STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, February 26, 2013

HUU NDIO UKWELI WA SAKATA LA TIMBULO



TANGU jana kumekua na story zilizoenea mitaani kuhusu Mwanamuziki Timbulo kukamatwa na madawa ya kulevya Nchini Burundi. Baadhi ya watu wanas3ma wameona picha kupitia mtandao wa facebook ambazo zimemuonyesha timbulo akiwa chini ya ulinzi wa police na kidhibiti chake cha madawa haya ambayo yamefungwa kwa mfano wa pipi?

Ilinibidi nimtafute timbulo kupitia mtandao wa whatsup ambapo nilimuona akiwa active kama dkk kumi zilizopita mara baada ya kupata habari hizo

Timbulo amesema ni kweli alihisiwa kuwa amebeba madawa ya kulevya kitu kilichowafanya wanausalama kuomba kumkagua na kweli kumkuta na Pipi ambazo mara nyingi zimekua ni mfumo wa kubebea madawa ya kulevya katika begi lake, lakini katika maelezo ya timbulo anasema hazikuwa dawa za kulevya kweli bali ni mfano wa dawa ambazo alifanyia shooting katika movie yake ya hivi karibuni na kusahau kuzitoa. Hata hivo kutokana na maelezo yake anasema alihisiwa zaidi kubeba mzigo huo kutokana na mtu aliekuja kumpokea kusadikika kuwa katika biashara hiyo.

Timbulo alikua nchini burundi kwa shughuli zake za kimuziki akiwa ametokea Bukoba alikokua na shows huko lakini pia ikiwa ni mwendelezo wa safari ya kumfikisa Younde Cammeron ambako pia alikua anaenda kwa shughuli zake za kimuziki. Safari zote hizo ziliishia hapo baada ya tukuo hilo na hivi mpaka naingia mtamboni timbulo aliniambia yupo jijini mwanza kwa safari ya kurudi Dar Es Salaam.
CHANZO:UDAKU SPECIAL

Simba, Mtibwa wavuna Mil 62, kivumbi cha VPL kesho


Na Boniface Wambura
Mechi namba 121 ya Ligi Kuu ya Vodacom iliyochezwa juzi (Februari 24 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa Mtibwa Sugar kuibuka ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba imeingiza sh. 239,686,000.
Watazamaji 10,669 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo ambayo viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 14,577,252.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 9,467,694.92.
Viingilio cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo waliokata tiketi hizo walikuwa 9,491 na kuingiza sh. 47,455,000 wakati idadi ndogo ya washabiki ilikuwa ya kiingilio cha sh. 20,000 kilichovutia washabiki 105 na kuingiza sh. 2,100,000.
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 7,412,162.26, tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh. 4,447,297.36, Kamati ya Ligi sh. 4,447,297.36, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,223,648.68 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,729,504.53.

Wakati huo huo; michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaendelea kesho (Februari 27 mwaka huu) kwa  mechi tano zitakazochezwa katika viwanja tofauti.
Vinara wa ligi hiyo Yanga wataikaribisha Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwa viingilio vya sh. 5,000 (viti vya bluu na kijani), sh. 8,000 (viti vya rangi ya chungwa), sh. 15,000 (VIP C na B) na sh. 20,000 (VIP A).
Mechi nyingine za ligi hiyo ni Coastal Union vs Ruvu Shooting (Mkwakwani, Tanga), Polisi Morogoro vs Mgambo Shooting (Jamhuri, Morogoro), JKT Ruvu vs Toto Africans (Azam Complex, Dar es Salaam) na Mtibwa Sugar vs Tanzania Prisons (Manungu, Morogoro).



TFF 'yawachinja', yasimamisha Waamuzi, Makamisaa

Mwamuzi Mathew Akrama (mwenye mpira mguuni) mmoja wa walioondolewa VPL

Na Boniface Wambura
Mwamuzi Msaidizi wa FIFA, Ferdinand Chacha ameondolewa kuchezesha mechi za VPL baada ya kupata alama za chini kwenye mechi kati ya African Lyon na Simba iliyochezwa mwezi uliopita Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Waamuzi wanaopata alama 6.5 au chini ya hapo kati ya 10 zinazohitajika pia wanaondolewa kwenye mechi za VPL na FDL.
Waamuzi wengine walioondolewa kwa kutomudu mechi walizochezesha za VPL ni Mathew Akrama (Yanga vs Simba), Ephrony Ndissa (Yanga vs Simba), Ronald Swai (Yanga vs Mtibwa Sugar).
Walioondolewa kwa kupata alama za chini ni Alex Mahagi (Simba vs JKT Ruvu), Methusela Musebula (Toto Africans vs Coastal Union), Lingstone Lwiza (Toto Africans vs Coastal Union), Idd Mikongoti (Toto Africans vs Mtibwa Sugar) na Samson Kobe (Toto Africans vs Mtibwa Sugar).
Masoud Mkelemi aliyekuwa mwamuzi wa mezani katika mechi ya FDL kati ya Moro United na Villa Squad ameondolewa kwa kutofika kwenye mkutano wa maandalizi ya mechi (Pre-match meeting) na alichelewa kwa dakika tano kufika uwanjani.
Wakati huo huo, baadhi ya makamishna wa VPL na FDL wameondolewa na wengine kusimamishwa kusimamia mechi za ligi hizo kutokana na upungufu kwenye ripoti zao au kutowasilisha kabisa ripoti hizo TFF baada ya mechi.
Kamishna Mohamed Jumbe aliyesimamia mechi kati ya Mgambo Shooting na Simba ameondolewa kwenye orodha ya makamishna kutokana na ripoti yake kuwa na upungufu.
Makamishna wa mechi kati ya JKT Oljoro vs Yanga (Hakim Byemba), JKT Oljoro vs Kagera Sugar (Salum Kikwamba), Toto Africans vs African Lyon (Charles Komba), Coastal Union vs JKT Oljoro (Mohamed Nyange) wamesimamishwa hadi watakapowasilisha ripoti zao TFF.
Kwa upande wa FDL makamishna waliosimamishwa hadi watakapowasilisha ripoti zao TFF ni wa mechi kati ya Kurugenzi vs Polisi Iringa, Morani vs Mwadui, Polisi Mara vs Pamba, Polisi Mara vs Mwadui, Morani vs JKT Kanembwa na Pamba vs Polisi Dodoma.
Wengine ni Mwadui vs JKT Kanembwa, Polisi Tabora vs Morani, Polisi Dodoma vs Polisi Mara, Polisi Tabora vs Mwadui, Polisi Mara vs Morani, JKT Kanembwa vs Polisi Mara, Morani vs Rhino Rangers na Small Kids vs Mkamba Rangers.
Kamati ya Ligi imewakumbusha makamishna wote kuwa ni jukumu lao kuhakikisha ripoti zao zimefika TFF na kurekebisha upungufu wa jinsi ya kuripoti matukio yanayotokea uwanjani. Licha ya kutuma nakala kwa njia ya email, wanatakiwa pia kuwasilisha ripoti halisi (original) TFF.

Kocha Azam afungiwa, TFF yatembeza kibano kwa watukutu

Kocha wa Azam, John Stewart Hall (kushoto)

Na Boniface Wambura
Kocha Mkuu wa Azam, Stewart John Hall amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh. 500,000 kwa kushusha bukta yake na kumlalamikia mwamuzi msaidizi wakati wa mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya timu yake na Kagera Sugar iliyochezwa Januari 26 mwaka huu Uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi, Dar es Salaam.
Adhabu hiyo imetolewa na Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana mwishoni mwa wiki kupitia ripoti za michuano ya VPL na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu wa 2012/2013 inayoendelea hivi sasa na kufanya uamuzi mbalimbali.
Naye Kocha Msaidizi wa timu ya Mgambo Shooting, Denis Mwingira ametozwa faini ya sh. 500,000 kwa kumtolea lugha chafu mwamuzi kwenye mechi dhidi ya Mtibwa Sugar iliyochezwa Oktoba mwaka jana katika Uwanja wa Manungu.
Ally Jangalu ambaye ni Kocha Msaidizi wa Polisi Morogoro naye ameangukiwa na rungu la Kamati ya Ligi kwa kupigwa faini ya sh. 500,000 baada ya kutolewa kwenye benchi kwa kupinga uamuzi wa refa kwa sauti ya juu. Alitenda kosa hilo kwenye mechi kati yao na Kagera Sugar iliyochezwa Novemba 10 mwaka jana Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Matukio ya aina hiyo kwa kocha Jangalu yamekuwa ya kujirudiarudia ambapo Oktoba 13 mwaka jana katika mechi dhidi ya Azam iliyochezwa mjini Morogoro aliondolewa na mwamuzi kwenye benchi kwa kuchochea wachezaji wa timu yake wacheze rafu.
Naye Kocha wa timu ya Moro United inayoshiriki FDL, Yusuf Macho amepigwa faini ya sh. 200,000 kwa kumtolea lugha chafu refa baada ya mechi dhidi ya Transit Camp iliyofanyika Novemba 4 mwaka jana Uwanja wa Mabatini mjini Mlandizi.
Pia Kocha wa Burkina Faso, Hasheem Mkingie amepigwa faini ya sh. 200,000 baada ya kutolewa kwenye benchi kwa kutoa lugha chafu katika mechi ya FDL dhidi ya Mkamba Rangers.
Kiongozi wa Majimaji, Joseph Nswila ambaye aliingia uwanjani baada ya mechi dhidi ya Mlale JKT kumalizika na kuvamia waamuzi amefungiwa miezi sita.
Vilevile timu ya Azam imepigwa faini ya sh. 300,000 kwa kuchelewa kufika uwanjani kwenye mechi kati yao na JKT Oljoro iliyochezwa Novemba 7 mwaka jana katika Uwanja wao wa Azam Complex ulioko Chamazi, Dar es Salaam.
Pia Coastal Union imetozwa faini ya sh. 500,000 kutokana na washabiki wake kumrushia chupa za maji mwamuzi msaidizi namba mbili wakati wa mechi yao dhidi ya Simba iliyochezwa Oktoba mwaka jana Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Nayo klabu ya African Lyon imepigwa faini ya sh. 500,000 kwa timu yake kugoma kuingia kwenye chumba cha kubadilishia nguo wakati wa mapumziko katika mechi dhidi ya Coastal Union iliyochezwa Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, Oktoba 24 mwaka jana.
Timu ya Burkina Faso ya Morogoro imepigwa faini ya sh. 200,000 kutokana na kuonesha vitendo vya ushirikina kabla ya mechi yao dhidi ya Mbeya City iliyochezwa Oktoba 24 mwaka jana Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Faini ya ushirikina ya sh. 200,000 pia imepigwa timu ya Pamba baada ya kuonesha vitendo hivyo kwenye mechi yao dhidi ya Mwadui iliyochezwa Novemba 4 mwaka jana Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
Nayo Mkamba Rangers imepigwa faini ya sh. 200,000 baada ya washabiki wake kumtolea lugha chafu Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Morogoro (MRFA), Hamis Semka na kumrushia chupa za maji mwamuzi wa mezani katika mechi dhidi ya Mbeya City iliyochezwa mjini Morogoro.
Polisi Dodoma imepigwa faini ya sh. 200,000 kutokana na washabiki wake kuvamia uwanjani na kutaka kuwapiga waamuzi katika mechi yao dhidi ya JKT Kanembwa na kusababisha mipira miwili ya Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dodoma (DOREFA) kupotea.
Pia klabu kadhaa zimeandikiwa barua za onyo kwa timu zao kuchelewa kufika uwanjani au kutofika kwenye mkutano wa maandalizi ya mechi (Pre-match meeting). Klabu hizo ni Coastal Union, JKT Ruvu, Toto Africans, Simba, Green Warriors, Majimaji, Mkamba Rangers, Polisi Dodoma, JKT Kanembwa, Moro United.
Mchezaji Stanley Nkomola wa JKT Ruvu baada ya mechi dhidi ya Coastal Union alikwenda jukwaani na kuanza kupigana na washabiki. Pia kipa wa timu ya Transit Camp, Baltazar Makene baada ya mechi dhidi ya Tessema aliruka uzio na kwenda kupigana na washabiki.
Kwa vile masuala ya wachezaji hao ni ya kinidhamu yamepelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu inayoongozwa na Kamishna wa Polisi (CP) mstaafu Alfred Tibaigana kwa ajili ya kuchukuliwa hatua.


KAMATI YA UTENDAJI TFF KUIJADILI SERIKALI


Na Boniface Wambura
Sekretarieti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imepokea barua ya Serikali ikielezea uamuzi wa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara kutengua uamuzi wa Msajili wa Klabu na Vyama vya Michezo nchini kuidhinisha marekebisho ya Katiba ya TFF toleo la 2012.
Baada ya kupokea barua hiyo jana alasiri (Februari 25 mwaka huu), Sekretarieti iliwasiliana na Rais wa TFF, Leodegar Tenga ambaye ameagiza kuitishwa kikao cha dharura cha Kamati ya Utendaji kujadili tamko hilo.
Kikao hicho cha Kamati ya Utendaji ya TFF kitafanyika Jumamosi (Machi 2 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.

YANGA, KAGERA KESHO KISASI KITUPU

Kikosi cha Kagera Sugar

KIVUMBI cha Ligi Kuu Tanzania Bara kinatarajiwa kuendelea tena kesho nchini, huku pambano la jijini Dar es Salaam kati ya vinara Yanga dhidi ya wageni wao Kagera Sugar ni kama vita vya kulipizana kisasi.
Yanga inayoongoza msimamo wa ligi hiyo ikiwa imejiukusanyia pointi 39 itaikaribisha Kagera kwenye uwanja wa Taifa, ikiwa na kumbukumbu ya kipigo cha bao 1-0 ilichopewa katika mechi ya mzunguko wa kwanza walipoenda mjini Kagera.
Kikosi cha Yanga


Kadhalika Yanga itashuka dimbani ikiamini kuteleza mbele ya Kagera ni kutoa mwanya wa Azam waliopo nafasi ya pili ambao hawatakuwa uwanjani kwa kesho kwa vile wanaenda Sudan Kusini kuvaana na Al Nasir Juba, kuja kuwasogelea katika mbio zao za kuwania ubingwa wa ligi hiyo msimu huu.
Azam yenyewe wapo nafasi ya pili na pointi zao 36, huku Simba wanaoshikilia taji hilo kwa sasa wakiwa nafasi ya tatu na pointi 31, ambazo huenda zikapitwa kesho na Coastal Union itakayoikaribisha Ruvu Shooting kwenye uwanja wa Mkwakwani Tanga.
Kagera inayonolewa na mshambuliaji nyota wa zamani wa Majimaji Songea, Simba na Taifa Stars, Abdallah King Kibadeni, siyo timu ya kubezwa, japo rekodi zinaoonyesha inapocheza na Yanga nje ya uwanja wao wa nyumbani huwa haina madhara kama wakiwa Kaitaba.
Kikosi cha Kagera kinashika nafasi ya tano kikiwa na pointi 28 na ushindi wowote kwao utaifanya ilingane pointi na Simba, lakini pia kujiweka katika mazingira mazuri ya kuingia kwenye Nne Bora.
Rekodi kwa timu hizo mbili kwa misimu mitatu kuanzia ule wa 2010, unaoonyesha Yanga imeshinda mara tatu na kupoteza mara mbili.
Msimu wa 2010 Yanga walishinda mechi zote mbili  nyumbani na ugenini, ikiifunga Kagera jijini Dar mabao 2-0 katika mechi iliyochezwa Septemba, 22 na kuendeleza ubabe mjini Kagera kwa kuilaza Kagera bao 1-0 mechi iliyopigwa Februari 16, 2011.
Katika msimu uliopita, Yanga ilipata ushindi nyumbani Oktoba 14, 2011 kabla ya kwenda kulala katika mechi ya marudiano mjini Kagera iliyochezwa Machi 18, 2012 na msimu huu ilipata kipigo cha bao 1-0 mjini Kagera Oktoba 7, 2012 na haijulikani kesho nani ataibuka mshindi?
Mwechi nyingine zitakazochezwa kesho mbali na Yanga na Kagera na ile ya Coastal Union dhidi ya Ruvu Shooting, pia Mtibwa Sugar itakuwa nyumbani kuuikaribisha Prisons ya Mbeya, Polisi Moro itaialika Mgambo JKT na JKT Ruvu itaikaribisha Toto African uwanja wa Chamazi Complex, Dar es salaam.
  

KIVUMBI KINGINE CHA NGUMI IBF

 
Waghana Frederick Lawson na Issac Sowah wanatarajia kupanda ulingoni tarehe 8 Machi kugombea mkanda wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati (IBF AMEPG)  katika uzito wa Welterwweight kwenye uwanja wa Accra Sports jijini Accra, Ghana. Mabondia hao wamepangwa katika kapambanoi ya utangukizi wakati wa mpambano mkubwa wa kugombea mkanda wa dunia kati ya bondia wa Ghana na ambaye alikuwa bingwa wa dunia wa IBF katika uzito wa bantam Joseph Abgbeko na bondia Luis Melendez kutoka nchi ya Columbia iliyoko bara la Amerika ya Kusini.
 
 
Wawili hao wanatoka katika maskani ya Bukom iliyoko kwenye kiunga cha Lebanon jijini Accra kinachosifika kwa kutoa mabingwa wengi wa dunia. Kuingia kwa mabondia hawa wawili kwenye mpambano huo kutatoa burdani ya aina yake kwa mashabiki wa ngumi wa Ghana pamoja na nchi nyingi za Afrika ya Magharibi.
 Agbeko092907
              Bondia Joseph Agbeko baada ya moja ya ushindi wake
 
IBF inaipa pongezi sana nchi ya Ghana iliyokuwa inaitwa Pwani ya Dhahabu au Gold Coast kwa kuonyesha nia thabiti ya kuinua vipaji vya mchezo wa ngumi na kuufanya mchezo huu kurudi nyumbani.  Ghana inasikfika sana kwa kuweza kutoa mabingwa wengi wa nguni wa zamani ambao walisifika sana kwa uwezo wao wa kurusha masumbi wakiwamo D.K. Poison, Marvelous Nana Yaw Konadu, Azumah Nelson, Ike "Bazooka" Quartey, Alfred "Cobra" Kotey na Joseph King Kong Agbeko ambaye anatarajia kuonyesha makeke yake siku hiyo ya tarehe 8 Machi.

Tottenham Hotspur yaing'oa Chelsea, Gareth Bale awa shujaa

Tottenham Hotspur's Gareth Bale celebrates scoring his side's first goal against West Ham United on February 25, 2013
Gareth Bale (kulia) akishangilia bao na wachezaji wenzake wa Tottenham jana

LICHA ya kucheza ugenini, timu ya Tottenham Hotspur usiku wa kuamkia leo imefanikiwa kuishusha kwnye nafasi ya tatu Chelsea baada ya kupata ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya wenyeji wao West Ham United katika mechi pekee ya Ligi Kuu ya England.
Mabao mawili ya nyota Gareth Bale na moja ya mtoa benchi, Gylfi Sigurdsson iliotosha kuwapa vijana wa Andre Villa Boas, kuzoa pointi tatu na kufikisha jumla ya pointi 41 mbili zaidi ya Chelsea ambayo juzi ililala kwa Machester City na kuiporomosha hadi nafasi ya nne.
Bale alianza kufungua pazi kwa Tottenham dakikia ya 13 kabla ya Andy Carroll kusawazisha kwa mkwaju wa penati dakika ya 25 na kufanya hadi  mapumziko matokeo yawwe bao 1-1.
Kipindi cha pili Joe Cole aliiongezea wenyeji bao la pili katika dakika ya 58 kabla ya mtokea benchi, Sigurdsson kufunga bao la kusawazisha kwenye dakika ya 76 na wakati wengi wakiamini matokeo ya mchezo huo ni sare, Bale akapachika bao la ushindi dakika ya 90.

RAGE AWASHUSHUA WANAOTAKA AJIUZULU


MWENYEKITI wa klabu ya Simba, Ismail Aden Rage amewaumbua wale wote wanaomshinikiza ajiuzulu kufuatia mwenendo mbaya wa timu yao katika Ligi Kuu Tanzania Bara, akidai hatajiuzulu ng'o kwa madai yeye siyo mchezaji wala kocha ndani ya Simba hivyo hapaswi kusakamwa.
Hata hivyo alifichua kitu gani kilichopo nyuma ya wanaomshinikiza ang'oke akidai ni tabia yake ya uwazi na msimamo wake dhidi ya rasilimali na mapato ya Simba ndiyo chanzo cha kuonekana mbaya, japo uongozi wake unatimiza wajibu wake kama unavyopaswa katika kuhakikisha kila kitu kinaenda vema Msimbazi.
Rage alitoa msimamo huo jana alipozungumza na waandishi wa habari na kukuanusha taarifa kwamba huenda angeachia ngazi na badala yake alisema yeye bado yupo sana Simba, ingawa alisisitiza kuwa kamati ya utendaji ya klabu hiyo itakutana ili kujadili kinachoendelea ndani ya Simba.
Alisema maamuzi ya kamati hiyo huenda yaakatoka na maamuzi magumu na atayatangaza mbele ya mkutano wa wanachama atakaoutisha kuwapa kila kitu kinachoendelea ndani ya Simba kwa sasa na kuifanya timu yao kwenda kwa kusuasua katika ligi kuu.
"Wanaotaka mie nijiuzulu niwaulie mie nacheza namba ngapi au mie ni kocha?...Mimi ni mwenyekiti na wajibu wangu kuhakikisha timu inapata kila linalohitajika, kwa mfano hivi sasa Simba inatakiwa kwenda Angola kurudiana na Libolo ni wajibu wangu kuisafirisha klabu iwe na fedha au la, watu wabadilike," alisema.
Aliongeza, uwazi wake katika udfhibiti wa mapato na vitega uchumi vingine vya Simba ndiyo uliomtengenezea maadui, ila akahoji mbona wanachjama wanaomshikiniza kujiuzulu hawajawahi kuhoji zilipo fedha za wachezaji waliouzwa Ulaya kama akina Haruna Moshi 'Boban', Henry Joseph kama uongozi wao ulivyoweka kila kitu hadharani ilipowauza akina Mbwana Samatta, Patrick Ochan na sasa Emmanuel Okwi.
Juzi mara baada ya pambano la Simba na Mtibwa Sugar ambapo 'Mnyama' alilala kwa bao 1-0, kulikuwa na tetesi kwamba Rage alikuwa akijiandaa kujiuzulu kwa kuhisi anahujumiwa na watu ili aonekane hafai.
IBRAHIM MAOKOLA AJIFUA KWA MPAMBANO WAKE WA MACHI 2
Bondia Ibrahimu Maokola akifanya mazoezi ya kupiga punch bag akijiandaa na pambano lake dhidi ya Rajabu Majeshi litakalofanyika katika ukumbi wa DDC Magomeni Kondoa Machi 2 kusindikiza mpambano kati ya Maneno Osward na Japhert Kaseba.