Uwanja wa Soweto ambapo Mkutano wa
Chadema kufunga kampeni za kuwania Udiwani Kata ya Kaloleni Jijini
Arusha ulikuwa unafanyika umegeuka kuwa uwanja wa vilio baada ya
kinachodhaniwa kuwa bomu kulipuka na kuua watu watatu na zaidi ya 50
kujeruhiwa vibaya huku baadhi yao wakiwa wamevunjika miguu.
Katika Mkutano huo walikuwapo pia
Mwenyekiti wa Chadema na Mbunge wa Arusha Mjini, Mh Godbless Lema
sambamba na viongozi wengine wa Chadema Mkoa wa Arusha lakini bahati
nzuri Mbowe na Lema hawakudhurika moja kwa moja na mlipuko huo.
Mlipuko huo ulitokea mbele ya gari ambalo lilikuwa ni jukwaa la matangazo mara tu baada ya Mh Mbowe, Lema na viongozi wote waliokuwa jukwaa kuu kushuka chini na kujichanganya katikati ya watu wakikusanya michango ya watu, hali inayoashiria mrushaji huenda alilenga kuwajeruhi viongozi hao.
Miili ya marehemu na majeruhi walipelekwa hospitali ya Mt Meru lakini hawakupokelewa baada ya kilichoelezwa ni vurumai iliiyoletwa na mamia ya wafuasi wa Chadema waliokuwa na hasira baada ya wenzao kuuawa.
Hali ikiwa bado tete viwanjani hapo, magari kadhaa ya askari polisi yalifika huku askari wakiwa na silaha lakini walilazimika kupiga mabomu ya machozi kadhaa hewani na kisha kuondoka kutokana na baadhi ya wananchi waliokuwa na hasira kuwafuata na kupaza sauti wakitaka wawaue pia.

Kijana mmoja muuza machungwa aliieleza blogu hii kuwa aliyerusha bomu hilo alitokea upande wa nyuma ya jukwaa kuu na baadae kukimbilia nyumba zilizo jirani.