EBU angalia matangazo ya bidhaa zinazotengenezwa na wajasiriamali wa kike wa Tanzania...unadhani wakiwezesha zaidi si watafika mbali zaidi?!
STRIKA
USILIKOSE
Saturday, June 8, 2013
Wajasiriamali wanawake wazidi kupiga hatua Tanzania
EBU angalia matangazo ya bidhaa zinazotengenezwa na wajasiriamali wa kike wa Tanzania...unadhani wakiwezesha zaidi si watafika mbali zaidi?!
LICHA YA HUJUMA, STARS YAAPA KUIFANYIZIA MOROCCO
Straika wa Stars, Mbwana Samata (kushoto)akimiliki mpira wakati wa mazoezi yao kuelekea mechi yao ya leo usiku ya kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia 2014 dhidi ya Morocco mjini Marrakech. |
TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars usiku wa kuamkia leo ilifanyiwa kilichoonekana kuwa hujuma baada ya kufanyiwa vurugu na kuzimiwa taa ishindwe kufanya mazoezi kwenye uwanja wa utakaotumika kwa mechi ya leo, siku moja kabla ya mchezo wao dhidi ya wenyeji wao Morocco ya kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia 2014.
Sheria za FIFA zinasema timu mgeni, itapewa fursa ya kufanya mazoezi katika uwanja utakaotumika kwa mechi dhidi ya wenyeji katika muda ambao mechi itachezwa, lakini jana msafara wa Stars ulipofika Uwanja wa Marakech ulizuiwa kuingia ndani na askari wa uwanjani hapo.
Juhudi za kocha wa Stars, Kim Poulsen kuwaelewesha askari wa uwanja huo sheria ili wairuhusu timu kuingia uwanjani hazikuzaa matunda na ikabidi viongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) waingilie kati, nao pia wakachemsha.
Ikawadia zamu ya viongozi wa Kamati ya Ushindi ya Stars, inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premum Lager, ambao nao walichemsha, ndipo baadhi wa Watanzania waishio hapa na wachache waliosafiri kutoka Dar es Salaam walipoongeza nguvu.
Walikwenda kufungua geti kwa nguvu, wakawaweka kando askari waliokuwa wanawazuia na kuiingiza timu uwanjani kufanya mazoezi.
Hata hivyo, Stars ilipofika uwanjani ililazimika kusubiri tena, kwani wenyeji Simba wa Atlas walikuwa wakiendelea na mazoezi.
Baada ya nusu saa, Morocco walimaliza awamu yao na Stars wakaanza kupasha misuli moto. Hata hivyo, baada ya dakika 34, taa za uwanja huo zilizimwa na uwanjani kuwa giza totoro, lakini viongozi wa TFF wakaenda kuomba, zikawashwa na timu ikafanya mazoezi kwa dakika 10 zaidi.
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo, Amos Makalla aliyekuwapo wakati wa vurumai zote hizo, alisikitishwa mno na kitendo hicho akisema si cha kiungwana na si cha kiunamichezo.
Makamu wa Rais wa TFF, Athumani Nyamlani alisema Morocco walikuja kucheza Dar es Salaam walipokewa vizuri na wakahudumiwa vizuri hadi wanaondoka, ajabu leo wanaifanyia ‘unyama’ Tanzania.
Mkuu wa Msafara wa Stars hapa, Crescentius John Magori alisema watapeleka malalamiko FIFA, waandaji wa michuano ya kufuzu kwa Kombe la Dunia na kwa kuwa ushahidi upo, anaamini Morocco watachukuliwa hatua.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe alishauri Stars icheze chini ya angalizo kwa kuwasilisha barua FIFA mapema ili wakae wanajua kuhusu hali halisi Morocco.
Kwa ujumla kilichotokea leo kimewatia woga Watanzania wengi waliopo hapa kuelekea mchezo wa leo, ambao Stars inahitaji ushindi ili kujiimarisha katika mbio za kuelekea Brazil 2014.
Hata ulinzi wa msafara wa Stars kutoka hotelini hadi uwanjani hakuwa wa kutosha na ilishuhuidiwa mara kadhaa ukiingiliwa na magari mengine barabarani wakati timu ikienda uwanjani kwa mazoezi.
Wenyeji nchini Morocco wanasema inapowadia mechi, huwa wanaogopa kwa sababu mara nyingi hutokea vurugu ya damu kumwagika.
Kwa ujumla Stars inaingia katika mchezo wa leo katika hali ya wasiwasi na woga mkubwa.
Stars itashuka dimbani saa 3:00 usiku leo kwa saa za hapa sawa na saa 5:00 za Tanzania kucheza na Morocco.
Stars inashika nafasi ya pili katika Kundi C, ikiwa na pointi sita nyuma ya Ivory Coast yenye pointi saba, ambayo kesho itakuwa ugenini ikimenyana na Gambia katika mchezo mwingine wa kundi hilo.
Stars ilitua hapa Jumatatu ikitokea Ethiopia ambako iliweka kambi ya wiki moja na kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Sudan, ulioisha kwa sare ya bila mabao.
Kabla ya kuja hapa, Stars iliweka kambi ya wiki moja katika hoteli ya Tansoma, Dar es Salaam ikijifua Uwanja wa Karume na siku chache kabla ya kuondoka ilialikwa Ikulu na Rais Jakaya Kikwete, aliyewapa hamasa kwa hotuba nzuri.
Waziri Makamba avisuta vyama vya upinzani
Naibu Waziri, Januari Makamba |
NAIBU Waziri wa
Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Januari Makamba amesema dhamira ya kuwepo
kwa vyama vingi bado haijafikiwa tangu kuanzishwa kwake kutokana na kukosa
vyama na viongozi wenye dira kwa Taifa.
Aliyasema hayo leo
jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na wanafunzi wanachama wa Chama Cha
Mapinduzi ambao wanamaliza vyuo mbalimbali mkoa wa Dar es Salaam.
Makamba ambaye pia ni
Mlezi wa Vyuo Vikuu Tanzania alisema vyama
hivyo vimekuwa vikijikita katika kulalamika bila kuonyesha dira na mwelekeo
tofauti jambo ambalo linapelekea katika kufanya fujo ambazo zinakwamisha
jitihada za serikali.
Makamba alisema
Serikali inafanya kazi kutokana na mipango yake ambayo imejiwekea yenyewe hivyo
inaamini kuwa itafikia malengo yake bila kusukumwa na mtu.
“Kwa kweli najuta kwanini tuliruhusu uwepo wa
vyama vingi hapa nchini kwani lengo letu lilikuwa ni kudumisha demokrasia kitu
ambacho kimekuwa kinyume kwani vyama na
viongozi hao wamekuwa wakihubiri kinyume na dhima ya lengo husika,”
alisema
Naibu Waziri alisema
CCM ni chama ambacho kinaheshimika kitaifa na kimataifa hivyo wao wanaamini
kuwa heshima hiyo itaendelea kuwepo milele kwa milele.
Alisema vijana wa CCM
wahakikishe kuwa wanakisaidia chama na nchi kwa ujumla ili nchi isije kuchukuliwa na
vyama vya upinzani kwani itakuwa ni sawa na kuipeleka nchi kuzimu.
Aidha Mlezi huyo
aliwataka vijana hao wanaomaliza
kujiamini na kuthubutu kushiriki katika fursa mbalimbali zinazojitokeza ili waweze
kupata urahisi wa kushiriki katika chama na serikali kwani ni wajibu wao
kulitumikia Taifa.
Makamba alisema vijana
wanapaswa kushiriki katika harakati za kisiasa kwani hayupo mtu amnbaye atapata
jambo bila kulihitaji mwenyewe na kuondokana na dhana ya kutafutiwa kazi kama
wengi wanaofikiri.
Aliwataka wingi wao uwe
ni sehemu muhimu ya kutafakari muafaka wa Taifa la Tanzania ijao ikiwa ni
kushiriki katika ngazi mbalimbali za uongozi na kuondokana na dhana kuwa mwenye
uwezo wa fedha ndio sababu ya kushinda.
Mlezi huyo alisema
dhana ya fedha katika kutafuta uongozi ipo kwa baadhi ya watu kutokana na tabia ya
mtu mmoja mmoja lakini sio jambo la kusimamia kama kigezo.
Naibu Waziri aliwataka
vijana wa CCM kuondoa uoga katika maamuzi ambayo yanahusu maslahi ya Taifa na
jamii kwa ujumla iwapo sifa za uongozi unazo.
Makamba aliwaambia
vijana kutambua kuwa kiongozi wema wanatoka kwa mungu na kuachana na tabia ya
kulalamika kwakigezo kuwa nchi inaongozwa na wazee jambo ambalo wanalitengeneza
wenyewe.
Aidha aliwataka wasomi
kutafuta maandiko ambayo aliandika Hayati Mwalimu Nyerere kwani yana msingi
mkubwa katika kujitambua na kufanya maamuzi sahihi kuhusu nchi yao na uongozi
kwa ujumla.
Naye Mwenyekiti Vyuo Vikuu Wilaya ya Dar es Salaam Abubakari
Asenga alisema katika mahafal;i hayo wanafunzi zaidi ya mmia nne kutoka vyuo 28
vya mkoa wa Dar es Salaam walishiriki katika sherehe hiyo.
Asenga alisema huo ni
uataratibu ambao wamekuwa nao tangu kuoanzishwa kwa shirikisho hilo lengo
likiwa ni kuwatambua na kuwapatia vyeti vya utambulisho wao ndani ya CCM.
Alitaja vyuo ambavyo
vilishiriki ni pamoja na Mwalimu Nyerere, Ustawi, Ardhi, UDSM, IFM, CBE, DIT,
TSJ na vingine vingi.
Kwa upande wa msoma
risala kwa niaba ya wahitimu Innocent Nsena alisema wanakiomba Chama Cha Mapinduzi CCM
kuwatumia wahitimu wanaomaliza vyuo kwani wana ujuzi na uwezo wa kukabiliana
na changamoto za jamii pamoja na vyama
vya upinzani hapa nchini.
Aidha alisema wanavyuo
wanapendekeza maoni yao kuhusu rasimu ya katiba ambapo wanaomba nchi ya
Tanzania kutokubali kuwa na serikali ya shirikisho kwani uwezo wa nchi bado ni
mdogo kuendesha nchi ambayo bado ni change kuichumi.
Pia wanapendekeza
upatikanaji mpya wa kupata mgombea urais ili kuondoa mpasuko ambao unatokea
mara kwa mara baada ya uchaguzi kufanyika.
Alisema katika
mazingira yoyote yale Rais bora lazima atokee CCM ila kutokana na mazingira mbalimbali
ambayo yamekuwa yakitokea baada ya uchaguzi ni vyema wakatumia mfumo wa kujaza
dodoso ili wana CCM wapendekeze Rais wanayemuhitaji kwa manufaa ya Taifa.
Huyu ndiye Miss Sinza 2013 arithi taji la Miss Tanzania 2012
MREMBO Prisca Element
jana usiku alifanikiwa kumvua taji la kwanza Redd’s Miss Tanzania, Brigitte
Alfred baada ya kufanikiwa kutwaa taji la Redd’s Miss Sinza katika mchuano
mkali uliofanyika ukumbi wa Meeda, uliopo Sinza Mori, Dar es Salaam.
Brigitte mbali na
kushikilia taji la Redd’s Miss Tanzania ndiye pia aliyekuwa mrembo wa Redd’s
Miss Tanzania, hivyo kuvuliwa taji hilo la kwanza ni kudhihirisha
kinyang’anyiro cha kumsaka mrithi wake kimeshika kasi.
Katika shindano hilo
lililokuwa kali na la kuvutia, huku burudani ikinogeshwa na kundi la African
Stars ‘Twanga Pepeta’, nafasi ya pili ilichukuliwa na Happynes Maira na ile ya
tatu akaitwaa Sarah Paul.
Warembo wengine
wawili waliofanikiwa kuingia katika tano bora walikuwa ni Nicole Michael na
Nasra Hassan, ambao walitoa upinzani mkali katika shindano hilo lililokuwa
likifuatiliwa kwa karibu na watu wengi.
Akizungumza mara
baada ya kufanikiwa kutwaa taji hilo, Prisca alisema ana uhakika mkubwa wa
kufuata nyayo za Brigitte na kudai atahakikisha anaipigania Sinza kwa nguvu
zake zote ili iweze kufanya vyema katika Redd’s Miss Tanzania.
Brigitte alipoulizwa
kuhusu shindano hilo na kuvuliwa kwake taji, alisema anaamini kwa dhati mrembo
aliyechaguliwa atahakikisha kitongoji cha Sinza kinaendelea kufanya vizuri
zaidi katika mashindano hayo.
“Kikubwa zaidi ni
kujiamini na kufuata maelekezo unayopewa, lakini mrembo wetu naamini ana sifa
zote zinazostahili na ni matumaini yangu atasonga mbele zaidi katika hatua
inayofuata,” alisema.
Redd’s Miss Tanzania
kwa sasa inadhaminiwa na kinywaji cha Redd’s Original kinachozalishwa na
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).
Mfanyabiashara mbaroni kwa kulawiti wanafunzi
MFANYABIASHARA maarufu mjini Morogoro, Mohamed Mauji, anashikiliwa na polisi kwa
tuhuma za kuwaingilia kinyume na maumbile wanafunzi wawili wa Shule ya
Msingi Mwere B.
Tukio hilo linadaiwa kutokea wiki iliyopita kwenye eneo la mazingira ya ofisi ya mfanyabiashara huyo anayeuza vinywaji laini kwa jumla.
Akizungumzia tukio hilo kwa niaba ya Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Mkuu wa polisi wilaya ya Morogoro, Sadick Tindwa, alisema kuwa inadaiwa kutokea Mei 31 na kuripotiwa katika kituo hicho Juni 3 na wazazi wa watoto hao.
Alisema kuwa wazazi hao walieleza kuwa waliwabaini watoto wao baada ya kupewa taarifa na walimu wa shule hiyo kuwa watoto hao wamekuwa wakija shuleni na fedha nyingi za matumizi pamoja na vitu mbalimbali.
Mkuu huyo wa Polisi wilaya ya Morogoro alisema kuwa baada ya wazazi hao kupewa taarifa hizo, waliwauliza watoto hao na kueleza kuwa wamekuwa wakipewa na mtu waliyemtaja kwa jina la mzungu na kuwafanyia vitendo hivyo.
Alisema kuwa wazazi hao walipowapekua watoto wao waliwakuta wana michubuko katika sehemu za kutolea haja kubwa na kuamua kulifikisha suala hilo kwa afisa mtendaji wa kata Kingo jirani na mfanyabiashara huyo.
Mkuu huyo wa Polisi Wilaya ya Morogoro alisema kuwa afisa huyo mtendaji wa kata ya Kingo aliamuru suala hilo lifikishwe kwenye kituo cha polisi kwa ajili ya kufanyiwa upelelezi.
Alisema kuwa baada ya kulifikisha , jeshi la polisi lilimkamata mtuhumiwa huyo kwa ajili ya uchunguzi ikiwa pamoja na watoto hao kupelekwa hospitali ya rufaa ya Morogoro kuchunguzwa afya zao.
Hata hivyo, alipoulizwa na gazeti hili kuhusiana na tuhuma hizo, mfanyabiashara huyo alikiri kuwafahamu wanafunzi hao ambao wamekuwa wakipita nje ya ofisi yake na kuomba pesa ya soda na yeye aliwahi kuwapatia kiasi cha sh 500 lakini hajawahi kuwafanyia kitendo hicho.
Tukio hilo linadaiwa kutokea wiki iliyopita kwenye eneo la mazingira ya ofisi ya mfanyabiashara huyo anayeuza vinywaji laini kwa jumla.
Akizungumzia tukio hilo kwa niaba ya Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Mkuu wa polisi wilaya ya Morogoro, Sadick Tindwa, alisema kuwa inadaiwa kutokea Mei 31 na kuripotiwa katika kituo hicho Juni 3 na wazazi wa watoto hao.
Alisema kuwa wazazi hao walieleza kuwa waliwabaini watoto wao baada ya kupewa taarifa na walimu wa shule hiyo kuwa watoto hao wamekuwa wakija shuleni na fedha nyingi za matumizi pamoja na vitu mbalimbali.
Mkuu huyo wa Polisi wilaya ya Morogoro alisema kuwa baada ya wazazi hao kupewa taarifa hizo, waliwauliza watoto hao na kueleza kuwa wamekuwa wakipewa na mtu waliyemtaja kwa jina la mzungu na kuwafanyia vitendo hivyo.
Alisema kuwa wazazi hao walipowapekua watoto wao waliwakuta wana michubuko katika sehemu za kutolea haja kubwa na kuamua kulifikisha suala hilo kwa afisa mtendaji wa kata Kingo jirani na mfanyabiashara huyo.
Mkuu huyo wa Polisi Wilaya ya Morogoro alisema kuwa afisa huyo mtendaji wa kata ya Kingo aliamuru suala hilo lifikishwe kwenye kituo cha polisi kwa ajili ya kufanyiwa upelelezi.
Alisema kuwa baada ya kulifikisha , jeshi la polisi lilimkamata mtuhumiwa huyo kwa ajili ya uchunguzi ikiwa pamoja na watoto hao kupelekwa hospitali ya rufaa ya Morogoro kuchunguzwa afya zao.
Hata hivyo, alipoulizwa na gazeti hili kuhusiana na tuhuma hizo, mfanyabiashara huyo alikiri kuwafahamu wanafunzi hao ambao wamekuwa wakipita nje ya ofisi yake na kuomba pesa ya soda na yeye aliwahi kuwapatia kiasi cha sh 500 lakini hajawahi kuwafanyia kitendo hicho.
Moyes, Wenger katika vita ya kumwania Fabregas
KLABU ya Manchester United imeingia vitani dhidi ya mahasimu wao Arsenal baada ya kocha wake David Moyes kuweka bayana kwamba ipo tayari kumnyakua kiungo wa Barcelona Cesc Fabregas anayewindwa pia kurejeshwa Emirates na klabu yake ya zamani.
Moyes, amenukulia akisema angependa kumsajili kiungo wa zamani wa Gunners ambaye hata hivuo majuzi aliweka bayana nia yake ya kuendelea kusalia kwa mabingwa wa Hispania, Barcelona.
Kiungo alikaririwa akisema angependa kusalia Nou Camp Nou ili kupigania namba yake licha ya kusajiliwa Mbrazili mwenye thamani ya Paundi Mil 50, Neymer.
Hata hivyo Moyes amesema atafanya kila njia kumnyakua mshindi huyo wa Kombe la Dunia aliyenyakua na timu yake ya taifa katika fainali zilizopita za 2010 ili kujenga kikosi chake.
Mipango ya Fabregas kurejeshwa Ligi Kuu ya England ilianza kitambo hata kabla Moyes kuchukua nafasi ya Ferguson mwzi uliopita.
Mabingwa hao wanamhitaji kiungo huyo baada ya Paul Scholes kustaafu na Michal Carrick kuondoka huku Tom Cleverley akibebeshwa majukumu yote.
Licha ya viungo toka Brazil, Anderson na Mjapan Shinji Kagawa kufanya vyema Old Trafford, lakini wanaelezwa sio wa daraja la Fabregas na ndiyo maana Moyes anamtolea macho akichuana na Wenger aliyetangaza kutaka kumrejesha nyota wake huyo wa zamani aliyemuuza mwaka uliopita.
Moyes amnyakua kinda toka Uruguay
Guillermo Varela |
Valera mwenye umri wa miaka 19 aliyekuwa katika majaribio kwa mahasimu wa United, Manchester City msimu uliopita anakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Moyes tangu amrithi Sir Alex Ferguson.
Mabingwa hao wa England watalazimika kuilipa klabu inayoshikilia taji la Ligi Kuu ya Uruguay, Penarol kiasi cha Paundi Milioni 1 kwa ajili ya saini ya mchezaji huyo, japo uhamisho wake unaweza kufikia mpaka Paundi Mil 2.5.
Varela alinukuliwa na gazeti la The Sun akithibitisha suala la kuhamia kwake United akisema alikuwa afanyiwe vipimo hivyo jana kabla ya leo Jumamosi kujiunga na kikosi cha timu yake ya taifa ya vijana U20.
Pia mchezaji huyo alisema atajifunza Kiingereza ili aweze kumudu kuwasiliana na wenzake.
United imemnyakua mchezaji huyo kijana baada ya misimu michache kuwanyakua makinda wengine waliopo katika kikosi chake kutoka nchi za Amerika ya Kusini na Kati baada ya kuwavuta Javier Hernandes 'Chicharito', Angelo Henriquez na Wabrazil mapacha, Rafael na Fabio .
Duru za kimichezo zinasema tayari mchezaji huyo alishafanyiwa vipimo hivyo vya afya jana na hivyo kuwa rasmi mchezaji wa Old Trafford.
Subscribe to:
Posts (Atom)