Ribery (31), anayeitumikia Klabu ya Bayern Munich amekuwa mchezaji bora wa mwaka mara tatu nchini Ufaransa huku akiichezea timu ya taifa mechi 81 na kufunga mabao 16.
"Ninataka kujikita zaidi katika kuiangalia familia yangu na kuitumikia vema Bayern Munich na kutoa njia timu ya taifa kwa wachezaji wengi makinda," Ribery ambaye ameichezea Ufaransa katika fainali za Kombe la Dunia za 2006 na 2010 aliliambia Jarida la Ujerumani la Kicker.
Ribery ambaye alizikosa fainali za Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil kutokana na kuwa majeruhi, amekuwa mmoja wa nyota wenye vipaji tangu ametua Bayern kwa dau la paundi milioni 20 akitokea Marseille mwaka 2007, ametwaa ubingwa wa Bundesliga mara nne na mara moja Kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Kadhalika Ribery alishika namba tatu katika kinyang'anyiro cha tuzo ya Mchezaji Bora wa Dunia wa Mwaka 2013 (Fifa Ballon d'Or 2013), akimaliza nyuma ya Lionel Messi na mshindi Cristiano Ronaldo.
Uamuzi huo unamaana Ribery hatajumuishwa katika kikosi kitakachoshiriki michuano ya Euro 2016, ambayo itafanyika Ufaransa.
No comments:
Post a Comment