STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, May 15, 2015

STARS YAENDELEA KUJIFUA BONDENI








Na Baraka Kizuguto, Afrika Kusini
Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imeendelea na mazoezi katika uwanja wa Olympia Park kujiandaa na mchezo wa fungua dimba dhidi ya timu ya Taifa ya Swaziland.
Kocha mkuu wa timu ya Taifa Stars Mart Nooij amesema vijana wake wanaendelea vizuri na mazoezi, ikiwa leo ni siku ya pili kufanya mazoezi baada ya kufanya mazoezi ya kwanza jana jioni.
Nooii amesema japokuwa kuna hali ya hewa ya baridi katika mji wa Rustenburg, wachezaji wake wameanza kuizoea na kusema kwa kuwa bado kuna zaidi ya masaa 72 kabla ya mchezo wa awali watakua wameshaizoea hali ya hewa.
Kuhusu uwanja wa mazoezi, kocha Nooij amesema hali ya uwanja ni nzuri, uwanja una nyasi nzuri hali inayopelekea kikosi chake kufanya mazoezi katika mazingira mazuri.
Akiongelea mchezo wake wa kwanza wa ufunguzi dhidi ya timu ya Taifa ya Swaziland utakaochezwa siku ya jumatatu, amesema anawajua Swaziland ni timu nzuri, mara ya mwisho katika mchezo wa kirafiki walitoka nao sare, hivyo anawaanda vijana wake kupata ushindi katika mchezo huo.
Kikosi cha Swaziland kina wachezaji mchanganyiko wakiwemo wanaocheza ligi yao ya nyumbani na baadhi wanaocheza soka la kulipwa nchini Afrika Kusini.
Taifa Stars itacheza mchezo wa kwanza dhidi ya Swaziland katika Uwanja wa Olympia Park siku ya jumatatu saa 1.30 usiku kwa saa za huku, sawa na saa 2.30 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

Hapana! Ronaldo Kaongopa? Arukwa fedha za Nepal

http://i.dailymail.co.uk/i/pix/2015/02/08/256E0D7200000578-2944513-Ronaldo_looks_glum_after_being_left_on_the_turf_follow_a_challen-a-31_1423391475170.jpgSHIRIKA la Misaada la Save the Children limekanusha taarifa kuwa Cristiano Ronaldo ametoa msaada ya Euro Milioni 7 kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi nchini Nepal. 
Kauli ya shirika hilo imekuja kufuatia taarifa kuwa Ronaldo mwenye umri wa miaka 30 ametoa kiasi hicho cha fedha kwenda kusaidia waathirika wa tetemeko hilo. 
Katika taarifa ya shirika hilo imedai kuwa, Ronaldo akiwa Balozi wao amekuwa akipaza sauti kueleza matatizo wanayokutana nayo watoto duniani. 
Lakini taarifa hiyo iliendelea kudai kuwa ripoti za hivi karibuni kuwa Ronaldo ametoa fedha kwa shirika hilo la Save the Children kwa ajili ya waathirika wa Nepal sio za kweli. 
Zaidi wa watu 8,000 walifariki dunia kea tetemeko kubwa lililoikumba nchi hiyo Aprili 25 mwaka huu kabla ya lingine kutokea Mei 12 na kuua wengine karibu 110.