WACHEZAJI
tisa wa Kanembwa JKT pamoja na timu yao wanaolalamikiwa na Shirikisho la Mpira
wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kumpiga mwamuzi Peter Mujaya wanatakiwa kujitetea
mbele ya Kamati ya Nidhamu itakayokutana Jumapili (Februari 9 mwaka huu).
Utetezi
huo unaweza kuwa wa mdomo kwa walalamikiwa kufika wenyewe mbele ya kamati
itakayokutana saa 4 kamili asubuhi au kuuwasilisha kwa njia ya maandishi.
Kamati
ilikutana jana Jumatano (Februari 5 mwaka huu) kusikiliza malalamiko dhidi ya
wachezaji hao na timu yao kwa tukio hilo lililotokea Novemba 2 mwaka jana
kwenye mechi ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) dhidi ya Stand United FC iliyochezwa
Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
Wachezaji
hao ni Abdallah Mgonja, Bariki Abdul, Philipo Ndonde, Mbeke Mbeke, Mkuba
Clement, Mrisho Mussa, Nteze Raymond, Ntilakigwa Hussein na Uhuru Mwambungu.
Mlalamikiwa mwingine ambaye naye anatakiwa kujitetea ni timu ya Kanembwa JKT.
Ikiwa
chini ya Mwenyekiti wake Tarimba Abbas, Kamati hiyo baada ya kusikiliza malalamiko
dhidi ya wahusika na kupokea ushahidi wa aina mbalimbali kutoka kwa mlalamikaji
imesema ili iweze kutenda haki katika shauri hilo ni lazima walalamikiwa wapate
fursa ya kusikilizwa.
Katika
hatua nyingine, Kamati hiyo iliyokutana kwa mara ya kwanza tangu ilipoundwa
imesema imesikitishwa na vitendo vya fujo ndani ya mpira wa miguu, na kuwataka
watu wasijihusishe na aina yoyote ya fujo