STRIKA
USILIKOSE
Wednesday, June 26, 2013
Hawa ndiyo visura wa Redd's Miss Temeke 2013
Mrembo Hyness Oscar, akiwa katika pozi.
Mrembo Margreth Olotu, akiwa katika pozi.
Mrembo Latifa Mohamed, akiwa katika pozi.
Mrembo Mutesi George, akiwa katika pozi.
Mrembo Mey Karume, akiwa katika pozi.
Mrembo Stella Mgazija, akiwa katika pozi.
Mrembo Margreth Gerrad, akiwa katika pozi.
Mrembo Axsaritha Vedastus, akiwa katika pozi.
Mrembo Naima Ramadhan, akiwa katika pozi.
Mrembo Irine Rajab, akiwa katika pozi.
Mrembo Eastear Msulwa, akiwa katika pozi.
Mrembo Svtlona Nyameyo, akiwa katika pozi.
Mrembo Darlin Mmari, akiwa katika pozi.
Mrembo Narietha Boniface, akiwa katika
pozi.
Baadhi ya washiriki wa kinyang'anyiro cha Redd's Miss
Temeke 2013, wakiwa katika picha ya pamoja kwenye mazoezi yao juzi.
Washiriki wa kinyang'anyiro cha Redd's Miss Temeke 2013,
wakiwa katika picha ya pamoja kwenye mazoezi yao. Kutoka kushoto, waliosimama ni
Magreth Olotu, Narieth Boniface, Latifa Mohamed, Mutesi George,
Naima Ramadhan, Axarith Vedastus, Mey Karume, Easter Msulwa, Margreth Gerrad,
Svtlon Nyameyo na walikaa chini ni Hyness Oscar, Jamila Ramadhan, Irine Rajab,
Stella Mgazija na Darlin Mmari.
Ancelotti achekelea kutua Real Madrid
Kocha Carlo Ancelotti |
Muitalia huyo mwenye umri wa miaka 54 amesaidia mkataba wa miaka mitatu wa kuwanoa mabingwa hao wa kihistoria wa Ligi ya Mabingwa Ulaya na kutambulishwa rasmi leo Jumatano.
Aidha kocha huyo ameweka wazi hana mpango wa kustaafu mapema badala yake angependa kuendelea kuwepo Santiago Bernabeu kwa muda mrefu zaidi.
"Naupenda mpira wa miguu na kwanini Real Madrid imekuwa klabu ya ndoto yangu, na nashukuru leo ndoto hiyo imekuwa kweli," alisema Ancelotti.
"Sidhani kama Real Madrid itakuwa ndiyo mwisho wangu wa kufundisha, lakini nina matumaini nitakuwepo hapa kwa muda mrefu," alisema kocha huyo aliyewahi kuzinoa timu za Ac Milan na Chelsea.
Kocha huyo alijibu kiungwana alipotupiwa swali kutaka kulinganishwa na Jose Mourinho aliyempokea mikoba yake Madrid kwa kusema yeye na Mourinho ni makocha tofauti, japo anaendelea kumheshimu.
"Niko tofauti kiwasifu na Mourinho, lakini naendelea kumheshimu mno," alisema.
Barbatov haendi kokote atasalia Fulham
Dimitar Barbatov |
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 na aliyesaliwa na mkataba wa mwaka mmoja ilidaiwa alikuwa katika mipango ya kujiunga na klabu ya Zenit St Petersburg waliovutiwa naye.
Hata hivyo danchev alisema mkali huyo aliyewahi pia kukipiga Tottenham kabla ya kutua United ataendelea kusalia katika klabu hiyo.
"Ana mkataba wa mwaka mmoja zaidi na Fulham na atasalia hapa mpaka mtakata utakapoisha, " alisema wakala huyo na kuongeza;
"Anajisikia furaha hapa Fulham na anataka kubaki kwa mwaka mmoja zaidi. Hataki kujadili suala la klabu nyingine kwa sasa. Hata kama kuna klabu zinamhitaji binafsi anafurahia kuwepo kwake Fulham na anataka kusalia hapa. Anataka kucheza angalau zaidi ya miaka miwili."
Berbatov ameifungia Fulham mabao 15 katika Ligi kuu kwa msimu wake wa kwanza tangu ajiunge na timu hiyo akitokea Manchester United.
Mfalme Mswati II atua nchini apokewa na Makamu wa Rais
AMRI KIEMBA ACHEKELEA TUZO YA SPUTANZA
Amri Kiemba akishangilia moja ya mabao yake uwanjani |
KIUNGO
mshambuliaji wa timu za Simba na Taifa Stars, Amri Kiemba amewashukuru
waandaji wa tuzo za Mwanasoka Bora Tanzania, Chama cha Wachezaji Soka
Tanzania (SPUTANZA) kwa kumpa heshima hiyo ambayo haikutarajia baada ya
kutoka kwenye kipindi kigumu ndani ya klabu yake.
Akizungumza
na MICHARAZO mchana huu, Kiemba alisema heshima aliyepewa na SPUTANZA ya kuwa
Mwanasoka Bora kwa mwaka 2013, imemfanya ajisikie fahari na kutambua
kuwa wapo wanaokubali mchango wake katika soka la Tanzania.
"Nimefurahi
kwa kutwaa tuzo hii ya Sputanza, hata kama maandalizi yake yalikuwa ya
haraka haraka, lakini siku zote mwanzo mgumu na ninawapongeza na
kuwashukuru, nikiamini kwamba mchango wangu unathaminika kwa wadau,"
alisema Kiemba.
Kiemba, alisema anaamini tuzo hiyo ni changamoto kwake kwa msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara inayotarajiwa
kuanza Agosti 24 mwaka huu.
"Kunyatua
tuzo hii ni changamoto kwangu kwa msimu ujao, watu watapenda kuona
nafanya kitu gani baada ya msimu uliopita kung'ara, lakini yote kwa yote
namuachia Mungu kwani yeye ndiye mpangaji wa kila jambo," alisema
Kiemba baba wa watoto wawili, Shaaban na Amri Kiemba Jr.
Kiungo
huyo aliyewahi kung'ara na timu za Kagera Sugar, Yanga na Miembeni
amenyakua tuzo hiyo baada ya kung'ara msimu uliopita akiifungia Simba
mabao 8 na pia kuipigania Stars kwenye mbio zake za kuwania Fainali za
Kombe la Dunia za mwakani, japo Tanzania imekwama.
Kabla
ya kurejea kwenye kiwango kilichowavutia makocha na mashabiki wa soka,
Kiemba alikaa nusu msimu wa 2011-2012 bila kucheza kupinga maamuzi ya
uongozi wa Simba kumtoa kwa mkopo kumpeleka timu ya Polisi Dodoma ambayo
ilikuja kuteremka daraja mwishoni mwa msimu huo.
Mbali na Kiemba tuzo hizo za SPUTANZA pia ilinyakuliwa na Salum Abubakar 'Sure Boy' wa Azam kama Mchezaji Bora Chipukizi, Hussein Sharrif 'Casillas' (Kipa Bora) na kocha Mecky Mexime wa Mtibwa aliyetangazwa kuwa Kocha Bora wa Mwaka.
GAPCO yazindua promesheni ya Relstar Oil
Wasanii wa kikundi cha Bombeso Cruw wakitoa burudani wakati wa promosheni ya Relstar Oil yanayotengenezwa na Kampuni ya Gapco. |
Yusuph Mlela aibukia kwa Miss Serena
Yusuph Mlela katika pozi |
Akizungumza na MICHARAZO, Mlela alisema filamu hiyoi aliyoigiza na wakali wenzake kama Salma Jabu 'Nisha' , Sabrina Rupia 'Cathy' na Seleman Abdallah 'Barafu' ipo katika maandalizi ya kuwachiwa wakati wowote kuanzia sasa.
Mlela alisema filamu hiyo ya kimapenzi na yenye mafunzo kwa jamii ni ya tatu kuzalishwa na kampuni yake tangu alipoianzisha hivi karibu kama njia ya kujikomboa.
"Kaka nimekamilisha filamu yangu mpya ambayo ni ya tatu kuzalishwa na kampuni yangu na itafahamika kwa jina la 'Miss Serena' ambapo imewashirikisha wakali kadhaa nikiwemo mimi mwenyewe, Nisha, Barafu na Cathy wa Kaole," alisema Mlela.
Mlela aliyetambulishwa kwenye ulimwengu wa filamu mwaka 2006 kupitia filamu ya 'Diversion of Love' kabla ya kujipatia umaarufu katika filamu zaidi ya 30 alizocheza mpaka sasa alisema kazi hiyo mpya ni moja ya kazi nzuri alizozalisha baada ya kutoa Angel na Poor Minds.
Mkali huyo ambaye pia ni mwanamitindo alisema mashabiki wake wakae mkao wa kula kupata burudani kabambe wakati akiwa 'location' kwa sasa akishirikishwa kwenye kazi mpya ya Wastara Juma 'Stara'.
Neymar, Suarez nani zaidi leo Kombe la Mabara, Hispania, Italia kesho
RIO DE JANEIRO, Brazil
WASHAMBULIAJI Neymar wa timu ya taifa ya Brazil na Luis Suarez wa Uruguay ni miongoni mwa nyota wanaotarajiwa kuwa kivutio leo wakati mataifa hayo hasimu kisoka yatakapokutana katika mechi yao ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho inayoendelea nchini Brazil.
Brazil ambao ni wenyeji wa michuano hiyo, walitinga nusu fainali kwa kishindo, wakiwafunga Japan na Mexico bila kuruhusu lango lao na kisha kuishindilia Italia magoli 4-2 katika mechi yao ya mwisho ya hatua ya makundi.
Uruguay walifuzu kwa hatua ya nusu fainali baada ya kulala 2-1 mbele ya Italia na kisha kushinda mechi nyingine zilizofuata za hatua ya makundi dhidi ya Nigeria na Tahiti.
Hadi sasa, timu zote zimeonyesha kuwa na uwezo mkubwa wa kupachika mabao na mechi yao leo inaweza kuwa miongoni mwa mechi za kusisimua zaidi katika michuano hiyo.
Mbali na Neymar aliyetua Barcelona hivi karibuni, Brazil inatarajiwa pia kuwategemea nyota wake waliong'ara zaidi kwenye michuano hiyo hadi sasa ambao ni pamoja na Marcelo wa Real Madrid, Paulinho wa Corinthians anayewaniwa na Tottenham Hotspur, Oscar wa Chelsea, Thiago Silva wa PSG na Fred.
Kwenye kikosi cha Uruguay, Suarez ambaye ni nyota wa kutumainiwa pia wa klabu ya Liverpool anatarajiwa kuwasumbua mabeki wa Brazil akishirikiana na nyota wenzake Edinson Cavani wa Napoli na Diego Forlan wa Inter Milan.
Neymar ana rekodi nzuri ya kuifungia Brazil magoli 24 katika mechi 35 huku Suarez akiandika historia kwa kuwa kinara wa muda wote wa upachikaji mabao katika timu ya taifa ya Uruguay baada ya kufunga magoli mawili waliposhinda 8-0 dhidi ya Tahiti na kufikisha magoli 36.
LEO, Jumatano
Nusu fainali ya kwanza
Brazil v Uruguay (saa 4:00 usiku)
KESHO, Alhamisi
Nusu fainali ya pili
Hispania v Italia (saa 4:00 usiku)
-----
Wakazi Ujiji wahimizwa kujenga tabia ya kulipa kodi
Mstahiki Meya wa Ujiji-Kigoma, Bakari Husseni Beji (kushoto) |
UONGOZI wa Manispaa ya Mji wa Ujiji mkoani Kigoma umewahimiza wakazi wa mji huo kujenga tabia ya kupenda kulipa kodi za manispaa hiyo kwa hiari kwa ajili ya kujiletea maendeleo badala ya kusubiri kushurutishwa.
Aidha Manispaa hiyo ilijikadiria kwa mwaka huu unaomalizika Juni 30 kukusanya jumla ya Sh Bil 1.3 kupitia vyanzo vyake vya fedha, lakini ikidai mpaka sasa lengo hilo halijatimia kutoka na wakazi wengi wa mji huo kuwa wagumu katika ulipaji wa kodi hasa zile za Majengo.
Akizungumza na MICHARAZO Mstahili Meya wa Manispaa ya Ujiji, Bakari Beji alisema uongozi wao umekuwa na wakati mgumu katika kukusanya kodi toka kwa wananchi wao kutokana na wengi wao kutokuwa na tabia ya kulipa kodi.
Mstahiki Meya huyo alisema kutokana na hali hiyo wamekuwa wakishindwa kufikia malengo ya kimaendeleo waliyojiwekea kutokana na tabi ya wakazi wa mji huo kushindwa kulipa kodi kwa hiari wakidhani fedha hizo zinahishia mikononi mwa watu, ingawa ukweli ndizo zinazosaidia huduma za kijamii.
Alisema kwa mfano kwa kipindi cha bajeti cha mwaka unaomalizika Juni 30, walikadiria kukusanya jumla ya Sh. Bil 1.3, lakini mpaka sasa japo bado hawajakaa chini kutathimini wamebaini lengo lao halijafikiwa kwa ufanisi.
"Kumekuwa na ugumu kwa wakazi wa mji wetu kulipa kodi hasa hizi za majengo, hivyo tunawahimiza wananchi hao kujenga tabia ya kulipa kodi hizi kwa ajili ya kujiletea maendeleo yao na mji wao kwa ujumla," alisema.
Mstahiki Meya huyo alisema pamoja na kwamba mara kadhaa wamekuwa wakitumia nguvu kulazimisha wakazi hao kulipa kodi wameona bado hajawajafanikiwa hivyo wameona boira watumie elimu ya uhamasishaji zaidi ili kuwaelimisha wananchi hao kujua umuhimu wa ulipaji wa kodi hizo.
"Tumeanza kuendesha kampeni za kuwaelimisha na kuwahamasisha wananchi umuhimu wa kulipa kodi kwa kutumia njia mbalimbali, tunaamini wakazi hao watabadilika na kusaidia kuiwezesha Manispaa yao kupata fedha na kuwaletea maendeleo ya kijamii," alisema Meya Beji.
Alisema Manispaa yao inapata ugumu katika ukusanyaji wa kodi ya majengo kuliko zile za Ushuru wa Masoko na Vizimba,Maegesho ya Magari, Ushuru wa Huduma ya Mji, Hoteli na Nyumba za Wageni na Mabango ya Matangazo.
Subscribe to:
Posts (Atom)