STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, March 2, 2013

Real Madrid yaizima tena Barcelona

 
KIKOSI cha vijana wa Jose Mourinho 'The Only One' kimeendeleza ubabe kwa vinara wa Ligi Kuu ya Hispaniam Barcelona baada ya jioni ya leo kuitandika mabao 2-1, ikiwa ni siku chache tangu waing'oe kwenye michuano ya Kombe la Mfalme kwa kipigo cha mabao 3-1.
Bao la mapema la Karim Benzema na lile la kipindi cha pili la Sergio Ramos yalitosha kuipa Real ushindi wa pointi tatu na kujaribu kupunguza pengo la pointi dhidi ya wapinzani wao hao wa jadi wanaoongoza msimamo wakiwa mbele ya pointi 13 wakiwa na 68 dhidi ya 55 za Real kwa sasa.
'Mchawi Mweupe' Lionel Messi aliifungia Barcelona bao la kufitia machozi katika dakika ya 18 ambalo hata hivyo halikuweza kufuta uteja kwa kikosi chake kilichokuwa uwanja wa ugenini, siku chache baada ya kulala nyumbani Nou Camp.

Polisi Moro, JKT Oljoro hakuna mbabe

Kikosi cha Polisi Morogoro

TIMU za maafande za Polisi Moro na JKT Oljoro jioni ya leo zimeshindwa kutambiana baada ya kutoka suluhu kwenye mechi pekee ya Ligi Kuu Tanzania Bara iliyochezwa kwenye uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Kwa sare hiyo Polisi Moro imeendeleza rekodi ya kutopoteza mechi yoyote katika duru la pili na kujiongezea pointi moja na kufikisha 16, ikijiondoa eneo la hatari.

BREAKING NEWS: ABIRIA ZAIDI YA 50 WANUSURIKA KUFA AJALI YA BASI MBOZI






ZAIDI YA ABIRIA 50 WA BSI LA SUMRY LITOKALO SUMBAWANGA KUJA MBEYA LIMEPATA AJALI MAENEO YA SONGWE MPAKANI MWA WILAYA YA MBOZI CHANZO CHA AJALI HIYO NI KUWA ROLI LA MIZIGO LA KAMPUNI YA KANJILAJI LILIKUWA LINAIPITA GARI NYINGINE HIVYO KUHAMIA UPANDE WA BASI LA SUMRY NA NDIPO DEREVA WA SUMRY AKAONA KUA WATAGONGANA USO KWA USO AKAAMUA KULIINGIZA SHAMBANI ILI KUJIOKOA KATIKA AJALI HIYO













 MOJA YA MAJERUHI BENO GILBET MKAZI WA ZANZIBAR ALIKUWA ANATOKEA SUMBAWAGA KWENDA ZANZIBAR SASA AMELAZWA KATIKA HOSPITALI YA TEULE YA IFISI

MAJERUHI MUSA KAPINUKE



MAJERUHI CHALES KAUZENI  15

MUUGUZI ELMAT KAKAKU AMESEMA WAMEPOKEA MAJERUHI 47 KATI YA HAO WAWILI WAMEPELEWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA BAADA YA HALI ZAO KUWA MBAYA ZAIDI




HABARI KAMILI YA AJALI HII TUTAWAFAHAMISHA BADO TUNAFUATILIA

PICHA NA MBEYA YETU

KUMEKUCHA PAMBANO LA SIMBA, LIBOLO KESHO


 


·       Liewig aahidi kupambana hadi mwisho

·       Poppe aahidi mamilioni kwa wachezaji

·       Kapombe asema Sunzu atawaua Waangola

Na Ezekiel Kamwaga, Kwanza Sul, Angola

KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Jean Elysee Liewig, amesema ana matumaini timu yake itapata matokeo mazuri katika mchezo wa kesho baina ya Wekundu wa Msimbazi na Libolo ya Angola.

Mechi hiyo imepangwa kuchezwa kesho kuanzia saa tisa alasiri katika Uwanja wa Estadio Libolo, uliopo katika mji mdogo wa Calulo jimbo la Kwanza Sul.

Katika mechi ya kwanza baina ya timu hizo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam wiki mbili zilizopita, Simba ilifungwa 1-0 na mabingwa hao wa Angola.

Hata hivyo, Liewig alisema ingawa matokeo ya kufungwa nyumbani hayakuwa mazuri, ana imani Simba nayo inaweza kufanya vizuri ugenini.

“Kama wao walitufunga kwetu kwanini sisi tusiwafunge kwao. Ukiangalia kwenye ile mechi ya kwanza wao walipata nafsi moja tu ya maana na wakaitumia. Sisi tulipata nafasi kama tatu hivi na hatukutumia vizuri hata moja,” alisema.

Liewig alisema ameridhishwa na ari na mazoezi mazuri ambayo Simba imefanya kwa wiki nzima kujiandaa na mechi hiyo na kwamba kuna dalili kuwa timu yake inaweza kufanya lisilotarajiwa.

Akizungumza na wachezaji katika kikao kilichofanyika katika Hoteli ya Anisaan Ritz ambako Simba imefikia, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba, Zacharia Hans Poppe, alitoa ahadi ya Sh milioni 10 iwapo watafanikiwa kuitoa Libolo.

Aliwataka wachezaji wa Simba kuwakumbuka mamilioni ya washabiki wao waliopo Tanzania ambão hawalali wala kula vizuri wakati timu yao kipenzi inapokuwa na matokeo mabaya.

Poppe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba na pia kundi la Friends of Simba, alisema ana imani kubwa na wachezaji wa timu yake kwa vile ndiyo bora Tanzania na kama wataamua kucheza kwa nguvu zao zote, matokeo mazuri yanawezekana.

“Nyie ni wachezaji wazuri sana. Kama nyote mtacheza kama timu na mkacheza kwa uwezo wenu wote, ni wazi kwamba mnaweza kuibuka na ushindi,” alisema.

Akizungumzia mechi ya kesho, nahodha msaidizi wa Simba, Shomari Kapombe, alisema mechi baina yao na Libolo itakuwa tofauti na ya kwanza kwa sababu ya kuwepo kwa mshambuliaji Mzambia, Felix Sunzu.

“Tulimkosa sana Sunzu kwenye mechi ya Dar es Salaam. Mipira ilikuwa haikai kule mbele na hilo lilikuwa tatizo kubwa, kubwa sana na hiyo ni kwa sababu Sunzu hakuwepo. Nadhani sasa tuna nafasi zaidi kuliko mara ya kwanza,” alisema.
Wakati huo huo Mwamuzi Nhleko Simanga Pritchard kutoka nchini Swaziland ambaye alichezesha mechi baina ya Wekundu wa Msimbazi na Al Ahly Shandi ya Sudan mwaka jana, ndiye atakayechezesha mechi ya kesho dhidi ya Libolo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyopatikana kutoka Chama cha Soka cha Angola leo asubuhi, mwamuzi huyo atasaidiwa na na wenzake Mkhabela Bhekisizwe, Mbingo Petros na Fabudze Mbongiseni ambão wote wanatoka Swaziland.

Kati ya hao, ni Nhleko na Petros pekee ambão ndiyo waliochezesha mechi ya Shandi ambayo Simba iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 yaliyofungwa na Haruna Moshi (77), Patrick Mafisango ambaye sasa ni marehemu (88) na Emmanuel Okwi (90).

Wachezaji wote hao watatu waliofunga katika pambano hilo hawatacheza katika mechi ya Libolo kwa sababu tofauti. Mafisango alifariki kwa ajali siku mbili baada ya kurejea kutoka Sudan kwenye mechi ya marudiano ambako Simba ilitolewa.

Okwi amehamia katika klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia na Boban ameshindwa kusafiri na timu kwenda Angola kwa sababu ya kushikwa na malaria kali.

Kamisaa wa pambano hilo lililopangwa kuanza majira ya saa tisa kamili kwa saa za hapa (sawa na saa 11 jioni kwa saa za Tanzania) anatarajiwa kuwa Mandla Mazibuko kutoka nchini Afrika Kusini.
KATIKA hatua nyingine BENCHI la ufundi la Simba SC jana limeukagua Uwanja wa Estadio Libolo itakakochezwa mechi ya kesho ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baina ya Wekundu na Libolo na kubaini siri nzito.
Vipimo vya Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Liewig, vilibaini kwamba uwanja huo una upungufu wa takribani mita sita kwa urefu na upana kulinganisha na viwanja vingi vya soka.

Kwa mujibu wa Liewig, uwanja huo umepunguzwa ukubwa ili kusaidia timu ya Libolo ambayo inafahamika sana kwa kufunga mabao mengi ya mipira iliyokufa (adhabu, kurusha n.k).

“Kutokana na hali hii, maana yake ni kwamba kila itakapokuja kona, itakuwa hatari kwa sababu kuna umbali mdogo kutoka kwenye kona hadi goli. Itakuwa hatari hivyohivyo kwenye mipira ya kurusha na ya adhabu. Ni muhimu tumeliona hili mapema,” alisema.

Alisema atawaeleza wachezaji wake kujiepusha kutoa kona au mipira ya kurusha bila ya sababu kwa vile inaonekana hiyo ndiyo silaha kubwa ya wapinzani hao wa Simba.

“Kama unakumbuka, hata goli lao la Dar lilitokana na mpira wa kurusha halafu ikapigwa krosi. Ndiyo maana nafikiri wameleta mechi hii huku badala ya Luanda ili watumie faida hii vizuri,” alisema.

Nchini England, Uwanja wa Britannia unaotumiwa na timu ya Stoke City inayocheza Ligi Kuu ya nchi hiyo unafahamika pia kwa kuwa mdogo kwenye eneo la kuchezea kuliko viwanja vingi vya nchi hiyo.

Hata hivyo, inaelezwa kwamba lengo kuu la kuuweka uwanja huo katika eneo hilo ni kutumia nguvu ya mipira ya kurusha na adhabu nyingine ambayo ndiyo silaha kubwa ya Stoke. Miaka miwili iliyopita, robô ya magoli yaliyokuwa yakifungwa na timu hiyo yalitokana na mipira ya kurusha ya Rory Delap.
NB: KAMWAGA anapatikana kutoka Angola kwa namba +244 946 273765
 

TFF YAOMBA KUMKABILI WAZIRI KUHUSU KATIBA

Rais wa TFF, Leodger Tenga
Na Boniface Wambura
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesema ipo haja kwa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara kufikiria upya uamuzi wake wa kutengua usajili wa Katiba ya TFF ya mwaka 2012 na kutaka itumike ya mwaka 2006, kwani hautekelezeki.

Akizungumza na waandishi wa habari leo mchana, mara baada ya kikao cha Kamati ya Utendaji, Rais wa TFF, Leodegar Tenga amesema ni muhimu jambo hilo likaangaliwa upya kwa sababu athari zake ni mbaya, na pengine Dk. Mukangara hakushauriwa vizuri kabla ya kufanya uamuzi huo.

“Kamati ya Utendaji ya TFF haitaki kubishana na Mheshimiwa Waziri hata kidogo, ila tunaamini wakati anatamka haya hakufahamu madhara yake, athari zake na ugumu wa utekelezaji wake. Kwa waliomshauri hili, wamemshauri vibaya,” amesema Rais Tenga.

Amesema rai ya TFF kwa Waziri ni kuwaita ili wamweleze ni kitu gani wafanye kunusuru mpira wa miguu wa Tanzania, kwani wanaamini jambo hili litakwisha baada ya kumwelimisha hasa kutokana na ukweli kuwa kabla ya kufanya uamuzi huo hakuwasikiliza.

Katika mkutano huo, Rais Tenga alianza kwa kusema kuwa TFF inaiheshimu sana Serikali, hivyo inaheshimu maagizo yaliyotolewa na Waziri, lakini akaongeza kuwa TFF ina wajibu wa kutoa ufafanuzi juu ya maagizo hayo.

Amesema lengo la kuelezea historia ya TFF ilikotoka ni kubaini migongano ya maagizo hayo na taratibu za TFF ambazo kwa bahati mbaya zinasigana na maagizo hayo.

Rais Tenga amesema TFF ni chombo cha wanachama, ambapo wanachama wake ni vyama vya mikoa, vyama shiriki na klabu za Ligi Kuu, na ina taratibu za kufanya uamuzi kwa mujibu wa Katiba yake na za wanachama wake ambazo zimeidhinishwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Amesema si TFF pekee, bali vyama vya nchi zote ambavyo vimeunganishwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), zinaheshimu na kufuata maagizo na miongozi ya shirikisho hilo la kimataifa la mpira wa miguu.

Rais Tenga amesema TFF haitakiwi kuingiliwa katika uongozi na uendeshaji wake, kwani jambo hilo likitokea rungu la FIFA litaiangukia TFF, na madhara yake ni makubwa. Miongozo ya FIFA inasisitiza uhuru wa wanachama wake katika uendeshaji shughuli za mpira wa miguu, na iko kwenye Katiba ya TFF.

“Sheria za nchi ndizo zilizozaa Katiba ya TFF. TFF ni chama kamili kinatakiwa kufanya uamuzi wake ili mradi uzingatie madhumuni ya kuanzishwa kwake. Leo TFF ikiacha mpira wa miguu na kuanza kujishughulisha na gofu, hapo Msajili ana haki ya kuingilia,” amesema Rais Tenga.

Kuhusu maagizo ya Waziri, Rais Tenga amesema kifungu cha 11 cha Sheria ya Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kinazungumzia usajili wa chama, na si marekebisho ya katiba, ingawa kanuni zinahusu marekebisho ambapo ameongeza kuwa uamuzi wa marekebisho ni wa Mkutano Mkuu na si Msajili.

“Ukienda kuomba viza, fomu unapewa na yule anayekupa viza. TFF tulipowasilisha marekebisho ya Katiba hatukupewa fomu. Msajili akasema sawa. Jambo la kujaza fomu si la TFF, ndiyo maana tunasema ipo haja ya jambo hili kufikiriwa upya.

“Usajili tayari umepita, kwamba Msajili hakutoa fomu, mwathirika anakuwaje TFF? Tunaona ni muhimu jambo hili likaangaliwa upya,” amesema Rais Tenga na kuongeza kuwa utaratibu wa kusajili Katiba ya 2006 ambayo ndiyo Waziri ameagiza itumike ulikuwa huo huo uliosajili Katiba ya 2012.

Akizungumzia historia ya TFF kutoka mikononi mwa BMT, Rais Tenga amesema ni zao za Katiba ya 2004 ambayo ilifanyiwa marekebisho ukumbini na kugongwa mhuri na Msajili hapo hapo na kuingia kwenye uchaguzi. Katiba hiyo ndiyo iliyoiondoa BMT kuisimamia TFF.

“Huko ndiko tulikotoka, si kwa kulazimishwa, bali kwa kupewa Katiba ya 2004. Katiba ina utaratibu mzima wa kufanya uamuzi. Maelekezo ya Waziri yamesahau huko tulikotoka siku nyingi. Uhalali wa marekebisho unatokana na ridhaa ya Mkutano Mkuu. Hiyo ni kwa mujibu wa Katiba yenyewe, hakuna nafasi ya BMT,” amesema.

Amesema katika maagizo ya Waziri, ameitaka TFF kufuata Katiba ya 2006 na kanuni za BMT, lakini Katiba hiyo hiyo ya 2006 haina nafasi ya BMT, na hata kama TFF ingetaka kutekeleza hilo haliwezekani.

“Kwa maagizo haya inaonekana Waziri kashauriwa vibaya. Tunajua hakuwepo katika nafasi hiyo (2004) wakati wa makubaliano kati ya Serikali na FIFA kuacha mpira wa miguu ujiendeshe wenyewe,” amesema Rais Tenga.

Pia amezungumzia umuhimu wa Katiba toleo la 2012, kwani kuna marekebisho mengi yalifanyika mwaka 2007, 2008, 2009 na 2011 ambapo ukiyafuta maana yake unakiweka pembeni Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA), Bodi ya Wadhamini, wanachama wapya (mikoa), Bodi ya Ligi, Kamati ya Rufani ya Uchaguzi, Leseni za Klabu na Kanuni za Fedha.

“Kwa uamuzi huu yote yaliyofanyika hayana maana. Waziri sidhani kama alikuwa anafahamu athari za maagizo yake. Kama angelijua asingefanya uamuzi huo. Si rahisi kurudi katika Katiba ya 2006. Hao wajumbe wa Katiba ya 2006 unawapata wapi? Maana yake hata vyama wanachama ni batili kwa vile vimerekebisha Katiba zao 2009 na 2010,” amesema Rais Tenga.

Amesema kwa Serikali kufuta, maana yake ni kutengua uamuzi wa TFF ambapo madhara yake ni nchi kufungiwa, ambapo timu za Taifa hazitacheza mpira, klabu hazitashiriki michuano ya kimataifa na wadhamini nao watakaa pembeni kwa vile hawawezi kudhamini timu ambazo hazishindani kimataifa.

“Dhana kwamba tukae tu tusicheze nje, ni dhana ya watu walio nje ya mpira wa miguu. Dhamira yetu ni kuhakikisha hatufungiwi. Waziri ametuagiza tupeleke barua FIFA kuwa ametengua marekebisho ya katiba. Hatupeleki hivyo, kwani hiyo ni Government interference, watatufungia.

“Nia yetu bado ni Waziri kutupa nafasi ya kutusikiliza,” amesema Rais Tenga na kuongeza kuwa kuhusu uchaguzi kwa vile FIFA wanakuja ombi la TFF kwa Waziri ni kuacha kwanza mchakato uendelee hadi ufike mwisho.

“FIFA wanakuja, tuwasubiri. Nilidhani utaratibu huo utaheshimika. Kama mtu wa mpira haitaki FIFA anataka nini? Ahadi yetu ni kuhakikisha watu wanapewa haki. Hiyo ndiyo ahadi yetu na tumeisimamia, na ndiyo maana FIFA wanakuja,” amesema.

Akijibu swali kuhusu waraka, Rais Tenga amesema marekebisho ya Katiba hayakufanywa kwa siri, ridhaa ya wajumbe wa Mkutano Mkuu kufanya marekebisho hayo kwa njia ya waraka ilipatikana ambapo 70 waliunga mkono na 33 walikataa.

Azam waenda Sudan Kusini kumalizia kazi

MSAFARA wa watu 30 wakiwamo wachezaji 20 na viongozi 10 wa klabu ya Azam wameondoka nchini afajiri ya leo kuelekea Sudan Kusini kwa ajili ya kumalizia kazi katika pambano la marudiano la Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji wao Al Nasir Juba.
Azam inatarajiwa kuvaana na Al Nasir kesho mjini Juba wakiwa na ushindi wa mabao 3-1 iliyopata katika mechi yao ya awali iliyochezwa nchini Tanzania wiki mbili zilizopita.Katibu Msaidizi wa Azam, Twalib 'Chuma' Suleiman, aliiambia MICHARAZO kikosi hicho kimeondoka alfajiri ya leo ikiwa na matumaini makubwa ya kwenda kuing'oa Al Nasir licha ya kukiri kwamba hawatadharau mchezo huo.
Chuma, alisema waliondoka katika msafara huo wa leo ni pamoja na wachezaji 20 wakiwamo makipa; Mwadini Ally na Aishi Manula, mabeki; Joackins Atudo, David Mwantika, Himid Mao, Malika Ndeule, Waziri Salum na Luckson Kakolaki.
Aliongeza wachezaji wengine ni viungo ni Kipre Balou, Jabir Aziz, Ibrahim Mwaipopo, Salum Abubakar, Humphrey Mieno, Abdi Kassim 'Babbi' na Khamis Mcha 'Vialli', huku washambuliaji wakiwa ni John Bocco 'Adebayor', Kipre Tchetche, Seif Abdallah, Brian Umony na Gaudence Mwaikimba 'Caroll'. 

Kwa upande wa uongozi msafara huo umeambatana na Katibu Mkuu, Nassor Idrissa, ambaye anakuwa mkuu wa msafara, Mameneja, Patrick Kahemela, Jemedari Said, Ibrahim Shikanda na Abubakar Mapwisa.
Benchi la ufundi linaoongozwa na kocha mkuu, John Stewart Hall na wasaidizi wake, Kally Ongalla na Idd Abubakar, pia wamo Dardenne Paul na Yusuf Nzawila.

Mwanamke ajipiga sindano 54 ili kukuza makalio yake











MWANAMKE mmoja nchini Marekani, ameeleza jinsi alivyonusurika kifo kufuatia hatua yake ya kuongeza makalio kwa kupiga sindano zenye kemikali mitaani.
Karmello mwenye umri wa miaka 23 kutoka mji wa Detroit, Michigan, anasema anasema amalizika kupiga sindano za kuongeza makalio 54 katika kipindi cha miaka mitatu ili kutimiza dhamira yake ya kuwa na mwili anaoutaka mwenyewe.
Anasema, kiasi cha sindano alichopiga ni sawa na lita kadhaa za maji, alitumia kiasi cha dola 15,000.
Kutokana na gharama kubwa ya kurekebisha mwili, Karmello alikuwa akifanya kazi hiyo kwa wataalamu wa mitaani, na kwamba alielezwa kama anahitaji zaidi kujenga makalio makubwa, apige sindano zingine 36.
Wakati wanawake wengine wamekuwa wakifanya hivyo kwa kufanyiwa upasuaji na kuongeza madini laini ya plastiki kwenye makalio, Karmello kwake ilikuwa tofauti kabisa, kwani yeye aliamua kupiga sindano.
Akieleza mkasa huo,  Karmello alisema kazi hiyo alikuwa akiifanya kupitia mtaalam mmoja mwanamke aliyekuwa akikutana naye kwenye hotel.
Karmello anasema ametumia kiasi kikubwa cha pesa kurekebisha makalio yake, na alikuwa akipata ushawishi zaidi kupitia kwa mwanadada mwingine aliyechanganyikia na kazi ya kuongeza makalio, Vanity Wonder.
Wonder, anadaiwa kutumia zaidi ya paundi 10,000 ili kujenga aina ya makalio aliyokuwa akiyataka.
Hata hivyo, dada huyo anasema alinusurikia kifo baada ya moja ya sindano aliyopiga kumpa maambukizo kwenye makalio.
Karmello anasema baada ya kuongeza makalio, aliamua kwenda kwa mtaalamu wa upasuaji wa kuongeza na kurekebisha mwili, Dr Anthony Youn, Karmello ambapo alimwambia hatari aliyonayo baada ya kuongeza makalio.
Uchunguzi wa Youn kupitia picha za  X-ray, zinaonyesha jinsi makalio ya mwanadada huyo yalivyo laini kama sponji na hiyo ni hatari kubwa kwake, kwani kama angepiga sindano zingine zingeweza kumsababishia kifo mara moja.
Karmello anaonye athari za kuongeza makalio kwa kutumia sindano akisema ni hatari sana.
“Kabla sijapiga sindano, makalio yangu yalikuwa saizi namba nne, lakini sasa niko kwenye saizi namba 10,” alisema mwanadada huyo.
“Nina furaha kwa sababu sikuwahi kuwa na makalio makubwa kama ilivyo sasa.
“Najisikia kama mwanamke aliyekamilika, mwenye umbo zuri na kuvutia. Kweli nina furaha kubwa kufanikisha hili.”
Mwanadada huyo anasema anajivunia kwa kiasi kikubwa umbo lake kwa sasa na jinsi anavyowateka watu wengi.
“Nimekuwa sehemu ya macho ya watu wengi kwa jinsi wanavyoniangalia kila nipitapo.
“Nimeweza kupata kile nilichokuwa nikihitaji katika maisha yangu kwa muda mrefu,’ alisema wakati akihojiwa katika kipindi maalum cha televisheni kinazungumzia maisha hali ya watu nchini Marekani
Kwa kawaida kazi ya kuongeza makalio hufanyika kwa kupiga sindano zenye silicon.
Karmella anasema alikuwa na rafiki yake, Vanity Wonder ambaye naye alikuwa kinara wa kuongeza makalio, na kuna wakati fulani ilibaki nusura apoteze maisha kutokana kuendekeza sana zoezi la kuongeza mwili.
Wakati wa kazi hiyo, Vanity hakujua kama anaweza kupata madhara makubwa kufuatia kuongeza mwili kupita kiasi mpaka alipopata tatizo kubwa lililotishia maisha yake.
Katika maelezo yake, Karmello alisema alikwenda kwa daktari na kumweleza dhamira yake ya kuongeza ukubwa wa makalio, na mtaalamu huyo alimweleza kwamba hilo ni jambo linalowezekana tena katika kipindi kifupi.


CHANZO:NIPASHE