STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, March 5, 2014

Yanga kuivaa Alh Ahly J'2 usiku, kikosi kuondoka leo usiku

Kikosi cha Yanga kilichoibana Al Ahly kwa kuilaza 1-0 jijini Dar jumamosi iliyiopita
IMETHIBITIKA kuwa, wawakilishi pekee wa Tanzania kwenye mashindano ya Klabu Bingwa Barani Afrika timu ya Young Africans itacheza mchezo wa marudiano siku ya jumapili jijini Cairo dhidi ya timu ya Al Ahly ukiwa ni mchezo utakaotoa picha halisi ni timu gani itasonga mbele katika hatua ya 16 bora.
Ikiwa ni takribani siku tano kabla ya kufanyika mchezo wenyewe wenyeji Al Ahly wameshindwa kuweka wazi ni uwanja gani utakaotumika kwa ajili ya mchezo huo huku Meneja wa klabu hiyo Abdoulazi akisema huenda mchezo ukachezwa jijini Cairo au Alexandria na kusema majibu kabili yatapatikana siku ya jumatano mchana.
Wenyeji wameiandalia timu ya Young Africans kufikia katika Hoteli ya Baron iliyopo maneneo ya Uwanja wa michezo wa kimataifa Cairo huku pia wakiipangia timu kufanya mazoezi katika uwanja wao uliopo eneno la Nasri City.
Katika mchezo wa awali uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Young Africans ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Al Ahly ambao ni mabingwa watetezi wa kombe hilo shukrani kwa bao la Nahodha wa timu Nadir Haroub "Cannavaro" aliyetikisha nyavu dakika ya 82 ya mchezo.
Mara baada ya mchezo huo kikosi cha mholanzi Hans Van der Pluijm kiliingia kambini jana jioni katika hotel ya Ledger Bahari Beach tayari kwa maandalizi ya mchezo marudiano ambapo timu imeendelea kufanya mazoezi katika uwanja wa Boko Beach Veterani.
Kuelekea mchezo huo wa jumamosi tayari uongozi wa Young Africans ulishaanza kufanya maandalizi ya safari ambayo inatarajiwa kuwepo kabla ya mwisho mwa wiki hii huku msafara ukitarajiwa na kuwa idadi ya watu 35, wakimwemo viongozi, benchi la ufundi pamoja na wachezaji 19.
Hali ya wachezaji ni nzuri, kiafya, fikra na morali ya kuelekea mchezo wenyewe bado ni kubwa kwani bench la ufundi na wachezaji wanaamini maandalizi wanayoyafanya yatasaidia kupelekea kupata ushindi katika mchezo huo na kuweza kusonga mbele katika hatua ya 16 bora.
Baadhi ya wachezaji wanaotarajiwa kuondoka usiku wa leo kuifuata Al Ahly ni makipa Deogratius Munishi 'Dida' na Juma Kaseja, Nadir Haroub 'Cannavaro, David Luhende, Oscar Joshua, Kelvin Yondani, Simon Msuva, Mrisho Ngasa, Haruna Niyonzima, Didier Kavumbagu, Juma Abdul, Frank Domayo, Mbuyu Twite, Rajab Zahir na Said Bahanuzi.
Okwi na Kiiza, wataungana na kikosi hicho Alhamisi wakitokea Lusaka, walipo na timu yao ya Taifa ya Uganda ( The Cranes) ambayo jana ilikuwa inacheza na Zambia (Chipolopolo) mechi ya kimataifa ya kirafiki.
Yanga inahitaji ushindi au sare ya aina yoyote ili iweze kusonga mbele kwenye michuano hiyo.
Maandalizi ya sehemu ya kambi ambapo timu itafikia jijini Cairo tayari yanaendelea vizuri kwa kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania ambapo kwa upande wa klabu ya Young Africans Afisa Habari Baraka Kizuguto tayari yupo nchini Misri kwa siku ya pili akiendelea kuweka mambo sawa.
Mchezo wa jumapili unatarajiwa kufanyika katika uwanja wa Arab Contractors uliopo jijini Cairo huku mechi hiyo ikichezwa bila ya mashabiki kufuatia Serikali ya Misri kuzuia mashabiki wa soka kutokana na mashabiki hao kufanya vurugu katika mchezo wa Fainal ya Super Cup dhidi ya CS Sfaxien na kupelekea askari kadhaa kujeruhiwa.

Wawili waongeza mkataba Arsenal na kumpa ahueni Wenger

350594_heroaBaada ya kupoteza mechi yake iliyopita ya ligi kuu ya England klabu ya Arsenal leo imewapa habari nzuri mashabiki wake baada ya kutangaza wachezaji wao wawili wameongeza mikataba ya kuendelea kuitumikia klabu hiyo.
Nahodha wa timu hiyo Mjerumani Per Mertesacker na kiungo Thomas Rosicky wote wametangazwa kuongeza mikataba yao.
“Tunayo furaha kutangaza kwamba Mertesacker na Rosicky wameongeza mikataba ya kuendelea kuwepo hapa,”  Arsene Wenger aliuambia mtandao rasmi wa klabu hiyo.
“Ni wachezaji wazuri na wenye uzoefu, na wameshaonyesha kila siku kwamba wanaweza kucheza kwenye level ya juu.’ – alimaliza Wenger.
Klabu hiyo hata hivyo haijatoa namba ya miaka kamili ya muda wa mikataba mipya.

Mourinho 'aizuga' Mancehster City mbio za ubingwa England

Jose Mourhino (kulia) na kocha wa Manchester City Manuel Pellegrini  wakisalimiana enzi wakiwa Hispania
LONDON, England
KOCHA wa Chelsea, Jose Mourinho amesema watakuwa wanabadilisha nafasi za mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England na Manchester City kutokana na kikosi hicho cha Manuel Pellegrini kuwa na mechi mkononi.
Miamba hiyo ya Stamford Bridge inaizidi City kwa pointi sita baada ya mwishoni mwa wiki kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Fulham, lakini mabingwa wa Kombe la Ligi (Capital One Cup) wana mechi mbili mkononi na wastani mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa kuliko Chelsea.
Pellegrini anawinda mafanikio makubwa kwa kutwaa makombe matatu baada ya kuiongoza City kushinda 3-1 dhidi ya Sunderland Jumapili kwenye Uwanja wa Wembley na kutwaa ubingwa wa Capital One Cup, jambo ambalo Mourinho anasisitiza kuwa kocha huyo raia wa Chile yupo katika nafasi nzuri ya mbio za ubingwa.
"Ninapenda kuwa na bahati mkononi, na City tu ndiyo yenye bahati mkononi mwake," Mourinho alisema. "Kama nitashinda kila mchezo hadi mwishoni mwa msimu, zote 10 – kama hatutaweza labda hatutakuwa mabingwa.
"Kama [City] itashinda mechi zote 12 ilizo nazo, watakuwa mabingwa. Wana bahati mkononi mwao."

Wavuvi wawili wauwawa kwa risasi wakivua samaki mtoni

Na   Walter Mguluchuma, Katavi
WATU wawili  James  Mauto  21 Mkazi wa Kijiji  cha  Ugala Wilaya ya Mlele   na  January  Marekani  18 Mkazi wa Kijiji  cha Mtapenda  Tarafa ya Nsimbo Wilaya ya Mlele  mkoa  wa Katavi wameuwawa  kwa kupigwa  risasi   na Askari wa Geme Reserve wakati  wakiwa wanavua  samaki  ndani ya   Hifadhi  ya Pori la akiba la Ugala na mwenzao mmoja kujeruhiwa  kwa Risasi sehemu ya mbavu zake
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa  wa Katavi Dhahiri Kidavashari   tukio hilolilitokea hapo  Februari  28 mwaka huu majira ya saa  tisa Alasiri  ndani ya Hifadhi ya pori  la akiba la Ugala Wilayani Mlele Mkoa wa Katavi 

Alieleza siku hiyo ya tukio    James Mauti  na  Januari Marekani walikuwa wakivua samaki ndani ya mto Ugala uliko kwenye  Hifadhi  ya pori la akiba la ugala wakiwa na mwenzao mmoja  aitwaye  Seif Juma  40  Mkazi wa kijiji  cha Mtapenda  Tarafa ya Nsimbo Wilaya ya Mlele
Kamanda Kidavashari alisema  wakati wakiwa wanaendelea kuvua samaki ndani ya mto huo  alitokea Askari  wa Geme Reserve  ambae alikuwa amevalia sare   huku akiwa na silaha  bunduki  ambayo haikuweza kufahamika aina yake
Alisema Askari huyo aliwaamuru  wavuvi  hao wajisalimishe kwake  hata hivyo wavuvi  hao waliokuwa wakiendelea na uvuvi  kufutia amri hiyo ya Askari  waliamua kutupa nyavu zao walizokuwa wakivulia samaki  na kukimbia mbio  kila mmoja sehemu yake
Ndipo Askari huyo  alipoanza  kuwarushia  risasi  wavuvi  hao  na kuwauwa  kwa risasi James Mauto   na Januari  Marekani  na kumjeruhi Seif  Juma sehemu za  mgongoni na kwenye mbavu
Majeruhi  ambae ni Seif  Juma  alifanikiwa  kufika katika kijiji  cha Ugala  na  kutoa taarifa kijijini hapo kwa uongozi wa Serikali ya Kijiji juu ya tukio hilo  na aliweza kupatiwa msaada wa kukimbizwa katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda kwa ajiri ya matibabu
Kamanda Kidashari  alieleza  kuwa mvuvi huyo  ambae ni majeruhi  kwa kuhofia kukamatwa na kuhojiwa  na polisi  baada ya kufikishwa  Hospitali alitoroka  na mpaka sasa  haijajulikana mahari alipo na anatibiwa wapi majeraha yake ya risasi
Alisema  kutokana na tukio hilo kuhusishwa  na Askari  wa Geme  Reserve  katika hifadhi  hiyo  jeshi la polisi Mkoa wa Katavi  linawasiliana  na mkuu wa  kikosi cha  wanyama pori  mkoa wa Tabora  ambako ndio  walikuwa wametoka Akari waliohusika na tukio la mauwaji hayo
Alifafanua  kuwa  tayari mkuu wa Kikosi hicho  cha wanyama pori  ametuma kikosi chake kwenye eneo hilo la tukio  ilikubaini  ni Askari  gani waliokuwa kwenye  doria  eneo hilo  ili kuwabaini  na kisha  sheria ichukuwe mkondo wake  kwa askari  aliyehusika au waliohusika  kwa tukio la mauwaji hayo ya kinyama kwa binadamu hao.
Pambana na Climate Change

Petr Cech hakamatiki Tuzo ya Mchezaji Bora Czech

KIPA wa klabu ya Chelsea ya England, Petr Cech hashikiki katika Tuzo yta Mchezaji Bora wa Mwaka wa Jamhuri ya Czech baada ya kutangazwa tena kuwa mshindi wa mwaka 2013 ikiwa ni mara yake ya sita mfululizo kati ya saba aliyonyakua tuzo hiyo.
Cech (31) ameshinda tuzo hiyo kwa mara ya sita baada ya kupigiwa kura nyingi kutoka kwa wachezaji, makocha, viongozi wa shirikisho la soka na waandishi wa habari.
Kiungo wa Arsenal, Tomas Rosicky ameshika nafasi ya pili wakati mchezaji wa Freiburg, Vladimir Darida akishika ya tatu.
Kipa huyo ndiye tegemeo wa Chelsea inayopigana kunyakua ubingwa kwa msimu huu ikiwa chini na kocha aliyewahi kuipa mafanikio huko nyuma, Jose Mourinho.

Taifa Stars dimbani leo Namibia bila Samatta, Ulimwengu

Taifa Stars
Mbwana Samatta (kulia) atakayelikosa pambano la leo nchini Namibia

TIMU ya Taifa (Taifa Stars), itawakosa nyota wake wanaocheza soka nje ya nchi katika mechi ya kirafiki ya Kimataifa dhidi ya Namibia itakayochezwa leo kwenye Uwanja wa Sam Nujoma jijini Windhoek nchini humo.
Hatua hiyo inakuja baada ya Shirikisho la Soka nchini (TFF) kushindwa kupata usafiri wa uhakika wa kuwarejesha ndani saa 24 katika klabu yao, washambuliaji Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu wanaoichezea TP Mazembe ya DR Congo pamoja na Mwinyi Kazimoto anayeichezea Al-Makhiya ya Qatar.
Stars ya TFF (iliyoteuliwa na shirikisho hilo badala ya kocha), iliondoka nchini juzi alfajiri ikiwa chini ya Kaimu Mkurugenzi wa Ufundi wa shirikisho hilo, Salum Madadi, aliyeshika kwa muda nafasi ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Mdenmark Kim Poulsen, ambaye alitimuliwa wiki iliyopita.
Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura, aliliambia NIPASHE jijini Dar es Salaam jana kuwa, Stars itashuka dimbani bila ya wachezaji wake wanaosakata kabumbu la kulipwa nje ya nchi, Ulimwengu, Samata  na Kazimoto.
Alisema wachezaji hao wanakosekana baada ya TFF kukosa ndege ya kuwarudisha katika timu zao ndani ya saa 24 baada ya mechi hiyo kumalizika kama Kanuni za Fifa zinavyoelekeza.
"Ndege tulizopata zinapita Nairobi kwenda Lubumbashi Machi 8, wakati Samata na Ulimwengu wana mechi muhimu ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwishoni mwa wiki," alisema Wambura.
Aidha, Wambura alisema Stars itawakosa wachezaji Hassan Mwasapili na Edward Charles ambao wamekosa hati za kusafiria (passport).
Kutokana na kukwama kwa nyota hao, Stars sasa imebaki na wachezaji 15 wakiwamo makipa Mwadini Ally (Azam) na Shaban Kado (Coastal) aliyeitwa kuziba nafasi ya Ivo Mapunda (Simba) aliyefiwa na baba yake mzazi wiki iliyopita.
Mabeki ni Erasto Nyoni, Said Moradi na Aggrey Morris (Azam), Abdi Banda (Coastal) na Michael Aidan (Ruvu Shooting), wakati viungo ni Amri Kiemba (Simba), Jonas Mkude (Simba) na Himid Mao kutoka Azam FC.
Washambuliaji ni Athanas Mdamu (Alliance Mwanza), Haruna Chanongo (Simba), Khamis Mcha (Azam), Ramadhan Singano (Simba) na Juma Luizio kutoka Mtibwa Sugar.