STRIKA
USILIKOSE
Wednesday, November 6, 2013
MAAFA! WATU SITA WAUWAWA, 35 WALAZWA MAPIGANO YA WAFUGAJI NA WAKULIMA MVOMERO
WATU sita wamefariki baadhi watatu wakiwa wamechinjwa, huku watu wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa vibaya katika mapigano ya kugombea ardhi kati ya wafugaji na wakulima huko kijiji cha Lukindo wilaya ya Mvomero, mkoani Morogoro.
Taarifa zinasema kuwa, chanzo cha vita hivyo ambavyo vimeleta athari kubwa ikiwemo familia kuparaganyika kwa hofu ya mapigano hayo ni mifugo ya wafungaji kuingia katika shamba moja la mkulima na kula mazao.
Baada ya kitendo hicho kilichotokea jana kinaelezwa kuwa, mifugo ya wafungaji ikikamatwa na wakulima na kisha kutaka walipwe fidia ya Sh Milioni 3 na kushindwa kupatikana muafaka kabla ya Polisi kuja kuingilia kati.
Hata hivyo mbele ya polisi makundi hayo mawili yanadaiwa yalianza kupigana mawe na kufanya Polisi walienda kusuluhisha kutimka na ugomvi huo kuibuka upya mapema leo na kusababisha maafa hayo makubwa.
Inaelezwa watu sita wanne wakiwa ni wakulima wameuwawa wengine wakichinjwa kama kuku na wawili wakiwa ni wafungaji na watu 35 wamejeruhiwa vibaya katika miili yao kwa silaha za jadi na kulazwa hospitali ya Bwagala huko huko Mvomero kwa sasa.
Jeshi la Polisi linaelezwa limefanikiwa kutuliza mapigano hayo, lakini watu waliojeruhiwa wakiwa hoi baadhi wakijeruhiwa vibaya na kulazimisha kufanyiwa upasuaji kunusuru maisha yao, ingawa mashuhuda wanasema huenda idadi ya vifo vilivyotokana na mapigano hayo vikaongezeka.
Yanga, Azam, Mbeya City nani kukaa kileleni kesho
Wageni Mbeya City kuweka rekodi kesho kwa Azam? |
Mabingwa watetezi watamaliza vipi kesho kwa Oljoro? |
Yanga itaikaribisha Oljoro JKT kutoka Arusha kwenye uwanja wa Taifa, huku Azam na Mbeya zilizopo juu ya Yanga zikiumana zenyewe kwa wenyewe katika pambano litakalochezwa kwenye uwanja wa Chamazi.
Vinara Azam watafanya nini kesho kwa Mbeya City? |
Azam wanaongoza msimamo kwa tofauti na yamabo ya kufungwa na kufunga licha ya kulingana pointi na Mbeya City iliyoipanda daraja msimu huu zote zikiwa na pointi 26 kila moja, wakati Yanga wenyewe waliopo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 25.
Kutokana na hali hiyo iwapo Yanga itashinda na wapinzani wake kutoka sare watakalia kiti cha uongozi, lakini kama itashinda na Azam au Mbeya City ikashinda ina maana Yanga itashika nafasi ya pili na moja kati ya timu hizo mbili itaangukia katika nafasi ya tatu na nyingine kukalia kiti cha uongozi.
Tayari kumekuwa na tambo kwa timu za Azam na Mbeya City kuhusiana na pambano lao, lakini Yanga wenyewe wanaombea waendelee rekodi yao ya kutoa dozi kwa timu za maafande kwa kuikwanyua Oljoro JKT katika pambano lao huku wakiombea wapinzani wake kutoka sare.
Mechi nyingine kwa kesho itawakutanisha Rhino Rangers yua tabora itakayovaana na maafande wa Prisons ya Mbeya kwenye uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.
Je, ni Yanga, Azam au Mbeya City watauaga mwaka kileleni hadi mwaka 2014 au watauvuruga vipi msimamo wa ligi hiyo katika nafasi ya Tatu Bora? Tusubiri tuone hiyo kesho!
Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2013-2014
P W D L F A GD PTS
01.Azam 12 07 05 00 20 07 13 26
02.Mbeya City 12 07 05 00 16 07 09 26
03.Yanga 12 07 04 01 28 11 17 25
04.Simba 13 06 06 01 26 13 13 24
05.Kagera Sugar 13 05 05 03 14 09 05 20
06.Mtibwa Sugar 13 05 05 03 19 17 02 20
07.Ruvu Shooting 13 04 05 04 15 15 00 17
08.Coastal Union 13 03 07 03 10 07 03 16
09.JKT Ruvu 13 05 00 08 10 16 -06 15
10.Rhino Rangers 12 02 04 06 09 16 -05 10
11.Oljoro 12 02 04 06 09 16 -07 10
12.Ashanti 13 02 04 07 12 24 -12 10
13.Prisons 12 01 05 06 05 15 -10 08
14.Mgambo 13 01 03 09 03 23 -20 06
Wafungaji:
10- Tambwe Amisi (Simba)
9- Elias Maguri (Ruvu Shooting)
8- Hamis Kiiza (Yanga), Juma Luizio (Mtibwa Sugar)
7- Kipre Tchetche (Azam)
6- Themi Felix (Kagera Sugar)
5- Tumba Sued (Ashanti Utd), Didier Kavumbagu, Mrisho Ngassa (Yanga)
4- Peter Michael (Prisons), Jerry Santo (Coastal Union), Jerry Tegete (Yanga), Betram Mombeki (Simba), Bakar Kondo (JKT Ruvu)
3- Haruna Chanongo, Jonas Mkude (Simba), Paul Nonga (Mbeya City), Salum Machaku (JKT Ruvu), Jerry Santo (Coastal Union), Mcha Khamis (Azam), Amir Omary (Oljoro), Ramadhani Singano (Simba)
2- Haruna Moshi, Crispian Odulla (Coastal Union), Saady Kipanga (Rhino Rangers), Mwagani Yeya, Jeremiah John, Peter Mapunda,(Mbeya City), Godfrey Wambura (Kagera Sugar), Shaibu Nayopa (JKT Oljoro), Joseph Kimwaga (Azam), Shaaban Nditti, Shaaban Kisiga (Mtibwa Sugar), Said Dilunga (Ruvu Shooting)
1- Abdi Banda, Danny Lyanga (Coastal Union), Henry Joseph, Joseph Owino, Gilbert Kazze (Simba), Haruna Niyonzima, Nizar Khalfan, Simon Msuva, Frank Dumayo, Mbuyi Twitte, Oscar Joshua (Yanga), Iman Joel, Salum Majid, Mwalimu Musuku, Kamana Salum, Hussein Abdallah, Abbas Mohammed (Rhino Rangers), Gaudence Mwaikimba, Seif Abdallah, Aggrey Morris, John Bocco, Faridi Maliki, Hamphrey Mieno, Salum Abubakar, Erasto Nyoni (Azam), Steven Mazanda, Richard Peter, Deo Deus (Mbeya City), Laurian Mpalile (Prisons-OG), Shaaban Susan, Jerome Lembeli, Cosmas Ader (Ruvu Shooting), Masoud Ally, Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Shaaban Juma, Anthony Matangalu, Paul Maono(OG), Samir Luhava (OG), John Matei, Mwinyi Ally, Hussein Sued, Said Maulid (Ashanti Utd), Abdallah Bunu, Emmanuel Switta, Amos Mgisa (JKT Ruvu), Fully Maganga, Hamis Msafiri (Mgambo JKT), Seleman Kibuta, Daud Jumanne, Maregesi Marwa, Clement Douglas, Salum Kanoni (Kagera Sugar), Paul Malipesa, Expedito Kidulo, Nurdin Mohammed, Fikiri Mohammed (Oljoro JKT)
Matokeo yote ya mechi za Duru la KwanzaDURU LA KWANZA
Agosti 24, 2013
Yanga vs Ashanti United (5-1)
Mtibwa Sugar vs Azam (1-1)
Oljoro JKT vs Coastal Union (0-2)
Mgambo JKT vs JKT Ruvu (0-2)
Rhino Rangers vs Simba (2-2)
Mbeya City vs Kagera Sugar (0-0)
Ruvu Shooting vs Prisons (3-0)
Agosti 28, 2013
Mtibwa Sugar vs Kagera Sugar (1-0)
Rhino Rangers vs Azam (0-2)
JKT Ruvu vs Prisons (3-0)
Mbeya City vs Ruvu Shooting (2-1)
Mgambo vs Ashanti United (1-0)
Oljoro JKT vs Simba (0-1)
Yanga vs Coastal Union (1-1)
Sept 14, 2013
Simba vs Mtibwa (2-0)
Coastal Union vs Prisons (0-0)
Ruvu Shooting va Mgambo JKT (1-0)
Oljoro JKT vs Rhino Rangers (1-1)
Mbeya City vs Yanga (1-1)
Kagera Sugar vs Azam (1-1)
Ashanti United vs JKT Ruvu (0-1)
Sept 18, 2013
Prisons vs Yanga (1-1)
Simba vs Mgambo JKT (6-0)
Kagera Sugar vs JKT Oljoro (2-1)
Azam vs Ashanti United (1-1)
Coastal Union vs Rhino Rangers (1-1)
Mtibwa Sugar vs Mbeya City (0-0)
Ruvu Shooting vs JKT Ruvu (1-0)
Sept 21, 2013
Mgambo JKT vs Rhino Rangers (1-1)
Prisons vs Mtibwa Sugar (1-1)
Simba vs Mbeya City (2-2)
Kagera Sugar vs Ashanti United (3-0)
Sept 22, 2013
JKT Ruvu vs Oljoro JKT (0-1)
Azam vs Yanga (3-2)
Coastal Union v Ruvu Shooting (1-0)
Sept 25, 2013
Rhino Rangers vs Ashanti Utd (2-0)
Sept 28, 2013
Yanga vs Ruvu Shooting (1-0)
Rhino Rangers v Kagera Sugar (0-1)
Mbeya City vs Coastal Union (1-1)
Mgambo JKT vs Oljoro JKT (0-0)
Sept 29, 2013
Ashanti Utd vs Mtibwa Sugar (2-2)
JKT Ruvu vs Simba (0-2)
Prisons vs Azam (1-1)
Okt 05, 2013
Ruvu Shooting vs Simba (1-1)
JKT Ruvu vs Kagera Sugar (2-1)
Coastal Union vs Azam (0-0)
Oljoro JKT vs Mbeya City (1-2)
Okt 06, 2013
Mgambo JKT vs Prisons (0-1)
Yanga vs Mtibwa Sugar (2-0)
Okt 09, 2013
Rhino Rangers vs Mbeya City (1-3 )
Oljoro JKT vs Ruvu Shooting (2-2)
Azam vs Mgambo JKT (2-0)
Mtibwa Sugar vs JKT Ruvu (2-1)
Okt 12, 2013
Kagera Sugar vs Yanga (1-2)
Simba vs Prisons (1-0)
Ashanti Utd vs Coastal Union (2-1)
Okt 13, 2013
Ruvu Shooting vs Rhino Rangers (1-0)
Mgambo JKT vs Mbeya City (0-1)
Azam vs JKT Ruvu (3-0)
Mtibwa Sugar vs Oljoro JKT (5-2)
Okt 16, 2013
Ashanti Utd vs Prisons (2-1)
Okt 19, 2013
Kagera Sugar vs Coastal Union (1-0)
Oljoro JKT vs Azam (0-1)
Mtibwa Sugar vs Mgambo JKT (4-1)
Mbeya City vs JKT Ruvu (1-0)
Ashanti Utd vs Ruvu Shooting (2-2)
Okt 20, 2013
Simba vs Yanga (3-3)
Okt 23, 2013
Coastal Union vs Simba (0-0)
Prisons vs Kagera Sugar (0-0)
Yanga vs Rhino Rangers (3-0)
Okt 28, 2013
Simba vs Azam (1-2)
Ruvu Shooting vs Kagera Sugar (1-1)
Coastal Union vs Mtibwa Sugar (3-0)
Oljoro JKT vs Ashanti Utd (0-0)
Okt 29, 2013
Prisons vs Mbeya City (0-2)
Rhino Rangers vs JKT Ruvu (1-0)
Yanga vs Mgambo JKT (3-0)
Okt 31, 2013
Simba vs Kagera Sugar (1-1)
Nov 1, 2013
JKT Ruvu vs Yanga (0-4)
Nov 2, 2013
Mgambo JKT vs Coastal Union (0-0)
Azam vs Ruvu Shooting (3-0)
Mtibwa Sugar vs Rhino Rangers (1-0)
Mbeya City vs Ashanti Utd (1-0)
Nov 3, 2013
Prisons vs Oljoro JKT (0-1)
Nov 06, 2013
JKT Ruvu vs Coastal Union (1-0)
Ashanti Utd vs Simba (2-4)
Ruvu Shooting vs Mtibwa Sugar(2-2)
Kagera Sugar vs Mgambo JKT (2-0)
Nov 07, 2013
Azam vs Mbeya City (-)
Rhino Rangers vs Prisons (-)
Yanga vs Oljoro JKT (-)
Elias Maguri, Juma Luizio wazidi kukifukizia kiatu cha dhahabu Mtibwa, Ruvu zikitoka sare Mabatini
Juma Luizio 'Ndanda' |
Maguri amefunga mabao hayo katika pambano la timu yake kufungia duru la kwanza kwenye uwanja wa Mabatini, Mlandizi na kuonyesha dhamira yake ya kunyakua kiatu hicho cha dhahabu ambacho msimu uliopita kilichukuliwa na 'Pro' Kipre Tchetche.
Mabao ya wapinzani wao yaliwekwa kimiani na mshambuliaji anayezidi kuja juu nchini, Juma Luizio'Ndanda' ambaye alifikisha bao lake la nane msimu huu na kumfikia Hamis Kiiza huku akibakisha mawili kumkamata Tambwe.
Bao jingine la Mtibwa liliwekwa kimiani na kiungo mzoefu nchini, Shaaban Kisiga 'Marlon' na kuifanya timu yao ya Mtibwa kupata pointi moja na kufikisha pointi 20 na kushika nafasi ya sita ikiipisha Kagera kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.
JKT Ruvu wazinduka waikwanyua Coastal, Kagera yaua 2-0
JKT Ruvu iliyozinduka leo Chamazi |
Kagera iliyoikwanyua Mgmabo mabao 2-0 |
Nako Kaitaba mabao mawili ya Themi Felix na Seleman Kibuta yalitosha kuizima Mgambo JKT iliyosafiri hadi mjini Bukoba baada ya kuwanyuka mabao 2-0 katika pambano jingine la Ligi Kuu Tanzania Bara.
Kwa matokeo hayo Kagera imefikisha pointi 20 huku JKT Ruvu ikifikiosha pointi 15 na kusalia kwenye nafasi ya tisa katika msimamo wa ligi hiyo. Huku bao la Themi anayewania Tuzo ya Mwanasoka Bora inayoendeshwa na gazeti la MWANASPOTI imemfanya afike jumla ya mabao sita, huku Bakar Kondo akifika bao lake la nne katika orodha ya wafungaji inayoongoza na Amissi Tambwe wa Simba mwenye mabao 10 na kufuatiwa na Elias Maguri wa ruvu Shooting kisha Hamis Kiiza 'Diego' mwenye mabao nane akiwa na nafasi ya kuongeza idadi kwa vile timu yake ya Yanga itashuka kesho dimbani kuvaana na Oljoro JKT.
MAKAMBA MGENI RASMI TUZO ZA MWANASOKA BORA
NAIBU Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia, Mh. January Makamba
anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla ya utoaji wa tuzo kwa mwana
soka bora wa mwaka katika ligi kuu ya Vodacom mwaka 2013, itakayofanyika
katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Tuzo
hiyo itashuhudia wachezaji walioingia hatua ya Tano bora, AMRI KIEMBA,
HARUNA NIYONZIMA, SHOMARI KAPOMBE, THEMI FELIX, na KELVIN YONDANI
wakichuana kuwania umwamba wa soka Tanzania, Baada ya kupigiwa kura na
mashabiki na Kamati maalum chini ya Mwenyekiti wake Zamoyoni Mogela
kuchambua majina hayo kulingana na kura walizopata.
Akizungumza juu ya hafla hiyo, Mkuu wa
Kitengo cha Masoko na Mawasiliano Kelvin Twissa amesema, wanafurahi kuwa
sehemu ya maendeleo ya soka nchini na siku zote kampuni yake imekuwa
msitari wa mbele katika kuunga mkono michezo nchini, hususani mchezo wa
soka na kuhakikisha unakuwa moja ya ajira muhimu kwa watanzania.
“Vodacom tumeendelea kuwa wadau muhimu
katika mapinduzi ya soka la Tanzania, sasa mpira umekuwa zaidi ya
burudani kwa watanzania kutokana na chachu ambayo tumeiweka tangu tuanze
kudhamini ligi kuu, ambayo sasa imekuwa na ushindani mkubwa na thamani
yake inazididi kupanda siku hadi siku,” alisema Twissa.
Aidha Twissa amesema kampuni yake
itaendelea kushirikiana na wadau wengine wote wanaopenda maendeleo ya
soka bila kusita kutokana na namna ambavyo kampuni yake imejidhatiti
katika kuinua michezo nchini.
“Mafanikio yanayopatikana katika soka
letu sasa hayajapatikana hivivi ni kutokana na dhamira tuliyoiweka
katika kuinua mchezo huu wa soka na uwekezaji mkubwa tulioufanya hadi
sasa, watu ambao wanaleta mafanikio haya ni wachezaji ambao wamekuwa
wanapambana kufa na kupona kutoa burudani kwa Watanzania, Ni lazima
tuwaenzi wachezaji hawa kwa njia tofauti tofauti,” alisema Twissa.
Kwa upande wake Meneja Masoko wa MCL
Bernad Mukasa amesema kuwa, wamefurahi kushirikiana na Naibu waziri Mh.
Makamba katika utoaji wa tuzo hizi, ambazo zinatambua mchango wa
wanasoka nchini.
“Tuzo hizi zinatambulika rasmi kwa jina la zitaitwa MWANASPOTI
BORA WA SOKA WA VODACOM 2013. Ni za kipekee na za kwanza kabisa nchini
kwa wigo wa wachezaji wanaohusishwa, ushirikishwaji wa uteuzi wa
mshindi, na vigezo husika.” alisema Mukasa na kuongeza.
“Kwa mwaka huu, licha ya kumpata
Mwanaspoti Bora wa soka wa mwaka , pia tutatoa Tuzo kwa “categories”
zaidi ya 10 ikiwemo kocha bora, mwamuzi bora, mchezaji bora wa kike,
mchezaji bora chipukizi, “1st eleven”, goli bora, mchezaji
bora wa kigeni, Mchezi bora wa kulipwa anayecheza nje, na Kipengele
kingine kitajulikana siku ya ijumaa,” alisema Mukasa.
Mukasa alihitimisha kwa kutoa wito kwa
Watanzania kuendelea kuwapigia kura wachezaji hao kwa kuandika ujumbe
mfupi unaoanza na neno KURA kisha jina la mchezaji anayemchagua kati ya
hao waliotajwa na kisha kutuma kwenda namba 15678.
Simba yamaliza hasira zake kwa Ashanti, Tambwe, Mombeki nouma
Mombeki akitafuta njia ya kumtoka beki wa Ashanti huku, Haruna Shamte akiwa tayari kwa msaada (picha: Lenzi ya Michezo) |
KAMA walivyoanza ndivyo walivyomaliza duru la kwanza, Ashanti United 'Wana wa Jiji' wameshindwa kuhimili hasira za 'mnyama' baada ya jioni hii kukubali kipigo cha aibu cha mabao 4-2 kutoka kwa Simba.
Ashanti Utd iliyorejea Ligi Kuu msimu huu, ilikumbana na kipigo hicho kwenye uwanja wa Taifa ikiwa ni miezi karibu mitatu tangu walipolala kwa mabao 5-1 na Yanga katika mechi ya kufunga dimba la ligi hiyo.
Mabao mawili ya Betram Mombeki na mengine ya Ramadhani Singano 'Messi' na Amissi Tambwe yalitosha kuiangamiza Ashanti Utd ambayo kabla ya pambano hilo waliapa kutoa kisago kwa wapinzani wao hao.
Messi, ndiye aliyeanza kufungua karamu ya mabao ya Simba katika dakika ya 8 kabla ya Ashanti kusawazisha kwenye dakika za nyongeza za kipindi cha kwanza kupitia kwa Hussein Sued.
Kipindi cha pili kilianza kwa Simba kucharuka kwa kupata mabao ya harakaharaka kupitia Tambwe aliyefunga dakika ya kwanza tu ya kipindi hicho na kufikisha jumla ya mabao 10 katika orodha ya ufungaji bora.
Dakika ya nne baadaye Mombeki alifunga bao la tatu kabla ya kuongeza jingine dakika ya 15, wakati huo Ashanti ikiwa imerejesha bao jingine na la pili kwao kupitia mkongwe Said Maulid 'SMG' aliyevurumusha kombora lililomshinda kipa Abuu Hashim.
Kwa matokeo hayo Simba imefikisha jumla ya pointi 24 na kumaliza mechi zake za duru la kwanza, Ashanti ikisaliwa na pointi 10, huku pia ikijikuta ikimaliza pambano hilo bila kipa wake, Amani Simba kuwepo uwanjani kwa kulimwa kadi nyekundu na mwamuzi Andrew Shamba.
Kipa huyo alipewa kadi hiyo baada ya kuudaka mpira nje ya eneo lake akizuia kupigwa kanzu na nyota wa mchezo wa leo, Ramadhani Singano Messi.
NEWZ ALERT: MFANYAKAZI TBC APIGWA RISASI NA KUFARIKI
No comments
MFANYAKAZI
wa Shirika la Utangazaji Nchini TBC, pichani, RAMADHAN GIZE ameuawa kwa
kupigwa risasi na watu wanaosaidiwa kuwa ni majambazi usiku wa kuamkia
leo katika eneo la UBUNGO Maziwa Jijini DSM.
Tukio hilo limetokea baada ya watu hao kuvamia duka moja katika eneo hilo la UBUNGO MAZIWA kwa lengo la kupora, ambapo mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la MWARAMI RAJABU amejeruhiwa na watu hao wanasadikiwa kuwa ni majambazi.
Chanzo:MICHUZI
Msiba! DJ RANKEEM RAMADHANI HATUNAYE DUNIANI
KWA mujibu wa taarifa zilizopatikana jioni ya leo, zinaeleza kuwa mmoja wa Ma Dj Maarufu sana
hapa jijini Dar na Tanzania kwa ujumla ,Dj Rankeem Ramadhani amefariki mchana huu.
Inaelezwa kuwa DJ Rankeem aliyewahi kufanya kazi Radio One Stereo na vituo vingine mbalimbali alifariki kwenye hospitali ya Mwananyamala baada ya kufanyiwa upasuaji kutokana na tatizo la kidole utumbo.
Mwili wa mkali huyo katika kupangilia muziki aliyetingisha kwa miaka kadhaa, umehifadhiwa kwenye hospitalini hiyo ikifanywa mipango ya mazishi yake.
Mwili wa mkali huyo katika kupangilia muziki aliyetingisha kwa miaka kadhaa, umehifadhiwa kwenye hospitalini hiyo ikifanywa mipango ya mazishi yake.
Taarifa zaidi juu ya msiba huu zitaletwa kwenu kadri tukavyopata kwa undani zaidi ikiwemo kujua atazikwa lini na wapi, ingawa inaelezwa huenda akazikwa kesho jijini Dar es Salaam.
MICHARAZO inatoa pole kwa familia, ndugu jamaa na wadau wote wa habari na muziki kwa msiba wa gwiji hilo, na kuwataka kuwa na subira katika kipindi hiki kigumu kwa kukumbuka kuwa Sote tu wa Allah (SW) na Kwake Tutarejea.
MICHARAZO inatoa pole kwa familia, ndugu jamaa na wadau wote wa habari na muziki kwa msiba wa gwiji hilo, na kuwataka kuwa na subira katika kipindi hiki kigumu kwa kukumbuka kuwa Sote tu wa Allah (SW) na Kwake Tutarejea.
Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi-AMEN
Manchester City yaweka rekodi Ulaya, Juve, Man Utd wabanwa
Aguero akishangulia moja ya mabao yake ya jana kwa CSKA |
Bale akiwatungua Juve walipopata sare ya 2-2 |
Mabao mawili ya Sergio 'kun' Aguero na hat trick ya Alvaro Negredo yalitosha kuwavusha wakali hao wa EPL mbele ya Warusi hao.
Bapa la kwanza la Aguero lilitokana na mkwaju wa penati baada ya David Silva kuchezwa vibaya kisha kuongeza jingine kabla ya Negredo kufunga mabao mengine, huku yale ya wageni yote mawili yakifungwa na Doumbia.
Katika mechi nyingine za kundi hilo, Mabingwa watetezi Bayern Munich ilipata ushindi kiduchu wa bao 1-0 na kuendeleza rekodi ya kushindwa kwa asilimia 100 mbele ya Victoria, Juventus ya Italia ikiwa nyumbani ilijitutumua na kuibana Real Madrid na kutoka nao sare ya 2-2, japo walishindwa kuwazuia Cristiano Ronaldo na Bgareth Bale kuwatungua kwani wote wawili walifunga mabao ya wahispania hao.
Manchester United ikiwa ugenini ililazimishwa suluhu na Real Sociedad, huku Shakhtar Doneksk na Bayer Leverkusen nao wakitoka suluhu na mabinhwa wa Ufaransa PSG na Anderletch zikitoka pia sare ya 1-1.
Benfica ikiwa ugenini ililala kwa bao 1-0 kwa Olympiakos na Galatasaray ilikubali kichapo cha ugenini cha bao 1-0 toka kwa Kobenhavn.
Ligi hiyo itaendeela tena usiku wa leo kwa michezo minane baadhi ikiwakutanisha Arsenal itakayokuwa ugenini dhidi ya Borussia Dotmund, Barcelona dhidi ya Ac Milan na Ajax itaikaribisha Celtic.
Mechi nyingine ni kati ya Chelsea dhidi ya Schalke 04, Napoli watakaoumana na Olympique Marseille, Zenit na Porto na Atletico Madrid itakayoumana na Viena.
Subscribe to:
Posts (Atom)