Askari
wa Kikosi cha kutuliza Fujo Akizima Moto uliowashwa na wakulima
waliofunga barabara ya Morogoro Iringa Leo Asubuhi.Wakulima hao
walifunga Barabara hiyo kwa Lengo la kushinikiza kuonana na Mkuu wa Mkoa
wa Morogoro Dk Joel Bendera Ili
kutatua Mgogoro uliopo kati ya wakulima na wafugaji uliopo katika
vijiji hivyo.Askari wa jeshi la Polisi walilazimika Kutumia Mabomu ya
Machozi mara baada ya Wananchi wao kugoma Kuonana na Kamati ya ulinzi ya
Wilaya ya Mvomero Ikiongozwa na Mkuu Wa Wilaya ya mvomero
Wananchi wa Kijiji cha Mangae wakiwa wamefunga Barabara wakiwa wamishika mawe na Silaha za Jadi wakikataa kabisa kufungua barabara hiyo wakitaka Mkuu wa Mkoa kuja Kuoanana Nao.
Mabomu
ya machozi yametumika kuwatawanya wakulima wa eneo la Melela, Mvomero
mkoani Morogoro waliokuwa wamefunga barabara ya Iringa - Morogoro
wakimtaka Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera aende kusuluhisha
mgogoro uliopo baina yao na wafugaji. Wakulima
wa kijiji cha Mangae wilaya Mvomero wamefunga barbara kuu ya Morogoro
Wakulima hao ambao wanalima katika Mashamba yaliopo eneo la Mkangazi
baada ya wananchi kuvamiwa na kupigwa wakulima hao walikusanyikajana usiku na kufikia maamuziWakulima
hao wanadai kuwa wenzao watano jana wamevamiwa na wafugaji wa kabila la
Wamasai na kuwajeruhi vibaya kwa vitu vyenye ncha kali na kupelekea
kulazwa katika Hospitali ya Mkoa Morogoro.
Mkuu
wa Wilaya ya Mvomero, Anthony Mtaka alifika eneo hilo ambapo wananchi
hao walikuwa wamechoma matairi na kusababisha mgongamano mkubwa wa
magari yaendayo Iringa na yale yaelekeayo Moro lakini wakulima hao
walikataa kumsikiliza wakimtaka mkuu wa mkoa. Baada
ya vurugu kuwa kubwa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine
Shilogile aliwaaamuru vijana wake wawatawanye wakulima hao ambao
waligoma na kuanza kuwapiga kwa mawe kitendo kilichopelekea polisi
kupiga mabomu ya machozi na kufanikiwa kuwatawanya.Wananchi takribani 20
wamekamatwa na polisi katika vurugu hizo.Kwa sasa hali kidogo imetulia
na magari yameanza kupita eneo hilo
Askari wa
Jeshi la Polisi Wakiwa Onyo wakulima wa Kijiji Hicho Kabla ya Kuanza
Kutumia Mabomu ya Kutoa Machozi kwa Lengo la Kuwatanya
No comments:
Post a Comment