Wachezaji wa Yanga wakishangilia katika baadhi ya mechi zao za mwaka jana za Kagame ilipocheza Dar |
MABINGWA watetezi wa Kombe la Kagame, Yanga ya Tanzania imepangwa kundi l;a C pamoja na timu za Express ya Uganda, Vital'O ya Burundi na As Port ya Djibout, huku watani zao Simba wakiwekwa kundi A na El Merreikh ya Sudan na APR ya Rwanda.
Mbali na APR na Merreikh, kundi hilo A lina timu ya Elman ya Somalia, wakati kundi B l;ina timu za El Hilal ya Sudan, Ahli Shandi ya Sudan, Al Nasir Juba ya Sudan Kusini, Tusker Kenya na Super Falcon ya Zanzibar.
Michuano hiyo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi mwezi ujao na kumalizika mwanzoni mwa Julai, ambapo jumla ya timu 13 zitachuana katika kinyang'anyiro hicho.
Makundi hayo ni kama ifuatavyo:
Kundi A: El Merreikh (Sudan), Simba (Tanzania), Elman (Somalia) na APR (Rwanda).
Kundi B: El Hilal (Sudan), Ahli Shandi (Sudan), Al Nasri Juba (S.Sudan), Tusker (Kenya) na Super Falcon (Zanzibar)
Kunci C: Yanga (Tanzania), Express FC (Uganda), Vitalo (Burundi) na AS Port (Djibouti).