|
Mkurugenzi wa Zugo Gold Mining na Mwakilishi wa Wanawake, Maendeleo ya Vijana na Ajira kwa Wachezaji wa Shirikisho na Ngumi za Ridhaa Tanzania (*BFT), Zuwena Idd Kipingu akizungumza na wazazi kwenye hafla ya Mahafali ya 35 Shule ya Montesoty Nursery& Primary iliyofanyika leo |
|
Mkurugenzi
wa Zugo Gold Mining na Mwakilishi wa Wanawake, Maendeleo ya Vijana na
Ajira kwa Wachezaji wa Shirikisho na Ngumi za Ridhaa Tanzania (*BFT),
Zuwena Idd Kipingu akizungumza na wazazi kwenye hafla ya Mahafali ya 35
Shule ya Montesoty Nursery& Primary iliyofanyika leo |
|
Baadhi ya wazazi waliohudhuria Mahafali ya 35 ya Shule ya Montesory wakifuatilia maonyesho ya watoto wao |
|
Baadhi ya wazazi waliohudhuria Mahafali ya 35 ya Shule ya Montesory wakifuatilia maonyesho ya watoto wao |
|
Baadhi ya wahitimu wa shule ya Montesory wakionyesha maonyesho ya kitaaluma |
|
Wahitimu wa Montesory wakiimba kwenye sherehe za kuagwa zilizofanyika shuleni hapo mchana wa leo |
|
Wanafunzi wakionyesha michezo yao ya taaluma. Hapa wanaigiza kama wapo darasani na mwalimu wao aliyekaa pembeni kushoto |
|
Ikafuata burudani na kurudi 'magoma' hawa majamaa ni noma |
|
Sabri Omary akionyesha umahiri wa kunengua katima mahafali hayo |
|
Babu na wajukuu zake wakisimuliana hadithi kwa vitendo, Kuku na Bata wakimsikiliza Tembo |
|
Kama Muuguzi vile, mmoja wanafunzi wahitimu wa Montesory akijitambulisha kuwa ni Muuguzi kwa sababu ya kupata elimu...hilo ni onyesho la taaluma |
|
Watoto wakikabidhiwa vyeti na zawadi zao |
SHULE za Montesory na Ulongoni B zilizopo wilaya ya Ilala zimepewa kwa nyakati tofauti misaada ya tani moja ya Saruji sambamba na fedha taslim kwa ajili ya kuboresha majengo ya shule hizo.
Misaada hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa kampuni ya Zugo Gold Mining ambaye pia ni Mwakilishi wa Wanawake na Maendeleo ya Vijana na Ajira kwa Wachezaji wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT), Zuwena Idd Kipingu, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya shule hizo mwishoni mwa wiki.
Akizungumza kwenye mahafali ya 35 ya wanafunzi wa awali wa Shule ya Montesory, Zuwena alisema kwa ajili ya kuhakikisha wanafunzi wanapoa wasaa wa kusoma katika mazingira mazuri anajitolea tani moja ya simenti na Sh,. Mil. 1 kwa ajili ya kuendelez aujenzi wa shule hiyo iliyopo Ilala Boma.
Zuwena aliyemwakilisha Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa Kwa Wote (EOTF), Anna Mkapa katika mahafali hayo kama mgeni rasmi na kutangaza kutoa msaada huo ikiwa ni siku moja tu tangu akabidhi msaada kama huo katika Shule ya Ulongoni B.
"Bila kusubiri kuombwa nimeona majengo yenu hayajamalizika, hivyo najitolea kuwapa tani moja ya saruji na Jumatatu tuwasiliane ili niwakabidhi pamoja na Sh Milioni 2 za vifaa vya michezo na Sh Mil 1 ya kusaidia ujenzi huo," alisema.
Aliongeza kuwa, kama mmoja wa wanawake waliofanikiwa kujiendeleza kimaisha kupitia michezo anawasihi wazazi nchini kutowakataza watoto wao wenye vipaji mbalimbali kujihusisha na vitu vinavyohusiana na vipaji vya ili kuwatengenezea mazingira mazuri ya kujiajiri kupitia fani hizo.
Alisema yeye wakati akiwa mtoto alikuwa akichapwa mno na baba yake kwa kupenda kwake michezo, lakini alikuja kuwa mwanamke wa kwanza kunyakua mkanda mweusi katika karate na taekwondo na kuwa mfanyabishara mkubwa kwa sasa kutokana na fursa aliyopata kupitia kwenye michezo.
"Wazazi wasikazanie watoto wao kusoma tu, pia wawasaidie kuendeleza vipaji vyao kwa nia ya kuwatengenezea ajira wanapokuwa wakubwa," alisema Zuwena.
Katika mahafali hayo jumla ya wanafunzi 75 walihitimu masomo yao ya awali na kukabidhiwa vyeti pamoja na zawadi na mgeni rasmi huyo Zuwena Idd Kipingu, sambamba na kutoa burudani mbalimbali za taaluma na michezo.