Kocha Marcio Maximo |
Kikosi cha Yanga |
IMEFAHAMIKA
kuwa wachezaji watatu wa kigeni wa klabu ya Yanga kiungo Haruna
Noyinzima na washambuliaji wawili wa kimataifa wa Uganda Hamisi Kiiza
Diego na Emmanuel Okwi hatima yao ya kuendelea kuitumikia klabu hiyo
yenye maskani yake katika makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani iko
mikononi mwa kocha mpya wa klabu hiyo Mbrazil Marcio Maximo.
Habari
zilizoifikia rockersports kutoka kwa mmoja wa viongozi wa klabu hiyo
ambaye hakutaka jina jina lake kutajwa mtandaoni humu, amesema ujio wa
wachezaji wawili kutoka nchini Brazil mshambuliaji Geilson Santos
Santana "Jaja" na Kiungo mshamabuliaji Andrey Marcel Ferreira Coutinho
kunawaondoa mmoja wa wachezaji wa kigeni kutoka ukanda huu wa Afrika
mashariki kwa kuwa wachezaji hao wa Brazil walioletwa na Maximo si wa
majaribio bali wamekuja kufanya kazi.
Chanzo
hicho kimesema kwa mujibu wa kanuni za usajili za shirikisho la soka
nchini TFF ni dhahiri wachezaji wa kigeni wanatakiwa watano na mpaka
sasa Yanga imefikisha idadi ya wachezaji saba hivyo basi kuna hatari
kati ya Niyonzima na Okwi mmoja akaondoka Jangwani msimu huu.
Taarifa
zaidi zinasema kumekuwepo na mazungumzo yanayo endelea baina ya
wachezaji hao na kamati ya usajili ya klabu hiyo ambayo kimsingi
yanagusa juu ya namna ya kumalizana nao huku zoezi hilo likikumbwa na
presha kubwa kutoka kwa mashabiki wa klabu hiyo.
Rockersports
No comments:
Post a Comment