|
Simba walioendeleza sare zao katika ligi |
|
Yanga waliolala Kaitaba |
|
JKT Ruvu walioshindwa kulicheza gwaride la Polisi Moro |
WAKATI klabu ya Simba ikiendeleza wimbo lake la sare, watani zao Yanga wamezamishwa kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba kwa kulazwa bao 1-0 na Kagera Sugar, huku maafande wa JKT Ruvu wakilala uwanja wa Chamazi ikiwa ni wiki moja tangu wavunje rekodi ya kuwa timu ya kwanza kuifunga Azam.
Simba ikiwa kwenye uwanja wa Jamhuri ililazimishwa sare ya 1-1 na Mtibwa Sugar na kuendeleza rekodi yao ya kutoshinda katika michezo 12.
Simba walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Joseph Owino, Nahodha wa vijana wa Msimbazi, kabla ya wenyeji kuchomoa bao kupitia kwa Mussa Hassan Mgosi, huku beki wa zamani wa Yanga, David Luhende akikosa penati ambayo ingeweza kuisaidia Mtibwa kuibuka na ushindi.
Mjini Bukoba, Yanga ikiwa na furaha ya kushinda 3-0 dhidi yha Stand United, ilijikuta ikichezea kichapo cha bao 1-0 mbele ya Kagera Sugar huku nahodha wake, Nadir Haroub Cannavaro akilimwa kadi nyekundu kwa mchezo mbaya dhidi ya mfungaji wa bao pekee la wenyeji, Paul Ngwai.
Kipigo hicho kimepokewa kwa masikitiko na kocha Marcio Maximo aliyelallamikia wachezaji wa Kagera kujaingusha na mwamuzi kutokuwa makini katika mchezo huo mbali na kulalamikia ubovu wa uwanja wa Kaitaba ambao umekuwa ukiisumbua Yanga kila mara kwa kuchezea kichapo.
Katika pambano jingine lililochezwa uwanja wa Chamazi, JKT Ruvu ilizimwa na maafande wenzao wa Polisi baada ya kulala mabao 2-1.
Mabao ya washindi yaliwekwa kimiani na nyota wa zamani wa Simba na Taifa Stars, Danny Mrwanda aliyefunga yote mawili na lile la wenyeji waliokuwa wametoka kushinda mechi mbili mfululizo likiweka wavuni na Jaffar Kisoki kabla ya Polisi kusawazisha na kuata la ushindi.
Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea kesho kwa pambano moja tu kati ya Mgambo JKT itakayokuwa wenyeji wa Mbeya City.