|
Juma Nyosso enzi akiichezea Simba |
HATIMAYE beki kisiki wa zamani wa Simba na Coastal Union, Juma Said Nyosso amejiunga na kikosi cha Mbeya City ya Mbeya kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Akizungumza mara baada ya kuisaini mkataba huo kwenye ofisi za timu
zilizopo jengo la Mkapa Hall jijini Mbeya, Nyoso aliyewahi kucheza
pia Ashanti United, alisema amekubali
kujiunga na City kwa mkataba wa mwaka mmoja kwa imani kuwa utatosha
kuushawishi uongozi wa timu kumpa mkataba mrefu zaidi mara baada ya huu
wa sasa.
Kariobu nusu msimu beki huyo wa kati alikuwa hana timu yoyote anayoichezea tangu aachwe na Coastal mapema mzimu huu.
“City ni timu nzuri na imekuwa hivyo toka ilipoanzishwa miaka minne
iliyopita, matokeo yaliyoo sasa ni sehemu ya soka ambayo timu yoyote
inaweza kuyapata, nimekubari kujiunga na timu kwa mkataba wa mwaka mmoja
kwa sababu naamini uwezo wangu uwanjani utawashawishi viongozi kunipa
mkataba mrefu zaidi pindi huu utakapo malizika na nina amini hili
linawezekana kwa sababu nataka kukaa kwenye timu hii mpaka mpira wangu
utakapoisha” alisema Nyosso
Akiendelea zaidi beki huyo aliyewahi pia kucheza kwenye kikosi cha timu
ya Taifa ‘Taifa Stars’ alisema kuwa mafanikio iliyopata Mbeya City msimu
uliopita yamekuwa sababu kubwa ya yeye kukubari kujiunga na City huku
akiamini kuwa amekuja kuongeza nguvu kwenye timu bora ili kuhakikisha
mafanikio ya msimu uliopita yanafanikiwa tena.
K wa upande wake Katibu Mkuu wa City Emmanuel Kimbe alimshukuru Nyosso
kwa kukubari kujiunga na timu hii huku akiamini kuwa uzoefu alionao
mchezaji huyo utasaidia kuimarisha safu ya ulinzi kwenye kikosi cha
City.
“Tunamshukuru kukubari kujiunga nasi, imani yetu kubwa kwamba uzoefu
alionao utasaidia kuimarisha safu yetu ya ulinzi, hasa ukizingatia
matokeo tuliyopata katika michezo saba ya mwanzo wa Ligi hii” alisema
Kimbe huku kauli yake hiyo ikiungwa mkono na Kocha Mkuu Juma Mwambusi.
Kwa sasa Nyosso tayari yuko na kikosi cha City kilichosafiri kwenda mjini Songea kwa ajiri ya michezo ya kirafiki.