hiyo kutakuwa na mapambano mengine kadhaa ya utangulizi yatakayowahusisha mabondia machachari.
Kwa mujibu wa mratibu huyo mabondia watakaowasindikiza Pialali na Ngange ni pamoja na lile litakalowakutanisha Rashidi Haruna dhidi ya Kaminja Ramadhani.
Michezo mingine ni kati ya Halid Hongo atakayebiliana na Kishoki Mbish, huku Abdallah Samata atazidunda na Maono Alli 
Mgeni rasmi katika pambano hilo ambalo viiongilio vyake vinaanzia Sh. 5000 kwa viti vya kawaida na Sh. 8000 kwa V.I.P atakuwa ni bodnia Cosmas Cheka, mdogo wa bingwa wa zamani wa dunia wa WBF, Francis Cheka 'SMG'.
Pia katika mipambano hilo, kutakuwa na upatikanaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Floyd Mayweathar vs Manny Paquaio 2015 , Saul 'canelo' Alverez, Mike 'Iron' Tyson, Muhammad Ali, Felix Trinidad, Miguel Cotto na wengine wengi, huku vifaa vya mchezo vitagawiwa na kocha  Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine vitauzwa kwa gharama nafuu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha mchezo wa masumbwi nchini.

Kampuni ya Bima ya UAP yatoa elimu kwa wakulima Kanda ya Ziwa

Picha tofauti zinaoonyesha  Pamba zilizokuwa zimehifadhiwa katika ghla na kuungua na chini ni maafisa wa kampuni ya Bima UAP wakiwa na Meneja wa Kiwanda cha JIELONG Holdings Tanzania LTD Kiki Huwa Xu (kushoto).

Na Renatha Msungu
WANANCHI wa mkoa wa Shinyanga wamenufaika na elimu ya kutunza maghala ya chakula na pamba iliotolewa na kampuni ya bima ya UAP kwa ajili ya
kuzuia wasipatwe na majanga ya moto.
Elimu hiyo imetolewa kwa wakazi wa mkoa huo, baada ya mmiliki wa ghala la Jielong Holdings, Kiki Jielong kuunguliwa na ghala lake la pamba
lililopo nje kidogo ya mji wa Shinyanga, kwenye hafla ya kukabidhi hundi kwa ajii ya fidia hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Shinyanga jana, Meneja Maendeleo wa biashara wa UAP Raymond Komanga, alisema hii ni moja ya
faida ya kujiunga na bima ya nyumba ambayo inasaidia kutoa fidia ya hasara inayopatikana kwenye maghala kama hilo la Jielong.
Komanga alisema kutokana na hilo wameamua kutoa elimu kwa wafanya biashara na wamiliki wa maghala mkoani humo ili waweze kujikinga na athari ambazo  zinaweza kutokea wakati wowote.
Alisema wamekuwa wakipata kesi nyingi za aina hiyo na kuzitatua tu kwa wale ambao wamejiunga na bima kwa ajili ya kujikinga na majanga yanayotokea katika sehemu zao za kazi.
Alisema wameanza mkoani Shinyanga na wataendelea katika mikoa mingine ili kutoa elimu ya kujikinga na majanga mbalimbali ya moto na mengine yanayowatokea kila kukicha.
Alisema wananchi wengi hawajakata bima jambo ambalo linawapa shida mara baada ya kupata matatizo ya kuunguliwa na nyumba na kushindwa
kuzirejesha kwa wakati.
Kwa upande wake mmiliki wa ghala hilo na ambaye ni meneja Utawala wa kampuni ya Jielong, alisema wanaishkuru UAP kutokana na kuwarejeshea
fedha hizo haraka baada ya kupata ajali hiyo ya moto katika ghala lao.
Alisema wao ni wanachama wa muda mfupi lakini walipotoa taarifa mara moja watu wa bima walijitokeza na kuwasaidia kufidia gharama
zilizoungua katika ghala hilo la kuhifadhia pamba.
Akielezea chanzo cha moto ndani ya ghala hilo alisema umetokana na joto la ndani ya ghala baada ya bidhaa zilizopo ndani kubanana na kukosa hewa na kusababisha pamba kuwaka moto.
Alisema moto huo ulisambaa kwa kasi kubwa kutokana na kwamba pamba inashika moto kwa haraka kuliko kitu kingine.
Alisema anawashauri wafanya biashara ambao hawajakata bima wajitokeze kwenda kukata bima hiyo kwa kuwa ina manufaa makubwa sana, hasa wakati wa matatizo.
Meneja madai wa UAP Emmanuel Michael aliwataka wafanya biashara kuwa makini na bidhaa zao ili kuepusha majanga ya moto yasiwatokee.
Alisema wafanya biashara wengi wamekuwa wazembe kujifunza elimu ya kujikinga na majanga ya moto ambayo huwapatia hasara kubwa katika
biashara zao za kila siku.