STRIKA
USILIKOSE
Sunday, July 28, 2013
ZIARA YA RAIS JAKAYA KIKWETE WILAYANI KARAGWE KAGERA
Rais Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi ujenzi wa barabara ya Kagoma-Lusahunga katika wilayani Biharamulo Rais
Kikwete akipiga picha ya kumbukumbu na wananchi wa Ngara baada ya
kuzindua kivuko cha MV Ruvuvu katika mto Rusumo Rais
Kikwete akishiriki kupiga ngoma na kikundi cha utamaduni cha Ngara
wakati wa uzinduzi wa kivuko cha MV Ruvuvu katika mto Rusumo wilayani
Ngara Rais
Kikwete akisimikwa kuwa chifu wa Wahaya na kukakabidhiwa mgolole na
silaha za jadi za Wahaya katika sherehe ya kuzindua wilaya mpya ya
Kyerwa Rais
Kikwete akisimikwa kuwa chifu wa Wahaya na kukakabidhiwa mgolole na
silaha za jadi za Wahaya katika sherehe ya kuzindua wilaya mpya ya
Kyerwa Umati uliojitokeza katika sherehe za uzinduzi wa wilaya mpya ya Kyerwa Umati uliojitokeza katika sherehe za uzinduzi wa wilaya mpya ya Kyerwa Umati uliojitokeza katika sherehe za uzinduzi wa wilaya mpya ya Kyerwa Wananchi
wakimshangilia Rais Kikwete aliposimama kwa muda kuwasslimia wilayani
Karagwe akielekea Rusumo kuzindua kivuko cha Ruvuvu Wananchi
wakimshangilia Rais Kikwete aliposimama kwa muda kuwasslimia wilayani
Karagwe akielekea Rusumo kuzindua kivuko cha Ruvuvu Wananchi wakimshangilia Rais Kikwete baada ya kuzindua kivuko cha MV Ruvuvu jana Jumamosi Wananchi wakimshangilia Rais Kikwete baada ya kuzindua kivuko cha MV Ruvuvu Kivuko cha zamani kilichokuwa kikitumiwa na wananchi wa Ngara kuvuka mto Rusumo Kivuko kipya cha MV Ruvuvu katika mto Rusumo kilichozinduliwa na Rais Kikwete Rais
Kikwete akiongea na wananchi katika sherehe ya kuzindua mradi wa umeme
vijijini katika kijiji cha Nyaishozi, Wilaya ya Karagwe Rais Jakaya
Kikwete yuko mkoani Kagera kwa ziara ya kikazi ya siku nane(PICHA NA
IKULU)
Nape Nnauye ayakana kuwatusi wazee
KATIBU Mwenezi na Itikadi wa CCM, Nape Nnauye ameamua kuvunja ukimya na kutoa utetezi wake kuhusu kauli yake chafu iliyochapishwa na moja ya magazeti maarufu nchini lililotuhumu kuwatusi wazee waliopendekeza uwepo wa serikali tatu kwa madai kwamba wanaodai serikali hizo wanakaribia kufa
Huu ndiyo utetezi wake:
"Nimestushwa sana na stori ya gazeti la Mtanzania inayodai kuninukuu kuwa nimesema wazee waliopendekeza serikali tatu wanasubiri kufa!
Kwakweli nimesikitishwa sana hata na jinsi maneno ndani yalivyopangiliwa kiasi kwamba inanipa tabu kuamini kama mhariri aliipitia hii stori ukiachilia mbali kama aliyetumwa kuja kuandika stori alikuwa ni "too junior".
Nawaheshimu sana wazee wangu hawa hata kama nikipishana nao kimawazo siwezi kufikia kutamka maneno makali kiasi hicho.
Nilichosema ni kuwa ukilinganisha vijana na wazee, vijana wana wajibu mkubwa wa kuamua kesho yao badala ya kudhani kuna mtu atawaamulia. Hivyo wana wajibu mkubwa kwani takwimu zinaonyesha asilimia 60% ya idadi ya watu nchini ni vijana! Sasa sijui kama kwa mwandishi na mhariri wake tafsiri ndio hiyo?!!!
Imenisikitisha sana!
Nape Moses Nnauye
The CCM Secretary for Ideology & Publicity"
AT sasa aamua kupenda
AT katika poz |
Na Elizabeth John
BAADA ya kutamba na ngoma yake ya ‘Kitumbua’, mkali wa
muziki wa mduara nchini, Ally Ramadhan 'AT' anatarajia kuachia kazi mpya
inayokwenda kwa jina la ‘Anapenda’.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, nyota huyo alisema
kazi hiyo anatarajia kuisambaza katika vituo mbalimbali vya radio baada ya
kukamilika.
“Nashukuru Mungu kupata nafasi nyingine tena ya kurudi
katika kazi yangu baada ya kimya kisichojulikana," alisema.
Msanii huyo ambaye anajulikana kama mfalume wa muziki huo
kwa sasa alifanya vizuri na vibao mbalimbali kikiwemo Kifuu Tundu, Bao la Kate
na nyinginezo ambazo zilimpa umaarufu mkubwa katika tasnia ya muziki huo.
Pia mkali huyo yuko katika hatua za mwisho kukamilisha video
ya kazi yake inayoitwa ‘Kitumbua’, ambayo muda wote itaanza kuonekana kupitia
kwenye runinga runinga na akiamini utapata nafasi kubwa ya kuwakonga mashabiki
wa tasnia hiyo.
Hivyo, aliwaomba mashabiki kumuunga mkono katika kazi zake zijazo ili kuhakikisha anafikia malengo aliyojiwekea katika tasnia hiyo ya muziki wa kizazi kipya nchini hususan wa ‘Mduara’ ambao anaendelea kufanya vizuri na kutishia waliopo kwenye burudani hiyo.
Maugo, Mwakyembe wachezea vichapo Russia
Mada maugo |
Benson Mwakyembe |
MABONDIA Mada Maugo na Benson Mwakyembe waliondoka nchini na tambo za kufanya kweli nchini Russia wamejikuta wakiambulia vipigo toka kwa wenyeji wao waliopambana nao jana nchini humo.
Maugo yeye alikumbana na kipigo cha TKO ya raundi ya tano toka kwa Movsur Yusupov katika pambano la uzito wa Super Middle la raundi nane.
Bondia huyo mwenye maneno mengi alisalimu amri mwenyewe katika pambano hilo lililoichezwa kwenye viwanja wa Trade & Entertainment Centre 'Moskva' Kaspiysk.
Mabondia hap walioondoka wakiapa kwenda kuwashikisha adabu wapinzani wao wanatarajiwa kurejea nchini kesho kutwa tayari na maandalizi ya mapambano yao mengine.
Maugo anatarajiwa kupanda ulingoni Agosti 30 dhidi ya Thomas Mashali katika moja ya mapambano yatakayosindikiza pigano kati ya Francis Cheka na Mmarekani Findley Derrick la kuwania ubingwa wa WBF litakalochezwa Diamond Jubilee.
Hatimaye Mbowe asalimisha ushahidi wa bomu la Arusha Polisi
HATIMAYE Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), Freeman Mbowe, jana amewasilisha kwa maandishi ushahidi wake
makao makuu
ya Jeshi la Polisi mjini Dar es Salaam. Maelezo ya Mbowe ambayo jana
yaliwasilishwa, yamekuwa siri nzito, kwani yanatokana na msimamo wa
CHADEMA kudai wana ushahidi na tukio la mauaji ya mlipuko wa bomu
lililotokea Juni 15, mwaka huu mkoani Arusha.
Wakili wa Mbowe, Peter Kibatala alilithibitishia MTANZANIA
mjini Dar
es Salaam jana, kuwa aliwasilisha saa 5 asubuhi ambapo alipokelewa na
Mkuu wa Idara ya Operesheni za Upelelezi Tanzania (CID), Kamishna
Advocate Nyombi.
Baada ya kuwasilisha maelezo hayo, Wakili Kibatala alikataa katakata kuzungumzia kilichomo ndani ya maandishi hayo, kwa madai kuwa ni siri yao na polisi.
“Nathibitisha bila shaka, nimewasilisha majibu kwa niaba ya Mbowe leo (jana), makao makuu ya polisi kama tulivyokubaliana, lakini yaliyoandikwa humo ni siri…siwezi kuzijadili tusubiri kutoka kwao,” alisema Kibatala.
Hatua ya kuwasilisha majibu hayo kimaandishi, ilifikiwa Jumatano wiki hii katika mahojiano baina ya Polisi na Mbowe.
Siku hiyo, Mbowe aligoma kuwasilisha ushahidi wake polisi kama alivyotakiwa kwenye barua aliyoandikiwa na jeshi hilo Julai 17, mwaka huu, kwa kile alichosema hadi Rais Jakaya Kikwete atakapounda tume ya kijaji kuchunguza tukio hilo.
Katika barua hiyo, Mbowe alitakiwa kufika bila kukosa akiwa na ushahidi wa mauaji ya mlipuko wa bomu hilo.
Hata hivyo, Mbowe aliripoti kuitikia wito wa barua hiyo, lakini aliendelea kushikilia msimamo wake wa kutowasilisha ushahidi huo kwa polisi.
Jeshi la Polisi, limekuwa katika mvutano na Mbowe likimtaka kuwasilisha ushahidi kuhusu mlipuko wa bomu hilo, katika Uwanja wa Soweto wakati wa mkutano wa kuhitimisha kampeni za uchaguzi mdogo wa madiwani katika kata nne na kuua watu wanne na kujeruhi wengine 70, katika uwanja huo ushahidi ambao alidai anao.
Endapo Mbowe atakutwa na hatia ya kutokuwa na ushahidi huo, atakumbwa na adhabu ya miaka mitatu jela au faini ya Sh 500,000.
Hii ni kwa mujibu wa Jeshi la Polisi katika barua yake kwa Mbowe, ikunukuu kifungu cha sheria ya kifungu cha 10(2) na (2A) cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai nchini, sura ya 20, kama ilivyorekebishwa mwaka 2002.

Aibu kwa Taifa! Watanzania wengine wanaswa na 'unga' ughaibuni
Baadhi ya Dawa za kulevya zikiwa zimenaswa |
WIKI chache baada ya watanzania kadhaa akiwamo video Queen', Agnes Gerrard 'Masogange' na nduguye Mellisa Edward kunaswa Afrika Kusini na dawa za kulevya, watanzania wengine wawili wamekamatwa na dawa hizo huko Hongkong.
Taarifa zilizochapishwa na serikali ya nchi hiyo imesema watanzania hao ni kati ya abiria watatu walionaswa kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa nchi hiyo juzi wakiwa na 'unga' wenye thamani ya Dola za Kimarekani Milioni 3.34.
Taarifa hiyo imekuja siku chache tu baada ya mmoja wa wafungwa waliokamatwa nchini humo kwa kosa na kuingiza dawa hizo za kulevya kutuma waraka unaoeleza Tanzania ilivyochafuka ughaibuni kwa biashara hiyo kiasi kwamba Wabongo wanapekuliwa uchi wa nyama wafikapo uwanja wa ndege wa Hongkong.
Mfungwa huyo aliweka bayana namna biashara hiyo ilivyokithiri na kuhusisha vigogo wa serikali, wabunge na hata watu wenye thamani ya ulinzi na usalama wa raia.
Jisomee taarifa hiyo ya kukamatwa kwa watanzania hao ikiwa ni muendelezo wa raia wa Taifa hilo lililokuwa na sifa nzuri mbele ya macho ya dunia kunaswa wakiingiza dawa hizo katika mataifa mengine baadhi ikielezwa wamenyongwa CHINA na kuhukumiwa vifungo vya muda mrefu kama kilichowakuta mabondia wa Tanzania nchini Mauritius hivi karibuni.
Taarifa hiyo ya serikali ya Hongkong ilipachikwa katika tovuti yao juzi Julai 26, 2013.
Hong Kong Customs yesterday (July 25) detected three drug trafficking cases, with seizures totally valued at $4.78 million, in the department's escalated anti-narcotics efforts to combat drugs.
Customs officers at the Hong Kong International Airport (HKIA) intercepted a 26-year-old incoming male passenger arriving from Tanzania for clearance yesterday afternoon and seized 1.6 kilogrammes of heroin concealed in two false compartments of his hand carry briefcase. The drugs would fetch a value of about $1.28 million.
Later in the evening, Customs officers at the HKIA intercepted another 45-year-old man from Tanzania for clearance. On suspicion of concealment of drugs inside his body, the suspect was escorted to hospital where he discharged 204 grammes of heroin after staying for one day. The value of the drugs was about $0.16 million. The suspect is still in the hospital.
In the same evening, Customs officers intercepted a 28-year-old man at a carpark in Tai Kok Tsui. Approximately 2.03 kg of cocaine camouflaged as snacks were found inside a plastic bag carried by him.
Customs officers later escorted the suspect to a domestic flat nearby for a search and seized 1 kg of cocaine and 290 grammes of crack cocaine there. The total value of the seizure was about $3.34 million.
A Customs spokesperson said today (July 26) that all three suspects in the three cases were arrested for drug trafficking. The cases are still under investigation.
Under the Dangerous Drugs Ordinance, drug trafficking is a serious offence. The maximum penalty is life imprisonment and a fine of $5 million.
Ends/Friday, July 26, 2013
Issued at HKT 23:43

Mama amchoma mwanae mikono kisa kala samaki badala ya maharage
MTOTO Bryton Evarist (9) mkazi wa Temeke, Uwanja wa
Taifa jijini Dar es Salaam, amejeruhiwa vibaya baada ya kuunguzwa mikono
kwa kubanikwa kwenye jiko la mkaa na mama yake mzazi.
Mwanamke aliyefanya unyama huo ni Asa Barnaba (24), ambapo inadaiwa baada ya tukio hilo alimfungia ndani kwa muda wa wiki mmoja na kumlazimisha kula na kuoga kwa kutumia mikono aliyomuunguza.
Tukio hilo linadaiwa kufanywa wiki tatu zilizopita majira ya usiku, baada ya mtoto huyo kudaiwa kula samaki wa kitoweo.
Akisimulia mkasa huo akiwa Hopitali ya Temeke, mtoto huyo ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tatu Shule ya Msingi Kibasila, alisema mama yake alichukua hatua hiyo baada ya kukasirishwa na kitendo hicho.
Alisema siku ya tukio, alirudi nyumbani mapema akitokea shuleni, alipofika nyumbani kwao alikuta chakula pamoja na mboga mbili aina ya maharage na samaki.
Bila ya kutambua kwamba samaki hao waliwekwa kwa ajili ya kitoweo cha usiku, aliamua kula na kuyaacha maharage.
"Mama aliporudi na kukuta nimekula samaki, aliniuliza kwa nini nimekula, lakini nilikataa kwa kuogopa kupigwa," alisema.
Hata hivyo, baada ya kubanwa sana, mtoto huyo aliamua kukubali kula ndipo mama yake alipochukua jiko la mkaa lenye moto na kumuweka mikono yake juu ya moto uliokuwa unawaka.
"Alichukua mikono yangu na kuniweka kwenye jiko, nilihisi maumivu makali sana," alisema.
SIRI YABAINIKA
Akiongea na NIPASHE Jumamosi, Afisa Ustawi wa Jamii wa Manispaa ya Temeke, Sharifa Ally, alisema mtoto huyo aligundulika kufanyiwa unyama huo baada ya wiki moja akiwa katika hali mbaya.
Alisema aligundulika baada ya kutoroka na kwenda kuomba msaada kwa wapita njia ili wamsaidie kumpeleka hospitali.
"Inashangaza sana kuona mama mzazi akiwa na moyo wa kikatili, muda wote alikuwa akienda kazini na kumuacha mtoto wake ndani akioza mikono," alisema Sharifa.
Sharifa, alisema hatua hiyo ilisaidia mtoto huyo kupelekwa kituo cha Polisi cha Chang'ombe na kisha kufikishwa Hospitali ya Temeke.
"Akiwa hospitalini, sisi Ustawi wa Jamii na Jeshi la Polisi tulisimamia kwa karibu matibabu yake pamoja kuangalia namna na kumfungulia kesi mhusika," alisema.
MAMA AKIRI
Mama wa mtoto huyo alipoulizwa sababu ya kufanya kitendo hicho, alisema aliamua kumchoma moto mtoto wake baada ya kuchoshwa na tabia yake ya wizi kwa muda mrefu.
"Huyu mtoto ana tabia ya wizi, mwanzo alikuwa akiniibia hela ndani, nilimuonya sana na wakati mwingine nilimpiga lakini hakusikia, ndipo alipokula mboga niliamua kumchoma moto ili asirudie," alisema Asa.
Hata hivyo, alisema anajutia kufanya tukio hilo na hakufikiria kwamba mtoto wake angepata majeraha kama aliyonayo kwa sasa.
Baba wa mtoto huyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Evarist akiongea kwa simu kutoka mkoani Kigoma, alisema bado hajapata taarifa ya tukio hilo na alionyesha kusikitishwa kwake.
"Aisee! sijapata kabisa taarifa ya jambo hilo, nasikitika sana," alisema na kukata simu.
Alipotafutwa Kamanda wa Mkoa wa Polisi wa Temeke, Engelbert Kiondo kwa njia ya simu, hakupatikana baada ya mtu aliyepokea kueleza yupo nje kikazi.

CHANZO:
NIPASHE
Lion Boy amtwanga Mthailand kwa KO
Omari Kimweri |
BONDIA Mtanzania Omari Kimweri 'Lion Boy' anayefanya shughuli zake
nchini Australia ameendelea kutamba katika nchi hiyo baada ya jana
kumtwanga kwa KO ya raundi ya kwanza bondia Ekkalak Saenchan wa Thailand ikiwa ni mchezo wake wa 16 tangu aingie katika ngumi za kulipwa nchini humo
Bondia huyo ambaye anaitangaza vyema nchi ya Tanzania Kimataifa ameahidi
kuenderea kutoa vipigo kwa mabondia mbalimbali pindi wakutanapo
ulingoni
Bondia huyo aliyezaliwa Tanzania katika jiji la Dar es salaam mwaka1982
amekuwa gumzo nchini humo kwa kuonesha mchezo mzuri unaowavutia raia
wengi wa Australia na kuweza kuwa bondia namba moja katika nchi hiyo huku
katika Dunia akishikilia nafasi ya 52 katika mabondia 450 duniani wenye
uzito wa light flyweight
Anasema lengo lake kubwa ni kuukamata ubingwa unaotambulika kimataifa Duniani wa WBA World light flyweight title unaoshikiliwa na bingwa namba moja Duniani ,Roman Gonzalez na IBF light flyweight title unaoshikiliwa na John Riel Casimero wa Philippines ambao wanamuumiza kichwa.
Uchaguzi Mkuu wa BFT sasa Oktoba 26 Morogoroooo!
UCHAGUZI Mkuu wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT) ambao ulikwama kufanyika Julai 7 mwaka huu jijini Mwanza sasa utafanyika Oktoba 26 mjini Morogoro.
Kwa mujibu wa taarifa iiyotolewa na Katibu Mkuu wa BFT, Makore Mashaga kwa MICHARAZO ni kwamba uamuzi wa tarehe hiyo na eneo jipya la kufanyia uchaguzi huo ulitolewa juzi na Kamati ya Utendaji ya shirikisho hilo iliyokutana jijini Dar es Salaam na kuudhuriwa na viongozi wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT).
Uchaguzi huo ulikwama kufanyika kama ulivyopangwa kutokana na idadi ndogo ya wagombea waliojitokeza, nafasi nyingine zikikosa kabisa wagombeaji na idadi ndogo ya wapiga kura iliyoshindw kufikia kolamu.
Mashaga alisema kuwa baada ya kamati kukaa chini na kujadili cha kufanya hatimaye iliamriwa uchaguzi huo sasa upafanyike Oktoba kutoa muda wa kujitokeza kwa wagombea huku wakipewa maelekeo na BMT wanahyotakiwa kutekeleza ndani ya siku 90.
Katibu huyo alisema maelekezo waliyopewa ni pamoja na kurekebisha katiba yao ili kulingana na maagizo ya msajili wa vyama vya michezo na ile a Shirikisho la Ngumi la Kimataifa (AIBA).
Pia kuhakiki uhai wa wanachama wake na kusajili wengine kulingana na maekelezo ya katiba ya BFT pamoja na kuhakikisha BFT inajamasisha wadau kuijitokeza kuwania uongozi katika uchaguzi huo.
"Baada ya maamuzi hayo ni kwamba sasa BFT tunaanza upya mchakato wa uchaguzi huo na kwamba safari hii utafanyika Morogoro Oktoba 26," alisema.
Uongozi wa sasa BFT uliingia madarakani Machi 2009 baada ya waliokuwa viongozi wa shirikisho hilo chini ya akina Shaaban Mintanga kujiuzulu kutokana na kashfa ya dawa za kulevya iliwahusisha mabondia waliokamatwa Mauritius walipoenda kushiriki michuano ya Afrika.
Taarifa rasmi ya BFT hiyo hapo
Subscribe to:
Posts (Atom)