STRIKA
USILIKOSE
Saturday, February 22, 2014
HII NDIYO TOP 10 YA WALIONG'ARA KIDATO CHA NNE
WASICHANA Wasichana waliofanya vizur kwenye mtihani huo wameongozwa na Robina Nicholaus (Marian Girls), Magrath Kakoko (St Francis), Joyceline Leonard Marealle (Canossa), Safarina W Mariki, Abby T Sembuche na Janeth Urassa (Marian Girls). Wengine ni Angle Ngulumbi (St Francis), Getrude James Mande wa Precious Blood (Arusha), Violet Mwasenga wa St Francis na Catherine Swai kutoka Marian Girls.
WAVULANA
Wavulana waliofanya Vizuri ni Sunday Mrutu wa Anne Marie, Nelson Rugola Anthony na Emanuel Mihuba Gregory wote kutoka Kaizirege, Razack Hassan wa St Matthew’s (Pwani) na Hamis Msangi kutoka Eangles (Pwani). Wengine ni Joshua Zumba wa Uwata (Mbeya), Brian Laurent na Mohamed Ally wa Marian Boys (Pwani), Shahzill Msuya wa St Amedeus (Kilimanjaro) na Shabani Hamisi Maatu wa Mivumon Islamic Seminary (Dar es Salaam).
Simba, Azam kuvuna nini kesho Dar?
Simba itavuna nini kwa JKT Ruvu? |
JKT Ruvu itaendelea kuwa urojo kesho katika ligi kuu mbele ya Simba? |
Azam watahimili vishindo vya Prisons baada ya kung'oka Kombe la Shirikisho Afrika? |
Prisons wataendeleza ubabe wao walioonyesha kwenye mechi za duru la pili kesho kwa Azam au...?! |
Mechi hizo mbili zitachezwa kesho jijini Dar es Salaam zikiwa ndiyo pekee katika mfululizo wa Ligi Kuu Tanzania bara kukamilisha mzunguko wa 19.
Azam wanaorejea kwenye ligi baada ya kung'olewa kwenye Kombe la Shirikisho la Ferroviario de Beira wataivaa Prisons kwenye uwanja wa Chamazi, nje kidogo ya jiji, huku Simba itaikaribisha Ruvu inayonolewa kwa sasa na kocha Fred Minziro kwenye uwanja wa Taifa.
JKT walikuwa wahanga wa Prisons kwa kukubali kipigo cha 6-0 na kuweka rekodi ya kufungwa mabao nande katika mechi mbili zilizopita, kipigo kingine walipewa na ndugu zao Ruvu Shooting ambayo leo imekumbana na dhahama kwa kulazwa mabao 7-0 na watetezi Yanga.
Mechi hizo zinasubiriwa kwa hamu kwa sababu ndizo zinazoweza kubadilisha msimamo wa ligi hiyo kwa timu zilizopo kwenye Nne Bora, kwani Azam ikishinda itarejea kwenye nafasi yake ya kwanza ambayo imechukuliwa na Yanga jioni ya leo baada ya ushindi wake dhidi ya Ruvu.
Simba nayo ikishinda itaiengua Mbeya City na kukalia nafasi ya tatu baada ya vijana hao wa Juma Mwambusi kuchezea kipigo toka kwa Coastal Union jijini Tanga jioni ya leo.
Simba ina pointi 32, tatu nyuma ya Mbeya City, lakini ikiwa na uwiano mzuri ya mabao ya kufunga na kufungwa.
Azam wenyewe wana pointi 36, mbili zaidi ya Yanga wanaoongoza sasa kwa pointi 38, hali inayofanya mechi za kesho kuwa na msisimko mkubwa mashabiki wakitaka kuona Prisons itaendeleza rekodi yake ya kukusanya pointi 10 katika mechi zake nne za duru la pili na kuvunja mwiko wa Azam kupoteza mchezo!
Wana Lambalamba ndiyo timu pekee ambayo haijapoteza mechi yoyote katika ligi ya msimu huu na katika mechi zake za duru la pili imekuwa ikigawa dozi nene hali inayoifanya Prisons kuwavaa wapinzani wao hao kwa tahadhari kubwa.
Tayari timu zote nne zimekuwa zikitambiana kila moja ikidai imejiandaa kushinda, lakini matokeo ya mwisho yatategemea baada ya dakika 90 kwa namna timu hizo zilivyopigana katika kuwakabili wapinzani wao.
Simba ambayo imekuwa na mwenendo mbovu tangu duru la pili lianze itataka ushindi ili kutuliza munkari wa mashabiki na wanachama wao baada ya kujikuta wakipoteza pointi saba kati ya tisa katika mechi zao tatu zilizopita ikiambulia sare mbili dhidi ya Mtibwa Sugar na Mbeya City na kulazwa na Mgambo JKT.
Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2013-2014
P W D L F A GD PTS
01.Yanga 17 11 05 01 41 12 29 38
02.Azam 16 10 06 00 29 10 19 36
03.Mbeya City 19 09 08 02 24 16 08 35
04.Simba 18 08 08 02 33 16 17 32
05.Kagera Sugar 19 06 08 05 16 15 01 26
06.Coastal Union 19 05 10 04 14 09 05 25
07.Mtibwa Sugar 19 06 07 06 23 23 00 25
08.Ruvu Shooting 19 06 07 06 20 26 -06 25
09.Mgambo 19 05 05 09 12 27 -15 20
10.Prisons 17 04 07 05 15 16 -01 19
11. JKT Ruvu 18 06 01 11 13 27 -14 19
12.Oljoro 20 02 09 09 15 30 -15 15
13.Ashanti 18 03 05 10 15 30 -15 14
14.Rhino Rangers 19 02 07 10 12 23 -11 13
Real Madrid yapanda kileleni Hispania
MABAO matatu yaliyofungwa na Illaramendi katika dakika ya 34, Gareth Bale la dakika ya 72 na lile la Isco la dakika ya 81 yalitosha kuipaisha Real Madrid hadi kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Hispania (La Liga) walipoifumua Elche mabao 3-0.
Madrid wakiwa uwanja wa nyumbani wa Santiago Bernabeu ilionyesha dhamira ya kupata ushindi kwa Illarramendi kufunga bao kwa pasi ya Pepe, bao lililodumu hadi mapumziko.
Bale mchezaji ghali kuliko wote katika usajili, alitupia bao la pili akimalizia kasi ya Xabi Alonso kabla ya Karim Benzema kumtengea Isco kufunga bao la tatu.
Kwa ushindi huo, Madrid imefikisha pointi 63 na kuziengua kileleni Barcelona na Atletico Madrid zenye pointi 60 kila moja ambazo zina mchezo mmoja mkononi, Barca wakitarajia kushuka dimbani muda mchache baadae ugenini dhidi ya Real Sociedad, huku wenzao wakitarajiwa kucheza kesho.
Arsenal, Man City, West Ham 'zaua' England
Wachezaji wa Arsenal wakishangilia moja ya mabao yao leo |
Wachezaji wa West Ham United wakishangilia mabao yao |
Yaya Toure akifunga bao lililoipa ushindi Manchester City |
Vijana wa Gunners wakiwa uwanja wa nyumbani wa Emirates ilipatra ushindi huo ikitoka kulala mabao 2-0 dhidi ya Bayern Munich katika Ligi ya mabingwa wa Ulaya.
Mabao ya Oliver Giroud aliyefunga mawili katika dakika ya tano na 31 kabla ya Tomas Rosicky kufunga la tatu dakika ya 42 na kwenda mapumziko wakiongoza kwa mabao 3-0.
Kipindi cha pili kilianza kwa Arsenal kuongeza bao la nne likifungwa Laurent Koscielny katika dakika ya 57 na bao pekee la Sunderland likifungwa na Giaccherini' katika dakika ya 81.
Ushindi huo umeifanya Arsenal kubaki nafasi ya pili nyuma ya Chelsea kwa tofauti ya pointi moja, Arsenal ikiwa na 59 na Chelsea 60 huku wakifuatiwa na Manchester City ilipata ushindi wa 1-0 nyumbani dhidi ya Stoke City.
Bao hilo pekee katika mchezo huo uliochezwa uwanja wa Etihad lilifungwa na Yaya Toure katika dakika yua 70.
Katika mechi nyingine Hull City imepata ushindi mnono ugenini kwa kuilaza Cardiff City mabao 4-0, huku West Bromwich ikilazimishwa sare ya 1-1 na Fulham waliotangulia kupata bao mapema.
Nayo West Ham United ikiwa nyumbani iliishindilia Southampton kwa mabao 3-1.
Mechi inayotarajiwa kuchezwa muda mfupi ujao ni kati ya mabingwa watetezi, Manchester United iliyopo ugenini dhidi ya Crystal Palace.
KILELE CHA MIAKA 10 YA ‘LADY IN RED’ KUFANYIKA NYUMBANI LOUNGE
* Kutolewa vyeti maalum
* Wadau kukata keki ya pamoja
* Slim kutumbuiza
Na Andrew Chale
KILELE cha Miaka 10 na ‘After Party’ ya onesho la mavazi la ‘Lady
in Red Super Brand’ kinatarajia kufikia
tamati usiku wa Jumamosi, Februari 22, ndani ya Ukumbi ulio na mgahawa wa
kisasa na hadhi ya juu wa kwa jiji la Dar es Salaam, wa Nyumbani Lounge, huku
kukitarajiwa kuwa na surprise mbali mbali kwa wadau watakaojitokeza.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Fabak Fashions, Asia Idarous Khamsin, wandaaji wa Lady in red,
kila mwaka hapa nchini, alisema, ‘after party’ hiyo ni maalum kwa ajili ya kutoa shukrani na vyeti maalum kwa wadau wanaoliunga mkono jukwaa la Lady in red kwa kipindi chote
hadi kufikia hapo ambapo pia watapata wasaha wa kukata keki ya ukumbusho.
“After party ya miaka 10 ya Lady in red, kwa mwaka huu
itakuwa ya aina yake sambamba na surprise, hivyo nyote munakaribishwa na hakuna
kiingilio na kwa watakaokuwa tayari kujiunga siku maalum pale Nyumbani Lounge, wafike katika duka la Fabak Fashion, lililopo jirani na kituo cha Msasani, Kwa Mwalimu
Nyerere au kwa kupiga simu namba 0713263363
ama 0784263363” alisema Asia Idarous.
Na kuongeza kuwa, pia tiketi maalum za bure zitatolewa
mlangoni Nyumbani Lounge, kwa wadau watakaofika. Aidha, alisema msanii wa
muziki wa kizazi kipya, Slim Guapo Sosa anayetamba na kibao cha ‘ LOVE YOU ’ na
vingine vingi anatarajiwa kuwakonga nyoyo watakaojitokeza kwenye ‘after party’
hiyo.
Party hiyo imedhaminiwa na
wadhamini mbali mbali wakiwemo Times fm, Michuzi media group, mo blog,
Nyumbani Lounge, Darling air, G one Media na wengine wengi.
Mwisho
Mtibwa Sugar yaona mwezi yainyuka Ashanti, Mgambo haikamatiki
Ashanti United waliyolazwa na Mtibwa Sugar |
Mtibwa Sugar iliyoona mwezi |
Oljoro JKT waliogeuzwa asusa na Mgambo mjini Arusha |
Mgambo inayoendelea kugawa dozi kwa wapinzani wao katika Ligi Kuu |
Mabao ya Mohammed Mkopi na Abdallah Juma ya kila kipindi yalitosha kuipa Mtibwa iliyokuwa uwanja wa nyumbani wa Manungu Complex pointi tatu muhimu vijana hao wa Mecky Mexime katika ligi hiyo inayozidi kuchanja mbuga.
Mshambuliaji wa zamani wa Simba, Mussa hassan Mgosi, alilimwa kadi nyekundu katika mchezo huo kabla ya timu yake kupata bao la ushindi lililofungwa na Abdallah Juma.
Katika mechi nyingine ya ligi hiyo, Rhino Rangers ikisafiri ugenini kuumana na wenyeji wa Kagera Sugar walishindiliwa bao 1-0 lililoifungwa na Suleiman Kibuta katika dakika ya nne na kuzidi kujiweka pabaya kwenye janga la kushuka daraja.
Nao Mgambo JKT ambao kwenye duru la pili wameonekana kuamka waliendeleza ubabe wao kwa kuichapa Oljoro JKT nyumbani kwao kwa mabao 2-1, mechi iliyochezwa kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha.
Chelsea yazidi kujikita kileleni yailaza Everton
Terry alifunga bao hilo katika dakika ya tatu ya nyongeza ya mchezo huo uliochezwa 'darajani' ambao ulionekana kama ungeisha kwa sare na kuweka reheni nafasi ya timu hiyo kuendelea kuongoza msimamo.
Ushindi huo umeifanya Chelsea kufikisha jumla ya pointi 60 baada ya mechi 27, na kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo ambapo michezo mingine inaendelea jioni hii huku Arsenal ikiwa nyumbani inaongoza 3-0 mpaka sasa.
Ushindi huo umeifanya Chelsea kufikisha jumla ya pointi 60 baada ya mechi 27, na kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo ambapo michezo mingine inaendelea jioni hii huku Arsenal ikiwa nyumbani inaongoza 3-0 mpaka sasa.
Yanga yaua Taifa, Mbeya City yafa Mkwakwani
Emmanuel Okwi akimtoka kipa wa Ruvu Abdallah Ramadhani na kuifungia Yanga bao la tatu (Picha: Francic Dande) |
Coastal walioifanyizia Mbeya City Mkwakwani Tanga |
Mbeya City waliopoteza mechi yao ya pili katika ligi msimu huu baada ya kuwa wagumua duru la kwanza |
Yanga na Al Ahly zitavaana Jumamosi kwenye uwanja wa Taifa katika mechi ya mkondo wa kwanza ya raundi ya kwanza huku Wamisri hao wakitoka kutwaa taji la Super Cup kwa kuilaza CS Sfexien ya Tunisia.
Al Ahly ilitoa kipigo cha mabao 3-2 kwa Watunisia wakishuhudiwa na kocha msaidizi wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa aliyetumwa kwenda kuifanyia ushushushu ambaye alitua Taifa Yanga ikiua Ruvu.
Yanga iliyopiga kambi yake Bagamoyo iliisambaratisha Ruvu iliyo chini ya Mkenya, Tom Olaba kwa mabao ya haraka haraka ya kipindi cha kwanza kupitia kwa Didier Kavumbangu na Simon Msuva.
Wachezaji hao waliofunga mabao mawili kila mmoja katika mechi hiyo walifunga mabao hayo ndani ya dakika mbili tu za kuanza kwa mchezo huo kabla ya Mrisho Ngassa na Emmanuel Okwi kuongeza mengine mawili na kufanya waende mapumziko wakiongoza 4-0.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na Yanga kuongeza bao la tano kupitia tena kwa Didier kabla ya Hamis Kiiza 'Diego' kuongeza jingine la sita dakika ya 69 na Msuva akamalizia kazi.
Kwa ushindi huo Yanga imerejea kileleni ikiing'oa Azam ambayo itashuka dimbani kesho dhidi ya Prisons kwa kufikisha pointi 38 na mabao 41 ya kufunga, huku Didier na Kiiza wakifikisha mabao 9.
Pia ushindi huo umeifanya Yanga kuweka rekodi ya kipigo kikubwa kutolewa msimu huu ikipiku vile vya Simba na Mgambo JKT na Prisons dhidi ya JKT Ruvu zilizoisha kwa mabao 6-0 kila moja.
Katika mechi nyingine iliyochezwa mjini Tanga, Mbeya City imekuwa urojo kwa Coastal Union kwa kulazwa mabao 2-0 kwenye uwanja wa Mkwakwani Tanga.
Mabao ya washindi yamefungwa na Mohammed Miraji dakika nane za mwisho kabla ya kumalizika kwa pambano hilo na kuifanya Coastal kuwa timu ya pili kuidungua Mbeya City baada ya Yanga na kufikisha pointi 25.
Subscribe to:
Posts (Atom)