Baadhi ya nyota wa zamani wa Simba walioitwa katika timu ya Tanzania All Stars |
Wengine wametoka katika kikosi hiki cha Yanga |
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana jana jijini Dar es Salaam zinasema kuwa kikosi hicho kitakuwa chini ya Kocha Charles Boniface akisaidiwa na Fred Felix 'Minziro' na Jamhuri Kihwelo ‘Julio’.
Mbali na Mwameja na Manyika wachezaji wengine wanaounda kikosi hicho ni mabeki; Nsajigwa Shadrack, Mecky Mexime, Boniface Pawasa, John Mwansasu, Abubakar Kombo, George Masatu na Habib Kondo,
Viungo Suleiman Matola, Shaaban Ramadhani, Salvatory Edward, Sabri Ramadhani ‘China’, Yussuf Macho, Abdul Mashine, Abdul Maneno, Mao Mkami, Steven Nyenge, Madaraka Suleiman, Akida Makunda na Mtwa Kihwelo.
Washambuliaji ni Monja Liseki, Iddi Moshi, Dua Said, Emmanuel Gabriel, Said Maulid, Thomas Kipese, Nasor Mwinyi ‘Bwanga’, Edibilly Lunyamila, Mohamed Hussein ‘Mmachinga’, Clement Kahabuka, Madaraka Suleiman na Akida Makunda.
Safu ya uongozi ya timu hiyo ya Tanzania ni pamoja na Mtemi Ramadhani, Hasannai Mnyenye, Omar Gumbo na Hamis Kisiwa na daktari wake ni Dk Mwanandi Mkwankemwa.
Wachezaji magwiji wa Real Madrid waliotamba kuanzia La Liga, wakacheza ligi nyingine za Ulaya, Kombe la Ulaya, Ligi ya Mabingwa na Kombe la Dunia waliowahi kuchezea Real Madrid watakuja nchini Agosti 22 kwa ziara maalum pamoja na kucheza mchezo wa kirafiki na kikosi maalum cha wachezaji nyota wa Tanzania Agosti 23, kabla ya kufanya ziara ya kitalii katika vivutio mbalimbali, ikiwemo kupanda mlima Kilimanjaro.
Real Madrid inakuja nchini kwa mwaliko wa kampuni ya Tanzania Sisi ni Nyumbani (TSN), chini ya Mkurugenzi wake Mkuu, Farough Baghozah.
Miongoni mwa nyota wanaotarajiwa kuja na Real nchini ni pamoja na Wanasoka Bora wa zamani wa Dunia, Mfaransa Zinadine Zidane, Mreno Luis Figo na Mbrazil, Ronaldo Lima.
Magwiji hao wa Real tayari wamekwishafanya matangazo ya ziara yao nchini wakisema wana hamu mno ya kukanyaga ardhi ya Tanzania.
Kampuni ya Vodacom Tanzania ni miongoni mwa makampuni yaliyojitokeza kudhamini ziara pamoja na Fastjet, Tropical, Pembe Flower, Lake Gas, EFM Radio na Ladger Plaza Bahari Beach.
Wito umetolewa kwa makampuni zaidi kujitokeza kudhamini ziara hiyo ya kihostoria nchini.