Na Walter Mguluchuma, Katavi
WATU
wawili James Mauto 21 Mkazi wa Kijiji cha Ugala Wilaya ya Mlele
na January Marekani 18 Mkazi wa Kijiji cha Mtapenda Tarafa ya
Nsimbo Wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi wameuwawa kwa kupigwa risasi
na Askari wa Geme Reserve wakati wakiwa wanavua samaki ndani ya
Hifadhi ya Pori la akiba la Ugala na mwenzao mmoja kujeruhiwa kwa
Risasi sehemu ya mbavu zake
Kwa
mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari
tukio hilolilitokea hapo Februari 28 mwaka huu majira ya saa tisa
Alasiri ndani ya Hifadhi ya pori la akiba la Ugala Wilayani Mlele Mkoa
wa Katavi
Alieleza
siku hiyo ya tukio James Mauti na Januari Marekani walikuwa
wakivua samaki ndani ya mto Ugala uliko kwenye Hifadhi ya pori la
akiba la ugala wakiwa na mwenzao mmoja aitwaye Seif Juma 40 Mkazi wa
kijiji cha Mtapenda Tarafa ya Nsimbo Wilaya ya Mlele
Kamanda
Kidavashari alisema wakati wakiwa wanaendelea kuvua samaki ndani ya
mto huo alitokea Askari wa Geme Reserve ambae alikuwa amevalia sare
huku akiwa na silaha bunduki ambayo haikuweza kufahamika aina yake
Alisema
Askari huyo aliwaamuru wavuvi hao wajisalimishe kwake hata hivyo
wavuvi hao waliokuwa wakiendelea na uvuvi kufutia amri hiyo ya Askari
waliamua kutupa nyavu zao walizokuwa wakivulia samaki na kukimbia
mbio kila mmoja sehemu yake
Ndipo
Askari huyo alipoanza kuwarushia risasi wavuvi hao na kuwauwa
kwa risasi James Mauto na Januari Marekani na kumjeruhi Seif Juma
sehemu za mgongoni na kwenye mbavu
Majeruhi
ambae ni Seif Juma alifanikiwa kufika katika kijiji cha Ugala na
kutoa taarifa kijijini hapo kwa uongozi wa Serikali ya Kijiji juu ya
tukio hilo na aliweza kupatiwa msaada wa kukimbizwa katika Hospitali ya
Wilaya ya Mpanda kwa ajiri ya matibabu
Kamanda
Kidashari alieleza kuwa mvuvi huyo ambae ni majeruhi kwa kuhofia
kukamatwa na kuhojiwa na polisi baada ya kufikishwa Hospitali
alitoroka na mpaka sasa haijajulikana mahari alipo na anatibiwa wapi
majeraha yake ya risasi
Alisema
kutokana na tukio hilo kuhusishwa na Askari wa Geme Reserve katika
hifadhi hiyo jeshi la polisi Mkoa wa Katavi linawasiliana na mkuu
wa kikosi cha wanyama pori mkoa wa Tabora ambako ndio walikuwa
wametoka Akari waliohusika na tukio la mauwaji hayo
Alifafanua
kuwa tayari mkuu wa Kikosi hicho cha wanyama pori ametuma kikosi
chake kwenye eneo hilo la tukio ilikubaini ni Askari gani waliokuwa
kwenye doria eneo hilo ili kuwabaini na kisha sheria ichukuwe
mkondo wake kwa askari aliyehusika au waliohusika kwa tukio la
mauwaji hayo ya kinyama kwa binadamu hao.
Pambana na Climate Change
No comments:
Post a Comment