STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, July 18, 2014

Maximo ashikilia hatma ya wachezaji wa3 Yanga

Kocha Marcio Maximo
Kikosi cha Yanga
IMEFAHAMIKA kuwa wachezaji watatu wa kigeni wa klabu ya Yanga kiungo Haruna Noyinzima na washambuliaji wawili wa kimataifa wa Uganda Hamisi Kiiza Diego na Emmanuel Okwi hatima yao ya kuendelea kuitumikia klabu hiyo yenye maskani yake katika makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani iko mikononi mwa kocha mpya wa klabu hiyo Mbrazil Marcio Maximo. 
Habari zilizoifikia rockersports kutoka kwa mmoja wa viongozi wa klabu hiyo ambaye hakutaka jina jina lake kutajwa mtandaoni humu, amesema ujio wa wachezaji wawili kutoka nchini Brazil mshambuliaji Geilson Santos Santana "Jaja" na Kiungo mshamabuliaji Andrey Marcel Ferreira Coutinho kunawaondoa mmoja wa wachezaji wa kigeni kutoka ukanda huu wa Afrika mashariki kwa kuwa wachezaji hao wa Brazil walioletwa na Maximo si wa majaribio bali wamekuja kufanya kazi.
Chanzo hicho kimesema kwa mujibu wa kanuni za usajili za shirikisho la soka nchini TFF ni dhahiri wachezaji wa kigeni wanatakiwa watano na mpaka sasa Yanga imefikisha idadi ya wachezaji saba hivyo basi kuna hatari kati ya Niyonzima na Okwi mmoja akaondoka Jangwani msimu huu.
Taarifa zaidi zinasema kumekuwepo na mazungumzo yanayo endelea baina ya wachezaji hao na kamati ya usajili ya klabu hiyo ambayo kimsingi yanagusa juu ya namna ya kumalizana nao huku zoezi hilo likikumbwa na presha kubwa kutoka kwa mashabiki wa klabu hiyo.
Rockersports

Jose Mourinho amchokonoa Wenger kuhusu Sami Khedira

Sami Khedira
KLABU ya Chelsea imepata nguvu mpya ya mapambano ya kupata saini ya Sami Khedira kufuatia wakala wake kudai kuwa hakuna mazungumzo yoyote yaliyofikiwa mpaka sasa na Arsenal.
Meneja wa 'The Blues' Jose Mourinho amefanikisha usajili wa mlinzi wa kushoto Filipe Luis akitokea Atletico Madrid kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni £18 na sasa anajipanga kwa ajili ya kiungo wa kimataifa wa Ujerumani Khedira.
Hapo kabla ilikuwa imefahamika kuwa Arsenal imekamilisha dili la uhamisho wa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27 kwa ada ya pauni milioni £20, lakini walikwama kufikia makubaliano ya mshahara wake wa wiki ambao nyota huyo alikuwa akitaka zaidi ya pauni £180,000.
Amekaririwa wakala wa Khedira, Jorg Neubauer akisema 
 ‘Hatuko kwenye mazungumzo na Arsenal. Sidhani kama ada itakubalika, vinginevyo wange kwisha kunipatia taarifa.’
Khedira amekuwa akimpendeza Mourinho tangu wakati huo akiwa bosi wa Real na inaelezwa kuwa huenda Mourinho akamvuta Stamford Bridge.
Recruit: Chelsea boss Jose Mourinho has already acquired Diego Costa and Filipe Luis
Usajili: Bosi wa Chelsea Jose Mourinho amesha msajili Diego Costa na Filipe Luis

Wakati hayo yakiwa hivyo, Chelsea imethibitisha makubaliano na mlinzi wa kushoto wa Atletico Fillipe Luis.
Mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 28 atakamilisha uhamisho wake baada ya kufanikisha kipimo cha afya na makubaliano ya maslahi binafsi.
Usajili wa Mourinho unaendelea akiwa bado katika ushawishi kwa Khedira, matumaini yake ya kumsajili Antoine Griezmann aliyethaminishwa kwa pauni £20 na klabu yake ya Real Sociedad huenda yakagonga mwamba kufuatia upinzani mkubwa kutoka kwa vilabu vya Monaco na Liverpool.
Blue: Chelsea have confirmed the signing of Brazilian defender Filipe Luis (left)
Chelsea imethibitisha kumsajili mlinzi wa kibrazil Filipe Luis

Serengeti Boys wapo njema kuwavaa Amajimbos U17

KOCHA Mkuu wa Serengeti Boys, Hababuu Ali Omari amesema morali ya wachezaji wake ipo juu kwa ajili ya mechi dhidi ya Afrika Kusini (Amajimbos) itakayochezwa leo.
Mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 itafanyika kwenye Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi jijini Dar es Salaam kuanzia saa 10 jioni. 
Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari kwenye ofisi za TFF jijini Dar es Salaam, Kocha Hababuu amesema nia ya kikosi chake ni kuhakikisha wanafika kwenye fainali za Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Niger. 
“Tunaiheshimu Afrika Kusini, lakini hatuiogopi. Morali ya wachezaji ipo juu na wanajiamini. Kimsingi wanajua kuwa hii ndiyo njia ya wao kutokea kwenye mpira wa miguu, kwa hiyo lengo ni kushinda,” amesema Kocha Hababuu. 
Naye Kocha wa Afrika Kusini, Molefi Ntseki amesema anaziheshimu timu za Tanzania, na changamoto aliyonayo ni kuhakikisha kuwa anashinda mechi hiyo kwani mara ya mwisho kwa timu yake kushiriki fainali za Afrika ilikuwa miaka sita iliyopita. Kiingilio katika mechi hiyo ni sh. 2,000 na tiketi zitapatikana uwanjani kwenye magari maalumu.

Mambas kutua mchana huu kuwafuata Stars Taifa

http://cdn1.portalangop.co.ao/angola/pt_pt/files/highlight/2014/2/10/0,278d8f7f-0422-46b1-b24f-eba7dd500a60--r--NjQweDM0Mw==.jpg
Kikosi cha Mambas
KIKOSI cha Mambas toka Msumbiji inatarajiwa kuwasili mchana huu tayari kwa pambano lao dhidi ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars litakalochezwa Jumapili, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 
Mambas itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 7.30 mchana kwa ndege ya LAM ikiwa na msafara wa watu 37 ambapo kati ya hao, 25 ni wachezaji. 
Wachezaji watakaokuwa kwenye msafara huo ni; Almiro Lobo, Apson Manjate, Bone Mario Uaferro, Dario Ivan Khan, Edson Sitoe, Eduardo Jumisse, Gelicio Aurelio Banze, Helder Pelembe, Josemar Machaisse, Elias Pelembe, Isac Carvalho na Jeffrey Constatino. 
Wengine ni Manuel Fernandes, Manuel Uetimane, Mario Sinamunda, Momed Hagi, Reginaldo Fait, Reinoldo Mandava, Ricardo Campos, Saddan Guambe, Simao Mate Junior, Soares Victor Soares, Stelio Ernesto, Vando Justino na Zainadine Junior. 
Timu hiyo itafikia kwenye hoteli ya Accomondia, na itaondoka Jumapili mara baada ya kumalizika kwa mechi hiyo itakayochezeshwa na mwamuzi Mahmoud Ashour.

UJERUMANI YAKWEA KILELE UBORA DUNIANI, TANZANIA HAIJAMBO

Mabingwa wapya wa Dunia, Ujerumani
MABINGWA wapya wa Dunia, Ujerumani imepaa hadi kileleni mwa viwango vya ubora wa soka duniani ikiwa ni mara ya kwanza kwao katika miaka 20, FIFA ilitangaza jana.
Ushindi wa 1-0 katika mechi ya fainali umewainua hadi nafasi ya kwanza katika orodha ya viwango hivyo, nafasi moja juu ya wapinzani wao wa mechi ya fainali, Argentina, ambao wamepanda kwa hatua tatu hadi nafasi ya pili.
Uholanzi wamepaa kwa hatua 12 hadi kushika nafasi ya tatu kufuatia mwendo wao mzuri uliowashuhudia wakimaliza wa tatu katika Kombe la Dunia nchini Brazil.
Hispania wamelipa gharama ua kushindwa kusonga mbele kutoka katika hatua ya makundi nchini Brazil kwa kuanguka kutoka katika nafasi ya kwanza hadi ya nane, huku Colombia, Ubelgiji na Uruguay zikichukua nafasi za juu yao.
Wenyeji Brazil, waliosambaratishwa kwa magoli 7-1 dhidi ya Ujerumani katika nusu fainali katika matokeo yaliyostua zaidi kwenye michuano hiyo, wameanguka kwa hatua nne hadi kushika nafasu ya saba.
England wameanguka kwa hatua 10 hadi kushika nafasi ya 20 katika orodha hiyo ya viwango, nafasi ambayo ni ya chini zaidi kwao tangu Mei 1996, baada ya mwendo mbaya kwenye Kombe la Dunia ambao vipigo katika mechi mbili za ufunguzi ziliwapa rekodi mbaya zaidi katika miaka 50.
Katika orodha hizo Tanzania imejitoa kimasomaso kwa kukwea kwa nafasi saba kutoka nafasi ya 113 mpaka 106 huku kwa upande wa Afrika nako kukiwa na mabadiliko kwa Algeria kuongoza kwa kuwa katika nafasi ya 24 walikufuatiwa na waliokuwa vina Ivory Coast katika nafasi ya 25.
'Top 10' ya Dunia inaongozwa na 1. Ujerumani, 2. Argentina, 3. Uholanzi, 4. Colombia, 5. Ubelgiji, 6. Uruguay, 7. Brazil, 8. Hispania, 9. Uswisi, 10. Ufaransa.
Tanzania imepaa kwa nafasi hatua 7 hadi kushika nafasi ya 106 duniani wakati wapinzani wao wa Jumapili kwenye kuwania kufuzu kwa hatua ya makundi ya kuwania kucheza fainali za Mataifa ya Afrika 2015, Msumbiji nao wakipaa kwa hatua nne hadi kushika nafasi ya 114 duniani.
5-Bora ya Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati inaongozwa na Uganda inayoshika nafasi ya 87 duniani, Kenya (95, duniani), Tanzania (106), Rwanda (109) na Ethiopia (110).
'Top 10' ya Afrika inaundwa na Algeria inayoshika nafasi ya 24 duniani, Ivory Coast (25, duniani), Nigeria (34), Misri (36), Ghana (38), Tunisia (42), Guinea (51), Cameroon (53), Burkina Faso (58) na Mali wanaoshika nafasi ya 60 duniani.

 

Miili 100 yaokotwa ajali ndege 'iliyodunguliwa' Ukraine


Mabaki ya miili zaidi ya 100 yameokotwa jirani na eneo ilipoanguka ndege ya Malaysian Airlines kule Grabovo jirani na mpaka wa Ukraine na Urusi . 

 
Reuters iliripoti mapema Alhamisi kuwa ndege hiyo yenye namba MH17 ilianguka jimboni Donetsk ikiwa njiani kuelekea Kuala Lumpur ikitokea mjini Amsterdam, Uholanzi.
 
Kuna taarifa zisizo rasmi kuwa ndege hiyo ‘imetunguliwa’ na aidha majeshi ya Ukraine, ama waasi wanaoiunga mkono Urusi, vyanzo mbalimbali vya habari vimeripoti.
 
Waokoaji wamesema miili imeokotwa katika eneo la umbali unaozidi kilometa 15 toka ndege ilipoanguka.
 
“Hatuwezi kuthibitisha kama ndege hiyo imetunguliwa ama la,” alisema Rais wa Ukraine Petro Poroshenko.
 
“Hata hivyo, tunasisitiza kuwa Ukraine haijarusha makombora yoyote angani leo,” aliongeza.
 
Katika taarifa iliyotolewa mapema leo, Malaysian Airlines ilidai ilipoteza mawasiliano na ndege hiyo mnamo saa 8 na dakika 15 GMT.
 
Tovuti ya The Guardian inaripoti kuwa vyanzo toka ndani ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Ukraine vinadai ndege hiyo ilitunguliwa na kombora toka mfumo wa kurusha roketi hewani unaojulikana kama BUK.
 
Teknolojia ya BUK ilikuwa maarufu sana Urusi miaka ya 1970, na ilirithiwa na bado yaendelea kutumika na zile zilizokuwa Jamhuri za Kisovieti, ikiwamo Ukraine.
 
Wachambuzi sasa wanahoji walorusha kombora hilo wamelipataje, huku baadhi wakidai hiyo ni uthibitisho tosha kuwa waasi wanaoiunga mkono Urusi wako nyuma ya ‘shambulizi’ hilo.
 
Kati ya watu 295 walokuwa ndani ya ndege hiyo aina ya Boeing 777, 280 walikuwa abiria na walobaki ni wahudumu na marubani.
 
Picha zilizotupwa katika mitandao ya kijamii na tovuti mbalimbali zinaonyesha masalia ya ndege hiyo yenye rangi za bluu na nyekundu yakifuka moshi.


Picha hizo zimeamsha hisia kali, zikiukumbusha umma kuhusu ajali nyingine inayohusisha ndege ya Malaysia namba MH370 ilopotea toka Machi, huku ikiwa haijaonekana.
 
Mataifa mbalimbali yanaendelea na jitihada za kutathmini kama raia wake walikuwamo ndani ya ndege ‘ilotunguliwa,’ huku baadhi ya mashirika ya ndege, ikiwemo Emirates, Lufthansa, British Airways na Aeroflot, yakisitisha safari zote kwenya anga la Ukraine.

Chanzo: Mwananchi

Hii ndiyo idadi ya waliokufa ajali kati ya Januari-Juni 2014

mpinga
Kamanda Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga akiweka mambo hadharani
  TATHIMINI YA MATUKIO YA AJALI ZA
 BARABARAN JAN-JUNE 2013/2014

Takwimu zinaonyesha kuwa juhudi zetu zimefanikiwa kwa kupunguza ajali na majeruhi, ingawa kuna ongezeko la watu waliofarika katika ajali kwa Jan – June 2014.
S/N0
JAN-JUNE 2013 JAN –JUNE 2014 ONG/PUNG (%)
1 IDADI YA AJALI 11,311 8,405 -          2,906     (26%)
2 VIFO 1,739 1,743                  4   (0.2%)
3 MAJERUHI 9,889 7,523 -          2,366     (24%)


 MIKOA ILIYOONGOZA KWA AJALI ZA BARABARANI KIPINDI JAN-JUNE 2014:-

i)        Kinondoni   – idadi ya ajali      2,140 (25.5%)
ii)      Ilala              - idadi ya ajali – 1,561 (18.6%)
iii)    Temeke      - idadi ya ajali – 1,351 (16.1%)
iv)    Morogoro     –  idadi ya ajali – 514 (6.1%)
v)      Kilimanjaro – idadi ya ajali – 332 (4%)

Kwa mkoa wa DSM peke yake ni ajali 5,052 ( 60.2%)

MIKOA ILIYOONGOZA KATIKA KUPUNGUZA IDADI
YA AJALI ZA BARABARANI KIPINDI JAN-JUNE 2013/2014

MKOA Jan-June 2013 Jan-June 2014 Punguzo

Kinondoni 3059 2140      919 (30%)

Pwani 738 303      435 (59%)

Arusha 563 164      399 (71%)
4 Kilimanjaro 697 332      365 (52%)
5 Morogoro 631 514      117 (19%)

    TAKWIMU ZA MAKUNDI YALIYOATHIRIKA
NA AJALI ZA BARABARANI KIPINDI JAN-JUNE 2013/2014.

     JAN-JUNE 2013 JAN- JUNE 2014      TOFAUTI
KUNDI VIFO MAJERUHI VIFO MAJERUHI VIFO MAJERUHI
MADEREVA 124 725 117 527 -7 -198
ABIRIA 476 4,112 529 3,135 53 -977
W/PIKIPIKI 359 2,460 358 1,928 -1 -532
W/BAISKELI 202 560 177 304 -25 -256
W/MIGUU 550 1,926 548 1,603 -2 -323
W/MIKOKOTENI 28 106 14 26 -14 -80
JUMLA 1,739 9,889 1,743 7,523 4 -2,366
AJALI ZA PIKIPIKI- JAN-JUNE 2013/2014.
 Takwimu zinaonyesha kuwa tumeweza kupunguza ajali, vifo na majeruhi katika ajali za Pikipiki kwa kipindi cha Jan-June 2013 ikilinganishwa na Jan- June 2014.
Jan-June       2013 Jan-June 2014 ONG/PUNG
IDADI YA PIKIPIKIZILIZOHUSIKA 3,720 3,170 -          550 (15%)
IDADI YA AJALI 3016 2402 -          614 (20%)
VIFO 457 423 -          34 (7%)
MAJERUHI 2963 2301 -          662 (22%)

Hemed, Senga waonja Pishi la Kajala

MSANII nyota wa filamu nchini Hemed Suleiman anatarajiwa kuonekana katika kazi mpya ya Kajala Masanja iitwayo 'Pishi'.
Filamu hiyo miongoni mwa filamu tatu zilizoandaliwa na mwanadada huyo kupitia kampuni yake ya Kay Entertainment na imewashirikisha wasanii wengine nyota wakiwamo wachekeshaji mahiri nchini Senga, Asha Boko, Tausi na Mzee Onyango.
Akizungumza na MICHARAZO, Kajala alisema tofauti na filamu yake anayotarajia kuiachia hivi karibuni ya 'Laana', ndani ya Pishi ni ucheshi mtupu na yeye mwenyewe akiicheza kikomedi.
"Wengi wanadhani Kajala ni sistaduu aliyezoea kucheza filamu za kimapenzi tu, ndani ya 'Pishi' ni vunja mbavu mwanzo mwisho ikikusanya 'vichwa' adimu kama Asha Boko, Senga, Onyango na wengine," alisema.
Alidokeza filamu hiyo mpya itatoka mwishoni mwa mwezi ujao ili kutoa nafasi ya filamu yake ya 'Laana' iliyoigizwa na wasanii kama Ahmed Salim 'Gabo', Mama Sonia, Mama Kawele na Pastor Myamba kupata nafasi sokoni.

Toni Kroos atambulishwa Real Madrid

Done deal: Kroos holds up his No 8 shirt at his unveiling in Madrid
Toni Kroos akiwa na jezi yake mpya ya Real Madrid

Golden boy: The former Bayern Munich man was integral during Germany's World Cup triumph
Kroos akipiga akionyesha maufundi yake

MCHEZAJI Toni Kroos amekamilisha uhamisho wake wa Pauni Milioni 24 kujiunga na Real Madrid kutokea kwa mabingwa wa Ujerumani, Bayern Munich.
Bayern walitangaza jana usubuhi kuwa wamefikia makubaliano na Real juu ya mchezaji huyo na uhamisho utafanyika mara moja.
Mkataba wa Kroos ilikuwa unamalizika majira ya kiangazi mwakani na mshindi huyo wa Kombe la Dunia amesaini mkataba wa miaka sita katika dimba la Santiago Bernabeu.
Kroos alitambulishwa rasmi jana na hapa chini ni baadhi ya picha zilizopigwa katika utambulisho wake ndani ya dimba la Bernabeu.
Kroos ametua Real akiiacha kwenye mataa klabu ya Manchester United iliyokuwa ikimfukuzia.

DIEGO COSTA AJIFUNGA MITANO DARAJANI

MSHAMBULIAJI wa Atletico Madrid, Diego Costa amekamilisha usajili wa kujiunga na Chelsea kwa kusaini mkataba wa miaka mitano na klabu hiyo ya London.
Ada ya uhamisho ya mshambuliaji huyo inaaminika kuwa ni paundi milioni 32.
"Nina furaha sana kujiunga na Chelsea," alisema Costa. "Kila mmoja anafahamu kwamba hii ni klabu kubwa katika ligi ya ushindani mkubwa na nina furaha sana kuanza maisha mapya nchini England."
Costa anakuwa mchezaji wa tatu kutua Chelsea kufuatia kusajiliwa kwa Cesc Fabregas kutoka Barcelona na Mario Pasalic (19) kutoka klabu ya Croatia ya Hajduk Split.
Mshambuliaji huyo alifunga magoli 36 katika mechi 52 alizochezea Atletico Madrid msimu uliopita ambao walitwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Hispania kwa mara ya kwanza tangu 1996 na walifika hatua ya fainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
BBC

Ze Gunners wazidi kujiimarisha England

Striking a pose: Debuchy said he was excited to be playing Champions League football again
KLABU ya Arsenal imezidi kujiimarisha kwa kumsajili beki wa kulia wa Ufaransa, Mathieu Debuchy kutokea klabu ya Newcastle United.
Debuchy, 28, amesajiliwa kwa nia ya kuziba pengo la beki wa kulia, Mfaransa mwenzake, Bacary Sagna aliyetimka Emirates na kujiunga na mabingwa wa Ligi Kuu, Manchester City majira haya ya kiangazi mwaka huu.
Debuchy alijivunia usajili huo na akasisitiza kuwa umuhimu wa ligi ya mabingwa ndio kichocheo cha yeye kujiunga na Asernal.
“Najivunia kujiunga na klabu kubwa kama hii na kuvaa rangi zake, ni moja ya klabu kubwa zaidi duniani,” beki huyo wa kulia aliuambia mtandao wa Asernal.com.
“Naangalia mbele nikiwa na Aserne Wenger na kuisaidia timu kuendeleza mafanikio ya msimu uliopita ya kutwaa kombe la FA”.
“Kucheza tena ligi ya mabingwa ni furaha kubwa kwangu na nitajitahidi kadri ya uwezo wangu kuisaidia Asernal kushindania kombe”
Debuchy amewasili  Arsenal kurithi mikoba ya Bacary Sagna ambaye hakuonesha kiwango kikubwa katika fainali za Kombe la Dunia akiwa na Ufaransa.
Kutua kwa mcjhezaji huyo kumekuja siku chache baada ya kumnasa mshambuliaji nyota wa Barcelona, Alexis Sanchez kutoka Chile.