TIMU ya Sevilla ikiwa uwanja wa ugenini ilipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Almeria na kujiweka katika nafasi nzuri katika mbio zao kwenye Ligi Kuu ya Hispania, La Liga.
Sevilla ilijikuta ikisubiri hadi kwenye kipindi cha pili kuweza kupata mabao yake hayo ambayo yalifungwa na Iborra katika dakika ya 58 kabla ya Coke kuongeza jingine dakika tano baadaye na kuifanya timu hiyo kufikisha pointi 36 na kushika nafasi ya nne.
Mashabiki wa soka wanatarajia kupata burudani baadaye wakati Barcelona itakayokuwa nyumbani itaikaribisha mabingwa watetezi wa ligi hiyo, Atletico Madrid zinazofukuzana nyuma ya vinara Real Madrid ambayo jana ilizinduka katika ligi hiyo klwa kushinda mabao 3-0 dhidi ya Espanyol.
STRIKA
USILIKOSE
Sunday, January 11, 2015
Mgambo JKT yaitoa nishai Ruvu Shooting Mkwakwani
Mgambo JKT waliopata ushindi dhidi ya Ruvu Shooting |
Ruvu Shooting inayonolewa na kocha Mkenya, Tom Oloba ilishindwa kuhimili vishindo vya maafande wenzao licha ya tambo zilizokuwa zikitolewa na uongozi wa klabu hiyo chini ya Msemaji wao, Masau Bwire.
Bao hilo la wenyeji liliwekwa kimiani na Full Maganga katika dakika ya 44, likiwa ni bao la kwanza kwa mchezaji huyo ambaye amekuwa na kismati cha kuzitungua Simba na Yanga.
Kwa ushindi huo Mgambo imefikisha pointi 12 na kuchupa kutoka nafasi ya 12 hadi nafasi ya nane wakiing'oa Ruvu Shooting ambayo imesaliwa na 11.
Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya mchezo wa leo:
P W D L F A GD Pts
01. Mtibwa Sugar 08 04 04 00 11 04 07 16
02. JKT Ruvu 10 05 01 04 10 09 01 16
03. Yanga 08 04 02 02 11 07 04 14
04. Azam 08 04 02 02 10 06 04 14
05. Kagera Sugar 09 03 05 01 07 04 03 14
06. Polisi Moro 10 03 05 02 09 08 01 14
07. Coastal Union 09 03 03 03 09 08 01 12
08. Mgambo JKT 09 04 00 05 05 09 -4 12
09. Ruvu Shooting 10 03 02 05 05 08 -3 11
10. Stand Utd 10 02 05 03 07 12 -5 11
11. Ndanda Fc 10 03 01 06 10 14 -4 10
12. Simba 08 01 06 01 07 07 00 09
13. Mbeya City 08 02 02 04 03 06 -3 08
14. Prisons 09 01 04 04 06 08 -2 07
Wafungaji Bora:
5- Didier Kavumbagu(Azam)
4- Rama Salim (Coastal), Danny Mrwanda, Simon Msuva (Yanga) Ame Ally (Mtibwa), Samuel Kamuntu (JKT Ruvu)
3- Ally Shomari, Emmanuel Okwi (Simba), Rashid Mandawa (Kagera Sugar), Jacob Massawe (Ndanda)
2- Shaaban Kisiga, (Simba), Nassor Kapama (Ndanda) Salum Kanoni (Kagera), Aggrey Morris (Azam), Najim Magulu, Jabir Aziz (JKT Ruvu), Amissi Tambwe, Jerry Tegete (Yanga), Ibrahim Kihaka (Prisons), Mussa Mgosi (Mtibwa), Heri Mohammed, Mussa Said (Stand Utd), Ally Nassor (Mgambo), Malimi Busungu (Mgambo), Nicolaus Kabipe (Polisi)
1- Joseph Owino (Simba), Coutinho, Kelvin Yondan, Haruna Niyonzima, Jaja (Yanga), Deo Julius, Steven Mazanda (Mbeya City), Bakari, Imani Mapunda, Said Bahanuzi (Polisi-Moro), Kipre Tchetche, Aggrey Morris, SHomar Kapombe, John Bocco (Azam), Ernest Joseph, Paul Ngalema, (Ndanda), Jacob Mwaitalako, Laurian Mpalile, Amir Omary, Hamis Mahingo (Prisons), Lutimba Yayo, Kennedy Masumbuko, Joseph Mahundi, Hussein Sued,Itubu Intembe (Coastal), Ramadhani Pella, Full Maganga (Mgambo), Said Mkopi, Vincent Barnabas (Mtibwa), Amos Mgina, Najim Magulu, (JKT Ruvu), Salum Kamana, Shaaban Kondo (Stand Utd), Paul Ngwai, Atupele Green(Kagera Sugar), Juma Nade, Abdulrahman Mussa, Thomas Mathayo , Hamis Kasanga ,Zubeiry Dabi (Ruvu Shooting)
Inter Milan yatamba nyumbani,
Vita ya Inter Milan dhidi ya Genoa leo |
Inter ikiwa nyumbani ilipata ushindi huo kupitia mabao ya Palacio katika dakika ya 12, Mauro Icardi dakika ya 39 na Nimanja Vidic dakika mbili kabla ya mechi kumalizika, huku bao la wageni lilifungwa na Izzo dakika ya 85.
Katrika mechi nyingine za ligi hiyo,
Atlanta ikiwa nyumbani imelazimishwa sare ya 1-1 na Chievo Verona, Cagliari ikainyoa Cesena mabao 2-1 na Fiorentina ikipata ushindi mtamu nyumbani dhidi ya Palermo baada ya kuinyoa mabao 4-3.
Nayo Hellas Verona ikiitafuna Parma waliowafuata kwao kwa mabao 3-1 na Mahasimu wa jiji la Roma, AS Roma na Lazio zilishindwa kutambiana kwa kutoka sare ya 2-2 na Sampdoria iliilaza Empoli kwa bao 1-0 baadaye Napoli watakuwa wenyeji wa vinara Juventus.
Arsenal yaitoa nishai Stoke City Sanchez azidi kung'ara
Wachezaji wa Arsenal wakipongezana |
Laurent Koscielny akifunga bao la kwanza la Arsenal kwa kichwa |
Ushindi huo umekuja wakati Arsenal ikitoka kupokea kipigo cha mabao 2-0 toka kwa Southampton, ambapo kiungo Mesut Ozil, alirejea uwanjani katika pambano hilo la Emirates baada ya kuwa nje miezi mitatu.
Wenyeji walianza kuandika bao dakika ya 6 kupitia Koscielny kabla ya Sanchez kuongeza la pili dakika ya 33 na kuja kuongeza jingine dakika nne tangu kuanza kwa kipindi cha pili.
Katika pambano hilo Arsenal ilijikuta ikimpoteza beki wake Mathieu Debuchy aliyeumia bega mapema na nafasi yake kuchukuliwa na Bellerin dakika chache baada ya Koscielny kufunga bao la kuongoza kwa kichwa akimaliza krosi ya Sanchez ambaye kwa mabao mawili ya leo amefikisha mabao 12 katika ligi hiyo anayoicheza kwa msimu wa kwanza.
Kwa ushindi hio Arsenal imefikisha pointi 36 na kulingana na Southampton na kukamata nafasi ya tano wakati wapinzani wao wamesaliwa na pointi26 na kusalia kwenye nafasi ya 11.
Muda mchache ujao Manchester United watakuwa uwanja wa Old Trafford kupepetana na Southampton katika mechi nyingine ya ligi hiyo ambayo baadhi ya nyota wa Man Utd waliokuwa nje kwa majeraha watarejea dimbani.
Wachezaji hao ni Daley Blind na Angel di Maria ambao wapo kwenye kikosi cha kwanza cha kocha Louis Van Gaal.
Subscribe to:
Posts (Atom)