STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, July 14, 2013

Tanzania wenyeji Tamasha la Kimataifa kupinga vita vya Ujangili

Rais wa Miss Utalii Tanzania
KAMPUNI ya Africa Tourism Promotion Centre kwa kushirikiana na kampuni ya Miss Tourism Tanzania Organisation, wameandaa tamasha la kimataifa la Safri kuu ya Kitalii Tanzania “Tanzania Great Safari Tour 2013” kuanzia Mwezi Agost hadi Septemba 2013 nchini Tanzania.
Lengo la kuhamasisha vita dhidi ya Ujangili wa Wanyama Pori (Uwindaji Haramu) , Misitu (Mazingira na Uvunaji Haramu wa Mazao ya Misitu) ,Maliasili za Baharini (Uvuvi Haramu), pia kuhamasisha Utalii wa Ndani na kutangaza Vivutio vya Utalii waTanzania kitaifa na kimataifa. 
Tamasha hilo la Safari Kuu ya Kitalii la Tanzania Great Safari Tour 2013, litajumuisha na kuhusisha mashindando ya mbio za Nyika za Kimataifa za ANT POACHING INTERNATIONAL MARATHON, NATIONAL PARKS INTERNATIONAL MARATHON, WILDLIFE TOURISM INTERNATIONAL MARATHON,sambamba na msafara mkuu wa kitalii Tanzania wa kutembelea na kupiga picha za Televisheni, Video, Filamu na Minato za Makala, Matangazo, Magazeti, Majarida, Tovuti, Mitandao ya Kijamii na vipindi maalum vya Televisheni,Redio na Filamu.
Tanzania ni miongoni mwanchi chache Duniani zilizojaliwa kuwa na vivutio vingi na vya pekee vya Utalii Duniani, kuanzia Hifadhi za Taifa, Mapori ya Akiba, Hifadhi za Bahari, Maeneo ya Kihistoria, Maajabu ya Dunia, Hifadhi za Wanyama Pori na Utajili mkubwa wa Utamaduni wa kuvutia. 
Ndiyo maana sekta ya Utalii nchini ni moja ya sekta tegemezi na kiongozi katika pato la Taifa na kuingiza fedha za kigeni. Utalii unachangia zaidi ya 18% ya pato la Tifa, 24% ya Pato la fedha za kigeni la Taifa na zaidi ya 12% ya ajira zote nchini kila mwaka.
Serikali ya Tanzania imekuwa ikifanya juhudi kubwa za kukuza na kuendeleza sekta ya utalii nchini, ikiwa ni pamoja na juhudi kubwa za kutangaza Utalii na vivutio vya utalii vya Tanzania kitaifa na kimataifa lakini pia kulinda na kuhifadhi maliasili za Taifa za Utalii, kupitia wizara ya maliasili na utalii na mamlaka zake tanzu za Utalii nchini,ikiwemo Bodi ya Utalii(TTB), Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA), Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro(NCAA), Mamlaka ya Huduma za Misitu (Tanzania Forest Services), Mamalaka ya Wanyama Pori na Mamlaka ya Hifdhi ya Mambo Kale. 
Juhudi hizo sasa zimezaa matunda katika kukuza utalii nchini tofauti na miaka ya nyuma, hata hivyo pamoja na mafanikio hayo sekta ya Utalii nchini sasa inakabiliwa na changamoto nyingi ,lakini kubwa ikiwa ni Ujangili wa uwindaji Haramu na Uvunaji Haramu wa Mazao ya Misitu na Majini, lakini pia changamoto ya Utalii wa Ndani na Utangazaji wa Vivutio vya Utalii Kitaifa na Kimataifa.
Changamoto hizi hasa ya Ujangili, imekuwa ni tishio kubwa kwa ustawi na ukuaji wa sekta ya Utalii nchini, kutokana na kukua na kuongezeka kwa uwindaji haramu na uvunaji wa nyara za maliasili za misitu na bahari, ambayo sasa imekuwa ni janga la Taifa na tishio la kutoweka kwa baadhi ya wanyama Pori ,Viumbe Bahari na Misitu. Tunaamini kuwa, wakati sasa umefika ,tena wakati sahihi kwa sekta Binafsi kuungana na sekta za Umma katika kupigana na kuhamasisha vita dhidi ya uwindaji Haramu,Uvuvi Haramu na Uvunaji haramu wa Misitu nchini, lakini pia katika kutangaza vivutio vya utalii Kitaifa na kimataifa na pia kuhamasisha utalii wa Ndani. 
Kutokana na kukua kwa sekta ya Utalii Duniani na kuwa moja ya sekta muhimu katika uchumi Duniani, mataifa mengi duniani na Afrika  ikiwemo Tanzania na nchi jirani na Tanzania zimewekeza kwa kiasi kikubwa na kufanikiwa sana katika ushirikiano na uungaji mkono wa hali na mali wa juhudi za asasi binafsi za kutangaza na kupromoti utalii  na vita dhidi ya Ujangili kama Africa Tourism Promotion Centre na Miss Tourism Tanzania Organisation.
Tanzania Great Safari Tour ni jibu na tafsiri ya vitendo ya sera za taifa za Utalii, Wanyama Pori, Misitu na Utamaduni, ambapo matukio ya kimataifa ya Mbio za Nyika za Ant Poaching International Marathon, National Parks Marathon, Wildlife Tourism International Marathon, sambamba na ziara ya washiriki wa kitaifa na kimataifa wa Tanzania Great Safari Tour, katika Hifadhi za Taifa, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Maeneo ya Kihistoria, Maeneo ya Kitamaduni, Maeneo ya Hifadhi za Bahari, Maeneo ya Hifadhi za Misitu na Vivutio vingine vya Utalii nchini, huku wakihamasisha vita dhidi ya UJangili, wakihamasisha Utalii wa Ndani, Utalii wa Kitamaduni, Utalii wa Mikutano, Utalii wa Mazingira na kutangaza Vivutio vya Utalii vya Tanzania Kitaifa na Kimataifa. 
Tanzania Great Safari Tour 2013, ni Safari Kuu ya Kitalii ya Kihistoria likiambatana na ushiriki mkubwa wa vyombo vya habari vya kitaifa na kimataifa, ambayo itawaweka na kuwakutanisha pamoja wasanii wa kitaifa na kimataifa wa Filamu, Urembo, Mitindo, Muziki, Ngoma za Asili na Maigizo lakini pia wanamichezo wa kitaifa na kimataifa wa Mpira wa Miguu, Riadha, Mpira wa Kikapu, Mpira wa Mikono, Mpira wa Meza, Rugby sambamba na wanadiplomasia na waandishi wa Habari wa Televisheni, Redio, Magazeti, Makala, Majarida na Mitandao ya Kijamii kitaifa na kimataifa.
Tanzania Great Safari Tour 2013, ni fulsa nyingine kwa Tanzania kutangaza Utalii na Kuhamasishisha Vita Dhidi ya Uwindaji Haramu,Uvuvi Haramu, Uharibifu wa Mazingira na Ujangili kwa Ujumla, kwani matukio yote ya Tanzania great Safari Tour 2013 yataonyeshwa na kurushwa moja kwa moja (LIVE) kutoka Tanzania na kuonekana Duniani kote kupitia Televisheni, Tovuti, Internet na Mitandao ya Kijamii, huku Promo DVD na DVD za Filamu ya ziara zima zikigawanywa Katika vyombo mbalimbali vya habari na Taasisi za Kidiplamasia, Mashirika ya ndege, Vyuo Duniani kote. 
Matukio katika zira hiyo ni pamoja na Mbio Live za Ant Poaching International Marathon 2013, National Parks International Marathon 2013, Wildlife Tourism International Marathon 2013, Great Safari Wildlife Fashion & Talent Show 2013, Ant Poaching Street Carnival 2013, Great Safari Ant Poaching Sports Bonanza 2013 na Mdahalo wa kitaifa wa Ujangili, Utalii na Utalii wa Ndani. Washindi wa fainali za Taifa za Miss Utalii Tanzania , watashiriki katika Tamasha hilo ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kwenda kushiriki katika mashindano ya Dunia ya Miss Tourism World 2013 huko Equatorial Guinea Octoba mwaka huu na Miss Tourism United Nation 2013 huko Florida Marekani Novemba mwaka huu.
Kaulimbiu ya Tamasha la Tanzania great Safari Tour 2013, ni “Stop Poaching, Protect Wildlife – Tourism is Life, Culture is Living” (Piga Vita Ujangili, Linda Wanyama Pori – Utalii ni Maisha, Utamaduni ni Uhai wa Taifa).
Asante.

Erasto Gideon Chipungahelo
Mwenyekiti Mtendaji
Africa Tourism Promotion Centre na Miss Tourism Tanzania Organisation

Wawili wafa ajali ya basi la Najma



BASI la kampuni ya Najma linalofanya safari zake kati ya Dar es Salaam na Nachingwea, limepata ajali kwenye daraja la Mkapa, Ikwiriri baada ya kugonga pikipiki na kusababisha vifo vya watu wawili papohapo. Chanzo cha ajali hiyo ni moshi mkali uliotanda kwenye eneo la ajali kutokana na moto uliokuwa unaunguza majani yaliyopo pembezoni mwa barabara ya kusini mara baada ya kumaliza daraja la Mkapa. Basi hilo lilikuwa linatokea Nachingwea kwenda Dar es Salaam. Watu waliofariki ni wale waliokuwa kwenye pikipiki. Ajali hiyo imetokea majira ya saa 6:40 mchana. Hata hivyo gari hilo halikupinduka isipokuwa imeharibika vibaya sehemu ya mbele. Baada ya ajali hiyo, dereva alisogeza gari kwenye kituo cha polisi cha Ikwiriri na baada ya kutoa maelezo, polisi wameenda eneo la tukio kuchukua maiti. Mtoa habari hii ni miongoni mwa watu waliokuwa abiria kwenye basi hilo. Namba ya gari ni T 599 CBL aina ya YUTONG.
Polisi imethibitisha juu ya tukio la ajali na vifo vya watu hao wawili wakazi wa hapo hapo Ikwiriri na kueleza chanzo ni moshi mzito uliotokana na kuchomwa kwa taka kando ya barabara na kufanya madereva wasione njia na kwamba dereva wa basi anashikiliwa kwa uchunguzi zaidi.

Mwili wa Mama Prof Jay wapumzishwa Kinondoni

Waombolezaji wakiweka maua
 
Muda wa kuweka maua
Waombolezaji waliohudhuria
Watu wakifukia kaburi
Mafundi wakilijengea kaburi
Kaburi likiwa limekamilika

Mwili wa marehemu ukitolewa nyumbani kupelekwa makaburini
Picha Kwa Hisani Ya Michuzi Blog

Stars yaenda kambini jijini Mwanza

Na Boniface Wambura
TIMU ya Taifa (Taifa Stars) imeondoka leo asubuhi (Julai 14 mwaka huu) kwenda Mwanza ambapo itapiga kambi ya siku kumi kujiandaa kwa mechi ya marudiano dhidi ya Uganda (The Cranes) kutafuta tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini.
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imeondoka kwa ndege ya PrecisionAir na itafikia hoteli ya La Kairo wakati mazoezi yatafanyika Uwanja wa CCM Kirumba kulingana na programu ya Kocha Mkuu Kim Poulsen.
Wachezaji walioko katika kikosi hicho ni Juma Kaseja, Aggrey Morris, Mwadini Ally, Ally Mustafa, Shomari Kapombe, Kevin Yondani, Erasto Nyoni, Haroub Nadir, Mwinyi Kazimoto, Frank Domayo, Mrisho Ngasa, Khamis Mchana, Amri Kiemba, Salum Abubakar, Simon Msuva, John Bocco, Vincent Barnabas, Mudathiri Yahya, Athuman Idd na Haruni Chanongo.
Mechi ya marudiano itachezwa kati ya Julai 26 na 28 mwaka huu kwenye Uwanja wa Nelson Mandela ulioko Namboole nje kidogo ya Jiji la Kampala. Tarehe rasmi itapangwa na Shirikisho la Vyama vya Mpira wa Miguu vya Uganda (FUFA) siku kumi kabla ya mechi.

Tenga awashukuru Wajumbe Mkutano Mkuu TFF

Rais wa TFF, Leodger Tenga akiwahutubia kwenye mkutano wa jana wa TFF
Na Boniface Wambura
RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga amewashukuru wajumbe wa Mkutano Mkuu kwa michango yao, na utulivu waliouonesha katika kupitisha marekebisho ya Katiba ya TFF ya 2013.
Amesema marekebisho hayo yatawasilishwa kesho (Julai 15 mwaka huu) kwa Msajili wa Klabu na Vyama vya Michezo kwa ajili ya kupitishwa ili mchakato wa uchaguzi uweze kuanza mara moja.
“Tutamuomba Msajili atusaidie kusajili haraka Katiba yetu ya 2013 ili tuingie katika mchakato wa uchaguzi. Kama tulivyotangaza awali tumepanga kufanya uchaguzi Septemba 29 mwaka huu, na tusingependa tarehe hiyo ipite,” amesema Rais Tenga wakati akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kikao cha Kamati ya Utendaji.
Katika kikao chake, Kamati ya Utendaji  imepitisha Kanuni za Maadili, Kanuni za Nidhamu, na marekebisho kwenye Kanuni za Uchaguzi yanayotokana na kuundwa kwa Kamati ya Maadili.

Stars, The Cranes yaingiza Mil 113

https://sphotos-b.xx.fbcdn.net/hphotos-ash4/p480x480/1006233_699315590082862_452426371_n.jpg
Na Boniface Wambura
PAMBANO la kwanza la mchujo la kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ligi za Ndani (CHAN) kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Uganda (The Cranes) iliyochezwa jana (Julai 13 mwaka huu) limeingiza sh. 113,268,000 kutokana na watazamaji 17,121.
Tiketi za kushuhudia mechi hiyo ziliuzwa kwa sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 30,000.
Mgawanyo wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ni sh. 17,278,169.49 wakati wa gharama za uchapaji tiketi ni sh. 7,809,104.
Asilimia 15 ya uwanja sh. 13,227,108.98, asilimia 20 ya gharama za mechi sh. 17,636,145.30 na asilimia 5 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 4,409,036.33.
Asilimia 60 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 52,908,435.91 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 2,645,421.80 ambayo ni asilimia 5 kutoka kwenye mgawo wa TFF.

Majina ya askari waliokufa Darfur haya hapa!


MAJINA ya Wanajeshi saba wa Tanzania waliokufa kwenye shambulio la ghafla mjini Darfur yamepatikana.
Askari hao waliokufa ambao walikuwa kwenye vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa huko nchini Sudan ni Sajenti Shaibu Othman, Koplo Oswald Chaula, Koplo Mohamed Juma, Koplo Mohamed Chikilizo, Pte. Rodney Ndunguru, Pte. Peter Werema na Pte. Fortunatus Msofe.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kwenye mtandao ni kwamba askari hao walizingirwa na waasi hao na kushambuliwa ambapo 7 walikufa na wengine 14 akiwemo askari Polisi wa Tanzania kujeruhiwa na kukimbizwa hospitalini.

Mungu azilaze roho za askari wetu mahali pema peponi, Amina.

Mbowe avamiwa na Polisi nyumbani kwake, kisa...!

KUNDI la polisi wenye silaha za moto juzi usiku walivamia nyumbani kwa Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, kwa nia ya kumkamata.

Askari hao wanaokisiwa kufikia saba, wakiwa na silaha nzito katika gari la wazi waliwasili nyumbani kwa Mbowe majira ya saa saba na nusu usiku na kuwaamuru askari wanaolinda nyumbani kwake kumtoa Mbowe nje ili waonane naye.

Walinzi wa Mbowe walihoji uhalali wa ukamataji huo na kuwataka polisi wawaoneshe hati ya kumkamata, lakini hawakuweza kuionesha, hali iliyozusha wasiwasi kwa walinzi wa kiongozi huyo.

Hata hivyo walinzi hao waliwaambia polisi hao kuwa Mbowe ambaye pia ni kiongozi mkuu wa kambi ya upinzani bungeni alikuwa safarini, jibu ambalo lilipokewa kwa shingo upande na askari hao.
Polisi hao baada ya kuona wameshindwa kukamilisha kazi hiyo, waliwaachia walinzi hao namba ya simu 0754-085600 ya Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Ernest Kimola, wakiwaagiza kuhakikisha wanamwambia Mbowe awasiliane na kamanda huyo.
RCO amsukumia RPC, akana
Hata hivyo, alipohojiwa na Tanzania Daima Jumapili kwa njia ya simu, Mkuu wa Upelelezi Kimola aligoma kuzunguzia suala hilo na kumtaka mwandishi kuwasiliana na mkuu wake wa kazi, ambaye ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Kamilius Wambura, akidai ndiye mwenye haki ya kutoa ufafanuzi wa jambo hilo.
Unajua mimi si msemaji wa polisi, wasiliana na kamanda wa mkoa, maana ndiye mwenye uwezo wa kutoa maelezo,” alisema Kimola na kukata simu. Lakini alipopigiwa simu Kamanda Wambura aliruka kimanga, kwa mshangao, akidai kutojua lolote kuhusiana na polisi kuvamia nyumbani kwa Mbowe.
Kwa kweli ndiyo napata taarifa hizo kutoka kwako, kuwa kiongozi huyo alifuatwa na polisi, maana silijui suala hilo hata kidogo,” alisema Wambura, naye kama alivyofanya Kimola akakata simu.
Kauli ya CHADEMA
Lakini wakati Kimola akikataa kusema chochote, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, alisema kuwa alizungumza kwa njia ya simu na Kimola kuhusiana na kitendo cha polisi kuvamia nyumbani kwa kiongozi huyo wa juu wa kisiasa, na kudai kupewa majibu ya kushangaza.
Akizungumza jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika Manzese, Wilaya ya Kinondoni, Dk. Slaa alisema Kimola alijitetea akidai kwanza kukana kufika nyumbani kwa Mbowe usiku wa manane. Pili, alisema kuwa hawakwenda kumkamata Mbowe, isipokuwa kufanya naye mazungumzo na kisha wangemwacha.
Slaa alisema kitendo hicho kimewashitua na ni cha kinyama na kilichokiuka sheria za nchi na haki za binadamu. Aliongeza kwamba, daima wamekuwa wakilishutumu Jeshi la Polisi kwa kutumika vibaya kukandamiza wapinzani, lakini mara zote CHADEMA kimepuuzwa na sasa jeshi hilo limeamua kuvamia makazi ya viongozi wa kisiasa kwa madhumuni yasiyoeleweka.
Alisema haijulikani nini kingetokea ikiwa Mbowe angekuwa ndani, ikiwa walinzi wangeamua kugoma kumwachia kiongozi wao. “Tuna hofu kubwa na usalama wetu, maana pale wangeweza kufanya lolote, hata kumuua na kisha kutoa matamshi kuwa walikuwa wanajibishana kwa risasi, kama ambavyo imekuwa jadi ya askari polisi kutoa taarifa za uongo na upotoshaji wanapoua watu,” alisema Slaa.
Alisema ikiwa polisi walikuwa na shida ya kweli, wangemwita kwa njia sahihi na si kumvamia na kuingilia uhuru wake na wa familia yake kama wanakamata gaidi ama jambazi hatari.
Dk. Slaa alisema Mbowe anayo ofisi inayojulikana, na kama kweli hakukuwa na jambo baya lililopangwa na polisi hao wasingeweza kufanya uhuni kama walioufanya.
“Kama wanaweza kuvamia nyumbani kwa kiongozi mkubwa kama Mbowe wakiwa na silaha nzito, itakuwaje kwa viongozi wa kawaida na raia?” alihoji Slaa.
Kutokana na tukio hilo la kuogofya, CHADEMA imemtaka Rais Jakaya Kikwete kuwaeleza Watanzania maana ya matukio haya ambayo yamedhamiria kuleta vurugu kubwa nchini. Kadhalika, wamemtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Said Mwema, kuueleza umma kile kilichokusudiwa na askari wake kuvamia nyumbani kwa Mbowe mithiri ya jambazi.
Itakumbukwa pia kuwa hivi karibuni askari polisi wa Mkoa wa Arusha walivamia nyumbani kwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, wakiwa na silaha nzito na mbwa, na kumkamata, kisha kumtupa rumande kwa siku nzima.


SOURCE: JAMII FORUM

Inasikitisha! Sheikh mwingine ajeruhiwa kwa tindikali



VITENDO vya viongozi wa kidini nchini kushambuliwa na watu wasiofahamika vimeendelea tena safari hii,  Shekhe Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Said Juma Makamba akijeruhiwa vibaya kwa kumwagiwa maji yanayohisiwa kuwa tindikali na watu wasiojulikana juzi usiku akiwa nyumbani kwake jijini Arusha.

Shekhe Makamba, ambaye amelazwa katika Wodi ya Majeruhi kwenye Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru, amejeruhiwa vibaya maeneo ya usoni, kifuani na mgongoni huku akiendelea na matibabu.

Akizungumza kwa tabu, shekhe huyo alisema tukio hilo lilitokea saa 5 usiku wa kuamkia jana nyumbani kwake kwa Mromboo Arusha, wakati akijiandaa kulala baada ya kutoka kuswali Swala ya Tarawei.

Shekhe Makamba ambaye pia ni Imamu wa Msikiti wa Sekei mjini Arusha, alisema baada ya swala hiyo alirejea nyumbani kwake akisindikizwa na vijana wawili ambao walikuwa wakiswali pamoja na kuingia ndani ya nyumba yake ili kulala.

Alisema hata hivyo, kabla ya kulala alikwenda kujisaidia katika choo cha nje na kwamba wakati akirudi ili aingie ndani akipitia nyuma ya nyumba ghafla alimuona mtu akiwa amesimama jirani na mlango.

Alieleza kuwa wakati akitaka kumwangalia zaidi alishtukia mtu
huyo akiinua mkono na kumwagia maji yaliyompatia maumivu makali usoni na kifuani.

‘’Wakati natoka msalani nikipitia uwani kwangu niliona kama mtu ameinama pembeni yangu wakati najaribu kumsogelea ili nijue ni nani nilihamaki mtu huyo akinimwagia maji yaliyonisababisha maumivu makali sana yenye asili ya moto na ngozi kuanza kubabuka,’’ alisema shekhe huyo.

Aliongeza kuwa baada ya tukio hilo alianza kupiga kelele kuomba msaada ambapo majirani walijitokeza na kumpa msaada wa kumpeleka hospitali, kwa vile wakati huo macho yake yalikuwa hayaoni na wakati wote alikuwa  akilia.

Pamoja na kujeruhiwa vibaya sehemu za usoni, kifuani na  mgongoni, pia ana majeraha  kwenye mikono na machoni na hali yake bado ni mbaya japo madaktari wanaendelea kumpatia matibabu.

Kaimu Katibu wa Bakwata Mkoa wa Arusha, Abdallah Masoud akizungumzia tukio hilo alieleza kushitushwa nalo akisema limefanana na lile la Katibu wa Bakwata Mkoa wa Arusha, Abdulaziz Jonjo ambaye mwaka jana alilipuliwa kwa bomu nyumbani kwake akiwa amelala.

Alisema kuwa matukio hayo yamekuwa yakijirudia huku wahusika wakishindwa kutiwa mbaroni na kudai kuwa matukio hayo yanahusiana na masuala ya kigaidi. Aliongeza kuwa pamoja na kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi, lakini wamekuwa hawapati matunda ya kukamatwa kwa watuhumiwa ingawa alisema wanajulikana.

Kwa upande wake,  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alisema polisi wameanza uchunguzi wa tukio hilo na kwamba taarifa zitatolewa pindi washukiwa watakapotiwa mbaroni kwani uchunguzi bado unaendelea na kwamba hakuna  mtu anayeshikiliwa hadi sasa.

Tukio hilo ni mfululizo wa matukio ya kushambuliwa kwa viongozi wa kidini baada ya kuuwawa kwa kupigwa risasi kwa viongozi wa Kikristo na kisha kumwagiwa tindikali na kuuwawa kwa viongozi wa Kiislam visiwani Zanzibar.

Ubunifu! Hata watanzania wanaweza ila basi tuu

Mwangoka akiwa ndani ya gari lake

Umeuona mlango? Mwangoka akishuka garini

Akifunga mlango

Akionyesha siti ya abiria wake

Juu tumeweka kupitisha upepo


Umeona dashboard yake ilivyo

Mbunifu Kenneth Joseph Mwangoka akiwa katika pozi

Gari hilo linaloonekana kwa mbele

Kishoka napiga hivi

Bomba la kutolea moshi ndilo hili

Watu wakilishangaa gaari hilo

Umeona vitendea kazi vyake

Usukani wake ni mbao tu kweli msimu ni mali

Muonekano wa gari hilo kwa nyuma

rivasi kama kawa

TANZANIA imejaliwa watu wenye vipaji na ujuzi mkubwa katika nyanja ya Sayansi na Teknolojia ila kuna vitu vidogo vinavyowakwaza kusimama na kwenda sambamba na wataalam wa mataifa mengine ambao wapo mbali katika suala la vipaji na ubunifu.
Mifano michache ni watu wanaomudu kutengeneza magobole, mashine mbalimbali na vitu vingine na hata wabunifu wa mrusho wa matangazo ya radio, ambao badala ya kuwezeshwa hupata vikwazo ikiwamo kunaswa na vyombo vya dola na kufunguliwa mashtaka ilihali wangeweza kutumika kuitangaza Tanzania.
Hapo juu ni mmoja wa wabunifu wa Kitanzania aliyeweza kutengeneza gari ambalo alitumia muda wa miezi sita kulikamilisha kwa kuokoteza vifaa na kulipambana kiasilia kwa kutumia malighafi ya misitu.
Majina yake kamili ni Kenneth Joseph Mwangoka ambaye alikuwa moja ya vivutio katika Maonyesho ya Biashara ya Sabasaba kwa ubunifu wa gari hilo linalotumia injini ya Toyota S1na kuongeza ubunifu wao kiasi kwamba gari hilo lililomgharimu kiasi cha Sh Milioni 8.6 kutembea kutoka sehemu mbalimbali nchini.
Mwangoka anayeishi Iringa, anasema lengo lake ni kuhakikisha anakuja kutengeneza vitu zaidi ya gari hilo la aina yake.

Bingwa wa RCL, zitakazopanda FDL kufahamika leo


BINGWA wa Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) na timu tatu zitakazopanda Ligi Daraja la Kwanza (FDL) zinatarajiwa kufahamika leo wakati timu nne zilizofanikiwa kutinga Nusu Fainali za RCL zitakaporudiana katika viwanja viwili tofauti .
Friends Rangers ya jijini Dar es Salaam iliyodunguliwa bao 1-0 na Polisi Jamii ya Mara itakuwa dimba la nyumbani la Azam Complex, Chamazi katika pambano la marudiano ambapo kama itafanikiwa kulipa kisasi na kushinda kwa idadi kubwa itakata tiketi ya kupanda daraja la kwanza.
Mshindi yoyote wa mechi hiyo ya leo inayotarajiwa kuwa ngumu, itaungana na timu mbili zitakazokuwa nazo uwanjani leo kwenye uwanja wa Kambarage Shinyanga kati ya Kimondo Sc ya Mbeya na Stand United Fc ambazo zimeshajihakikisha kupanda daraja ila zinawania ubingwa wa ligi hiyo ya RCL.
Timu hizo mbili za Stand United na Kimondo zitarudiana kuwania ubingwa, huku Kimondo ikiwa mbele kwa ushindi wa bao 1-0 iliyopata katika mchezo wa kwanza uliocherzwa kwenye uwanja wa
Timu hizo sasa zitacheza Jumapili (Julai 14 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamazi. Polisi Jamii ilishinda bao 1-0 mechi ya kwanza iliyochezwa Julai 6 mwaka huu Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine ya Mbeya.

Wanajeshi 7 wa Tanzania wauwawa Darfur

WANAJESHI saba wa Tanzania, ambao ni miongoni mwa kikosi cha Umoja wa Mataifa, cha kulinda amani katika jimbo la Darfur nchini Sudan, wanadaiwa kuwa wameuawa.
Taarifa zilizolifikia gazeti hili jana zilisema kwamba wanajeshi hao wa Tanzania, wamekufa kutokana na mashambulizi yaliyofanywa na waasi wanaopigana na Serikali.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, miili yao wanajeshi hao bado ipo nchini Sudan ikisubiri taratibu za kusafirishwa kuletwa nchini.
Hii ni mara ya kwanza kuripotiwa kwa idadi kubwa ya wanajeshi wa Tanzania wanaolinda amani katika nchi mbalimbali kufa kwa wakati mmoja.
Agosti mwaka jana wanajeshi watatu wa Tanzania huko Darfur waliripotiwa kuuawa kwenye tukio kama hilo.
Msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) , Kanali Kapambala Mgawe alipoulizwa kwa njia ya simu kuhusu vifo vya wanajeshi wa Tanzania huko Darfur, alisema kuwa naye amesikia, lakini hana taarifa rasmi kwa mujibu wa taratibu za kiofisi.
Hii ni mara ya pili kwa wanajeshi wa Tanzania kuuawa katika Jimbo la Darfur, ambapo Agosti mwaka jana, Kanali Mgawe alinukuliwa na vyombo vya habari akithibitisha kutokea kwa vifo vya askari watatu ambao gari lao lilizolewa na maji walipokuwa wakivuka mto uliokuwa umefurika maji.
Kanali Mgawe aliwataja askari hao kuwa ni Sajini Julius Chacha, Sajini Anthony Daniel na Koplo Yusuph Said na kwamba askari wengine walinusurika baada ya kuogolea.
Tanzania ina askari 850 kwenye kikosi cha Umoja wa Mataifa cha Kulinda Amani jimbo la Darfur, ambao ni sehemu ya askari 1,081 wa kulinda amani katika jimbo la Darfur.
Wanajeshi hao wa Tanzania wametawanywa kwenye miji ya Khor Abeche na Muhajeria kusini mwa Darfur.
Aprili mwaka huu Tanzania ilipeleka wanajeshi wa kulinda amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), kupambana na kikundi cha waasi wa nchi hiyo M23 kinachopigana kuiangusha serikali ya DRC.
Majeshi ya Tanzania yalipelekwa kulinda amani chini ya Umoja wa Mataifa. Tanzania inaungana na nchi za Afrika Kusini na Malawi kukamilisha kikosi cha wanajeshi 3,000. Tanzania imepeleka wanajeshi 850.

MWANANCHI 

NB: Taarifa ambazo MICHARAZO imezipata asubuhi zinasema kuwa Jeshi linatarajiwa kutoa taarifa rasmi juu ya tukio hilo la Darfur saa 3 asubuhi katika Makao Makuu ya Jeshi hilo Upanga, Dar es Salaam.

Rais Kikwete awatunuku Maafisa wa JWTZ

Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiingia katika uwanja wa gwaride wa Chuo Cha Mafunzo ya Kijeshi (TMA) Monduli, Arusha, tayari kwa kutunuku kamisheni kwa Maafisa wa JWTZ jana Julai 13. Pamoja naye ni Mkuu wa Chuo hicho Meja Jenerali V.K. Mritaba. Jumla ya wahitimu 205, wakiwemo wanawake 25, wametunukiwa kamisheni na kuwa Luteni Usu, ambapo wahitimu wawili ni wa kutoka Uganda na Visiwa vya Shelisheli.
 Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua  gwaride katika  Chuo Cha Mafunzo ya Kijeshi (TMA) Monduli, Arusha, kabla ya kutunuku kamisheni kwa Maafisa wa JWTZ  jana Julai 13.
 Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akitunuku kamisheni kwa maafisa katika Chuo cha  Cha Mafunzo ya Kijeshi (TMA) Monduli, Arusha, kabla ya kutunuku kamisheni kwa Maafisa wa JWTZ  jana Julai 13. Jumla ya wahitimu 205, wakiwemo wanawake 25, wametunukiwa kamisheni na kuwa Luteni Usu, ambapo wahitimu wawili ni wa kutoka Uganda na
Visiwa vya Shelisheli.
Meza kuu wakati wa sherehe za  kutunuku kamisheni kwa Maafisa wa JWTZ  jana Julai 13. Jumla ya wahitimu 205, wakiwemo wanawake 25, wametunukiwa kamisheni na kuwa Luteni Usu, ambapo wahitimu wawili ni wa kutoka Uganda na Visiwa vya Shelisheli.

Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akimpa zawadi  Ofisa Kadet  Ngodoke kwa kuibuka mwanafunzi bora wa jumla mwaka huu katika Chuo Cha Mafunzo ya Kijeshi (TMA) Monduli, Arusha, kabla ya kutunuku kamisheni kwa Maafisa wa JWTZ  jana Julai 13. Jumla ya wahitimu 205, wakiwemo wanawake 25, wametunukiwa kamisheni na kuwa Luteni Usu, ambapo wahitimu wawili ni wa kutoka Uganda na Visiwa vya Shelisheli.
Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akimpa zawadi Ofisa Kadet  D.G.L. Wong- Pool toka Visiwa vya Ushelisheli kwa kuibuka mwanafunzi bora wa kigeni wa jumla mwaka huu katika Chuo Cha Mafunzo ya Kijeshi (TMA) Monduli, Arusha, kabla ya kutunuku kamisheni kwa Maafisa wa JWTZ jana Julai 13. Jumla ya wahitimu 205, wakiwemo wanawake 25, wametunukiwa kamisheni na kuwa Luteni Usu, ambapo wahitimu wawili ni wa kutoka Uganda na Visiwa vya Shelisheli.
Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akiongea na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange baada ya sherehe za kutunuku kamisheni kwa Maafisa wa JWTZ  jana Julai 13. Jumla ya wahitimu 205, wakiwemo wanawake 25, wametunukiwa kamisheni na kuwa Luteni Usu, ambapo wahitimu wawili ni wa kutoka Uganda na Visiwa vya Shelisheli.

Kim akiri Stars imefungwa kizembe

Kocha Kim Poulsen (Kati)
KOCHA Mkuu wa timu ya taifa, Taifa Stars, Kim Poulsen amesema uzembe uliofanywa na wachezaji wake katika pambano lao la jana dhidi ya Uganda The Cranes ndiyo iliyowaponza kupoteza mchezo huo wa awali wa kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN).Stars ilipoteza mchezo huo kwa kulala bao 1-0 lililofungwa katika kipindi cha pili na nyota wa the Cranes anayeichezea SC Villa, Dennis Iguma na kuzima tambo za Stars kwamba wangeishikisha adabu wapinzani wao hao kutokana na asilimia kubwa ya kikosi chao ni kile kile kilichokuwa kikiwania fainali za Dunia 2014.
kiri kwamba vijana wake hawakustahili kupoteza mechi
Akizungumzia matokeo hayo baada ya mchezo huo, Kocha wa Stars, Kim Poulsen amesema mpira wa miguu ni mchezo wa kufunga mabao ambapo timu ilipata nafasi nzuri katika dakika ya kwanza tu lakini ilishindwa kuibadili kuwa bao.
“Uganda walitengeneza nafasi moja tu katika kipindi cha kwanza wakati sisi tulikuwa nazo kadhaa. Kipindi cha pili tuliwapa nafasi wakafunga bao lao. Lakini kwa kifupi kama wao wameweza kufunga hapa (Dar es Salaam), hata sisi tunaweza kufunga Kampala,” amesema Kim akizungumzia nafasi ya timu yake kusonga mbele.
Timu hizo zitarudiana jijini Kampala kati ya Julai 26 na 27 mwaka huu ambapo mshindi ndiye atakayepata tiketi ya kwenda kwenye fainali za tatu za CHAN zitakazofanyika Afrika Kusini. Stars ilicheza fainali za kwanza za CHAN zilizofanyika mwaka 2009 nchini Ivory Coast.
Katika hatua nyingine baadhi ya wadau wa kandanda walikiponda kikosi cha Stars kwa mchezo wa jana kwa kudai ni kama hawakujua walikuwa wanatakiwa kufanya nini uwanjani.
Kipa wa zamani wa kimataifa wa Simba ambaye kwa sasa ni kocha, Spear Mbwembwe alisema hajawahi kuona Stars ikicheza kichovu kama mechi ya jana, akisema kwa mtazamo wake ni wachezaji wawili tu waliokuwa wakitimiza wajibu ambao ni winga Mrisho Ngassa na beki Aggrey Morris.
"Wengine hawakuwa mchezoni kabisa na kibaya zaidi mabadiliko yaliyofanywa ya kutolewa kwa Nyoni na kuingiwa Luhende wakati nilidhani Kapombe na Nyoni wangebadilishana nafasi tu na tumeona kilichotokea," alisema.
Mbwembwe alisema ni lazima Stars ifanye kazi ya ziada kwa mechi ya marudiano aliyoikatia tamaa kwa madai haoni kitakachobadilisha matokeo ikizingatiwa wachezaji ni wale wale na kocha yule yule tena ugenini.
"Mie nadhani kuna haja TFF ikafanya jambo moja la muhimu, lazima Poulsen apewe kocha ambaye yupo 'active', sidhani kama Sylveter Marsh anamfaa kocha wakati kwa miaka miwili sasa hana timu yoyote anayofundisha," alisema Mbwembe.
Kocha huyo alisema tatizo la kubebana ndilo linalogharimu ska la Tanzania kusonga mbele licha ya mikakati mizuri na kocha bora iliyonayo Tanzania, yaani Kim Poulsen kutoka Denmark.
Kipigo cha jana ni cha tatu mfululizo kwa Tanzania baada ya vipigo viwili vya awali toka Morocco na Ivory Coast walioumna nao katika mechi za marudiano ya kuwania Fainali za Kombe la Dunia za Brazili.

Wajumbe TFF wapitisha Katiba Mpya


Mwakilishi wa FIFA katika mkutano huo wa TFF, James Johnson akihutubia

Rais Leodger Tenga na Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah wakiwa na Mwakilishi wa FIFA, James Johnson,


 

Baadhi ya Wajumbe wa TFF katika mkutano huo

Na Boniface Wambura
WAJUMBE wa Mkutano Mkuu Maalumu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) uliofanyika jana (Julai 13 mwaka huu) wamepitisha marekebisho ya Katiba yake, hivyo mchakato wa uchaguzi unatarajia kuanza wakati wowote.

Wajumbe zaidi ya 100 walihudhuria Mkutano huo uliofanyika ukumbi wa NSSF Waterfron, Dar es Salaam na kufunguliwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera aliyewataka wajumbe kuhakikisha kiwango cha mpira wa miguu nchini kinakuwa.

Mkutano huo uliokuwa chini ya uenyekiti wa Rais wa TFF, Leodegar Tenga umefanya marekebisho ya Katiba kutokana na maelekezo ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA). James Johnson kutoka Idara ya Wanachama ndiye aliyeiwakilisha FIFA katika mkutano huo.

Aprili mwaka huu FIFA ilisimamisha mchakato wa uchaguzi wa TFF, na kuagiza kwanza yafanyike marekebisho ya Katiba ili kuingiza Kamati ya Maadili, na Kamati ya Rufani ya Maadili ambavyo ndivyo watashughulikia matatizo ya kimaadili kwa familia ya mpira wa miguu nchini.

Mbali ya kamati hizo, mabadiliko hayo pia yametengeneza ngazi mbili za kushughulikia masuala ya kinidhamu ambazo ni; Kamati ya Nidhamu na Kamati ya Rufani ya Nidhamu.

Kamati ya Utendaji ya TFF chini ya Rais Tenga itakutana kesho (Julai 14 mwaka huu) kwa ajili ya kuteua wajumbe watakaounda Kamati hizo ili kuruhusu kuanza mchakato wa uchaguzi ambao FIFA iliusimamisha hadi vitakapoundwa vyombo hivyo.