STRIKA nyota wa
Barcelona, Luis Suarez amesema ilikuwa ngumu kukubaliana na ukweli wa
kumng’ata beki wa Italia Giorgio Chiellini katika michuano ya Kombe la
dunia nchini Brazil.
Nyota huyo wa kimataifa wa Uruguay aliyejiunga na Barcelona akitokea Liverpool kwa kitita cha Pauni Mil. 75
alifungiwa miezi minne kutokana na tukio hilo.
Akihojiwa strika huyo amesema
alikuwa akiona vigumu kukubali alichokifanya kwani yeye ni binadamu kama
walivyo wengine.
Suarez, 27, amesema alikuwa
hataki kumsikiliza yeyote au kuongea na yeyote kwa sababu alikuwa hataki
kukubaliana na ukweli.
Suarez alimuomba radhi Chiellini Juni 30 zikiwa
zimepita siku sita toka afanye tukio baada ya Uruguay kushinda bao 1-0
dhidi ya Italia, msamaha ambao ulipokelewa na beki huyo na kueleza
matumaini yake kama Shirikisho la Soka Duniani-FIFA lingeweza
kumpunguzia adhabu hiyo.
Kabla kuomba radhi Suarez alikanusha kwa kudai
kuwa aliteleza bahati mbaya na usoni mwa Chiellini na kumuangukia jambo
ambalo lilikuwa kama vichekesho kwani tukio hilo lote lilionekana katika
picha za video.
STRIKA
USILIKOSE
Wednesday, October 15, 2014
Ronaldo alibeba Ureno, Ujerumani bado gonjwa Ulaya
Ronaldo akishangilia bao lake lililoiua Denmark nyumbani kwao |
Wachezaji wa Ireland wakishangilia bao lao la kusawazisha dhidi ya Ujerumani |
Mabingwa wa Dunia, Ujerumani wakihenyeka uwanjani dhidi ya Jamhuri ya Ireland |
Ujerumani inayouguza kichapo cha mabao 2-0 ilichopewa na Poland wikiendi iliyopita ilishindwa kulinda bao lake na kujikuta wakilazimishwa sare ya baoa 1-1 nyumbani na Jamhuri ya Ireland waliochomoa bao 'jioni'.
Ton Kroos aliiandikia wenyeji bao la kuongoza dakika ya 71, lakini wageni walikaza msuli na kulirejesha dakika za nyongeza kupitia John O'shea na kufanya timu hizo kugawana pointi huku Poland wakilazimishwa sare ya mabao 2-2 na Scotland ikiwa nyumbani.
Matokeo ya mechi nyingine ni kwamba Ureno ikiwa ugenini iliizabua Denmark kwa bao 1-0 lililofungwa na nahodha wake Cristioano Ronaldo katika dakika ya lala salama mashabiki wakiamini kuwa timu hizo zimetoka suluhu na kuifanya Ureno kufikisha jumla ya pointi tatu na kushika nafasi ya tatu.
Katika mechi nyingine za michuano hiyo, Gibraltar imeendelea kutoa takrima baada ya kugongwa nyumbani mabao 3-0 na Georgia, San Marino kulazwa mabao 4-0 nyumbani na Uswisi, wakati Visiwa vya Faroe walilala nyumbani pia kwa bao 1-0 kutoka kwa Hungary, Finland ikafa pia nyumbani kwa mabaop 2-0 kw akipigo cha Romania na Ugiriki ikaendeleza unyonge kwa timu zilizocheza nyumbani jana kwa kulazwa mabao 2-0 na Ireland ya Kaskazini.
Kivumbi Afrika, Nigeria vs Sudan, Uganda v Togo hapatoshi!!
Watetezi Nigeria |
Sudan |
Ghana |
Uganda watacheka kama hivi leo kwa Togo |
Cameroon iliyong'ang'aniwa katika mechi iliyopita na Sierra Leone itakuwa nyumbani kurudiana na majirani zao hao, wakati Togo iliyoiduwaza Uganda The Cranes mjini Kampala itaialikia wapinzani wao hao katika pambano la kusisimua.
Mabingwa watetezi waliofumuliwa mjini Khartoum na wenyeji wao Sudan itajiuliza nyumbani huku Angola na Lesotho zitaonyeshana kazi mjini Luanda.
Mechi nyingine za makundi hayo zitakuwa kama ifuatavyo;
Ghana vs Guinea
Zambia vs Niger
Côte d'Ivoire vs Congo DR
Egypt vs Botswana
Cape Verde Islands vs Msumbiji
Mali vs Ethiopia
Burkina Faso vs Gabon
South Africa vs Congo
Tunisia vs Senegal
Algeria vs Malawi
Msiba! Muimbaji wa zamani Extra Bongo afariki dunia
Suzuki enzi za uhai wake |
Seleman Ramadhan Suzuki Sauti ya Malaika enzi za uhai wake |
Kwa mujibu wa mwanamuziki mwenzake ambaye alikuwa akifuatilia afya yake kipindi akiugua, Ramadhani Mhoza 'Pentagone' ameiambia MICHARAZO, Suzuki amefariki akiwa nyumbani eneo la Magomeni Kagera, jijini Dar es Salaam na huenda akazikwa leo au kesho.
Pentagone aliyefanya kazi na mwanamuziki huyo aliyekuwa na uwezo wa kutunga, kuimba na kurapu katika bendi za Levent Musica 'Wazee wa Kumuvuzisha' na Extra Bongo, alisema Suzuki alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Kisukari na alikuwa akitibiwa nyumbani kwa dawa za kienyeji.
"NIlitaka kukutaarifu kubwa swahiba yetu Suzuki hatunaye kwani amefariki usiku wa leo na kwa sasa tunaangalia mipango ya mazishi kwa kuwasiliana na ndugu zake wa karibu," alisema Pentagone ambaye kwa sasa anaiimbia African Stars 'Twnaga Pepeta'.
Enzi za uhai wake, Suzuki anayetokea Kigoma alitamba na bendi za Tabiora Jazz kabla ya kutua Morogoro katika bendi ya Mikumio Sound iliyowahi kutamba na albamu ya Mlinzi wa Godown kabla ya kuitua Levent Musica na baadaye yeye na wanamuziki wenzake watatu, Bob Kissa, Pentagone na Athanas Montanabe walihamia kwa mpigo Extra Bongo na kupakua albamua ya Mjini Mipango.
Mungu Ailaze Roho ya Marehemu Mahali Pema Peponi na MICHARAZO inatoa pole kwa wote walioguswa kwa namna moja au nyingine na msiba huio na kuwaomba kuwa na moyo wa Subira kwa kukumbuka kuwa 'Kila Nafsi Itaonja Mauti' na Sisi ni wa Mola na Kwake Hakika Tutarejea'.
Subscribe to:
Posts (Atom)