STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, January 19, 2014

Yanga sasa kumaliza na Simurq PIK kesho Uturuki


Na Baraka Kizuguto, Uturuki
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Young Africans kesho jumatatu saa 8 mchana kwa saa za nchini Uturuki sawa na saa 9 kamili kwa saa za Afrika Mashariki itashuka dimbani kucheza mchezo wake wa mwisho wa kirafiki dhidi ya timu ya Simurq PIK inayoshiriki Ligi Kuu nchini Azerbajain katika viwanja vya Side Manavgat.
Kocha mkuu wa Young Africans mholanzi Hans Van Der Plyum amesema watautumia mchezo huo kama sehemu ya mwisho ya maandalizi ya kujianda na Ligi Kuu ambayo inatarajiwa kuanza mwishoni mwa wiki ijayo ambapo watoto wa jangwani watafugua dimba dhidi ya Ashanti United uwanja wa Taifa.
Mchezo wa kesho utakua mgumu pia, kwani timu ya Simurq PIK ina wachezaji wazuri ambao wanatoka sehemu mbali mbali dunianina ipo katika nafasi ya tano katika msimamo wa Ligi Kuu nchini kwao, hivyo nadhani kitakua kipimo kizuri cha mwisho kabla ya kurejea nchini Tanzania
Akiongelea kikosi chake mara baada ya mazoezi ya asubuhi, Hans amesema anashukuru mungu maendeleo ya timu ni mazuri, mabadiliko yapo na wachezaji wanaonekana kumuelewa hivyo anaamini kadri siku zinavyokwenda timu itakua katika kiwango kizuri zaidi.
"Nimeshashuhudia michezo miwili mmoja tukishinda 2-0 dhidi ya timu ya Altay SK Lidi Daraja la pili Uturuki na jana tukitoka sare ya 0-0 dhidi ya timu ya KS Flumartari ya Ligi Kuu Albania, kwa kweli nawapongeza vijana wanaonyesha kweli wanajua wajibu wao na kucheza kwa kufuata maelekezo ya walimu" alisema Hans.
Aidha Hans amesema ni jambo njema timu imecheza jumla ya michezo mitatu, ikishinda miwili na kutoka sare mchezo mmoja, huku ikifunga mabao 5 na kutokuruhusu nyavu zake kutikisika hii yote inayonyesha timu imeiva tayari kwa mashindano yanayotukabili.
Mpaka sasa hakuna mchezaji majeruhi hata mmoja kufuatia kiungo Hassan Dilunga kupona malaria na kuungana na wenzake katika mazoezi.

Olaba ampotezea Maguri, adai anawaamini vijana alionao

http://images.supersport.com/2014/1/AFC-Tom-Olaba-1-300.jpg
Kocha Tom Oloba

Elias Maguri aliyetimkia Umangani
KOCHA mpya wa Ruvu Shooting, Mkenya Tob Olaba amempotezea kiaina mshambuliaji nyota wa timu hiyo aliyetimkia Umangani, Elias Maguri, akisema asingependa kumjadili kwa sababu anawaamini vijana alionao watambeba kwenye mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara inayoanza duru la pili wikiendi ijayo.
Pia alisema kikosi chake hakitacheza mchezo wowote kwa sasa badala yake atautumia muda uliosalia kabla ya kuanza kwa duru la pili la ligi kurekebisha makosa aliyoyaona kwenye michezo mitatu ya kirafiki waliyocheza ili Alhamis waifuate Prisons-Mbeya wakiwa kamili gado.
Akizungumza na MICHARAZO, Olaba aliyetua katika klabu hiyo kuziba nafasi ya Charles Boniface aliyehamia Yanga kama kocha msaidizi, alisema hapendi kuwazungumzia Maguri na Ally Kani waliotimikia nje ya nchi kwa sababu hajawahi kuwanoa tangu atue kikosini hivyo hajui ubora na udhaifu wao.
Olaba alisema kadhalika huwa ana kawaida ya kumuamini mchezaji yeyote anayejituma na kujitambua hivyo vijana aliowakuta na kuanza kujipanga upya pamoja anawaamini watafanya kazi zote kwa manufaa ya Ruvu hivyo hakuna haja ya wadau wa Ruvu kuwafikiria akina Maguri.
"Sijawahi kumuona wala kujua uwezo alionao Maguri au huyo Kani, hivyo sitaki kuwajadili kwa sasa kwa vile nawaamini vijana nilionayo wanaweza kazi na kuisaidia Ruvu, kwangu kila mchezaji ana nafasi sawa mradi tu wajitume na kuisaidia timu," alisema.
Alisema kuanzisha mjadala wa akina Maguri klama wameacha pengo au la ni kutaka kuiyumbisha timu kwa kuwakatisha tamaa wachezaji waliopo aliowasifia kuwa ni wakali na waliomkuna wakimpa matumaini ya kumfikisha kule anakopataka kama kocha mkuu wa timu hiyo.
Kuhusu maandalizi ya mechi yake ya fungua dimba itakayochezwa dimba la Sokoine Mbeya, Olaba alisema hatacheza tena mechio yoyote ya kujipima nguvu kwa sasa kwa vile walizocheza zinatosha na badala yake atajikita katika kurekebisha makosa aliyoyagundua ili kwenda kuivaa Prisons wakiwa wamekamilika.
"Tutakuwa tukirekebisha kila baada ya mchezo mmoja wa Ligi Kuu, kwa sasa namalizia dosari chake hasa suala la pumziko na umakini kwa wachezaji ili tuende kuivaa Prisons tukiwa na uhakika wa kuzoa pointi zote tatu kabla ya kuangalia mechi itakayofuata baada ya hapo," alisema Olaba kocha wa zamani wa Mtibwa na klabu kadhaa za nchini Kenya ikiwamo timu ya taifa, Harambee Stars.
Elias Maguri ndiye aliyekuwa mfungaji bora wa klabu yake ya Ruvu Shooting akiwa na magoli 9 kwenye Ligi Kuu nyuma ya kinara, Amissi Tambwe wa Simba mwenye mabao 10, na kukosekana kwake kunaelezwa kama kunaweza kuiadhiri timu hiyo katika mechi za duru la pili chini Olaba.

Hilo ndilo Baraza Jipya la Mawaziri Tanzania

Capture
Rais Jakaya Kikwete

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amewahamisha na kuwateua baadhi ya Mawaziri na Naibu Mawaziri kama ifuatavyo:-
OFISI YA RAIS
Hakuna mabadiliko.

OFISI YA MAKAMU WA RAIS
Waziri wa Nchi (Muungano) – Hakuna mabadiliko
Mhe. Eng. Dr. Binilith Satano MAHENGE (Mb)
Waziri wa Nchi (Mazingira).
Mhe. Ummy Ali MWALIMU (Mb)
Naibu Waziri

OFISI YA WAZIRI MKUU
Hakuna mabadiliko

WIZARA
WIZARA YA FEDHA
Mhe. Saada Mkuya SALUM (Mb) – Waziri wa Fedha
Mhe. Mwigulu Lameck NCHEMBA (Mb) – Naibu Waziri wa Fedha
Mhe. Adam Kighoma Ali MALIMA (Mb)- Naibu Waziri wa Fedha

WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
Hakuna mabadiliko

WIZARA YA KATIBA NA SHERIA
Mhe. Dkt. Asha-Rose Mtengeti MIGIRO (Mb)-Waziri wa Katiba na Sheria
Naibu Waziri – Hakuna mabadiliko

WIZARA YA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI
Hakuna mabadiliko

WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA
Waziri – Hakuna mabadiliko
Mhe. Janet Zebedayo MBENE (Mb) – Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara

WIZARA YA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA
Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi (Mb)- Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

WIZARA YA UJENZI
Hakuna mabadiliko

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
Mhe. Mathias Meinrad CHIKAWE (Mb)- Waziri wa Mambo ya Ndani
Naibu Waziri – Hakuna Mabadiliko

WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII
Mhe. Dkt. Seif Seleman RASHIDI (Mb)- Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii
Mhe. Dkt. Kebwe Stephen KEBWE (Mb)- Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
Waziri: Hakuna mabadiliko
Mhe. Jenista Joakim MHAGAMA (Mb) – Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi

WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO
Waziri: Hakuna mabadiliko
Mhe. Dkt. Pindi Hazara CHANA (Mb) – Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto

WIZARA YA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI
Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Dismas KAMANI (Mb) – Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
Mhe. Kaika Saning’o TELELE (Mb)- Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi

WIZARA YA KAZI NA AJIRA
Hakuna mabadiliko

WIZARA YA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA
Hakuna mabadiliko

WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI
Waziri – Hakuna mabadiliko

Mhe. George Boniface Taguluvala SIMBACHAWENE (Mb) – Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
WIZARA YA MAJI
Waziri – Hakuna mabadiliko
Mhe. Amos Gabriel MAKALLA (Mb)- Naibu Waziri wa Maji

WIZARA YA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA
Waziri – Hakuna mabadiliko
Mhe. Godfrey Weston ZAMBI (Mb) – Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika

WIZARA YA UCHUKUZI
Hakuna mabadiliko

WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO
Waziri – Hakuna mabadiliko

Mhe. Juma Selemani NKAMIA (Mb) – Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
Mhe. Lazaro Samuel NYALANDU (Mb)-Waziri wa Maliasili na Utalii
Mhe. Mahmoud Hassan MGIMWA (Mb)-Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii

WIZARA YA NISHATI NA MADINI
Waziri – Hakuna mabadiliko
Naibu Waziri (Madini) – Hakuna mabadiliko

Mhe. Charles Muhangwa KITWANGA (Mb)
Naibu Waziri (Nishati)

Balozi Ombeni Y. Sefue
KATIBU MKUU KIONGOZI
Ikulu
DAR ES SALAAM

19 Januari, 2014

KILICHOFANYIKA

- Hakuna Mabadiliko Ofisi ya Rais
- Ofisi ya Makamu Wa Rais - Naibu Waziri Kitwanga amehamishwa na nafasi yake imejazwa na Mhe. Ali Mwalimu.
- Mwigulu Nchemba amekuwa Naibu Wizara ya Fedha (Sera). Aliyekuwa nafasi hiyo sasa ni Waziri Kamili.

- Uchumi na Mapato sasa anatoka Janet Mbene na inajazwa na Adam Malima.
- Asharose Migiro sasa ni Waziri wa Katiba na Sheria.
- Ulinzi na Kujenga Taifa => Hussein Mwinyi.
- Mambo ya Ndani - Mathias Chikawe.
- Afya na Ustawi wa Jamii - Naibu wake sasa ni Waziri Kamili; naibu wa sasa ni Dr. Kebwe S. Kebwe.

- Mulugo ameondoshwa rasmi serikalini. Nafasi yake imejazwa na Jenista Muhagama.

- Pindi Chana amejaza nafasi ya Ummi Mwalimu - Jinsia na watoto.
- Mifugo na Maendeleo ya Mifugo - Titus Kamani atakuwa Waziri mpya. Naibu ni Telele na hivyo Wizara nzima imepata mawaziri wapya.

- Ole Medeye OUT - Simbachawene kachukua nafasi yake (Naibu wa Prof. Tibaijuka).
- Naibu Kilimo - Godfrey Zambi.
- Habari - Naibu ni Juma Nkamia.
- Nyalandu amekuwa Waziri Kamili. Naibu ni Mahmood Hassan Mgimwa.

- Muhongo na Naibu wake wamebakizwa. Nishati atachukua Charles Kitwagwa akiichukua toka kwa Simbachawene.