Kagera Sugar walioifyatua JKT Ruvu |
Kagera ilipata ushindi huo kwenye uwanja wa Kambarage-Shinyanga baada ya kuilaza maafande hao wa JKT kwa bao 1-0.
Ushindi huo ni wa pili mfululizo kwa timu hiyo kwenye uwanja huo tangu walipohamia wakitokea CCM Kirumba walipokuwa wakiambulia vipigo mfululizo.
Kwa ushindi huo Kagera imefikisha pointi 21 na kushika nafasi ya tatu, pointi nne nyuma ya Azam na Yanga wanaongoza wakiwa na pointi 25 ingawa timu hizo mbili zina michezo miwili mikononi zaidi ya Kagera.
Kagera wenyewe wamecheza michezo 15 wakati Azam na Yanga wamecheza mechi 13 tu ingawa katikati ya wiki hii watakuwa viwanja kucheza viporo vyao.
Simba wamechupa nafasi ya nne baada ya kuisulubu Polisi Moro mabao 2-0 uwanja wa Jamhuri Morogoro kwa kufikisha pointi 20 baada ya mechi 14.
MSIMAMO LIGI KUU TZ BARA 2014-2015
P W D L F A GD Pts
01. Yanga 13 07 04 02 15 07 08 25
02. Azam 13 07 04 02 22 12 10 25
03. Kagera Sugar 15 05 06 04 12 11 01 21
04. Simba 14 04 08 02 15 11 04 20
05. Mtibwa Sugar 14 04 07 03 15 14 01 19
06. Polisi Moro 15 04 07 04 12 13 -1 19
07. Coastal Union 15 04 07 04 11 10 01 19
08. JKT Ruvu 15 05 04 06 14 15 -1 19
09. Ruvu Shooting 14 05 04 05 10 11 -1 19
10. Mbeya City 14 04 05 05 09 11 -2 17
11. Ndanda Fc 15 04 04 07 13 18 -5 16
12. Stand Utd 15 03 06 06 13 18 -5 15
13. Mgambo JKT 13 04 02 07 07 15 -8 14
14. Prisons 13 01 08 04 10 12 -2 11
Wafungaji:
8- Didier Kavumbagu(Azam)
6- Samuel Kamuntu (JKT Ruvu), Ame Ali (Mtibwa), Rashid Mandawa (Kagera Sugar)
5-Danny Mrwanda (Yanga), Kipre Tchetche (Azam)
4- Rama Salim (Coastal), Simon Msuva (Yanga), Emmanuel Okwi (Simba), Nassor Kapama (Ndanda), Heri Mohammed (Stand Utd)
3- Ally Shomari (Mtibwa), Jacob Massawe (Ndanda),Frank Domayo (Azam), Malimi Busungu (Mgambo), Achidilele (Stand Utd), Atupele Green (Kagera)