STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, August 11, 2015

Yaya Toure aibeba Man City, ikishinda ugenini

Yaya Toure akifunga moja ya mabao yake usiku wa jana kuisaidia Manchester City kushinda ugenini mabao 3-0
http://img.bleacherreport.net/img/images/photos/003/494/423/hi-res-b27d356a2da129aaa8e144db5c571976_crop_north.jpg?w=630&h=420&q=75
Vincent Kompany akishangilia bao lake lililokuwa la tatu kwa Man City
Ivorian midfielder Toure wheels away in celebration as Fernandinho congratulates his team-mate for the early strike
Oyooo Oyoooo! Man City wakishangilia mabao yao jana usiku
MANCHESTER City imeanza vyema msimu mpya wa Ligi Kuu ya England baada ya kupata ushindi wa mabao 3-0 ugenini dhidi ya West Bromwich.
City ilipata ushindi huo usiku wa kuamkia leo, huku Mwanasoka Bora wa Afrika, Yaya Toure akifunga mabao mawili na kuipeleka timu yake kileleni mwa msimamo baada ya raundi ya kwanza.

Kiungo huyo wa kimataifa wa Ivory Coast, Yaya Toure aliyefunga alianza kuifungia Manchester City dakika ya tisa baada ya shuti lake la umbali wa mita 20 lililombambatiza Boaz Myhill na kutinga nyavuni, kabla ya kufunga la pili dakika ya 24.

Nahodha wa Man City, Vincent Kompany akakamilisha ushindi mnono katika mchezo wa kwanza wa timu yake kwa kufunga bao la tatu dakika ya kwa kichwa 59.  

Mchezaji mpya, Raheem Sterling aliyesajiliwa kutoka Liverpool, alicheza vizuri katika kikosi cha City jana, lakini akapoteza nafasi nzuri na ya wazi ya kufunga.

Arsene Wenger awashushua wapambe nuksi

http://xmedia-nguoiduatin.cdn.vccloud.vn/149/2014/8/12/Arsene%20Wenger.jpg
BAADA ya kuanza Ligi Kuu ya England kwa kipigo cha nyumbani cha mabao 2-0 kutoka kwa West Ham United, Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amewashushua wanaolazimisha afanye usajili ili kuimarisha kikosi chake kwa kusema huwa hakurupuki.
Wenger amesema kuwa hatakurupuka kukimbilia sokoni kutafuta wachezaji wapya kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili wa kiangazi baada ya kipigo cha kushtusha walichopewa.
Kipa Petr Cech ndio sura mpya pekee iliyotua Emirates katika kipindi hiki cha usajili na ameonekana kuanza vibaya kibarua chake hicho toka atoke Chelsea.
Kuna tetesi kuwa Wenger ameshatenga fungu kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid, Karim Benzema.
Lakini meneja huyo amesema hatakurupuka kusajili kwasababu ya kupoteza mchezo wao kwanza katika ligi kwani jambo la msingi ni kuangalia walipokosea na kurekebisha.

Depay ajiapiza kuhusu jezi No. 7

http://images.thepeoplesperson.com.s3-eu-west-1.amazonaws.com/wp-content/uploads/2015/06/12150615/memphis.jpg
Depay
UKISIKIA kujishtukia ndiko huku, Mshambuliaji Mpya wa Manchester United, Memphis Depay amesem ana uhakika kuwa ataweza kuitendea haki jezi namba namba aliyopewa na klabu hiyo kama nyota wengine waliowahi kuivaa.
Depay alipewa namba hiyo mashuhuri baada ya Angel Di Maria kuondoka kwenda PSG na kufuatia nyayo za nyota wengine waliowahi kuvaa jezi kama Cristiano Ronaldo, David Beckham, Eric Cantona na George Best.
Nyota huyo wa kimataifa wa Uholanzi amesema yuko tayari kuitendea haki jezi hiyo kama ilivyokuwa kwa nyota wengine na kutamba kuwa atafanikiwa akiwa Old Trafford.
Depay aliendelea kudai kuwa anafahamu changamoto yake na historia lakini ana uhakika ataendelea kuimarika zaidi na kupata mafanikio kama ilivyokuwa kwa wengine.
Manchester ilianza Ligi Kuu ya England kwa kupata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Tottenham Hotspur kwa bao la kujifunga la beki wa Spurs Kyer Walker.