Yanga Kila la Heri katika mechi yenu ya kesho dhidi ya FC Platinum |
WAKATI Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu wa nchini TFF, Jamal Malinzi ikiwatakia
kila la kheri wawakilishi pekee wa Tanzania kwenye kombe la Shirikisho Afrika, Yanga, kikosi cha timu hiyo kimeondoka leo nchini kuelekea Zimbabwe.
Yanga wameondoka leo majira ya asubuhi kuwahi pambano lao la kesho dhidi ya FC Platinum litakalochezwa kwenye Uwanja
Mandava uliopo Gweru Bulawayo.
Rais wa TFF, Jamal Malinzi
amesema Young Africans hawapaswi kubweteka na ushindi walioupata awali
wa mabao 5-1, kikubwa wanapaswa kwenda kupambana kusaka ushindi ugenini
ili kuweza kufuzu kwa hatua inayofuata ya timu 16.
Endapo
Young Africans itafanikiwa kuwatoa FC Platinum itaingia katika hatua ya
16 bora na itakutana na mshindi kati ya timu za Benifica de Luanda ya
Angola au Etoile du Saleh ya Tunisia.
Yanga wakiwa na ari kubwa wameondoka leo nchini na kuahidi kuendelea kuwapa raha watanzania kwa kupata ushindi ugenini mbele ya wachimba madini hao wa Bulawayo.
Yanga inahitaji sare ya aina yoyote na hata kama itapoteza mechi hiyo ya marudiano chini ya mabao manne inaweza kusonga mbele kwa ajili ya raundi ya pili.
Kikosi cha wachezaji 18 na viongozi saba wameondoka wakisema wanaenda kupambana kuhakikisha Tanzania inaendelea kuwepo miongoni mwa wawakilishi wa michuano ya kimataifa baada ya Azam, KMKM na Polisi kung'oka mapema.