STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, August 1, 2013

Picha za utupu zanaswa ukumbi wa Kanisa Dar



Kiongozi wa Kanisa la Greek Orthodox duniani, Papa Theodor’s II ameamuru kufungwa kwa ukumbi uliopo ndani ya eneo la kanisa hilo lililopo Kiwanja Namba 7509 katika Barabara ya Ali Hassan Mwinyi jijini Dar es Salaam kufuatia kuwepo kwa picha za utupu za wanawake ukutani..


Papa huyo alifikia uamuzi huo Februari 19, mwaka huu baada ya kutua nchini ambapo alifanya mazungumzo na Rais Jakaya Kikwete.
 Mbali na mazungumzo na JK, alipata nafasi ya kutembelea ukumbi huo ulio kwenye eneo la kanisa hilo ndipo ‘alikutana’ na picha za wanawake wa Kiafrika na Kizungu zikiwa zimetundikwa ukutani wakiwa kama walivyozaliwa.


Mbali na picha hizo za utupu, pia kulikuwa na picha ya mwanamitindo maarufu Bongo, Mariam Julius Odemba. Picha yake ilimwonesha akiwa amevaa nguo ya heshima na maandishi juu ya picha yakiwa yameandikwa; ‘Thanks British Legion for all your support. Miriam Odemba, 1st Oct 1999’.  

Imeelezwa kuwa baada ya kutua nchini, papa huyo alilala katika nyumba iliyo karibu na kanisa na klabu hiyo na usiku wakati akisali alishangaa kuwaona wanaume, tena wenye mwonekano mzuri wakiingia katika eneo hilo la kanisa akasitisha sala.

Kilichomshangaza zaidi ni kuwaona wanaume hao wakiwa na wasichana wabichi na baada ya kufika klabuni walikuwa wakipiga kelele huku muziki ukisikika kwa sauti ya juu.

 
 Kufuatia hali hiyo, aligundua kwamba watu hao walikuwa wakinywa pombe hadi usiku wa manane jambo ambalo ni kinyume na maadili ya imani hiyo.


“Kesho yake Papa Theodor’s aliamua kutembelea ndani ya klabu hiyo ndipo aliposhuhudia picha hizo chafu nyingi zikiwa zimetundikwa ukutani na chupa tupu za vinywaji vikali.

“Kuona hivyo papa alimuagiza kiongozi wa Bodi ya Wadhamini wa Kanisa, Dimitri Kimon akutane na mapadri wote mwezi wa nne (uliopita) na kujadili hilo nia ikiwa ni kurejesha usafi na kuondoa uchafu huo kanisani hapo.

“Katika mkutano huo waliamua kufunga na kuomba kisha kumtafuta wakili ili aweze kuwatoa waliokuwa wakiendesha ukumbi huo,” kilisema chanzo.

Chanzo kiliongeza kuwa, Julai 8, mwaka huu viongozi hao waliamua kufunga geti la kanisa hilo na kuimarisha ulinzi kwa kutumia kampuni ya ulinzi ili kuzuia wanachama wa klabu hiyo kuingia eneo hilo isipokuwa waumini.
 Kiongozi wa kanisa  hilo.

 Habari zinasema viongozi wa kanisa hilo waliwaambia waliokuwa wakiendesha ukumbi huo kwamba kiongozi wao mkuu hakupendezwa na picha chafu za ukutani na alihoji endapo dini nyingine zikigundua uchafu huo wataelewekaje kwa jamii?

Kuna madai kwamba wengi waliokuwa wakiingia kwenye ukumbi huo ni vigogo katika ngazi ya mawaziri na wabunge ambapo waandishi wetu walibahatika kuona jina la mbunge mmoja likiwa limeorodheshwa katika kitabu cha waliokuwa wakiingia.

Mwanachama mmoja wa klabu hiyo ambaye hakutaka jina lake kuandikwa  kwa madai kuwa si msemaji, alisema wanakusudia kufungua kesi mahakamani ili kupinga adhabu ya kufungwa ukumbi huo kwa kuwa wapo eneo hilo kwa muda mrefu.

“Sisi tupo katika eneo hili na tumefanya shughuli zetu siku zote hizo, tunashangaa leo kuona kanisa linatufungia geti. Ni lazima tutachukua hatua za kisheria,” alisema mwanachama huyo.

Mwandishi wetu alimpata wakili wa kanisa hilo ambaye pia ni Katibu Myeka, Edward Chuwa alipoulizwa kuhusu mgogoro huo alikiri kuwepo.

“Ni kweli kuna huo mgogoro kati ya kanisa na waendesha klabu hiyo lakini kwa kuwa mimi ni wakili naomba nisiseme chochote kwa sababu za kimaadili,” alisema Chuwa.

Naye wakili wa waendesha klabu hiyo, Evodi Mmanda alipopigiwa simu na kuulizwa kuhusu mgogoro huo naye alikiri kuwepo.

“Mgogoro huo naujua lakini kwa kuwa mimi ni wakili wao siwezi kusema chochote kutokana na maadili ya kazi yangu.” alisema Mmanda bila kusema ni lini kesi hiyo itasikilizwa. 

Credit : Uwazi  via  GPL

Azam kutimkia Bondeni kucheza mechi nne ratiiba kamili hii hapa!

Azam FC  inasafiri jumamosi hii kuelekea afrika ya kusini kwa maandalizi ya ligi kuu na itacheza michezo minne kama ifuatavyo
Tarehe 5 August, Azam Fc vs Kaizer Chiefs, 
Tarehe 7 August Azam Fc vs Mamelodi Sundows, 
Tarehe 9 August Azam Fc vs Orlando Pirates,
Tarehe 12 August Azam Fc vs Moroka Swalows
Kikosi cha Azam
KLABU ya soka ya Azam Fc, inatarajiwa kuondoka nchini keshokutwa kwenda Afriki Kusini kuweka kambi yao kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2013-2014.
Kwa mujibu wa taarifa za klabu hiyo timu hiyo ikiwa nchini humo itacheza mechi nne kabla ya kurejea nchini kuisubiri Yanga katika pambano la Ngao ya Hisani Agosti 17 na kisha kuifuata Mtibwa Manungu katika pambano la fungua dimba la Ligi Kuu.
Ratiba hiyo iliyotolewa na klabu hiyo inaonyesha itashuka dimbani Agosti 5 dhidi ya Kaizer Chiefs kabla ya siku moja baadaye kuwava Mamelodi Sundowns.
Baada ya siku moja yaani Agosti 9 Azam itaumana na Orlando Pirates na kumalizia ziara na kambi yao ya nchini humo kwa kuvaana na Moroka Swallows Agosti 12.

Maajabu ya Dunia! wanandoa waliozaliwa siku moja wafa siku moja wakiwa na miaka 94

WANANDOA katika jijini la California waliozaliwa siku moja na kuoana miaka 75 iliyopita wamefariki siku moja wakiwa na miaka 94.
 Couple Born on Same Day, Married 75 Years, Die One Day Apart

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Long Beach Press Telegram, Helen na Les Brown walifariki Julai 16 na 17 mwaka huu wote wakiwa na umri wa miaka 94.

Zach Henderson, Mmilikii wa Grosari moja ijulikanayo kwa jina la Ma N’Pa iliyopo Long Beach alinukuriwa wakisema kuwa alikuwa akiwaona wapendanao hao kila siku iitwayo kwa Mungu na kuuita uhusiano wao kuwa “ a Wonderful Blessing”.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Press –Telegram imesema kuwa wote walizaliwa siku moja yaani Desemba 31, 1918 na pia walianza kuwa pamoja mwaka 1937 katika masomo ya sekondari.

Imejulikana kwamba wanandoa hao walikuwa waamini wa Mashahidi wa Yehova (Jehova Witnesses) waliobarikiwa kuwa na mtoto wao Les Brown Jr.

Henderson anasema imani yao kwa Mwenyezi Mungu ndio iliyozidi kuimarisha ndoa yao hadi kufikia hapo.

Mtoto wao Les Brown Jr alinukuriwa akisema “Walikuwa pamoja kila siku kwa miaka 75, hakika upendo wao ulirandana” 

Post Telegram limeripoti kuwa Les Brown alikuwa akiumwa ugonjwa wa Parkison’s na mkewe Helen Brown alikuwa akisumbuliwa Kansa ya tumbo hadi mauti yao yalipowakuta

"She was completely cognitive," Henderson said, describing how he found Helen Brown a few days before she died. "It seems like she was waiting for Les to be comfortable and they were going to move on to something else with each other."

Ibada ya pamoja itafanyika siku ya Jumamosi mchana kwa ajili ya kuwakumbuka wanandoa hao huko Long Beach, California.

CHANZO: JAIZMELALEO/ABC NEWS/YAHOO NEWS

Watu 7 wanusurika kufa ajali ya Ndege Longido

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj1DmrEfl1anJUzU-aq9ZKrxtChtAM8ILw5c0EHEak7ECequsrmy29HWPXmMZNPDJXbucKkDbGvTUoWDUMGpujXOW5EwFxYaW5Hop0RhIDE_GbqWx51fQ1sCNL73rjzBO-CJLGm2Kf4fqBN/s320/Catalina+Aircraft+-+Canadian+Vickers+PBY-5A+Canso+-+G-PBYA+-+5242+NET.jpgWATU 7 wamenusurika kupoteza maisha baada ya ndege waliyokuwa wakisafiria kuanguka na maeneo ya Longido Mkoani Arusha juzi Jumanne.

Duru za Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha zimesema majira ya saa 8 za mchana katika kijiji cha Merugwayi ndege aina ya CESS iliyokuwa na namba za usajili TN/4206 ikiwa na marubani wawili ilipata ajali.

Taarifa hiyo ya Jeshi la Polisi imetaja chanzo cha ajili hiyo kuwa ni upepo mkali uliosababisha ishindwe kupaa katika uwanja wa ndege wa Merugwayi umbali wa mita 120 na kuanguka.

Habari zaidi zinasema ndege hiyo iliondoka Arusha majira ya saa 2 za asubuhi kuelekea wilayani Ngorongoro na baadaye ilirudi tena Arusha ikiwa na Abiria watano ilipofika katika uwanja huo ilishuka kwa ajili ya kuchukua mgonjwa na ilipojaribu kuruka ilishindwa, na kupoteza mwelekeo.

Marubani waliokuwemo katika ndege hiyo ni Jaffer Shakir (23) na Patten Patrick (65).

Hata hivyo Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha ACP Japhet Lusingu amewataja majeruhi kuwa Nalepo MamaSita (38), Anna Laizer (21), Naninkoi Laizer (7), Benson Mukoya (28), Krizosto Malima (30).

Rubani wa ndege hiyo Jaffer Shakir ameumia  vibaya sehemu za usoni na amelazwa katika Hospitali ya Selian, Jijini Arusha kwa matibabu zaidi huku wengine wakiruhusiwa.  
 
Jaizmalaleo

Polisi wauwa jambazi mkoani Iringa, yanasa wahamiaji haramu toka Ethiopia

MTU anayeshukiwa kuwa jambazi ameuawa na mwingine akikamatwa wakati wakivamia duka la Santino Mdesa katika kijiji cha Mkonge kilichopo katika Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.
Aidha wahamiaji haramu watano kutoka nchini Ethiopia wametiwa mbaroni kwa kosa la kuingia nchini kinyemelea ikiwa siku chache tangu Rais Jakaya Kikwete kuchimba mkwara juu ya wahamiaji haramu kuzidi kuongeza nchini.
Akizungumzia tukio hilo ujambazi, Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa ACP Ramadhani Mungi amesema majambazi hao walifyatua risasi hewani ambapo wananchi walipobaini uwepo wa tukio hilo la Uharifu walizingira eneo hilo ambapo majambazi walitambua mbinu hizo na kukimbia.
Aidha kamanda Mungi amesema wananchi kwa kushirikiana na askari polisi waliwakimbiza majambazi hao na baada ya kuzidiwa nguvu, majambazi walitupa bunduki aina ya SMG iliyokuwa na Lisasi 21, na kisha kutelekeza usafiri wao wa Pikipiki, huku askari wakifanikiwa kumpiga kwa risasi mguuni jambazi mmoja aliyekufa wakati akipelekwa kupata matibabu.
Mungi amesema pia Polisi wamefanikiwa kumkamata mwananchi wa kijiji cha Kitayawa katika Wilaya ya Iringa ambaye amekuwa akitengeneza Bunduki za kienyeji.
Katika tukio lingine kamanda Mungi amesema, wamewakamata wahamiaji haramu watano kutoka nchi ya Ethiopia ambao walikuwa wamejificha katika poli la mashamba ya kijiji cha Mazombe, katika Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa, na kuwa wahamiaji hao walikuwa wanaelekea nchini Afrika Kusini.
Akithibitisha kukamatwa kwa wahamiaji hao haramu, ofisa uhamiaji mkoa wa Iringa Ali Nassor amesema wahamiaji hao haramu wakiethiopi wapo chini ya ulinzi kwa hatua zaidi.

Bondia Mtanzania alivyomchakaza Mthailand


 Bondia Mtanzania Omari Kimweri  anayefanya shughuli zake Australia kulia akinyooshwa mkono juu kuashira ushindi wake baada ya kumtwanga  Ekkalak Saenchan  wa Thailand kwa KO raundi ya kwanza.

Bondia Mtanzania Omari Kimweri  (kulia) akimsukumia makonde mazito mfululizi bondia Ekkalak Saenchan  wa Thailand na kufanikiwa kumtwanga kwa kwa KO raundi ya kwanza mwishoni mwa wiki iliyopita.
Bondia Mtanzania Omari Kimweri  anayefanya shughuli zake Australia akimsikilizia mpinzani wake baada ya kumtwanga kumi nzito na kuhesabiwa wakati wa mpambano wake ambapo mpinzani wake toka Thailand alishindwa kuendelea na hivyo kutangazwa mshindi wa KO ya raundi ya kwanza