WASOMAJI WETU TUNAOMBA RADHI KAMA UTAKWAZIKA NA PICHA ZIFUATAZO.
Mtoto
mmoja aliyelalaliwa na kusababisha kifo chake na basi la Zuberi T.119
AZZ lilokuwa likitokea Mwanza kuelekea jijini Dar-es-salaam na kupinduka
katika eneo la kijiji cha Tumaini kata ya Issuna wilaya ya Ikungi
wakati likimkwepa bibi aliyekuwa akikatisha barabara.(Picha na Nathaniel
Limu).
Mmoja wa majeruhi akiwa amelazwa katika Hosptali ya Mkoa ya Singida.
Mmoja wa majeruhi akiongea na waandishi wa habari katika Hospitali ya mkoa mjini Singida.
Basi
la Zuberi T.119 AZZ lilokuwa likitokea Mwanza kuelekea jijini
Dar-es-salaam na kupinduka katika eneo la kijiji cha Tumaini kata ya
Issuna wilaya ya Ikungi wakati likimkwepa bibi aliyekuwa akikatisha
barabara.(Picha na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu, Singida
BASI
la kampuni ya Zuberi T.119 AZZ lililokuwa linatokea jijini Mwanza
likielekea jijini Dar-es-salaam,limepinduka na kusababisha vifo vya
abiria wawili na kujeruhi vibaya wengine arobaini wakati likimkwepa
bibi mmoja aliyekuwa anakatisha barabara.
Ajali
hiyo imetokea jana saa 7.30 mchana katika barabara kuu ya Sindida
–Dodoma eneo la kijiji cha Tumaini kata ya Issuna wilaya ya Ikungi
mkoani Singida.
Afisa
wa makosa ya jinai mkoa wa Singida (RCO), Thobias Sedoyeka amesema kuwa
basi hilo lililokuwa likiendeshwa na Fadhili Kalembo (35),lilipofika
eneo la tukio,bibi mmoja alijitokeza akiwa anavuka barabara.
Amesema
dereva wa basi alijitahidi kumkwepa bibi huyo lakini ghafla bibi
alirudi tena barabarani kitendo kilichosababisha basi hilo kupinduka na
kuserereka hatua zaidi ya 50 wakati likimkwepa kwa mara ya pili.
“Basi
hili lilimlalia mtoto mdogo ambaye aliweza kutolewa baada ya basi la
Zuberi kunyanyuliwa na wichi ya lori ambalo lilikuwa linapita katika
barabara hiyo”,amesema.
Kwa
upande wake Mganga Mfawidhi wa hospitali ya mkoa ya mjini Singida,
Deogratus Banuba amesema kuwa wamepokea maiti moja iliyotokana na ajali
ya basi la Zuberi na kwamba bado wanaendelea kusubiri mwili wa mtoto
aliyefia eneo la ajali.
“Kwa
upande wa majeruhi,tumepokea majeruhi 40 ambao wameumia vibaya sehemu
mbalimbali ya miili yao ikiwemo kuvunjika mikono na miguu.Kati yao
wanne,mikono yao imesagika vibaya na tumejitahidi kuirudisha katika hali
yake”,amesema Dk.Banuba.
Amesema kuwa majeruhi wengine wanne,wao wamewapa rufaa ya kwenda hospitali ya KCMC Moshi mjini mkoa wa Kilimanjaro.
Chanzo: Mo blog
No comments:
Post a Comment