STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, September 23, 2014

Mama Mkwe wa Jennifer Mgendi huyooo Mtaani

FILAMU mpya ya muimbaji wa nyimbo za Injili, Jennifer Mgendi iitwayo 'Mama Mkwe' inatarajiwa kuigizwa sokoni siku ya Alhamisi baada ya kukwama kuachiwa jana Jumatatu kama ilivyokuwa imepangwa.
Aidha Muinjilisti huyo amewataka mashabiki wake wasiikose kupata darasa la kutosha.
Jennifer alisema filamu hiyo itaachiwa rasmi Septemba 25 baada ya jana kukwama kwa sababu zilizo nje ya uwezo wake ikiwa ni wiki kadhaa tangu kumalizika kurekodiwa kwake na kusema kwa ujumbe uliopo ndani yake, mashabiki hawapaswi kuikosa.
Muimbaji huyo alisema, kisa cha Mama anayeingilia ndoa ya mwanae wa kiume akitaka kupatiwa mjukuu ni mambo ambayo yamekuwa yakiwakumba wanajamii wengi na kusambaratisha ndoa zao bila kutaka.
"Ni mambo yanayotokea ndaniya jamii na kuwaachia watu machungu, sasa waigizaji wameonyesha uhalisia wa mambo namna ndoa nyingi zinavyosambaratika kwa sababu ya mambo kama hayo," alisema.
Katika filamu hiyo, Jennifer ameigiza na wasanii wengine wakali kama kina Mussa Banzi, Bahati Bukuku, Christine Matai, Bibi Esther na wengine.
"Itakuwa mtaani Alhamisi, mashabiki wasikose kuona uhondo huu. Mama Mkwe ni zaidi ya kazi zangu za nyuma kwa namna ilivyosukwa na kutendewa haki na wasanii walioigiza," alitamba Jennifer.

ACT Tanzania yakana kuwa mamluki Tanzania

http://www.mtizamohuru.co.tz/wp-content/uploads/2014/03/act.jpgNa Kipimo Abdallah
CHAMA cha Alliance for Change and Transparency (ACT-Tanzania) kimekanusha  tuhuma zinazotolewa na baadhi ya wanasiasa kuwa  ni chama kilichokuja kubomoa vyama vya upinzani hapa nchini.
Hayo yamesemwa na Katibu wa Mawasiliano na Uenezi wa ACT -Tanzania Mohammed Massaga wakati akizungumza na mwandishi wa MICHARAZO ofisi kwake jijini Dar es Salaam.
Massaga aliomba vyama hivyo kuacha kufanya siasa nyepesi na kujikita katika hoja ili kuhakikisha kuwa upinzani unakuwa na nguvu ili viweze kukitoa chama tawala CCM madarakani.
Alitoa wito kwa watanzania kuviunga mkono vyama vya siasa ambavyo vinaonyesha ni madhubuti ya kukabiliana na ubadhirifu wa rasilimali za Taifa ili kufikia malengo ya maisha bora ambayo kwa sasa yamekwama.
Katibu huyo wa Mawasiliano na Uenezi alisema iwapo vyama vya upinzani vitakuwa na umoja na ushirikiano wa dhati zipo dadli tosha za kukiondoa chama tawala madarakani.
Alisema wapo baadhi ya viongozi ambao wanashindwa kufanya siasa na kubakia kulalamika jambo ambalo linachelewesha mabadiliko.
"Ndhani unaona mwenyewe tatizo la siasa za Tanzania ni wanasiasa kushutumiwa na kuacha kufanya siasa za kweli ambazo zinaweza kuleta mabadiliko kwa jamii ya Kitanzania" alisema
Massaga alitolea mfano wa mchakato wa Bunge Maalum la Katiba linaloendelea mjini Dodoma kuwa ni matumizi mabaya ya fedha za Serikali.
Kwa upande mwingine Massaga alisema katika kujenga chama chao cha ACT- Tanzania wamefanikiwa kuvuna wachama wapya zaidi ya 11,800 katika mikoa 12 ya Tanzania Bara kwa kipindi cha mwezi Agosti mwaka huu.
Katibu huyo wa Mawasiliano na Uenezi ACT alisema kwa sasa chama hicho kina wanachama zaidi ya 187,000 nchini kote hivyo juhudi zao ni kuongeza wanachama wengi zaidi kwa kutumia itikadi yao ya demokrasia ya jamii.
Alisema chama hicho kilifanya ziara katika mikoa 12 ambayo Tanga, Singida, Shinyanga, Simiyu, Geita, Tabora, Mara, Mwanza, Lindi, Kigoma, Pwani na Mtwara ambapo wamepokelewa kwa nguvu kubwa.
Massaga alisema pamoja na kuvuna idadi hiyo ya wanachama wamefanikiwa kusimika viongozi wa muda katika majimbo 68 ya Tanzania bara na viongozi wa kata na matawi kwenye majimbo hayo.
"Kwa kifupi tumepata mafanikio makubwa katika kipindi hiki cha miezi minne tangu kupewa usajili wa muda kwani kila tunapopita tunapokelewa kwa nguvu zote jambo ambalo linatupa matumaini ya kufanya vizuri kwenye chaguzi zijazo", alisema.
Katibu huyo wa Mawasiliano na Unezi wa ACT-Tanzania alisema katika kuhakikisha kuwa wanafikia malengo katika medani za siasa Tanzania wataendelea kuwaelimisha wanachama juu ya kujitokeza kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa.

Fainali za Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar zayeyuka

https://www.venturesonsite.com/news/wp-content/uploads/2014/06/qatar-chronicle-qatar-2022-stadiums.jpgIMEBAINIKA wazi kuwa ni ndoto kwa Fainali za Soka za Kombe la Dunia za mwaka 2022 kufanyika Qatar.
Mjumbe wa kamati ya utendaji ya Shirikisho la Soka Duniani,FIFA, Theo Zwanziger amefichua kuwa ni vigumu fainali hizo kuchezwa nchini humo kutokana na hali ya joto kali katika nchi hiyo.
Zwanziger ambaye ni raia wa Ujerumani aliliambia jarida la michezo la Bild jana kuwa anadhani mwisho wa siku michuano ya Kombe la Dunia 2022 haitafanyika katika nchi hiyo. 
Mjumbe huypo aliendelea kudai kuwa watabibu wamesema hawatakubalia kuwajibika kama michuano hiyo itafanyika katika hali ya hatari kama hiyo. 
Japo Qatar wamesisitiza ambao ni matajiri wakubwa wa mafuta wamesisitiza kuwa wanaweza kuandaa michuano hiyo majira ya kiangazi kwa kutumia teknolojia ya vipoza hewa katika viwanja vyake, sehemu za mazoezi na mahali watakapofikia mashabiki bado kumekuwa na wasiwasi mkubwa kuhusiana na afya za wachezaji na mashabiki watakaokuja kushuhudia michuano hiyo. 
Zwanziger amesema anajua wanaweza kuweka vipoza hewa viwanjani lakini Kombe la Dunia halichezwi viwanjani pekee kwani mashabiki kutoka duniani kote watakwenda na kusafiri katika hali hiyo ya joto jambo ambalo ni hatari kwa afya na maisha yao. Michuano ya mwaka 2022 imekuwa ikileta mjadala mkubwa huku rais wa FIFA Sepp Blatter akikiri kuwa walifanya makosa kuipa Qatar kuandaa michuano hiyo na kutaka kuangalia uwezekano wa kuamisha michuano hiyo ichezwe katika majira ya baridi.

AS Vita yanusa Fainali za Afrika, yainyuka Sfaxien

http://www.congoplanet.com/pictures/news/as_v_club_congo_kinshasa_football_vita_z.jpgKLABU ya AS Vita ya DR Congo imeanza vema mbio zake za kucheza Fainali za Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuinyuka CS Sfaxien ya Tunisia mabao 2-1.
Mabao ya Vita katika mchezo huo uliochezwa katika Uwanja wa Tata Raphael jijini Kinshasa yalitupiwa kimiani na Firmin Ndombe Mubele na Heritier Luvumbu Nzinga huku lile la kufutia machozi la Sfaxien likifungwa na Ali Maaloul. 
Ushindi huo unaiweka katika nafasi nzuri Wakongo hao kwa mechi ya marudiano itakayofanyika wikiendi hii mjini Tunis.
Vita watakwenda katika mchezo wao wa marudiano wakihitaji sare ya aina yoyote inaweza kuwapeleka fainali ambapo watakutakana na aidha ES Setif ya Algeria au TP Mazembe ya DRC. 
Sfaxien ambao ni mabingwa wa Kombe la Shirikisho na Super Cup walionekana kuzimiliki vyema dakika 20 za mwisho katika mchezo huo lakini walishindwa kutafuta nafasi ya kusawazisha. 
Katika mchezo wa kwanza 'ndugu' zao TP Mazembe walichapwa mabao 2-1 na wapinzani wao ambao watarudiana nao wikiendi hii mjini Lubumbashi na kama timu hizo za Kongo zitafuzu fainali itakayopigwa  Octoba 25-26 na Novemba 1-2 itakuwa ni mara ya kwanza kwa timu Chini ya Jangwa la Sahara kukutana pamoja katika hatua hiyo.

Kifo cha Ebosse chaiponza JS Kabylie, lupango miaka miwili

http://i.ytimg.com/vi/nRgfnT26dgY/0.jpg 
KLABU ya JS Kabylie ya Algeria imefungiwa kushiriki katika michuano ya Afrika kwa miaka miwili kufuatia shambulio lililosababisha kifo cha mchezaji wa kimataifa wa Cameroon Albert Ebosse. 
Uamuzi umechukuliwa na Shirikisho la Soka barani Afrika-CAF katika kiakao chake kilichofanyika jijini Addis Ababa, Ethiopia. 
Kabylie ilimaliza katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu nchini humo hivyo kuwapa nafasi ya kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani. 
Hatua hiyo ya CAF imekuja kufuatia Shirikisho la Soka la Algeria kuitaka Kabylie kucheza mechi zake za nmyumbani bila ya mashabiki katika uwanja huru msimu huu. 
Ebosse alifariki dunia hospitalini mwezi uliopita kutokana na majeraha ya kichwa yaliyosababishwa na kupigwa na kitu kizito na mashabiki wa klabu hiyo ambao walikasirishwa na kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa wapinzani wao USM Algers.

Rooney, Gerrard wapigwa 'madongo' England

http://www1.pictures.zimbio.com/gi/Wayne+Rooney+Steven+Gerrard+England+v+Ukraine+ygx0xe1DQpXl.jpg

MWANZO mbaya wa msimu kwa klabu za Manchester United na Liverpool unachangiwa na manahodha wao wawili Wayne Rooney na Steven Gerrard, imeelezwa.
Mchambuzi wa soka wa Goal.com, Greg Stobart, amesema "upendeleo" wanaopata Rooney na Gerrard kwa kuwa manahodha na kuachwa waendelee kubaki uwanjani licha ya kucheza chini ya kiwango, kunazigharimu timu hizo hasa katika zama hizi ambazo hata nyota wakubwa wa kimataifa huachwa benchi.
Wakati Juan Mata alianzia benchi na Di Maria na Radamel Falcao nao wakamalizia mechi wakiwa benchi, Rooney aliendelea kunufaika kwa "upendeleo" wa kubaki uwanjani kwa dakika 90 zote, licha ya kupiga shuti moja tu langoni mwa Leicester katika kipigo chao cha 5-3 juzi Jumapili.
Kuna maswali yanayohoji kama Rooney anastahil nafasi kikosi pamoja na wakali kama Falcao, Di Maria na Robin van Persie. Tabia yake ya kupooza mpira haiendani na falsafa ya kocha Louis Van Gaal ya soka la kushambulia.
Van Gaal said alisema Ijumaa iliyopita kwamba Rooney, kwa kuwa nahodha, anatarajia kuendea kunufaika na "upendeleo" wa kuanza katika mechi ngingi zaidi msimu huu na kubaki uwanjani kwa muda mrefu zaidi linapokuja suala la kocha kufanya mabadiliko. Jambo hilo linampa uhakika mchezaji ambaye wengi wanaona kwamba hastahili kuanza katika kikosi chenye sura mpya cha Manchester United. Na kipigo cha 5-3 dhidi ya Leicester juzi ni mfano unaoonyesha ni kwa nini.
Alionekana akiwawakia kwa hasira wachezaji wenzake, ikiwamo kumshukia beki yosso Tyler Blackett (20) kufuatia Leicester kufunga goli la 3-3, lakini Rooney alionyesha kutojielewa kwani yeye ndiye aliyepoteza mpira uliozaa goli hilo.

Bilioni 20 zahitajika kutatua tatizo la Ajiora nchini

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj-F5hwnHLukOOHecjhZ-ghBDejeN6VOEVNIpFPCcLyvhzRQSnpxPJQMoPK0TMjEI6_GHXln6t7ZsHQv5IPO-4lzTHCdxZsY5zg0yjg0u1lXUwCocg-aXzVOF9kMVqArWiwC4b0HCaqkiE/s1600/2.JPG
Dk Kisui (kushoto) akifafanua jambo
Na Kipimo Abdallah
WIZARA ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imesema inahitaji shilingi bilioni 20 kila mwaka ili iweze kupunguza tatizo la ajira hapa nchini.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Uwezeshaji na Uhamasishaji wa Wizara hiyo Dk. Steven Kisui  wakati akijibu swali la mwandishi wa habari hii.
Alisema bajeti wanayotengewa haitoshelezi mahitaji ya vijana jambo ambalo linachelewesha juhudi za kupunguza ukubwa wa tatizo hilo ambalo linatajwa kama janga la Taifa.
Dk. Kisui alisema mahitaji ni makubwa kutoka kwa vijana mbalimbali nchini ambao wamejiunga katika SACCOS ila uwezo wa Serikali ni mdogo hivyo zoezi hilo
linachukua muda kutatuliwa.
"Kusema ukweli bajeti ya shilingi bilioni 6 hatuwezi kufikia malengo lakini tutaenda hivyo hivyo hadi tufikie muafaka,kwani kiukweli ni ndogo mnno", alisema.
Kisui alisema juhudi za Wizara ni kuhakikisha kuwa hicho kidogo kinachopatikana kinawafia walengwa ambao watakuwa wamefikia vigezo pamoja na ukweli kuwa bilioni 20 zingeweza kutatua tatizo.
Kwa upande wake Kaimu Mkuu Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali Concilia Nyibitanga alisema hadi kufikia sasa ni Halimashauri 42 kati ya 169 ambazo vijana wake ndio wametengeneza vikundi vya SACCOS.
Alisema mwamko wa Halimashauri kuhakikisha kuwa vikundi vinakuwepo imekuwa mdogo sana jambo ambalo linakwamisha juhudi za Serikali.
"Pamoja na juhudi za serikali katika kuhakikisha kuwa vijana wanafikiwa bado mwamko ni mdogo sana katika Halimashauri nyingi jambo ambalo linaweza kuwa kikwazo", alisema.
Nyibitanga alisema fedha hizo ambazo zinakopeshwa kwa riba ndogo lengo lake ni kuhakikisha kuwa vijana wanajiajiri ili kuhakikisha kuwa wanakabilianana changamoto zinazowakabili.

Kajala kuzindua Mbwa Mwitu kesho Mlimani City

Kajala katika pozi
Kava la picha hiyo ya Mbwa Mwitu inayozinduliwa kesho Mlimani
NYOTA wa filamu nchini Kajala Masanja 'Kajala' kupitia kampuni yake ya Kay Entertainment inatarajiwa kuzindua filamu ya aina yake kesho usiku.
Filamu hiyo inayofahamika kama 'Mbwa Mwitu' itazinduliwa kwenye ukumbi wa Mlimani City kwa watu maalum walioalikwa kuhudhuria.
Kinachoifanya filamu hiyo kuwa ya kipekee ni muda mfupi iliyonayo wa dakika 15 tu, 10 ikiwa ni filamu yenyewe na tano za 'ducumentary' ya baadhi ya vijana waliokuwa wakiunda kundi la Mbwa Mwitu lililotikisa jiji.
Mtunzi na muongozaji wa filamu hiyo, Leah Richard 'Lamata' aliiambia MICHARAZO kuwa, filamu hiyo inasimulia visa na mikasa ya kundi la Mbwa Mwitu lililohusishwa na uvamizi na uporaji wa watu jijini Dar es Salaam.
"Uzinduzi utafanyika Mlimani Sept 24 (kesho) na ndani ya filamu hiyo ya dakika 10 ina nyongeza ya dakika tano za mahojiano ya waliokuwa vijana wa 'Mbwa Mwitu' ambao wameacha uhalifu huo," alisema Lamata kwa niaba ya Kajala ambaye ni mmoja wa washiriki wa filamu hiyo.
Mbali na Kajala wengine walioicheza ni Hemed Suleiman 'PHD', Grace Mapunda 'Mama Kawele', Mwinjuma Muumin, Abort Rocca, Hassain Hussein na Abdul Karim.
Kundi la Mbwa Mwitu na yake ya Watoto wa Mbwa, Boda kwa Boda na Bad Face yalitikisa jiji kwa vitendo vyao ya kihalifu kabla ya jeshi la Polisi kuyashughulikia huku baadhi ya washirika wao kuuwawa na wananchi.

PSPF kudhamini Siku ya Msanii Tanzania kwa Sh Mil 10

http://www.8020fashionsblog.com/wp-content/uploads/2013/09/pspf.pngNa Kipimo Abdallah
MFUKO wa Pensheni wa PSPF  umetoa shilingi milioni 10 kwa ajili ya kudhamini siku ya Msaani Tanzania.
Hayo yamesemwa na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF Abdul Njaidi wakati akizungmza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Alisema lengo la PSPF kujitolea kudhamini siku hiyo na katika kuangalia sekta nzima ya sanaa kwa kuwawezesha, kuwapa mafunzo wasanii ili waweze kujikwamua kiuchumi hapa nchini.
Njaidi alisema PSPF imekuwa ikijikita katika kuwapatia mafao watumishi wa sekta mbalimbali zilizo rasmi kwa miaka mingi ila kwa kipindi cha hivi karibuni hata sekta isiyo rasmi inahusishwa wakiwepo wasanii.
"Kwa kuanza sisi PSPF tumeamua kudhamini siku ya Msanii Tanzania kwa kutoa milioni 10 ambapo tunaamini zitasaidia mchakato huo", alisema.
Aidha Njaidi alisema pamoja na kudhamini siku hiyo PSPF inaendelea na kupokea wanachama kutoka sekta mbalimbali ambao wapo tayari kwa malengo yao baadae.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Haak Neel Production Company Limited Geofrey Katulo alisema  siku ya Msanii ni mradi uliobuniwa na Baraza la SanaaTaifa (BASATA) na utaendeshwa kwa ubiia wa Haak Neel  Production Company Limited.
Alisema mradi huo ulibuniwa ili kuungana na wenzao duniani kuadhimisha siku siku ya kimataifa ya Msanii ambayo huadhimishwa kila ifikapo Oktoba 25 kwa lengo la kumtambua msaani, kazi zake pamoja na mchango wake katika jamii.
Katula alisema kauli mbiu ya siku ya msaanii mwaka 2014 ni "Sanaa ni Kazi" ambapo fani zitakazohusika katika maadhimisho hayo ni taarabu, muziki wa dansi, ngoma za asili, muziki wa msanii kutoka nje ya nchi.
Fani zingine ni uchezaji shoo, dansi za mitaani, bongo fleva, maonyesho ya mitindo ya mavazi, sanaa kwa watoto na maonyesho ya sanaa za ufundi pamoja na semina.