|
Ndanda Fc waliporomoka hadi mkiani katika msimamo wa Ligi ikiuaga 2014 na kukaribisha 2015 |
|
Didier Kavumbagu akishangilia moja ya mabao yake na wachezaji wenzake Himid Mao na Aggrey Morris |
BAO la kuongoza la Azam limemzindua Didier Kavumbagu ambaye alikuwa hajafunga muda mrefu kuwakimbia washambuliaji wenzake na kuongoza msimamo wa orodha ya wafungaji bora katika Ligi Kuu Tanzania Bara, huku Amissi Tambwe akifungua akaunti ya mabao Jangwani.
Didier alifunga bao la kuongoza la Azam leo na kumfanya kufikisha mabao matano na kuongoza orodha ya wakali wa mabao wakati ligi kuu ikimaliza mwaka 2014 na kusubiri kuendelea tena mwakani.
Simon Msuva aliyefunga bao la pili la Yanga naye ameingia kwenye orodha ya wakali wa mabao akiwa na mabao manne akilingana na wachezaji wengine, Danny Mrwanda wa Yanga, Rama Salim (Coastal Union), na Ame Ally (Mtibwa)
Ligi ikiaga mwaka 2014, Mtibwa ipo kileleni, huku Ndanda ikiachiwa nafasi ya mkiani na Mbeya City waliowanyuka bao 1-0 leo jijini Mbeya.
Ndanda inazibeba timu zote ikiwa na pointi sita, wakati Mbeya City kwa ushindi wa leo imechupa hadiu nafasi ya 12.
Msimamo kamili wa ligi hiyo baada ya kumalizika kwa mechi za raundi nane ni kama ifuatavyo;
P W D L F A GD Pts
01. Mtibwa Sugar 08 04 04 00 11 04 07 16
02. Yanga 08 04 02 02 11 07 04 14
03. Azam 08 04 02 02 10 06 04 14
04. Kagera Sugar 08 03 04 01 07 04 03 13
05. Coastal Union 08 03 03 02 09 07 02 12
06. Polisi Moro 08 03 03 02 08 07 01 12
06. JKT Ruvu 08 03 01 04 07 08 -1 10
07. Ruvu Shooting 08 03 01 04 05 07 -2 10
08.Stand Utd 08 02 04 02 06 10 -4 10
09.Simba 08 01 06 01 07 07 00 09
09. Mgambo JKT 08 03 00 05 04 09 -5 09
12. Mbeya City 08 02 02 04 03 06 -3 08
13. Prisons 08 01 04 03 06 07 -1 07
14. Ndanda Fc 08 02 00 06 08 13 -5 06
Wafungaji Bora:
5- Didier Kavumbagu (Azam)
4- Rama Salim (Coastal), Danny Mrwanda, Simon Msuva (Yanga) Ame Ally (Mtibwa)
3- Ally Shomari, Emmanuel Okwi (Simba), Rashid Mandawa (Kagera Sugar)
2- Shaaban Kisiga, (Simba), Nassor Kapama (Ndanda) Salum Kanoni (Kagera), Aggrey Morris (Azam), Najim Magulu, Samuel Kamuntu, Jabir Aziz (JKT Ruvu), Amissi Tambwe, Jerry Tegete (Yanga), Ibrahim Kihaka (Prisons), Mussa Mgosi (Mtibwa), Heri Mohammed (Stand Utd), Ally Nassor (Mgambo), Malimi Busungu (Mgambo), Nicolaus Kabipe (Polisi)
Mechi zijazo;
Jan 03, 2014
Coastal Union vs JKT Ruvu
Ruvu Shooting vs Kagera Sugar
Azam vs Mtibwa Sugar
Stand United vs Polisi Moro
Mbeya City vs Yanga
Jan 4, 2015
Mgambo JKT vs Simba
Prisons vs Ndanda