STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, June 21, 2015

Kamara, Ngoma watua Jangwani kilaini, Azam Mmh!

http://taarifa.co.tz/wp-content/uploads/2015/05/donald-ngoma.jpg
Ngoma
http://api.ning.com/files/-hwEeqCyyzcUDSa8niMV*j4Gexh4YMQlbQbOpDDsm5bj8CsNc1iWuShfdoofoJoxVS3yme2QGbewS7taPYct0Vd6GrOaJlx*/2.JPG
Kamara mwenye jezi nyeusi akiwa na wachezaji wenzake wa Yanga
KAMATI ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limebariki ongezeko la wachezaji wa kigeni kutoka watano hadi saba na kwa maana hiyo imetoa fursa kwa wachezaji waliokuwa wakiwaniwa na Yanga, Donald Ngoma wa Fc Platimuz ya Zimbabwe na Lansana Kamara toka Sierra Leone kuwa na nafasi kubwa ya kukipiga Jangwani.
Kadhalika ongezeko hilo ambalo hata hivyo limeenda kinyume na maombi ya Umoja wa Klabu ya kutaka wachezaji wa kigeni wafikie 10, litazinufaisha Azam na Simba zilizokuwa zikiipigia debe ongezeko hilo. 
Ebu isome mwenyewe taarifa ya TFF juu ya maamuzi yao ya Kamati ya Utendaji iliyokutana jana visiwani Zanzibar

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI - RELEASE NO. 101
TAREHE 20 JUNI, 2015
MAAMUZI YA KAMATI YA UTENDAJI
Kamati ya Utendaji ya TFF imefanya kikao chake cha kawaida leo tarehe 20/06/2015 katika ukumbi wa Wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo kisiwani Zanzibar,

Baadhi ya maamuzi yake ni haya yafuatayo:

  1. TUNZO ZA VODACOM.
Baada ya kuzingatia  mapungufu yaliyojitokeza katika uteuzi wa tuzo za ligi kuu ya Vodacom msimu wa 2014/15, Kamati ya utendaji imeagiza Rais wa TFF aunde kamati maalum ya kusimamia mchakato wa utoaji wa tuzo za Vodacom. Kamati hii itazingatia umuhimu wa kuhusisha idara za ufundi za TFF katika zoezi hilo na wadhamini na ligi watahusishwa kwa ukaribu katika zoezi hili.

  1. KANUNI ZA LIGI 2015/16.
Kamati ya utendaji ilipitia rasimu ya kanuni za ligi kuu, FDL na SDL za msimu ujao wa 2015/16.
Mabadiliko makubwa yaliyofanywa ni kwenye maeneo yafuatayo:

  1. LESENI ZA VILABU.
Kamati ya utendaji imesisitiza kuwa hakuna klabu itakayopitishiwa usajili wake kama kupewa leseni ya klabu ya msimu.( Club Licencing).

  1. WAAMUZI.
Kamati ya utendaji imeridhia wazo la kamati ya maamuzi kuwa kuanzia msimu 2015/16 kutakuwa na jopo maalum ya waamuzi ( Elite referees) litakalochezeshwa mechi zote za ligi kuu.

Waamuzi hawa watakuwa ni 16 wa kati, 32 wa pembeni na 4 wa akiba. Hii itasaidia kuongoza ufanisi katika uamuzi. (refereeing).

  1. MGAWANYO WA MAPATO YA MILANGONI.
Vilabu vimeongezwa mgawanyo wa mapato  ya milangoni na sasa vitakuwa vinachukua asilimia 60% ya mapato ya mlangoni, makato mengine ni 18% VAT na 15% gharama za uwanja.

  1. UDHIBITI WA WACHEZAJI.
Kanuni ilikuwa inatoa fursa timu ya kuamua mechi ipi mchezaji asicheze baada ya kuwa na kadi tatu za njano imefutwa.

  1. KUSAJILI MIKATABA YA WACHEZAJI.
Kuanzia sasa mikataba kati ya wachezaji na klabu itakayotambuliwa na TFF itakuwa ni ile ambayo ni nakala halisi zilizopigwa muhuri na lakiri ya TFF  na kusajiliwa kwenye kumbukumbu ya TFF. Vilabu na mwachezaji watapewa nakala hizi baada ya  kusajiliwa na TFF.

  1. WACHEZAJI WA KIGENI.
Kamati ya utendaji imeamua kuwa kuanzia msimu 2015/16 idadi ya wachezaji wa kigeni watakaosajiliwa na klabu ya ligi kuu itakuwa 7 (saba) wachezaji wote hawa, wote wataruhusiwa kucheza kwa wakati wote.

Mikakati ya kusajiliwa wachezaji hawa ni haya yafuatayo:
  1. Mchezaji awe ni mchezaji wa timu za Taifa za nchi yake ( Senior, U23, U20, U19, U17 nk) au
  2. Mchezaji awe anacheza katika ligi kuu ya nchi yake au nchi nyingine wakati anasajiliwa.

  1. Kila mchezaji wa kigeni atakayesajiliwa atalipia ada ya maendeleo. Mpira wa vijana ya dola 2,000 kwa kila msimu atakyocheza hapa nchini. Fedha hizi zitapelekwa katika mfuko wa maendeleo ya mpira (Football Development Fund).

Pia imeamriwa kuwa mikataba ya vilabu na wachezaji iliyo hai itaendelea kutambuliwa na TFF. Na kwa wale ambao tayari wapo nchini wataruhusiwa  kuuhisha (to renew) mikataba yao iwapo watakubaliana na vilabu vyao.

4. LESENI ZA MAKOCHA
Kamati ya utendaji imeamua kuwa kuanzia msimu huu, Kocha wa timu ya ligi kuu sharti awe na leseni B ya CAF au itakayolingana nayo kutoka katika mashirikisho mengine duniani na kocha msaidizi awe na leseni C ya CAF, hii ni kwa misimu mitatu.
Kuanzia msimu wa 2018/2019 kocha wa Ligi Kuu atatakiwa kuwa na leseni A ya CAF au inayolingana na hiyo kutoka katika mashirikisho mengine duniani.

Aidha Kamati ya Utendajji ya TFF imemteua Meshack Bandawe kuwa mjumbe wa bodi ya mfuko wa  maendeleo ya mpira wa miguu - TFF (FDF), Bandawe ni meneja wa PPF kanda ya ziwa.


IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)


Argentina yaifumua Jamaica kidude, yatinga robo fainali

Argentina
Safi sana kijana, Higuain (kulia) akipongezwa na Messi na Di Maria baada ya kufunga bao la mapema

Argentina 4
Messi akikikusanya kijiji kama kawaida yake
Argentina 5
Gonzalo Higuain akishangilia bao lililoivusha Argentina robo fainali za Copa America
BAO la dakika 11 ya Gonzalo Higuain kutokana na pazi murua ya Angel di Maria imeiwezesha Argentina kusonga mbele katika kundi lake kwenye michuano ya Copa America, huku Chile ikiitafanua Bolivia 5-0 na Uruguay na Paraguay wakitoshana nguvu katika mechi nyingine.
Argentina kwa ushindi huo imeongoza kundi lake la B kwa kufikisha pointi saba mbili zaidi ya Paraguay na zote zimesonga mbele hatua ya robo fainali.
Bolivia licha ya kupigwa mkono na Chile, lakini timu hizo mbili zimefuzu hatua ya robo fainali kutoka kundi A, huku kundi C likitarajiwa kutua washindi wao leo sambamba na timu mbili zitakazoungana na zilizofuzu moja kwa moja. Timu tatu za Uruguay, Venezuela na Ecuador zinawania nafasi ya Best Looser katika michuano hiyo.

Utukutu wamponza Neymar, afungiwa mechi nne Copa America

Mshikemshike baada ya Neymar kuzua tafran kwa kupiga mpira ulio 'mbabua' mgongoni mchezaji wa Colombia
Neymar (10) akizozana na wachezaji wa Colombia huku akizuiwa na wenzake wa Brazil
Neymar vurugu
Kwani we unataka nini? Neymar akizozana na wachezaji wa Colombia huku mwamuzi akiteta naye
AMA kweli hasira hasara! Straika tegemeo na nahodha wa timu ya taifa ya Brazil, Neymar Jr anatarajiwa kuikosa michuano ya Copa America inayoendelea nchini Chile baada ya kufungiwa kucheza mechi nne. 
Mshambuliaji huyo wa Barcelona mwenye umri wa miaka 23 alionyeshwa kadi nyekundu kwa kuzozana na wachezaji wa Colombia kufuatia kipigo cha bao bao 1-0 walichopata Brazil katika mchezo wao wa makundi. Mbali na kadi ya moja kwa moja, lakini inadaiwa kuwa Neymar alimtolea lugha ya matusi mwamuzi wa pambano hilo na ndiyo sababu ya kuadhibiwa kukosa mechi nyingine za ziada badala ya moja tu ya kadi aliyopewa.
Nyota huyo tayari anatumikia adhabu ya kutocheza mechi moja hivyo kumfanya kutokuwepo katika mchezo wa mwisho wa makundi dhidi ya Venezuela utakaochezwa usiku wa leo.
Lakini Shirikisho la Soka la Amerika Kusini sasa limepitia tukio hilo na kuongeza adhabu kwa nyota huyo baada ya kudaiwa ripoti ya mwamuzi ilitaarifa kumtusi. 
Mchezaji wa Colombia Carlos Bacca ambaye pia alipewa kadi nyekundu katika tukio hilo naye amepewa adhabu ya kutocheza mechi mbili huku wachezaji wote wakipewa nafasi ya kukata rufani kama hawakuridhika na adhabu.

The Cranes yamfukuzisha kazi kocha Nooij Taifa Stars

Bechi la ufundi
Kocha Stars na wenzake wakati wa wimbo wa Taifa kabla ya kuvaana na Uganda The Cranes
Kocha Nooij akisindikizwa na Polisi mara baada ya filimbi ya mwisho ya mchezo wa timu yake dhidi ya Uganda The Cranes am,bapo Stars ilichapwa mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Amaan Zanzibar.
Na Mwandishi Wetu Zanzibar

SAFARI ya Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imeifikia tamati baada ya Kamati ya Utendaji ya TFF, kutangaza kulipiga chini benchi nzima baada ya timu hiyo kucharazwa mabao 3-0 na Uganda The Cranes.
Stars ilitandikwa mabao hayo katika mchezo wa kwanza wa kuwania fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) zitakazofanyika mwakani Rwanda, uliochezwa kwenye Uwanja wa Amaan, visiwani hapa.
Mara baada ya pambano hilo ambalo lilikuwa la 18 kwa Stars chini ya Kocha Nooij ikiwa imeshinda mechi tatu tu, moja likiwa la mashindano Kamati ya Utendaji ya TFF ilikutana na kutoa taarifa ya kumtimua kocha huyo na wasaidizi wake na taarifa za chini chini zinapasha kuwa Charles Boniface Mkwasa na Abdallah Kibadeni huenda wakapewa timu.

TFF ilimpa kocha Mart Nooij mtihani wa mwisho na endapo atashindwa kuipeleka Taifa Stars, basi atafute njia ya kuondoka baada ya wapenzi wa soka nchini kuchoshwa na ipigo ya timu hiyo.


Wiki iliyopita, Taifa Stars ilipokea kichapo cha idadi kama hiyo cha mabao kutoka kwa Misri katika mchezo wa kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) zitakazofanyika mwaka 2017 nchini Gabon.


Katika mchezo huo ambao Stars ilicheza kama isiyo na mwalimu ilijikuta ikienda mapumziko ikiwa nyuma kwa bao 1-0. bao hilo liliwekwa kimiani na Sekisambo Erisa ambaye alikuja kufunga bao jingine na kufanya aitungie Stars mara mbili na lingine lilifungwa na Miya Farouk.

Kabla ya kuanza mchezo huo, Taifa Stars ilipata pigo baada ya mchezaji wake Oscar Joshua kuugua ghafla na kuukosa mchezo huo.


Kwa mara ya mwisho Stars ilifuzu kwa fainali hizo za Chan mwaka 2009 zilipofanyika kwa mara ya kwanza nchini Iory Coast na ilitolewa katika hatua ya makundi ikiwa chini ya Mbrazil Marcio Maximo.


Mara baada ya pambano hilo mashabiki wenye hasira walitaka kumtandika kocha Nooij kabla ya askari Polisi waliokuwa uwanjani kumuokoa.
Tangu mapema mara baada ya kufungwa bao la kwanza, mashabiki waliibadilika Stars na kuanza kuizomea na kuwafanya wachezaji kupoteza kujiamini na kusababisha kufungwa mabao mengine yaliyoiweka timu hiyo katika wakati mgumu kusonga mbele kwenye michezzo hiyo ya Chan.
Stars na Uganda zitarudiana wiki mbili zijazo na mshindi atakayesonga mbele ataumana na Sudan katika raundi inayofuata.
Chini ni taarifa ya TFF juu ya kusitisha kibarua cha Kocha Nooij.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
 20 JUNI, 2015
KAMATI YA UTENDAJI YASITISHA AJIRA YA NOOIJ
Kamati ya utendaji ya Shirikishi la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Katika kikao chake cha leo pamoja na mambo mengine ilipitia mwenendo wa Timu ya Taifa (Taifa Stars) ikiwa ni pamoja na kuhudhuria mchezo kati ya Tanzania na Uganda, kama sehemu ya tathmin ya mwenendo wa timu.

Kamati ya utendaji kwa kauli moja imeamua yafuatayo:

1.Ajira ya Kocha Mkuu Maart Nooij inasitishwa mara moja kuanzia  tarehe 21/June/2015.

2.Benchi lote la ufundi la Taifa stars limevunjwa kuanzia tarehe 21/06/2015.

3.Uongozi wa TFF utatangaza punde benchi jipya la ufundi la timu ya Taifa.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)