STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, July 13, 2013

Taifa Stars bado sana, yapigwa na The Cranes




LICHA ya ahadi tamu toka kwa kocha Kim Poulsen na kauli ya Rais wa TFF, Leodger Tenga kwamba timu ya taifa, Taifa Stars imeiva kwa mashindano, hali imekuwa tofauti jioni hii baada ya Stars kukubali kipigo cha bao 1-0 toka kwa Uganda the Cranes katika mechi ya mkondo wa kwanza ya kuwania kucheza CHAN.
Stars ikiwa na nyota wake karibu wote ukiondoa wawili tu wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi ambao haruhusiwi kuitumikia timu hiyo, ilikubali kipigo hicho kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Bao lililoizamisha Stars na kuwa na wakati mgumu kwenda kuiondosha The Cranes nyumbani kwao wiki ijayo liliwekwa kimiani na Iguma Dennis dakika moja tangu kuanza kwa kipindi cha kwanza.
Stars inaweza kujilaumu kwa kukosa mabao mengi ya wazi kutokana na nafasi zilizopotezwa na washambuliaji wake huku ikionekana kupwaya katika kiungo kusiko kawaida.
Kwa kipigo hicho Stars italazimisha kupata ushindi usiopungua mabao 2-0 iwapo inataka kuing'oa Uganda na kwenda Afrika Kusini mwakani kwenye Fainali hizo za timu za taifa zinazohusisha wachezaji wa ndani tu.
Pia ni kipigo cha tatu mfululizo kwa Stars baada ya vile ilivyopata katika michezo yake miwili ya kuwania kucheza Fainali za Kombe la Dunia za mwakani zitakazochezwa Brazili kwa kulala mbele ya Morocco kisha kucharazwa na Ivory Coast katika mechi zao za kundi C.

Maskini mwanachuo huyu, afa maji akiogelea

MSOMI wa mwaka wa kwanza Uhandisi wa Kompyuta wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Wendy Habakuki Lwendo amepoteza maisha yake jana jioni wakati akiogelea na wenzake katika bahari ya Hindi eneo la Kipepeo Kigamboni, jijini Dar.
Akisimulia tukio hilo, kaka wa Marehemu, Sammy Lwendo amesema mdogo wao alipatwa na maswahibu hayo akiwa na rafiki zake hao watatu wakiogelea baharini na wakati wanaogelea walikuwa katika eneo la kina kifupi cha maji yaliyokupwa na mara maji hayo yaka jaa na walipokuwa wakijaribu kutoka ndipo Wendy akazidiwa na maji.
Lwendo amesema kuwa wenzake walifanikiwa kumtoa majini lakini hali yake tayari ilikuwa mbaya na kwakuwa hawakuwa na ujuzi wa kutosha wa kutoa huduma ya kwanza kwa mtu aliyezama majini walihangaika kwa zaidi ya dakika 40 kumsaidia ndipo wakapata msaada wa Polisi kumkimbiza kituo cha afya Kibaoni huko Kigamboni lakini jitihada za kuokoa maisha yake ziligonga mwamba.
Aidha alisema kuwa mwili wa Marehemu ulihamishiwa katika Hospitali ya Wilaya Vijibweni na sasa ndugu wamefika na kuhamishia mwili huo Hospitali ya jeshi Lugalo.
Msiba kwa sasa upo Kinondoni nyuma ya Vijana, huku wakisubiriwa wazazi wa marehemu pamoja na ndugu wengine ili kujua taratibu kamili za maziko.
Wazazi wa Wendy, Mchungaji Habakuki Lwendo ni mwalimu wa Chuo cha Uchungaji Makumira mkoani Arusha.
Father Kidevu

TPBO YATAHADHARISHA KUHUSU FRANCIS CHEKA

Rais wa TPBO, Yasin Abdallah 'Ustaadh'
NINAWAPA TAARIFA RASMI KWAMBA TAREHE 30-08-2013 KATIKA UKUMBI WA DIAMOND JIJINI DAR--ES-SALAAM KUTAFNYIKA PAMBANO KUBWA LA NGUMI ZA KULIPWA KATI YA MTANZANIA FRANCIS CHEKA  NA MMAREKANI DERRICK FINDLEY , PAMBANO LA KUGOMBEA UBINGWA UNAOTAMBULIWA NA SHIRIKISHO LA NGUMI LA DUNIA [WBF].

HILI NI PAMBANO LA RAUNDI KUMI NA MBILI ZA DAKIKA 3 KILA RAUNDI NA MAPUMZIKO YA DAKIKA MOJA  KWA KILA RAUNDI. KATIKA UZITO WA SUPER MIDDLE [75 KGS]

PIA NINATUMIA FURSA HII KUWAFAHAMISHA RASMI KWAMBA BONDIA FRANCIS CHEKA ALISHASAINI MKATABA WA PAMBANO HILI TANGU MWEZI WA TANO .NA MASHARTI YA MKATABA HUO NI KWAMBA HARUHUSIWI KUCHEZA PAMBANO LOLOTE KWA SIKU 30 KABLA YA PAMBANO HILO NA MMAREKNI [FINDLEY] NA TAYARI AMELIPWA MALIPO YA AWALI[ADVANCE]

PAMBANO HILI LINAANDALIWA NA KAMPUNI YA HALL OF FAME BOXING &PROMOTION[USA] KWA KUSHIRIKIANA NA KAMPUNI YA NAI INCORPORATION COMPANY-LTD YA TANZANIA NA LITAKUWA CHINI YA USIMAMIZI WA NDANI WA TPBO-LTD.

WAAMUZI WA PAMBANO HILI WATATOKA AFRIKA KUSINI NA RAIS WA WBF MR HOWARD GOLDBEIG ATAKUWA KAMISHNA WA PAMBANO HILI KUBWA.

PIA SIKU HIYO HIYO MABONDIA MADA MAUGO NA THOMAS MASHALI WATAPANDA ULINGONI KUGOMBEA UBINGWA WA WBF -AFRIKA ,PAMBANO LA RAUNDI 12 LA UZITO WA SUPER MIDDLE PIA ALPHONSE MCHUMIA TUMBO ATAPAMBANA NA BONDIA KUTOKA MAREKANI DE-ANDRE MAC'COLL KATIKA PAMBANO LA RAUNDI 10 UZITO.

NDG WAANDISHI NINATOA TAARIFA HII KWENU PAMOJA NA VIONGOZI WA NGUMI ZA KULIPWA TANZANIA, KWA SABABU MOJA KUBWA, KUNA BAADHI YA WATU BILA KUFUATA TARATIBU ZA NGUMI KULIPWA WAMEKUWA WAKITUMIA VYOMBO VYENU VYA HABARI KUTANGAZA PAMBANO LINGINE LA FRANCIS CHEKA KWAMBA ATAPAMBANA NA MMALAWI CHIMWEMWE CHIOTCHA HALI WAKIJUA WAZI KABISA UTARATIBU WA MAPAMBANO  KAMA BONDIA AMESHASAINI MKATABA SEHEMU NYINGINE UKOJE. TPBO ILISHATOWA KIBALI KWA HALL OF FAME NA WASHIRIKA WAKE  CHA KURUHUSU PAMBANO HILO TANGU TAREHE 28 MAY 2013  MARA TU MAKUBALIANO YA FRANCIS CHEKA NA MAPROMOTA YALIPOFANYIKA ,KWA MASHARTI HAYO YA KUTOKUPIGANA PAMBANO LOLOTE SIKU 30 KABLA YA PAMBANO  NA MMAREKANI HUYO. NAKALA ZA MIKATABA TUNAYO [kama mtahitaji]

NA MAANDALIZI YA PAMBANO YANAENDELEA VYEMA ,NA MIPANGO YA USAFIRI KWA WAAMUZI NA MABONDIA KUTOKA MAREKANI INAKWENDA VYEMA.

NDG ZANGU KAMA MTAKUMBUKA VYEMA KUHUSU BONDIA KARAMA NYILAWILA ALIVYOPOTEZA UBINGWA WA DUNIA KWA KUSHINDWA KUTETEA BAADA YA BAADHI YA VIONGOZI WENZETU WALITOWA KIBALI KWA KARAMA KUPAMBANA NA CHEKA. .MJINI MOROGORO NA KUACHA KUTETEA UBINGWA WAKE WA DUNIA.

NDG ZANGU KATIKA KUTETEA KWAO KUTAKA CHEKA APAMBANE NA CHIMWEMWE ETI WANADAI WANAMUANDAA BONDIA FRANCIS CHEKA KWA PAMBANO LAKE NA MMAREKANI ,HII MBALI NA MASHARTI YA MKATABA KIUFUNDI  TU HAIKUBALIKI.

KWA SABABU KWA MASHARTI YA MKATABA HUO ,KAMA KWELI WANATAKA KUMUANDAA CHEKA HAWAPASWI KUTANGAZA PAMBANO BALI WAMUITE CHIMWEMWE AMSAIDIE MAZOEZI YAKE NDANI YA GYM KAMA SPARRING PATNER WAKE .

CHIMWEMWE NI BONDIA HATARI SANA NA TUNAZO  CD ZAKE NI LAZIMA ATAMUUMIZA CHEKA NIVYO KUVURUGA PAMBANO HILI KUBWA.

TUNAOMBA TUUNGANE WATANZANIA WOTE KATIKA KUFANIKISHA PAMBANO HILI KWA MANUFAA YA MABONDIA WETU KIMATAIFA.
 
IMELETWA KWENU NAMI;-
YASSIN ABDALLAH MWAIPAYA -USTAADH
RAIS - TPBO-LIMITED

Bint Mfalme wa Saudia akamatwa kwa unyanyasaji

 
MWANAMKE mmoja anayetajwa kuwa Binti wa Mfalme wa Saudi Arabia, Meshael Alayban, 42, amekamatwa katika jimbo la Carlifonia nchini Marekani na kutuhumiwa kuhusika na biashara ya watu.
Bi Alayban anakabiliwa na mashtaka ya kumlazimisha mama mmoja kutoka Kenya kufanya kazi kwa zaidi ya saa kumi na sita kila siku, na kumlipa kiasi kidogo cha pesa kuliko walivyokuwa wameafikiana.
Utawala wa eneo hilo, umesema kuwa bint mfalme huyo alichukua pasi ya kusafiria ya mama huyo, hatua iliyomfanya atoroke.
Mawakili wa mtuhumiwa huyo wametaja kesi hiyo kuwa mzozo kuhusu hali ya utendaji kazi.
Novemba mwaka uliopita, wapiga kura katika jimbo la Carlifonia, waliidhinisha sheria kali dhidi ya watu watakaopatikana na hatia ya kuhusika na ulanguzi wa watu.
Ikiwa atapatikana na hatia, Bi Alayban, huenda akahukumiwa kifungo cha miaka kumi na miwili gerezani, adhabu ambayo ni asilimia mia moja zaidi kuliko ilivyokuwa kabla ya wapiga kura kuidhinisha mageuzi sheria hiyo mpya.
Waendesha mashtaka wanasema Bi Alayban, ni mmoja wa wake sita wa Mwana Mfalme Abdulrahman bin Nasser bin Abdulaziz al-Saud, mmoja wa wanawe wa kiume wa familia moja ya kifalme nchini Saudi Arabia.

Mama huyo kutoka Kenya ambaye jina lake halijatolewa, aliajiriwa na Bi Alayban miaka miwili iliyopita, baada ya kusaini mkataba na shirika moja la kutoa uajiri nchini Saudia.
Mkenya huyo aliahidiwa kulipwa dola 1,600 kila mwezi na kuwa atafanya kazi kwa saa nane kila siku kwa siku tano.
Hata hivyo, Bi Alayban amekuwa akimlipa dola 220 kwa  mwezi na kulazimishwa kufanya kazi kwa zaidi ya saa 16 kila siku.
Mama huyo amedai, kupokonywa pasi yake ya kusafiria na alikabidhiwa muda mfupi tu kabla ya wao kusafiri kwenda Carlifonia na Bi Alayban.
Akiwa Carlifonia, alilazimishwa kufanya majukumu mengi zaidi ya nyumbani kwa familia ya watu wanane waliokuwa katika vyumba vinne tofauti, ambako amedai alizuiliwa mateka.
Wakati alifanikiwa kutoroka, alisimamisha basi moja na kwenda moja kwa moja hadi kituo cha polisi.
Bi Alayban alikamatwa siku ya Jumatano na kufikishwa mahakamani juzi Alhamisi.
Aliachiliwa huru kwa dhamani ya dola milioni tano na kuamriwa kurejesha pasi ya kusafiria ya amama huyo kutoka Kenya.
Aidha Bi Alayban sasa atavalia chombo maalum ambacho kitatoa maelezo ya mahala aliko na hataruhusiwa kuondoka Marekani hadi kesi hiyo itakapokamilika.
Viongozi wa Mashtaka walitaka jaji kumuachilia kwa dhamani ya dola milioni 20 au anyimwe dhamana kwa kuwa yeye ni tajiri mkubwa na aweza kutoweka.

Emirates hosts Iftar celebrations in Tanzania



Emirates Country Manager for Tanzania Abdulaziz Al Hai speaking to the Media during the Iftar dinner last evening in honour of its trade partners and the Media at the Hyatt Regency Dar es Salaam, the Kilimanjaro.
Emirates, one of the world’s fastest growing airlines, hosted Iftardinner last evening in honour of its trade partners and the media at the Marquee Hyatt Regency Dar es Salaam, The Kiimanjaro.

Speaking at the event, Emirates Country Manager for Tanzania Abdulaziz Al Hai thanked the Government of Tanzania, trade partners and the media for their outstanding and continuous support to the airline.

“Ramadan is a period of sharing and we are pleased that each one of you found time to join us as we celebrate Iftar,” said Al Hai. 
Our services in Tanzania have gone from strength to strength over the last 15 years and we owe our success to the very important partnerships we have with our trade partners, our loyal customers, as well as the media. This event is an amicable opportunity for us to show our appreciation for your vital role in the growth of Emirates in Tanzania. I am confident we can always count on your assistance going forward.”

He noted that the provision of excellent in-flight service and entertainment, ongoing network expansion and focus on developing innovative ways to improve customer comfort and convenience have been key in driving  success for Emirates in Tanzania.

“Our modern and convenient Dubai hub enables our customers to seamlessly connect to our ever-expanding global network,” Al Hai said. 

Emirates established operations in Tanzania in 1997. Currently, the airline flies daily from Julius Nyerere International Airport (JNIA) to Dubai, connecting passengers to 134 destinations in 77 countries across six continents.

EK 725 departs Dubai International Airport every day at 1015hrs and arrives at the Julius Nyerere International Airport (JNIA) in Dar es Salaam at 1455hrs. The return flight leaves JNIA at 1645hrs and lands in Dubai at 2320hrs every day.  
More information on offering conditions and bookings can be obtained fromwww.emirates.com/tz

'TAIFA STARS SASA YAIVA KWA MAPAMBANO'

Rais wa TFF, Leodger Tenga
Na Boniface Wambura
RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga amesema kikosi cha Taifa Stars sasa kina uwezo wa kushindana katika mashindano yoyote, kwani tayari kimeiva.

Akizungumza na wachezaji wa timu hiyo kambini kwao hoteli ya Tansoma, Dar es Salaam, Rais Tenga aliwaambia kuwa kiwango walichoonesha kwenye mechi zilizopita za mchujo za Kombe la Dunia dhidi ya Morocco na Ivory Coast kimethibitisha hilo.

“Kiwango mlichoonyesha katika mechi hizo kila Mtanzania anayewafuatilia amekiona, hivyo hatuna shaka kuwa mtatuwakilisha vizuri kwenye mechi ya kesho (leo) dhidi ya Uganda,” amesema Rais Tenga na kuwataka kupigana kwa ajili ya Tanzania.

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager leo (Julai 13 mwaka huu) saa 9 kamili alasiri Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam itacheza na Uganda (The Cranes) katika mechi ya kwanza ya raundi ya mwisho kuwania tiketi ya kucheza Fainali za CHAN zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini.

Rais Tenga amesema TFF, mdhamini Kilimanjaro Premium Lager, Kamati ya Ushindi na Watanzania kwa ujumla wanawaunga mkono kwani wamekuwa wakiboresha kiwango chao kila wanavyozidi kucheza mechi tangu wake chini ya Kocha Kim Poulsen, Mei mwaka jana.

Wakati huo huo, Rais Tenga ameahidi kumpatia tiketi ya kwenda Uganda kwenye mechi ya marudiano mshabiki Wiseman Mwakyusa Luvanda anayetembea kwa miguu kutoka Mbeya kuja Dar es Salaam kushuhudia mechi ya leo.

“Kama ni kweli anakuja kwa kutembea, huyu ameonyesha kiwango kikubwa cha uzalendo kwa timu ya Taifa, nitampatia tiketi ya kwenda Kampala kuishangilia Taifa Stars kwenye mechi ya marudiano,” amesema Rais Tenga.

…POULSEN, MICHO WATABIRI MECHI KALI

Makocha wa timu hizo Kim Poulsen wa Taifa Stars na Sredojvic Micho wa The Cranes wamesema mechi ya leo itakuwa ngumu kwa vile kila mmoja amejiandaa kuhakikisha anafanya vizuri.

Wakizungumza na Waandishi wa Habari jana, makocha wote waliezea ubora wa wapinzani wao, lakini wakasisitiza kuwa wanaingia uwanjani kuhakikisha wanashinda ili kujiweka katika mazingira mazuri kwa ajili ya mechi ya marudiano itakayochezwa Kampala wiki mbili zijazo.

Kim alisema Uganda ndiyo inayoongoza kwa ubora wa viwango vya FIFA katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati, hivyo ni changamoto kwao ingawa wachezaji wake tayari wamejipanga vizuri kwa ajili ya mechi hiyo.

Naye Micho aliyefuatana na nahodha wake Hassan Wasswa alisema Taifa Stars imekuwa ikifanya vizuri tangu iwe chini ya Kim, na itakuwa na wachezaji tisa wa kikosi cha kwanza kinachocheza mechi za mchujo za Kombe la Dunia wakati kwa upande wake atakuwa na wachezaji wawili tu.

WAKAZI WA TABORA WACHANGAMKIA MCHEZO WA POOL

Mchezaji wa Omari Azizi wa timu ya Pool ya Texas- Tabora akijiiweka tayari kupiga mpira wakati wa mazoezi ya klabu yao iliyofanyika mkoani hapo jana.

Mchezaji wa Texas Pool Mkoa wa Tabora Salum Kazuga akijitayarisha kupiga mpira wakati wa mazoezi ya klabu yao.

Mchezaji wa klabu ya Pool ya Texas-Tabora Shabani Ramadhani akijiandaa kupiga mpira wakati wa mazoezi ya timu yao iliyofanyika mkoani hapo jana.

Mchezaji wa Klabu ya Pool ya Texas ya Mkoa wa Tabora Hassani Sasi akijitayarisha kupiga mpira wakati wa mazoezi ya klabu yao iliyofanyika mkoani hapo.